I salute and love women!

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote duniani

Mmmm jaribu kufikiri haya

ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!

UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana . Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU:
Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!

HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE? http://www.jd-nyepesinyepesi.blogspot.com/
 
mmmh jdbulogu spoti?????????????????????????????????????????????????????????
 
Jibuni hoja bana!
Wanaume hawana uvumilivu huo, wao ni "one mistake-KWENU!:)
Hongereni sana akina mama!
 
dada yetu yule nae kumbe anacopy na kupaste, halafu kutwa kulalamika JF inamfuatilia, yeye katokana wapi na thread ya mpenzi Iribini...Ila msacha ulibamba na lijithread....big up Iribini
 
Ukweli ni kwamba wanawake wanatakiwa kuwa imara na si kuendekeza ujinga ujinga kama huu. Mwanamke aliye imara hawezi kuvumilia ujinga, unyanyaswaji, udhalilishwaji, na upuuzi mwingine unaofana na hayo.

Kwa hiyo mimi nasema super dupa big up kwa wale wanawake wote walio imara, wenye msimamo unaoongozwa na common sense na wenye maadili mazuri.

Hawa wengine walio ma weakling...heck they deserve the shitty treatment that they get from the low down, no good men that they deal with.
 
Kwa wanaume kama wanetundewa hivyo basi tusingekuwa na familia tena. manake kama akisamehe basi wenzie watamwita majina mengi kama Zezeta au utasikia eti KAPIGWA SHUNTAMA na mambo mengine mengi kama hayo. Best hata kama hii thread imerudiwa hiyo siyo hoja ya msingi kubwa ni kuwa hawa mama zetu siyo siri sijui wameumbwaje manane ni wenye kuwa na msamaha kama Mungu hata kama ungewakosea bado watakusamehe tu. Kwa hapa JF, tunao dada zetu ambao wanaonekana kuwa na msamaha kama FL,Lily, Woman of sabstance, Pretty na wengine wengi tu ila kumbuka no law that has no exception.
 
Lakini kwa nini wanaume wawatendee hivyo wanawake? Au kwa nini watu wapendanao watendeane hivyo (haijalishi nani anamtendea vibaya mwenzake kwani kuna wanawake nao huwatendea vibaya wanaume wao).

Mimi namheshimu zaidi mwanamke anayechukua msimamo na kukataa kudhalilishwa, kunyanyaswa, na kutendewa vibaya kama vile mtumwa. Misamaha samaha kuwaendekeza watendaji mabaya na kudhani kuwa hata wakikutendea vibaya utawasamehe tu. Kusamehe samehe ovyo ovyo ni kujiwekea precedent mbaya.
 
Kuna tukio nililiona MAISHANI:
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:

ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!

UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!

HIVI INGEKEWA WANAUME

TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Kwa leo acheni tu niwape

heshima zao wanawake wote:

this sickens
mnaondoa hata ladha halisi ya hii kitu sasa loh!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom