Elections 2010 Hukumu ya Igunga leo WANANCHI KUAMUA NANI AWE MBUNGE WAO

kumekuwa na tuhuma kila tunapokuwa na uchanguzi hapa nchini hasa zinazo husu kuchakachuliwa kwa matokeo. Nilikuwa na waomba wanaJF hebu tujaribu kutoa mawazo yetu ya kujenga, kuwa nini kifanyike ikiwa matokeo yatagundulika kuwa yamechakachuliwa.

Yaani kamanda unahofia kushindwa vita kabla ya mpambano? hapa suala sio jimbo la Igunga, suala hapa ni ushindi dhidi ya uchakachuaji, ni kulinda kura mpaka kieleweke. Labda itokee kwamba wana-Igunga walishauza jimbo kwa mafisadi.
 
unajitahidi kujifanya unaupinga ukweli wa mambo!!!!!!!!!! wewe ndo unayejifanya kujipa matumaini hewa! wewe pamoja na hao magwanda wako kwishnei!!!
Mechanical error kwenye nervous system.
 
Asante mkuu kwa taarifa.
Kwa makamanda tulio Igunga tupumzike ili tuamke kesho tukiwa na Nguvu za kutosha kwa ajili ya kulinda kura zetu.
Peeeeeeeeeooooooooooooooples...................
 
Naona ndio utakuwa muda rasmi wakung'oa CCM madarakani, pamoja na ukweli kwamba jeshi limewekwa standby Arusha, Mwanza, Mbeya, Shinyanga na Dar es Salaaam. Ombi letu kwa jeshi na polisi haswa wale wa vyeo vya chini ambao ndio wengi na ambao haki zao wananyimwa ni kuwa kusimama kulinda nchi na mali zake na sio kuua ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya tabaka la walio waroho wa madaraka. Ombi letu kwa jeshi na polisi ni kuwa waige mfano wa Jeshi na Polisi wa Misri, wasiwe vibaraka wa viongozi ambao ni vipofu na wasio kuwa tena credibility ya kuongoza hii nchi. Ombi letu kwa Jeshi na Polisi wa tanzania ni kuwa hakika damu ya kila mtanzania watayoimwaga kukidhi matakwa ya viongozi waporaji na wasiojali future ya tanzania itakuwa laana kwao na kwa vizazi vyao. Tunacho waomba jeshi na polisi kusimama upande wa upande utakoa shinda na kulinda matakwa ya watanzania kwa kuwa wanastaili ya kuchagua nani atakaye waongoza na sio kuchaguliwa na tume ya uchaguzi wa CCM kwa matokeo ya kuchakachuliwa.

Maoni yako kuhusu yule kamanda wa Mkoa wa Arusha wakati wa uchaguzi wa 2010 ni yapi? Kamanda yule yu wapi najua kuwa hayuko Arusha. CDM wanasema nini katika mambo na matukio kama haya.
 
Kuna habari kwamba uongozi wa CCM unahofia kuwa Chadema kwa kushirikiana na kundi la wana CCM wana mpango wa kuiba kura. Sababu ya hofu hiyo ni pale gari la viongozi wa juu wa CCM lilipopita eneo walipokua wasimamizi wa vituo, wakashangaa wasimamizi wakionyesha alama ya vidole viwili ikiwa ni ishara ya kuwa wao ni Chadema.
Taarifa zilizofuatia zikasema kwamba baada ya hapo na CCM ikaamua kuwapa baadhi ya mawakala fedha na inasemekana baadhi wamepewa laki moja moja na mashuhuda wametuambia hapa Nzega kwamba wameona wasimamizi 20 waliopokea fedha hizo. Tunakumbuka uchaguzi wa 1995 aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ali Ameir Mohamed alisema hatakubali matokeo maana CUF waliiba kura kule Zanzibar, matokeo yake CUF walionja joto ya jiwe na hadithi ndio hiyo kabla ya ndoa ya majuzi. More to come.

Wale wasimamazi wote wa uchaguzi wamewekwa na CCM. CDM wakisinda ni dhahiri wameshinda kihalali. Nape na wenzenu msipaparike kwa ishara ya vidole pekee.

Kwani wangewaonyesha dole la kati mngesuspect chama gani chenye hila?
 
khaaaaaaaaaaaa kwelitumechoka mana kila kukicha ni igunga tu utafkiri ni uchaguzi wa urais
 
Asante mkuu kwa taarifa.
Kwa makamanda tulio Igunga tupumzike ili tuamke kesho tukiwa na Nguvu za kutosha kwa ajili ya kulinda kura zetu.
Peeeeeeeeeooooooooooooooples...................
makamanda mnalala???????????? c'mon msije kutupotezea ushindi dakika za mwisho.nawaomba makamanda wote msilale muwe tayari kugundua mbinu chafu!!!
 
hahahahahaa,mkuu acha kuwapa watu matumaini hewa chadema washinde igunga???nakunywa tindikali labda wazoe wapiga kura toka arusha kiufupi kama sio ccm basi ni cuf,watz wameamka hawawezi kuongeza wasusia vikao bungeni kiufupi,dhambi ya tindikali kwa yule kijana,na kuudhalilisha uislamu italipwa kesho labda nafasi ya tatu mtashika lakini ubunge sahauni kabisa!
i.d.i.o.t
 
ukiona mwizi analia kuwa ataibiwa ujue kashikwa pabaya! wataipata habari yao!
 
Dondoo kutoka kwa chanzo cha habari cha ukweli:

  1. Mkutano wa Chadema ulikuwa funika mbaya.
  2. Helikopta iliongoza maandamano. Namaanisha helikopta ilikuwa juu ikienda mwenda wa raia, chini umati wa maelfu ya wananchi wakitembea kutoka afisi za Chadema kuelekea uwanja wa kampeni. Wa Jikoni anasema ilikuwa inaenda kijoti-joti. inastua kidogo, inaganda kidogo, mpaka uwanjani.
  3. Raia wako tayari kwa mabadiliko na wamejiapiza kuizika CCM kesho.
  4. Kura zitalindwa kwa gharama yoyote na mkurugenzi wa wilaya ametahadharishwa asijaribu kupindisha ukweli.
  5. Kura zitahesabiwa kituo kwa kituo, matokeo yakishapatikana, watu wataandamana kwenda ofisi za halmashauri kufanya hesabu za 'milinganyo sahili'.
  6. Kama hesabu jaitabalansi hapo kwenye (5) na CCM kujitangaza washindi, MOTO utawaka Igunga, Shinyanga, Mwanza, Arusha, Musoma, Dar Es Salaam, na popote ambapo kuna raia wanaotaka mabadiliko ya kweli.
  7. Polisi waliahidiwa posho za 30 000 kwa siku, lakini wanalipwa 5 000/ kwa siku. Nao hawadanganyiki japo hawawezi kusema hadharan
Chai kidogo:
Mh. Kasulubai(MB) kama mtoto wa Kigoma tu. Amesema CCM wameleta mchawi (mchawi kweli siyo masihara), lakini amewaambia Wana-Igunga kwamba huyo mchawi wao "agwinga ngogo gete bhaseya"

Jamani eeh, mnisamehe kuwacheleweshea updates...Wajikoni anapigiwa simu na watu wengi gafauti gafauti. wakati mwingine anaishiwa chaji.



CCM waacheni Wana-Igunga. Wanataka mabadiliko. Hatutaki kusikia mtu kapigwa risasi kafa tena huko. Mlikubali vyama vingi...sasa tunaomba mfaidi matunda yake, siyo kupiga fita.

Naenda kulala.


kalale salama mkuu uamke mweye nguvu kutujuza ili na sisi tufaidi bana, mweeeeeeee!
 
Hahahahahaa,mkuu acha kuwapa watu matumaini hewa chadema washinde igunga???nakunywa tindikali labda wazoe wapiga kura toka arusha kiufupi kama sio ccm basi ni cuf,watz wameamka hawawezi kuongeza wasusia vikao bungeni kiufupi,dhambi ya tindikali kwa yule kijana,na kuudhalilisha uislamu italipwa kesho labda nafasi ya tatu mtashika lakini ubunge sahauni kabisa!


Inatakiwa kuongezwa wakuunga hojaa na kugongameza/kusinziya wapambanajii wanawazalilisha mafisadi
 
Jamani siasa hizi,....
me na-reserve comment yangu hadi nione matokeo.
Huwezi jua anacho waza mtu aliyepo kwenye mkutano wa kampeni.

Nimeona makamba anajiapiza ccm kushinda.

Nimeona Jussa anajiapiza cuf kushinda,....

Chadema nao ndio balaa,hawako nyuma kujiapiza kushinda.

Swali ni je,....kwanini hamna chama hata kimoja kilicho sema kitakubari
matokeo?
Kila mmoja anataka kushinda,ni vigumu kuwa na wabunge watatu katika jimbo moja.
Otherwise tuna tanzamia vurugu kubwa igunga (God forbid)
 
Kukubali matokeo ndiyo kukomaa kisiasa, kila la heri wagombea, mshindi anasubiriwa mjengoni Dodoma kutetea maslahi ya watanzania!

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom