Huu wimbo wa zamani naupenda sana

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Habari za wkend,

Jamani kuna huu wimbo unaitwa AFRO wa les Wanyika mwenzenu unanichanganya sana. Kila niusikiapo natamani ninyanuke nicheze.

Na nyie wenzangu nyimbo gani ya zamani inawagusa?
 
usipate tabu neema
uliyoyafanya si mageni hapa dunianieeeeh.

Georgina pia.

Mapenzi yananivunja mgongo les wanyika

wifi zangu mna mambo

baba jeni bai bai, watoto watateseka mume wangu baba jeni bai bai

kuna twist moja nayo hunikumbusha sana old days ' nilikutana na mlofa mmoja, akanambia anatoka jela. Akasema nipe hela ya chakula. Kumbe uongo alidanganya. . .'
 
kuna mmoja wa moro jazz, unahusu kijana aliyekuja mjini juzi afu anajifanya mjanja. Mwishowe akapigwa na watoto wadogo.

Hata, ule wa medsenja kaleta balaa nyumbani kwa meneja bila kufahamul

mama nipe nauli nikamtafute monica, amekimbilia zambia ...
 
Kongosho, huo jamaa anaulizwa aliona wapi jogoo la shamba likawika mjini.

Kuna huu mwengine anasema, ooooh mama ulijua mimi masikini unanitesa buree oooh mama, mapenzi ya pesa mama ...kwa mbele ya wandugu mama mapenzi ya pesa si ya kweli..
 
kuna mmoja wa moro jazz, unahusu kijana aliyekuja mjini juzi afu anajifanya mjanja. Mwishowe akapigwa na watoto wadogo.

Hata, ule wa medsenja kaleta balaa nyumbani kwa meneja bila kufahamul

mama nipe nauli nikamtafute monica, amekimbilia zambia ...

Huo wimbo wa jamaa aliyetoka shamba unaitwa 'Jogoo la shamba...' wimbo wa Mbaraka Mwinshehe, Super Volcano.
 
Usitumie pesa kama fimbo mamaaa; wimbo wa Cosmas Chidumile.
 
Kuna wimbo mwengine unasema, oyaaa naingaya ohhh sijui wakongo wale dah! Kweli old is gold
 
Habari za wkend,

Jamani kuna huu wimbo unaitwa AFRO wa les Wanyika mwenzenu unanichanganya sana. Kila niusikiapo natamani ninyanuke nicheze.

Na nyie wenzangu nyimbo gani ya zamani inawagusa?

Kilio cha samaki- Remmy Ongala.
 
Kuleni kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa - Mwinamila, Tabora.
 
na huu pia hunikuna
'mtoto akililia wembe acha umkate . . .'
nadhani wa remmy
 
Kuna wimbo wa Balisidya uko hivi "kuna njama za kuhujumu na kudhulumu utu wa mwafrika, daima dumu eh. Njama hizi si ndogo ni kubwa, na zinaendeshwa usiku na mchana na mabepari wa dunia nzima eh. Udhalimu wa mabepari hao, kamwe hauwezi kufanikiwa bila ya kuwatumia waafrika wenzetu limbukeni wachache, wenye tamaa......"

sijui jamaa aliona mbali kiasi gani!
Huu unanifurahisha kwa maneno yake japo ala si nzuri sana
 
Dunia sasa imani imekwisha- marijani
pendo pendo si kulazimishana -marijani
rangi ya chungwa
majirani huzima radio ili wasikilize tunsvyogombana wametupachika majina wewe pwagu nami ni pwaguzi- DDC
Kauka nikuvae- OTTU
 
Habari za wkend,

Jamani kuna huu wimbo unaitwa AFRO wa les Wanyika mwenzenu unanichanganya sana. Kila niusikiapo natamani ninyanuke nicheze.

Na nyie wenzangu nyimbo gani ya zamani inawagusa?

vichwa hivi TOM MWALALA na JOHN NGEREZA...
Mimi kama kawaida yangu BAKULUTU ZOOOOOOTE from Joseph Kabasele & Grand Kale, Franco & TP n.k Songi langu la kila cku ni ile non stop ya Sam Mangwana Ilio beba Mabele,Ebale ya zaire na Faute ya cormentante..ni TAMUUU.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom