Huu wimbo wa zamani naupenda sana

Kuna wimbo huu unaitwa pesa na position wa madilu kama sikosei ni mtamu pia.
 
ndo huo
bwana ee, raha sana.
Kipindi hicho sina huyo mtoto mgongoni wala huyo anayekula hapo.

Uzee ni m*v* ya kuku
yatakuangukia tu
Huo wimbo wa jamaa aliyetoka shamba unaitwa 'Jogoo la shamba...' wimbo wa Mbaraka Mwinshehe, Super Volcano.
 
Kuna dude jingine nililisahau.....MV MAPENZI...lol
Heri ya wapendanao....moyo kama bahari...manahodha mimi na wewe....raha sanaaaaa
 
Kuna hii ya DDC mlimani wanasema , mwatusema sisi wanawake wabaya ni soo hawa jamaa wa zamani.
 
Mnasemaje kuhusu masafa marefu ya tancut almasi, kasaloo kyenga na kyenga songa
 
ule wa kifo hamuukumbuki???
au ndo mnaogopa...remmy...R.I.P
 
una balaa wewe

unanikumbusha, binti mmoja
yalimkuta ya dunia baada ya kufiwa wazazi
huu wimbo ndo ulikuwa hit, miaka hiyo.

ule wa kifo hamuukumbuki???
au ndo mnaogopa...remmy...R.I.P
 
Habari za wkend,

Jamani kuna huu wimbo unaitwa AFRO wa les Wanyika mwenzenu unanichanganya sana. Kila niusikiapo natamani ninyanuke nicheze.

Na nyie wenzangu nyimbo gani ya zamani inawagusa?

hapo mkubwa mwenzangu ungeandika...."wimbo gani wa zamani unawagusa"
 
Kajituliza kwake kasuku, hataki matata... ; Sijuhi ni wimbo wa nani - naupenda wimbo huu.
 
Nakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu
Najua hapa utabaki watasema mengi pia wabaya wetu mamaa
watafurahi....
Songi kali sana hii inaitwa masafa marefu- Tancut Almas
Kitambo sana.
 
Baba Paroko wa Bushoke-mkazi wange bojo kaziro tina maela ninabatobangye..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom