Huu wimbo wa zamani naupenda sana

Habari za wkend,

Jamani kuna huu wimbo unaitwa AFRO wa les Wanyika mwenzenu unanichanganya sana. Kila niusikiapo natamani ninyanuke nicheze.

Na nyie wenzangu nyimbo gani ya zamani inawagusa?

Mwanameka wa Marijani rajabu nomaa.. yani mtoto alivomtega Mussa mpk akaingia line, unanikumbusha Hawa alivomtega Adam kuleee Eden bustanini. halafu 'Cassanova' wa LeVert aaah mi HOI..!
 
oooh mme wangu ee ulinitaka radhi ee wataka oa mke mwingine wa pili uwezo huo wa kututunza unao aaah aaah matokeo ya penzi ee umezidi elemea kwa mke mdogo ee
 
Sasa mnayaona wazee, mambo anayofanya mke huyu anafikia hasa kukudharau wewe mama mzazi.
 
Maudhi ya Rohoni wa Ochestra Safari Sound enzi za Duku Duku nadhani ni wa 1981.
Nimepigwa ngwala wa Maquis du zaire wa 1978 na Penzi la Mwisho DDC Mlimani Park 1980. Tanzania iliwahi kuwa na miziki jamani, basi tu!
 
Bakulutu,

Huyo ngereza alikuwa mbongo?

John Ngereza alikuwa mtu wa Tanga, ila sijui ni mbondei au msambaa, wengi waliokuwa Simba wa Nyika na baadaye kuitwa Les Wanyika, akiwemo Issa Juma na profesa Omari, walitokea Tanga.
Pamela, Sina Makosa, Kajituliza Kasuku ni miongoni mwa classics zao
 
Embe dodo......umekwisha potea, kwa kunywa chang'aa, majengo siendi tena.....harambee, harambee!
 
Kuna wimbo sijui unaitwaje na umeimbwa na nani, nasikia tu neno "FATIMATA". Anaeujua umeimbwa na nani?

AMEIMBA Sam Mangwana ..mutoto kutoka Zimbabwe iliokulia Angola na kufanya kazi Congo na Ivory cost..
 
Jackie eee nitakuja nairobi, naota unaniletea kimfuko cha zambarau....vumilivu hula mbivu jackie eee kama sio kampala nairobi mama
 
Mpinga shetani,
Ahsante sana kwa kunipa historia nzuuri ya les wanyika.sasa hao kina ngereza wapo hai?
 
Jamani nani anaukumbuka ule wimbo wa yule jamaa aliyeapproach mdada wakakubaliana,yule jamaa aende kesho yake.
Yule jamaa kwenda kwa yule mdada kesho yake,akakuta maturubai,alipouliza akaambiwa dada yule kafariki!
Nikumbusheni tafadhali..
 
Kuna kitu NGAPULILA cha vijana orchestra, awamu ya pili pambamoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom