Kelema
Member
- Jun 2, 2011
- 37
- 8
Ni aibu sana. Tena aibu Kubwaaaaa! Utauweka wapi uso wako kwa kumchukua mchumba wa mwenzio? Nenda kamwombe msamaha, ukiwa umefuatana na mtu anayenheshimu sana, ili yaishe. Ujue huyo mwanaume atakuja tu kumpenda mwingine na akuache kama alivyomwacha rafiki yako. Uchungu utakupata. Bora wewe urudishe urafiki na dada yule, mumteme jemee ili akome kudhalilisha wanawake. Akatafute mwingine mpya, atakuwa amejifunza somo (labda). Kama ana "sikio la kufa" basi akafe peke yake. Na kama hamjapima ngoma, kapime ujue ni mzima? kama si mzima anza dawa mapemaaaaaa. Pole sana kwa mhusika. Mungu akawe faraja kwako. Tena umshukuru Mungu, kwamba umemgundua jamaa, ukamjua kabla ya ndoa. Je, ungeshafunga ndoa ukagundua ungefanyaje???? Mungu wako anakupenda sana dada.