Elections 2010 Hukumu ya Igunga leo WANANCHI KUAMUA NANI AWE MBUNGE WAO

Mfanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Igunga akipakia vifaa vya uchaguzi vitakavyotumika leo kwenye uchaguzi mdogo Wa Jimbo la Igunga

WANANCHI KUAMUA NANI AWE MBUNGE WAO

Daniel Mjema, Igunga

MACHO na masikio ya Watanzania, leo yanaelekezwa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, ambako wananchi watapiga kura kumchagua mgombea mmoja kati ya wanane wanaoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge, kuwa mbunge wao.Mgombea atakayechaguliwa atamrithi Rostam Aziz, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, ambaye alijiuzulu katika tukio lililohusishwa na mchakato wa kujivua gamba ndani ya chama hicho.

Rostam alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 1994 hadi alipojiuzulu Julai 13, mwaka huu.Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni Leonard Mahoma wa CUF Joseph, Dk Dalaly Kafumu wa CCM na Kashindye wa Chadema.

Wagombea wengine wanaoshiriki uchaguzi huo na vyama vyao kwenye mabano ni Said Cheni (DP), Heme Dedu (UPDP), Hassan Rutegama (Chausta), John Maguma (Sau), na Steven Mahuyi (AFP).

Wagombea wote mbali na kujinadi kwa sera za kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo tangu kampeni hizo zilipoanza Septemba 7, mwaka huu walikuwa wakipigana vijembe wakati wote wa kampeni.

Kazi ya wagombea hao na vyama vyao kunadi sera imekamilika jana na leo wakazi wa Igunga, wataamua nani awawakilishe bungeni kama mbunge wao.

Polisi waimarisha ulinzi Igunga

Msemaji wa Jeshi la Polisi katika uchaguzi huo, Isaya Mngulu aliliambia gazeti hili kuwa, jeshi hilo limejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakamilika katika mazingira ya amani.

"Hadi leo (jana) tunapozungumza hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani na tunaamini hali itaendelea kuwa shwari na tunavitaka vyama viwaelimishe wanachama na mashabiki wao umuhimu wa amani," alisema.

Mngulu alisema wapo polisi wa kutosha Igunga, kikiwamo Kikosi Maalumu cha Kutuliza ghasia (FFU) na kuonya watu kujaribu kuvuruga akisema watapambana na mkono wa dola.

"Nataka niwahakikishie wapiga kura kuwa wajitokeze kwa wingi na waende kupiga kura, ulinzi ni imara hakuna mtu atakayeletewa vurugu au kuzuiwa kupiga kura… kwa kweli tuko kamili," alisisitiza Mngulu.

Alisema katika kuimarisha ulinzi huo, polisi wamefungua komandi ndogo nane, maeneo yenye wananchi wengi ya Simbo, Mwisi, Nkinga, Sungwisi, Ziba, Mwanshimba, Igurubi na Itumba ambazo zitakuwa katika utayari wa kukabiliana na chokochoko yeyote.

Polisi wapeperusha bendera nyekundu
Magari ya polisi yanayotumika kusimamia ulinzi na usalama katika uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, yameonekana yakirandaranda mitaani usiku na mchana huku yakipeperusha bendera nyekundu.

Mengi ya magari hayo aina ya Toyota Land Cruicer rangi ya bluu yameonekana yakizunguka mitaani na askari wa FFU, hali inayotafsiriwa kuwa ni kudhihirisha kuwa, atakayeleta chokochoko atakiona cha moto.

Juzi gari lililosheheni lita 80,000 za maji ya kuwasha, nalo lilionekana likitoka mafichoni katika kituo cha polisi Igunga na kuzunguka mitaani, katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni kutoa ujumbe wa kuzatiti kwa jeshi hilo.

Msimamizi wa uchaguzi anena
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga, Protas Magayane, alilsema jana kuwa vifaa vyote vya kupigia kura vilianza kusambazwa jana asubuhi.

Magayane alisema jimbo hilo lina kata 26 na wapigakura waliojiandikisha 170,077 na kwamba ili kuharakisha usambazaji wa vifaa unaenda vizuri, wamekodi malori 52 yatakayokwenda kila kata mawili kusambaza vifaa hivyo.

Magayane aliwataka wapigakura wafike mapema vituoni wakiwa na vitambulisho halali vya kupigia kura na si fotokopi na kwamba, watakapomaliza kupiga kura waondoke maeneo hayo wakisubiri matokeo.

"Kuna wapigakura wali-scan vitambulisho vyao au kutengeneza fotokopi, Hivyo havitaruhusiwa bali waje na vitambulisho 'original' (halisi) na waepuke kuvaa sare yoyote ya chama au kufanya kampeni vituoni," alisema.

Hekaheka zatawala Igunga
Kumekuwa na hekaheka katika Jimbo la Igunga kwa siku mbili mfululizo sasa huku magari makubwa na madogo, baiskeli, bajaji, pikipiki na hata mikokoteni, ikipeperusha bendera za vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Lakini kubwa ni magari ya viongozi na wafuasi wa vyama vikubwa vitatu vinavyoonekana kukabana koo vya CUF, Chadema na CCM ambayo yamekuwa yakiporomosha muziki unaosifu vyama na wagombea wao.

Tambo za hapa na pale baina ya wafuasi wa vyama vya Chadema CCM na CUF zinaonekana wazi kwenye vijiwe, nyumba za burudani na makazi ya watu.

Mbali pilikapilika hizo, helikopta za vyama hivyo nazo zilipasua anga kuanzia asubuhi jana kuelekea maeneo ya mikutano ya hadhara ya kuhitimisha kampeni hizo zilizodumu takribani siku 25.

Igunga yaelemewa na wageni
MJI wa Igunga unaelekea kulemewa na wageni wengi wakiwa ni viongozi na makada wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo mdogo wa ubunge.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa nafa za kulala katika nyumba za kulala wageni sasa hivi zimekuwa adimu kutokana na wingi wa wageni hao huku baadhi ya wamiliki wakipandisha gharama za malazi kwa siku.

Kila nyumba ya wageni utakayopita sasa utakutana na kibao chenye maandishi "hakuna nafasi" kutokana na vyumba kujaa kunakochangiwa na kuwapo kwa nyumba hizo chache ikilinganishwa na idadi ya wageni waliopo.

Inakadiriwa kuwa wageni kati ya 3,000 na 6,000 wako Jimboni Igunga hivi sasa. Wengi wao ni viongozi wa kisiasa wakiwamo viongozi wa kitaifa, wabunge, makada, wapiga debe wa vyama na wanahabari.

Ujio huo wa wageni unaonekana kuwanufaisha zaidi wamiliki wa nyumba hizo ambao baadhi wamelazimika kupandisha gharama za malazi kwa kati ya asilimia 10 na 20 ikilinganishwa na bei za awali.

Baadhi ya madereva na wapiga debe wa vyama vya siasa hivi sasa wanalazimika kulala kwenye magari na wengine wa jinsia moja kulala wawili kwenye chumba kimoja kutokana na upungufu wa vyumba.

Lakini ujio huo wa wageni umeongeza mzunguko wa fedha katika jimbo hilo ambapo mama lishe mmoja alisema: "Kimsingi, uchaguzi huu ni neema kwetu, tunatamani ufanyike kila mwezi."

Wafanyabiashara wote, awe mama lishe, mmachinga, maduka ya nguo, migahawa na nyumba za starehe kama baa na kumbi za muziki wanaonekana kunufaishwa na ongezeko hilo la mzunguko wa fedha wilaya humo hivi sasa.
 
Hahahahahaa,mkuu acha kuwapa watu matumaini hewa chadema washinde igunga???nakunywa tindikali labda wazoe wapiga kura toka arusha kiufupi kama sio ccm basi ni cuf,watz wameamka hawawezi kuongeza wasusia vikao bungeni kiufupi,dhambi ya tindikali kwa yule kijana,na kuudhalilisha uislamu italipwa kesho labda nafasi ya tatu mtashika lakini ubunge sahauni kabisa!
Uislam umedhalilishwa kivipi?
Dogo usichanganye kati ya kohozi na Kamasi.

Tofautisha kati ya mtandio na Hijab ni kubwa sana.

Hijab ni vazi la Hishma kwa wanawake na wasichana wa kiislam.

Lakini mtandio wanavaa mpaka wenzako wa pale Corner Bar Ambiance ambao hukesha usiku kucha wakiuza nyama.
 
Kwa vile Dowans imeshalipwa mabilioni yao, jimbo la Igunga halina umuhimu wowte kwa CCM tena, ila watajitahidi kuligombea ingawa wakilikosa hawatalalamika kabisa.
 
Jamaa yake Ng'wanangwa aliyeko jikoni amekuwa akituleta habari za uhakika kutoka jikoni kabisa Igunga wiki hii.

Ameonyesha uwezo mkubwa wa kutoa habari kuliko hata watu wanaokula mshahara kwa kazi hiyo kama Gerald Hando na Ephraim Kibonde.

Ingawa namba zake za simu hatujapewa hivyo hatuna uwezo wa kuwasiliana naye direct, tunategemea leo atakuwa nasi kupitia kwa Mami Ng'wanangwa kutupa news za kituo kwa kituo ili tujijumlishie wenyewe na kuanza kuingia mitaani huku tuliko kusherehekea ukombozi.
 
Wabeja nkohi kwa taarifa...tunaomba watu wako(makamanda)wawe active kukupa taarifa za matokeo kwenye vituo na wewe utuwekee hapa mie nshaandaa kalikuleta yakufanya majumuisho na majumuisho nitafanya mwenyewe na kumtangaza mshindi sio mpaka tumsubiri Mkurugenzi.
 
Jamani siasa hizi,....
me na-reserve comment yangu hadi nione matokeo.
Huwezi jua anacho waza mtu aliyepo kwenye mkutano wa kampeni.

Nimeona makamba anajiapiza ccm kushinda.

Nimeona Jussa anajiapiza cuf kushinda,....

Chadema nao ndio balaa,hawako nyuma kujiapiza kushinda.

Swali ni je,....kwanini hamna chama hata kimoja kilicho sema kitakubari
matokeo?
Kila mmoja anataka kushinda,ni vigumu kuwa na wabunge watatu katika jimbo moja.
Otherwise tuna tanzamia vurugu kubwa igunga (God forbid)

Shida yako ni kwamba unajidai hutaki kuonekana uko upande gani. Lakini wenye uwezo wa kung'amua wameshakushtukia.
 
WANA-IGUNGA TWENDE SASA TUKAPIGE KURA MAPEMA MAPEMA TU

UCHAGUZI wa Igunga umeanza alfajiri hii watu wakijihimu kuelekea vituoni kutekeleza wajibu wao kama raia wema kwa kuzingatia katiba yetu inavyotamka.

Katika uchaguzi huu wa leo, wananchi wenye itikadi mbalimbali wanategemewa kushiri kujiamulia nani awe kiongozi wao mara baada ya FISADI Rostam kupigwa chini na dhambi zake mwenyewe ingawaje wananchi baado hatujamalizana naye hata kidogo.

Ni jumla ya vijiji vyote 98,na kata zote 26 za IGUNGA zitakazoshiriki katika uchaguzi huu wa leo. Kata zenyewe kwa majina ni kama ifuatavyo:
1. Bukoko
2. Chabutwa
3. Choma
4. Igoweko
5. Igunga

6. Igurubi
7. Isakamaliwa
8. Itumba (Igunga)
9. Itunduru
10. Kining'inila

11. Kinungu
12. Mbutu
13. Mwamashiga
14. Mwamashimba
15. Mwashiku

16. Mwisi
17. Nanga
18. Ndembezi
19. Ngulu
20. Nguvumoja

21. Nkinga
22. Ntobo (Igunga)
23. Nyandekwa (Igunga)
24. Simbo
25. Sungwizi

26. Ziba

NB: Ni matarajio yetu kwamba tangu hivi sasa JF tutaanza kupata taarifa mbali mbali kutoka Igunga kuhusiana na mazingira yote ya uchaguzi wa leo hadi zoezi zima litakapohitimishwa.

Wana-JF natumai mmekwishajipanga vizuri kote kama ilivyo ada.
 
Watu hamlali! wenzenu watafaidi maposho wakienda bungeni nyie mnakesha tu bila sababu za msingi! ngoja ukuche niende kanisani then nsubili game la arsenal na totenhum mie! ctaki kusikia upupu wa mambo ya siasa unatutia umasikini tu, bora tucngekuwa na vyama! najuta kuwepo kwa vyama vya siasa yaani nasikia hata kichefu chefu.
 
Mungu awabariki wana igunga wafanye maamuzi sahihi na alaaani njama zote za kuiba kura au kuchakachua matokeo. Mwisho wa siku uchaguzi uwe huru na wa haki na vyama vikubaliane na matokeo baada ya uchaguzi huru na wa haki.

Ieleweke kuwa njama zozote za kuiba kura ndizo zitavuruga amani na utulivu uliopo nchini, hata kama polisi wote Tanzania watenda Igunga.
 
Bwana mzee umeamka kwa kisirani kama mwana-CCM mwenye kushutumiwa ufisadi kwa taifa lake mkuu. We bora ukajihimu kanisani kwa kuwa ni mweupe sana kuhusu mabadiliko. Mabadiliko mtu humiminiwi kama chai bali ni lazima ukayapiganie kwa hali na mali ndipo ufanikishe pamoja na wengine wenye moyo.

Watu hamlali! wenzenu watafaidi maposho wakienda bungeni nyie mnakesha tu bila sababu za msingi! ngoja ukuche niende kanisani then nsubili game la arsenal na totenhum mie! ctaki kusikia upupu wa mambo ya siasa unatutia umasikini tu, bora tucngekuwa na vyama! najuta kuwepo kwa vyama vya siasa yaani nasikia hata kichefu chefu.
 
Mafuta taa na Sukari zinatosha kabisa kuiondoa ccm! Wana Igunga wameamka hawadanganyiki tena!
 
kila la heri kwa watanzania wote wanaopiga kura leo, ingawa macho na masikio yapo jimbo la Igunga
 
WATANZANIA TUJIONDOLEE ADHA ZA UCHAKACHUAJI KWENYE CHAGUZI ZETU KWANZA KWA KUANGAMIZA 'UJIMA' WETU WA KIMAWASILIANO NA KULINDA MAZINGIRA MAPYA TUYATAMANIYO KISHERIA

1. Wakala asikubali kupewa chakula, kinywaji wala msaada wowote ule na timu pinzani Watumewahi kulishwa madawa ya kulevya, kunyunyuziwa chlorofoam ili walale usingizi wa pono huku madudu yakifanyika.

2. Iwe ni jukumu la chama kulisha mawakala pale pale kituoni na wala si kwenda kutafuta chakula kwingineko.

3. Idadi ya mawaka isipungue wanne katika kila kituo. Na idadi hiyo iwe ikishika zamu kwa kuzingatia ratiba maalum inayopangwa na mkurugenzi wa uchaguzi wa chama na kupishana zamu kimaandishi mbele ya Kamanda Msimamizi wa chama katika ngazi ya kata.

4. Mawasiliano yaboreshwe zaidi na kutumika Satelite phones, kompyuta za mapajani zenye kutumia internet services zenye uwezo wa kutiririsha kila taarifa papo kwa hapo (ziwe zimewekewa zile programmes za kisasa zenye kuruhusu tu kuongea tu na maneno kubadilika maandishi) na radio calls za chama zenye kuruhusu minute-to-minute communication tangu ngazi ya kitongoji hadi makao makuu bila mawasiliano hayo kuingiliwa.

5. Haki ya raia kulinda kura zao kwa kuzingatia taratibu zilizowazi ihimizwe kisheria tangu sasa.

6. Kwa kuwa uchaguzi wa mwaka jana uliibwa katika ngazi ya kujumlisha kwenye kompyuta, fundisho hilo lituelekeze kudai haki ya vyama shiri vyote kuwa na ushiriki wa taarifa zote live kadiri zinavyoendelea kwenye tume ndivyo na wafwatiliaji kwenye makao makuu ya vyama husika wanavyoona.

Hili linawezekana kabisa sawa tu na taarifa za soko la fedha NASDAQ zinavyotiririshwa kutoka chanzo kimoja na washiri wote wa kwenye shughuli za soko hilo hufwatilia live kutoka majumbani mwao, barabarani na kadhalika.

Huo ndio msingi wa uwazi kwa kutumia teknolojia za kisasa kwenye uchaguzi - Tume ya Uchaguzi ya Taifa ibakie tu kwenye shughuli ya kuratibu mambo na wala SI KUHODHI TAARIFA AMBAZO KIMSINGI NI MALI YA WAPIGA KURA NA mali ya vyama shiriki.

Huo umangimeza wa Jaji Makame mpaka kujichagulia achakachue au la ni lazima tukaudhibiti kwa njia hii.

Yeyote anayeingiza taarifa zozote katika mfumo kama huo ni sharti

i. atambulike kisheria na kuweza kuwajibishwa kunapohitajika,

ii. alazimike kuingiza taarifa husika hadi mara tatu ili kusitokee madai ya kukosea kibahati mbaya,

iii. Kila mtu awe na uwezo wa kuona taarifa zote zinazohusiana na uchaguzi ila ngazi zitofautiane kwenye nani anaweza kubadilisha taarifa fulani kwenye system na mpaka akafanye hivyo ni sharti passwords wa wawakilishi wa vyama shiriki viwe vimesainishwa kila mtu kwa nafasi yake.

Computer expert wetu wanaweza kutengeneza kabisa programme kama hii ninayozungumza kama wazo haya.

iv. kwa njia hii Observers nao wanakua na nafasi zao humu.

NB: Siku zote CCM hutumia ujima wetu wa kimawasiliano kufanya madudu, let;s turn around the ballgame kwa faida ya wananchi walio wengi na wala si kwa ajili ya genge fulani tu.

Tundu Lissu tunahitaji mswada kuboresha sheria na taratibu za uchaguzi. Pia sheria itamke wazi kura kutunzwa na wapiga kura wenyewe mbele ya hadhara bila kufukuzwa mtu kituoni, muda gani matokea yatangazwe tangu mtu wa mwisho kutumbukiza kura yake, mambo gani yazingatiwe kikamilifu kwanza ndipo matokeo yatangazwe, nafasi na ushiriki wa vyombo vya habari katika kila hatua ya uchaguzi kuhakikisha HAKI NA UWAZI wakati wote.
 
MCH.TEMBA AMBAYE YUPO IKULU ZAMBIA AMEOTESHWA NA MIUNGU YAKE KUWA CCM IMESHINDA LAKINI MSHINDI WAKE YUPO KWENYE MACHELA.sou
 
MCH. ALPHONCE TEMBA ALIOTESHWA NA MIUNGU YAKE JUU YA USHINDI WA SATA NA SASA AMEITWA NA SATA ZAMBIA :source Gzt Nyakati leo
 
Back
Top Bottom