IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Ndugu Nsiande,unapotosha mada,ingefaa uweke post yako na utueleze kwa uzuri ili sie watz tusiolewa tujue kila kitu kuhusu dowans. Unasema rais anaweza kumteua mkurugenzi wa tanesco,una maanisha kuwa Board ya Tanesco haina mamlaka kwa ilo?Kila mtu anajua kuwa rais ana power zote na pia hata kutamka Nsiande hakamatwe na kuwekwa kizuizini bila kutoa sababu kwa umma lakini haimaanishi kuwa atatumia iyo power kutenda atakapojisikia sawa mkuu? Alaf kama unasema Dowans unaijua vizuri na wewe ulihusika kwenye Commission,kwa nini usiwe huru kuwataja hata wamiliki?mpaka dr.Slaa aseme. Nyie ndo watu tunaotaka mliongoze taifa lakini mnakaa nyuma ya hoja za watu,je taifa liwaeleweje? Come on,tetea wananchi bila woga!
 
[FONT=Book Antiqua, serif]Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.[/FONT]
[FONT=Book Antiqua, serif]
Sawa mkuu Salva tumekuelewa sasa ni nani mmiliki wa DOWANS atakayeenda kupokea sh 185bn?
[/FONT]
 
Ukiona waraka toka ikulu imepambwa na matusi kama vile KIZABIZABINA basi usisubiri sana mtu akueleze kwamba madai husika ni ya kweli kiasi gani. Taasisi ya heshima kutumia lugha za kihuni?

Kama Dr Slaa kajianzia tu uongo usio na msingi wowote basi hata nayo ikulu inahaki ya kutafuta sheria mahamani kuilinda na wala si kuandika lugha pungufu ya STAHA na kuisambaza kwa vyombo vya habari.

Mwandishi wa habari mwandamizi na mwenye historia inayoheshimika katika taaluma yake kama Dr Salva Rweyemamu alishindwa vipi kujizua na roho yake kutilia sahihi yake lugha kali kiasi hicho kwenda kwa jamii!!!
 
ni bora weye salva ungekaa kimya. Otherwise umeharibu kabisa.

Cha msingi hujatwambia ni nani basi mmiliki. Tuambieni ni nani mmiliki? nyie si ndio serikali kama hamjui basi prezo ndiye mmiliki.

Sikujua kama weye salva ni mtupu namna hii...............
 
Kama kweli Ikulu inaichukia Dowans kiasi cha kukanusha kuwa Kikwete si Mmiliki, mbona basi haitoi kauli juu ya kuichukia hiyo Dowans na kuwalaani wahusika kwa kuliingiza taifa katika hasara ya mabilioni? Mbona kimya. Kumbe Salva anajua kuwa Dowans ni mbaya na hivyo kumtaja mtu kuwa ni mmiliki ni kitu kibaya. Sasa kama si ubazazi kwa nini kisikemewe hicho kibaya Dowans, maana inaonekana kama Dowans ni Mzimu fulani tena unaolawiti watu kiasi kwamba kuambiwa wewe ni mmiliki wa huo mzimu unaruka kimanga kwa kuwa na wewe utaonekana ni mlawiti. Basi ukemee huo mzimu na uufutilie mbali. Vinginevyo ni kawaida ya Mtenda maovu kukiri huwa haiwezekani hadi anaingia rumande, atasema naonewa lakini haonekani kujutia. Kinachotoka moyoni na kinachoonekana usoni ni tofauti. Tunasubiri kauli ya Ikulu kuhusu Dowans, kama ilivyotoka kauli kuhusu katiba mpyaaa. Nawasilisha.
 
Nasisimikwa ni mwili jamani :A S 109:

RostamAziz.jpg
 
Kwa haraka haraka, nime note vitu vifuatavyo:

1. Taarifa hii imetolewa kutumia email binafsi ya Salva na si ya Ikulu. Imetolewa bila ya kuwa na official letter head ya Ikulu. This shows a lack of seriousness and professionalism.

2. Gazeti lenyewe limetoka tangu asubuhi mapema, lakini taarifa imetolewa saa 5:29 usiku, ikionesha kuwa imetolewa in a rush.

3. Salva anasema Tanzania Daima linamilikiwa na CHADEMA. Huu ni uongo, gazeti hili linamilikiwa na mfanyabiashara Freeman Mbowe na familia yake.

4. Lugha ya dharau, matusi, vitisho na kejeli imetumika mwanzo mpaka mwisho. Hii ni ishara kuwa Ikulu imetikiswa (imekuwa rattled to the core) na tuhuma za DK. WILLIBROD SLAA kuwa Kikwete ni mmiliki wa Dowans na hawana hoja za msingi za kueleza.

5. Katika taarifa yenyewe, haioneshi msimamo wa Kikwete kuhusu sakata la Dowans. Hii inaonesha kukwepa suala hili.

6. Hatari zaidi, Ikulu inasema kuwa ICC imeamua kuwa Dowans ilipwe na TANESCO kiasi cha sh bilioni 185. Huu ni upotoshaji mkubwa na wa kifisadi. Hukumu ya ICC inasema kuwa Dowans ilipwe $64.2 million, sawa na sh bilioni 97. Hiyo tofauti ya sh bilioni 88 ambazo Ikulu imeziongeza kwenye madai ya malipo ya Dowans zimetoka wapi na zinakwenda kwa nani?
 
Kwanini Salva anajibu kwa Jazba? kama kamsingizia ni kwanini Dk slaa asishtakiwe kwa kusema uongo ili ukweli ubainike?
 
Akili ya Rweyemamu na mawazo yake hayewezi kufanana wala kukaribiana na ya Dr. Slaa.
Slaa na mwamini, watasema tu mmiliki ni nani kwa makusudi au kwa kutojitambua kuwa wanamtaja
Kazi imeanza na safari hii mapema

mtu akiwa amechanganyikiwa anajuaje kuwa mwenzie kachanganyikiwa? Rweyemamu ndo amechanganyikiwa na hawezi kujilinganisha na Dr.Slaa. Kama dr ni mtu hatari mi nategemea anapaswa awe amewekwa kizuizini! Mnasubiri nini kumkamata Dr.Slaa na kumpeleka keko kwa uzushi tangu awataje kama mafisadi. Je kama slaa ni mzushi na amechanganyikiwa siku alipowataja mafisadi11,mbona mlikubali kuwa jk ni fisadi? Au kama hamkukubali mbona hamkukanusha?au mlikubali ufisadi upi,si ndo huu dr alioumaanisha tangu pale Mwembeyanga? Rweyemamu wewe umemtelekeza Baba yako,sasa nani mchanganyikiwa,slaa au wewe?? Kamsaidie Baba yako aliyekulea kwanza ndo utuambie haujachanyikiwa! Mzee Francis Kadogo anakufa njaa,anaishi kwa fedha ya kuuza gongo haramu,alaf wewe unasema sio chizi? Umelewa madaraka ndugu Salva Rweyemamu! Naweka thread mjadili salva!
 
...kwa hili bora Salva ungekaa kimya tungejua labda una chembe ya busara japo kidogo ipo kichwani mwako, sasa umeongea tumejua kuwa kwako hakiwezi kutoka kitu cha maana. Taarifa kutoka Ikulu haiwezi kuwa ya kihuni namna hii, kwa jinsi ulivyoandika kwa kejeli inadhihirisha wazi kuwa kuna jambo zaidi.

Kwa taarifa yako hatujawahi kumpuuza Dr. Slaa hata siku moja, ni yeye ndiye aliyeanzisha mwendo wa kuwashughulikia mafisadi wote mpaka sasa. Na safari hiyo haiwezi ikasitishwa kwa hoja za kipuuzi kama hizi.

Tupe taarifa kutoka Ikulu Dowans ni ya nani?
 
