I wish I could take it back...

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Jamani natamani ningerudi kama zamani...
Mkuu 'PCM' amelalamika kuwa siku hizi nimebadilika, mpaka akadhani kuna mtu ame-hack ID yangu.
Wakati najiunga JF, takribani mwaka mmoja uliopita, nilikuwa mstaarabu sana, coment zangu zilikuwa za kujenga, hakuna hata siku moja niliyokejeliwa kwa joindate yangu, unlike member wengi wapya.
Lakini kuanzia mwezi June mwaka jana, nikabadilika ghafla, nimepata ban 3 mpaka sasa hivi, ya mwezi, wiki na miezi minne. Hii kubwa nimeitumikia kwa mwezi na nusu, nikamwomba ROBOT akanifungulia,
ashukuriwe sana.
Nimekosa uvumilivu kabisa, nahisi na busara zimepungua, sijui ni nini bhandugu?
Wana-MMU?
Mnaweza kunisaidia kurudisha ile spirit yenye niliingia nayo JF? Nahitaji sana msaada wenu...
 
Hiyo ni wewe mwenyewe ujiulize na hakuna wa kukusaidia kurudisha bisara zilizopotea
Kaa chini ujiulize ni nini nimefanya na kwa nini imekuwa hivyo
Pole kwa ban
 
1.Kila wakati unapaswa kuchunga usemi wako,kabla haujaandika kitu fikiria kwa mapana hasara na faida zitakazotokana na hicho unachoandika,ukiona hasara au madhara yatakuwa mengi kuliko faida tafuta namna nyingine ya kujieleza au achana kabisa na hilo wazo.
2.Pia ni muhimu kuepuka mijadala inayolenga kuibua uhasama na mabishano yasiyo ya msingi.
Mimi si wa muda mrefu humu lakini nadhani kanuni nilizotaja zinahusika humu JF hata katika maisha ya kila siku.
 
Hujanistahi bali UMEJISTAHI!!
Ona umeshapiga hatua moja. . . ukiendelea hivyo utakuta busara nazo zinarudi taratibu.

naona ushapata pa kupumulia.
Kichwa cha thread kinanifunga, yangeshakuwa mengine hapa!
 
wakati mwingine watu wana-push batani yako ya mwisho.
Ukiwa mgeni unadhani aidha hujaelewa au ni bahati mbaya.
Ukikaa sana unausoma mchezo, unaamua na wewe kujilipua as jino kwa jino.

Lakini kwa sie watu wazima, mtu anakupiga dongo, unairuka komenti yake kama hujaiona. Sasa kama una spirit ya jino kwa jino utabaniwa hadi basi.
 
Kitendo cha kujijua kuwa haupo sawa ni hatua nzuri. Jiepushe na malumbano. Potezea mtu akikuudhi. Kama thread si ya kuleta mzaha na wewe usifanye mzaha. Andika yaliyo sahihi, mahala sahihi na kwa wakati sahihi.
 
Nimekumiss aise
Hujambo aise
 
Hiyo ni wewe mwenyewe ujiulize na hakuna wa kukusaidia kurudisha bisara zilizopotea
Kaa chini ujiulize ni nini nimefanya na kwa nini imekuwa hivyo
Pole kwa ban

unadhani hakuna wa kunisadia?
Watu wamesaidiwa kurudisha hamu ya kula mkuu, sembuse busara?
 
1.Kila wakati unapaswa kuchunga usemi wako,kabla haujaandika kitu fikiria kwa mapana hasara na faida zitakazotokana na hicho unachoandika,ukiona hasara au madhara yatakuwa mengi kuliko faida tafuta namna nyingine ya kujieleza au achana kabisa na hilo wazo.
2.Pia ni muhimu kuepuka mijadala inayolenga kuibua uhasama na mabishano yasiyo ya msingi.
Mimi si wa muda mrefu humu lakini nadhani kanuni nilizotaja zinahusika humu JF hata katika maisha ya kila siku.

noted.
 
unadhani hakuna wa kunisadia?
Watu wamesaidiwa kurudisha hamu ya kula mkuu, sembuse busara?

Ndo maana nasema ianzie kwanza kwako na jikubali
Then ignore ukishaona topic au thread au comment ya mtu ina maudhi achana nayo wala usijibu tena hama kabisa
Then uwe na kiasi kujipangia nini utajibu na kwa wakati gani na kwa nini ujibu
 
hapo nimekuelewa.
Vipi na kwenye muktadha wa kimaisha, maana nako nina tatizo kidogo.
 
hapo nimekuelewa.
Vipi na kwenye muktadha wa kimaisha, maana nako nina tatizo kidogo.

Even kwenye maisha kaka
ishi the way u like
Usipende na wala usiwe mtu wa hasira
Ignore hata mtu akikuudhi sometime chukulia yeye ni mpumbavu na achana nae usikunje sura wala kujibizana nae maana utajiumiza wewe
Take easy and uso wako upambwe na tabasam muda wote hata wakati wa mambo mazito maana Mungu anajua kuwa yapo na atakupa njia ya kuyakwepa na kuyamaliza
 
Back
Top Bottom