Elections 2010 HUJUMA dhidi ya SLAA katika mdahalo wa JK leo

Jamani nimetazama gazeti la leo la RAI, kwa kweli linatia kichefuchefu. Hivi hawa waandishi wa Rai wanaupeo unaofaa au kutosha kupewa nafasi ya keweza kutoa habari kwenye gazeti linalosomwa na umma yote ya Tanzania. Kwa kweli hii ni aibu, uchambuzi wa habari zao upo kijuu juu tu na ni kama vile hata editor pia ni mpumbuvu kuruhusu gazeti lake kutoa habari kama hizi.
 
kuna vichwa vya kupewa masawali na vikapaform, lakini kama mtu ni kilaza, basi ni kilaza tu, hata iweje, JK hata akipewa Maswali atachemsha tu, tatizo sio kumwongelea mtu bali kuongelea matatizo ya watu na jinsi ya kuyatatua
 
Haitutishi mzee wangu! Ninajiuliza swali moja hususan kutokana na ahadi za JK!

Hivi tunahitaji Materials au Tanzankia unahitraji mabadiliko ya usimamizi wa sheria na utekelezaji makini wa sera bila kuwaonea baadhi ya watu? JK amekua akiahidi vitu na sio mabadiliko wala maendeleo endelevu katika majukwaa na sitegemei atakua na kitu kipya!

Slaa ni mtambo na JK haoni ndani ata aje saa ngapi. Leo nimemsikiliza Clouds hana chochote nikaanza kujiuliza upeo wa waandishi waliokwenda kumhoji!

Ushindi unakuja! Aday to go!
 
Aliyeongea last week thursday amepata coverage kubwa kuliko anayeongea leo, amepata at least week nzima kwa vyombo vya habari kudadavua alichokisema,na kuwapa fursa wale ambao hawakupata bahati ya kuangalia kupata yaliyojiri, wananchi wamepata fursa ya kuchangia alichokise na wenzao,

na vile vile wale ambao walikosa fursa ya kukiona kipindi walipata fursa ya kuona recorded version ambazo ziko nyingi sana mitaani na kupata kutoka kwenye vyombo vingine vya habari kwa week nzima, huyu wa leo ijuu, coverage yake ni ndogo kwa kuwa haitakaa in two days watu wanaenda nunua bidhaa.
 
Ha! hivi hawajui ndo wanammaliza mfadhili wao? Hakika kikwete hana mshauri.. Wtz hatudanganyiki tena bora angekaa kimya kuliko huu mdahalo feki anaoufanya leo... Kama atakwenda kinyume na wagombea wenzie amekwisha...
 
Na mjue kuwa sasa hivi jamaa anajitahidi kukusanya kura za vijana kama mmebahatika kusikiliza clouds leo katika LEO TENA amejaribu sana kuongea sera zakuwavuta vijana.

ANGALIZO:-
Leo ni mwisho wa mwezi tarehe 29th Oct, vijana tayari hela ya mshahala ishaingia na mbaya zaidi leo ni ijumaa, kuna kundi kubwa la vijana litakuwa out.
Kesho ni jumamosi magazeti hayataandika habari hii kwa ajili ya muda wa printing, yataandika habari ya jana ya lipumba, kwa hiyo print media out.
Readership ya magazeti weekend huwa chini sana, na wananchi wa kawaida husoma zaidi magazeti ya michezo.


Coverage ya hii kitu ni ndogo isiwape tabu hata kidogo.
 
Kwisha kazi yake huyo, kuna watu wanaingia na but darasani halafu wanshindwa kuitumia.
 
Ndugu zanguni,


SWALI: Ngurumo wa Vox Media ambao wanaandaa mdahalo huu kwa nini anaruhusu hujuma hii yote dhidi ya SLAA?
Kwani hujuwi kama Ngurumo wa vox media ni muajiriwa wa Mbowe katika gazeti lake la Tanzania Daima??? pia kwani ni lazima mdahalo uandaliwe na akina ngurumo pekee? hiyo forum ya leo haijaandaliwa na Chombo chochote cha habari kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa ila vyombo vyote vya habari vimekaribishwa kutuma waandishi.
 
Msipoteze muda kuangalia mdahalo nendeni kuhakiki majina yenu. Maamuzi tayari tunayo sasa muda wa propaganda umekwisha. Hata kama hujaona jina lako nenda siku ya kupiga kura ukahakikishiwe katika daftari la wapiga kura. Au tuma ujumbe kenda 15455 utapata majibu mara moja. Msikae kusikiliza mzee wa KUKARIRI. :nono:
 
Kwa kutafakali what is the imlication/effect ya Kikwete kuzungumza na waandishi wa habari kwa wapiga kura leo hii. Natumaini mpaka dakika hii zaidi ya wapiga kura 95% wanajua watampigia nani sijui kama hotuba yake itakuwa na effect kubadili misimamo ya wengi kwa siku mbili hizi
 
kifo cha mtu alokunywa chupa za kusaga ni tofauti kifo mtu kufia usingizini, CCM wanatapatapa walichokunywa kina
wasokota tumboni lakini ni lazima wafe tu
 
ndugu zanguni,


taarifa nilizopata leo ni kuwa 'mdahalo' utakaoneshwa na itv leo usiku kuhusu mgombea urais wa ccm jakaya kikwete, umeingiliwa na mafisadi kuhakikisha kuwa unakuwa ni mkutano wa kampeni badala ya mdahalo.

kwanza kabisa, jukumu la kualika waandishi wa habari na washiriki wengine halifanywi na waandaaji wa mdahalo huo (rose mwakitwange na vox media ya ansbert ngurumo) bali limepewa timu ya kampeni ya kikwete.

sielewi kwa nini waandaji wa mdahalo huu wameruhusu uhuni huu haswa ikizingatikwa kuwa ngurumo yupo kwenye campaign team by dk. Willibrod slaa wa chadema.

waandishi watakaoalikwa kwenye mdahalo huo ni wale tu waliokuwepo kwenye kampeni ya kikwete. Waandishi hawa ndiyo wale walikuwa wanalipwa posho ya shilingi laki 1 kila siku na ccm na kuvishwa nguo zimeandikwa "kikwete press."

taarifa nilizopata ni kuwa tayari campaign team ya kikwete, akiwemo abdulrahman kinana, january makamba, prince bagenda na muhingo rweyemamu, wameandaa maswali ya kumbeba jk ambao waandishi hawa wamepewa waulize kwenye mdahalo.

waandishi hawa wamepewa maswali ya kumpamba kikwete na kumponda slaa kwenye mdahalo huo na tayari kikwete ameandaliwa majibu ambayo atayasoma.

hivi sasa, mwandishi wa tanzania daima, anayeitwa irene mark, ndiye amebeba bahasha kubwa yenye mialiko ya waandishi wa kikwete watakao hudhuria mdahalo huu. Mwandishi huyu amepewa pesa azunguke newsroom zote na kugawa mialiko hiyo kwa "carefully selected journalists" ambao walikuwa kwenye kampeni za kikwete.

cha ajabu mwandishi huyu yuko kwenye gazeti linalomilikiwa na freeman mbowe, mwenyekiti wa taifa wa chadema.

waandishi hawa wa kikwete ambao tutawaona kwenye mdahalo leo usiku wamepanga kufanya party kubwa ambayo itafadhiliwa na ccm ili kujipongeza kwa mchango wao kwenye ushindi wanaotarajia wa kikwete.

pia, ccm wamefanya hila makusudi ili mdahalo uliotia fora sana wa slaa usirudiwe tena kwenye tv yeyote hapa nchini mpaka uchaguzi upite.

timu ya kinana imewarubuni waandaaji wa mdahalo huu ili kikwete awe mgombea wa mwisho kuzungumza kwenye tv leo ili ujumbe wake ubaki kwenye akili za watanzania siku ya kupiga kura jumapili.

swali: Ngurumo wa vox media ambao wanaandaa mdahalo huu kwa nini anaruhusu hujuma hii yote dhidi ya slaa?

naomba kuwasilisha...

haiwezekani kila kitu kikawa hujuma. Ni lazima apatikane mtu wa kuanza na mwingine kumaliza. Dr slaa anajiamini ndio maana hakujali cha kuanza wala kumaliza. Kuhusu watu wa kukaribishwa, hata siku ile movenpick niliona watu wenye mwelekeo wa kupenda mabadiliko wengi zaidi.

Hilo lisikupe taabu. Cha muhimu ni sera kuwafkia wananchi husika.
 
This is too much. Hamjiamini hata kidogo. Simama dede acha kulialia mnakatisha tamaa.

Ni kutafuta sababu za kushindwa kwenye uchaguzi wakati uchaguzi wenyewe bado.
 
Wakuu tusisahau sala kuiombea nchi amani maana kuna kila dalili za ccm kuiingiza nchi machafukoni
 
Back
Top Bottom