Mediabrains andaeni mdahalo utaojikita kwenye hoja za mkataba wa DPW tu!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Jana ulifanyika mjadala mzuri ulioandaliwa na mediabrains lakini uliokosa balance nzuri ya watu waliostahili kuwa sehemu ya panel ile lakini hasa kukosa muda wa kutosha kudadavua mkataba wenyewe.

Sasa tunashauri Mediabrains waandae mdahalo mwingine ambao utajikita kwenye kuuchambua mkataba wenyewe bila kupoteza muda na mada za udini, uzanzibar n.k

Tunaomba huo mjadala washiriki watu waliojipambanua vizuri kuusoma na kuuchambua huo mkataba ili hoja zao zijibiwe na serikali wakisaidiwa na akina Kitila na Rostam! ikiwezekana spika Tulia pia.

Wafuatao waitwe kuwasilisha mada za kupinga huu mkataba 1) Tundu Lissu 2) Dr Slaa 3) Prof Tibaijuka 4) Dr Lwaitama 5) Advocate Mwabukusi 6) Prof Lipumba

Tuwe na mjadala wa siku nzima kwa faida ya Taifa ili wote tuelewe. Tulitegemea mjadala utakaokata kiu zetu kupitia bunge lakini uliishia kuwa mjadala wa upande mmoja na mipasho na imechangia kuchochea hofu kwa wananchi.

Mediabrains representative brother Kibanda na Prof Kitila kwavile umejipambanua kupenda midahalo tunaomba mdahalo huu haraka tufunge mjadala na kutoa mapendekezo.

Mdahalo uwe live kwenye media kubwa zote.
 
Unakosea sana, jambo lisilo ka kweli na lenye dhamira isiyo ya haki haliwezi kuwa na mjadala wenye mantiki.
 
Hawawezi, serikali ya mkoloni wa Tanganyika haiwezi kukubali hilo, tumeona jana mfano mdogo kwa waliojaribu kuandamana kile walichofanywa.

Samia kafungua nchi kwa papara mpaka sasa ametuacha uchi.
 
Pascal Mayalla ongea na mdogo wako kibanda uandaliwe mdahalo mwingine. Jana hoja za mkataba zilipata nafasi ndogo.

Serikali igharamie huo mdahalo kama lengo ni kufafanua hoja za mkataba.
 
Mijadala ipo kwenye street battles, tuache unafiki, uoga na uzuzu, haki Haiti kwenye Golden plate, ni jasho la damu
 
Ukiandaliwa mdahalo mkubwa kujikita kujadili huu mkataba itakuwa ni big plus hata kwa Mama Samia ambaye amejipambanua kutaka uhuru wa maoni.
 
Back
Top Bottom