Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,913
- 2,790
ni binti mzuri sana kwa kumtazama. mweusi wa kuvutia, umbo jembamba lililogawanyika, si mrefu si mfupi. uzuri wake ungekolea pale ambapo angepata hali bora zaidi ya kimaisha. nasikitika kusema nimeachana nae pamoja na yeye kunipenda upeo japo ni muda mfupi tu katika mahusiano yetu. niliumia kuona ninamwacha ingawa sikutaka kuwa nae. aliumia mara dufu yangu na maumivu yake niliyaona na kuyahisi. sikupenda hali yake. sikuipenda familia yake. sikuyapenda maisha yake ya awali. sikupenda anapoishi. sikulipenda kabila lake. nilimpenda yeye tu! ningetamani kuwa nae lakini ndoa ni mfumo. unahusisha koo mbili na zaidi na kuzifanya familia. yaweza kuwa ni ya kutunga ama ni kweli, lakini mapenzi ni nini? usitake kujua undani zaidi ila yatafakari haya kwa sasa.