Silva is talking the obvious! Hakuna aliyetegemea aseme ni kweli Ikulu inathibitisha Mkwere ndiye mmiliki mkubwa wa Dowans! Hahahahahaahah

Rev. Umesahau Gamba la chuo linasemaje? Ukweli ni kitu gani?
unategemea watoe kitu kinaitwa ukweli? hiyo kitu ni ya kufikirika....yaani SATISFACTION........Usanii mtupu....:target::target:
 
JK hawezi kuukwepa ukweli kuwa ana masilahi mazito ndani ya DOWANS.......na huu hapa ni ushahidi:-

a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuiongoza Tanesco ulijaa mizengwe kibao..............Dr. Rashid mwenyewe alikiri kuwa pamoja na kuwa nafasi hiyo ilitangazwa magazeti yeye hakuiomba ila JK alimwomba amsaidie kwenye nafasi hiyo...........Hivyo pamoja na sheria ya Tanesco kuweka wazi kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanesco atateuliwa na Bodi, JK aliingilia Bodi kinyume na sheria pale alipombandika swahiba wake pale Tanesco..........................Swali la kujiuliza JK alikuwa anatetea masilahi ya nani kwa kuiingilia Bodi ya Tanesco?

b) Kwa vile Dr. Rashid hakuwa ameteuliwa na Bodi ya Tanesco hivyo na yeye hakuona sababu ya kuishirikisha Bodi tajwa katika utoaji wa zabuni ya uzalishaji wa umeme kwa Richmond na hata zabuni hiyo haikupitishwa kwa Bodi ya zabuni na matokeo yake kampuni kivuli ikapewa kazi hiyo..........Kulingana na rekodi zilizopo Brella, Richmond haijawahi kusajiliwa hapa nchini na hivyoufanyaji wake wa kazi ulikuwa ni batili na haikupaswa kupewa zabuni tajwa............Haya ni makosa ya kijinai yaani "criminal negligence" na JK anashindwa nini kumkabidhi swahiba wake Takukuru? Hapa inaonyesha kabisa hoja za Dr. Hosea kwa Wikileaks ni za kweli ya kuwa JK ndicho kikwazo kikuu cha utawala bora hapa nchini...............

c) Baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme ikaikabidhi kazi hiyo kwa DOWANS ambao walitumia dola za kimarekani 7.5 milioni kununua mitambo hiyo ya kuzalisha umeme kazi ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wa Tanesco.........................na hivyo hawakuhitaji mzabuni yeyote..........................

d) Tanesco kwa matendo yao walimhalalisha Dowans kuwa mzabuni wa kumrithi Richmond bila ya kupata kibali cha Bodi ya zabuni....

e) Baada ya mkataba kuisha Tanesco wakaishinikiza serikali kununua mitambo ya DOWANS kwa bei ambayo ilikuwa ni zaidi ya mara 20 ya bei ambayo Dowans walinunulia mitambo tajwa.......na ili kuishinikiza serikali kuinunua mitambo ya DOWANS, Tanesco wakaamua kuitumia Mahakama Kuu kwa kuwazuia Dowans wasiondoke na mitambo yao kwa amri ya Mahakama.....................bila sababu za kimsingi.........

f) Kutokana na uvunjaji huo wa mkataba kwa kutumia visingizio vya kuwa Dowans hawajalipa kodi, Msuluhishi akaibandika Tanesco jumla ya Tshs 185 Bilioni ikiwa ni zaidi ya mara 18 ya gharama ambazo Dowans walinunulia ile mitambo...............

g) Mwanasheria Mkuu ametoa ushauri Dowans walipwe huku uamuzi huo haujatoa sababu ni maeneo yapi Tanesco ilikuwa imekiuka huo mkataba kitendo ambacho kwa AG makini angeligangamala kuhakikisha analifungua shauri upya hapa Dar kupinga tuzo ambayo hata sababu za Tuzo hiyo hazifahamiki.........................Katika hukumu hiyo Msuluhishi aliahidi kutoa sababu lakini sababu hizo hakuzitoa sasa mdaiwa ataonaje kuwa katendewa haki? Hivi tuna AG au tunambabaishaji ambaye anadai ameipitia hiyo hukumu na ameona ipo beneti na tuilipe tu...............Hawa ndiyo wateule wa JK ambao kazi yao kuu ni kujenga mazingira ya kulipora taifa hili changa..........

h) JK hayuko tayari kumfikisha mahakamani Dr. Idrissa Rashid kwa sababu alimpeleka pale Tanesco kwenda kulipora hilo shirika la umma na hasa ukizingatia ya kuwa JK alivunja sheria za tanesco kuhakikisha Dr. Rashid anakwenda pale tanesco kulifilisi shirika hilo na mzigo wa hasara hizo kutupiwa raia wanyonge ambao kosa letu ni kumvumilia JK ambaye hana sifa ya kuliongoza taifa hili masikini duniani........

i) Haya ni mazingira yanaonyesha ya kuwa JK ni mshiriki kwenye mradi wa Dowans na hata kama jina lake halipo ila linawakilishwa na swahiba wake wa karibu Rostam Aziz kama ushahidi huu kwenye hukumu ya Dowans unavyothibitisha ambao tanesco wenyewe waliutumia ................................

RostamAziz.jpg

Uchambuzi makini huu... jamaa you are really analyticall na umeweka hizi mambo vizuri. Thanks!
 
Salva mdogo wangu - Ipo siku ukweli utafahamika na wewe utakuwa wa kwanza kupigwa pingu - Hiyo ndiyo tabia ya historia!
 
Shuleni kwetu, mtu mmoja hakwenda mchakamchaka asubuhi kwa sababu aliuhusudu usingizi. Alipotafutwa na mwalimu wa zamu, akajifanya kichaa. Watu wakambeba kumpeleka hospitali ya vichaa. Akagoma akisema mimi siyo kichaa! Wakazidi kumbeba, naye akazidi kusema, mimi siyo kichaaxn. Je, wangemwaminije kama siyo kichaa? TAFAKARI....
!

sasa unamaanisha nini? kwa aliyesema kuwa Dr. Slaa ni kichaa na sisi tunakataa kuwa si kichaa ndo kusema yeye nikichaa au sisi tunaokataa ndo vichaa au Ikulu ndo vichaa au unamaanisha nini hebu tafakari wewe uliyetoa hypothetical example. Hao walimu walio mbeba huyo dent ndo walikuwa vichaa, Maana kumverify kuwa mtu ni kichaa anakuwa associated na number of events tena ambazo ni abnmomal. Sasa kati ya JK na DR wa Phd nani kafanya events ambazo ni abnormal? jibu ni JK, kila kitu kimyaaaaaaaaaa, anachekacheka tu, Epa kimyaaaa, Richmond Kimyaaa, Kagoda kimyaaaaaa, Dowans Kimyaaaa, yaani jamaa sijui yuko je . Hebu sema yes YOU CAN but not in this dumb events.
 
Ngoja Wikileaks ije imtaje jina kabisa ndipo atajua watu wana data za uhakika.

Kwi kwi kwi! hii imenikumbusha ile story ya yule kibaka aliyekimbiaga na torch ktk mfuko wake wa suruali(nyuma) ikiwa on, akajificha ktk kichaka bila kujua kuwa torch bado ipo on! mpaka jamaa wakaja wakamgusa kwa bega hahahah! JK in trouble!
 
Nsiande,

Kimsingi uko sawa kujibu hoja. Mimi nakushauri USOME TENA neno kwa neno, hoja za Bwana RUTASHUBANYUMA, kisha uone kama unajibu tena au unatoa hoja!
Hello,
Nimesoma na nimejibu pale ambapo nimeona hapako sawa, kwa kujibu kwangu sina maana kuwa nataka dowans walipwe hapana, najibu yale ambayo yameandikwa bila usahihi, ikiwa ni pamoja na dr Rashidi kuridhia richmond ilhali aliikuta, ni hayo tu ndugu
 
Back
Top Bottom