Huduma za afya nchini: Mkapa vs Kikwete.

Urgument za kitoto peleka kwenye NEC ya magamba, aliyekwambia lifespan inaongezeka kutokana na vibajaji nani?
Umefikiria suala la usahihi wa takwimu (reliability) hizo, vifo vingapi vinavyotokea vijijini haviripotiwi?? Mara ngapi takwimu zimechakachuliwa kufurahisha wakubwa??

Wakati unafanya inference ya lifespan inatokana na uongozi wa JK impact ya ongezeko la wasomi ambao wanajua umuhimu wa balanced diet na mazoezi uliiexclude vipi??

Tena hiyo ilikuwa ya mwaka 2010 ya mwaka 2011 ya UNDP ni 58.2 Years

Wewe mwenye argument za kikubwa lete data zako zinazokubalika duniani. Nnakuhakikishia huna, roho inauma.
 
Mkuu, tunajadili sekta ya afya. kama yapo aliyofanya Mkapa tujulishe. unakumbuka Mshahara wa daktari ulikuwa sh. ngapi wakati Mkapa anatoka madarakani?

Ujinga hautamuondoka binadamu maungoni kwa kuwa tu ameugundua, bali kwa yeye kuchukua hatua za kuukataa. Lakini ni heri kuutambua pia kwani ndio step ya kwanza ya kuukataa.

Mshahara wa daktari enzi hizi na mshahara wa daktari enzi zile sio jibu la ugumu wa maisha kwa daktari. Kama Mkapa alimlipa daktari sh 100,000 na mkate akamuuzia sh 120 hii si bora zaidi ya Kikwete anayemlipa daktari sh 250,000 na kumuuzia mkate sh 750? (Hili hutaliona mpk ujue hesabu)

Lengo la mada yako ni kuibua sura ya fulani anabugudhiwa kwa sababu ya dini yake na ndio maana mchekeleaji mkuu na mtoa like ni mdini namba moja, mzee wa uamsho zomba. Lkn labda mimi niwasaidie jambo ndugu zangu ambao mnaongozwa kwa hisia:

Ikiwa ni kweli Kikwete kafanya zaidi ya wooote waliomtangulia (km ulivyo mtazamo wenu), lkn wananchi wanaona kuwa upo uwezekano wa Kikwete huyo huyo kufanya zaidi ya hayo mengi yenu (kutokana na mtaji alionao), je ni dhambi wananchi kudai hilo kwa kuwa tu wa nyuma yake hakufanya kama yeye?

Ujinga wa namna hii unawafanya baadhi yenu kusema Kikwete ni zaidi ya Nyerere. Mnayasema haya kwa msingi wa fulani kajenga barabara Nyerere hakujenga. Nani kati yenu alijiuliza resources zetu zilikuwa exploited kiasi gani kipindi cha Nyerere na zinakuwa exploited kiasi gani wakati wa hawa tunaowasifia?

Niwakumbushe ndugu zangu mnaompinga Nyerere na kuleta udini kuwa, Nyerere aliyajua machungu yetu. Lakini hakuamini kuwa kula mbegu ndio suluhisho la njaa na ndio maana aliona ni vyema dhahabu zetu ziendelee kukaa ardhini mpk tutakapokuwa na maarifa ya kuzivuna na sio kuzigawa hovyo kama tunavyoona leo (3/100).

Tumieni akili zenu vyema. Mtu asipongozwe kwa kuwazidi wenzake bila kuangalia ametumia mtaji kiasi gani na hao wenzake wametumia kiasi gani. Tunataka kwenda mbele na sio kusifia 7 sehemu ambayo tulitaraji kupata 10 kwa kuwa tu mpata 7 kawavuka wenzake.
 
Last edited by a moderator:
Sote tunashuhudia jinsi madaktari wanavyomshambulia Rais Kikwete kwa shutuma za kutozipa kipaumbele huduma za afya nchini. Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa kipindi cha Mkapa hakukuwa na shutuma kali kiasi hiki. Nimejaribu kuchimbachimba ili kujua kwa nini shutuma hizi zimekuwa kali zaidi kipindi hiki nikagundua kuwa:

1. CT scanner ya kwanza Tanzania ilianza kutumia mwaka 2007 katika hospitali ya Muhimbili. Hii ni baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Sote tunajua kuwa madaktari mara nyingi hutumia mfano wa kipimo hichi kuwa ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyokosekana kwenye utoaji huduma bora za afya. Rais Mkapa hakununua CT scanner hivyo kuwaacha madaktari wasijue nini wanachokosa, na hivyo wakatulia tuliii. "Kimbelembele" cha Kikwete kutaka kuleta technologia ya kisasa nchini inamgharimu. Sasa madaktari washaijua CT scanner na wanataka zaidi na zaidi.

2. Magnetic Resonance Imaging machine ya kwanza Tanzania imeanza kutumika mwaka 2009 baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Mkapa alijua kuwa akileta hivi vitu, wataalam na wananchi watataka zaidi na matokeo yake "watamuona mbaya". Mkapa aliwafanya watanzania waamini kuwa vitu hivi kwa Tanzania haviwezekani kabisa, Kikwete amejaribu kuonyesha kuwa tunaweza kwa kiasi fulani - wananchi na wataalam baada ya kuona tunaweza kwa kiasi fulani sasa wanataka tuweze "to the fullest".

3. Kituo cha upasuaji wa moyo nchini kimeanzishwa baada ya rais Kikwete kuingia madarakani. Mkapa alijua kuwa ukishaleta mambo ya upasuaji wa moyo watanzania watataka zaidi, akayaacha. Sasa madaktari wanalalamika kwa nini kituo hicho hakina wataalam na vifaa vya kutosha.

4. Huduma ya kusafisha damu kwa figo la mashine, dialysis, imeanza kutolewa nchini baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Madaktari vijana wamepewa fursa za kwenda nchi mbalimbali kujifunza juu ya huduma hii. Baadhi yao wamesharudi nchini na wanatoa huduma hiyo. Miongoni mwa vijana hao ni viongozi wa mgomo wa kutaka huduma bora za afya na maslahi zaidi. Iwapo Kikwete angefanya kama Mkapa na kuacha huduma hii isipatikane nchini pengine madaktari wangeendelea kuamini kuwa hilo haliwezekani Tanzania na kuwa watulivu.

5. Baada ya kuona kuwa kuna vijiji havipati kabisa huduma ya usafiri wa wagonjwa, serikali ya Kikwete imebuni utaratibu wa kutumia Bajaj ili kila kijiji nchini kiwe na aina fulani ya huduma ya kwanza ya usafiri wa kuwafikisha wagonjwa sehemu ambayo watapata aidha usafiri bora zaidi au huduma bora ya afya. Jambo hili limefanya serikali ya Kikwete ishambuliwe sana, huku watu wakisahahu kuwa Mkapa aliona bora awaache wanakijiji hap bila huduma yoyote. Kwa vile Mkapa alikaa kimya kabisa kuhusu hili, hakulaumiwa. Kimbelembele cha Kikwete kutafuta utatuzi wa matatizo ya watu wa vijijini umemponza, sasa analaumiwa kwa kubuni njia ya kwasaidia watanzania.

6. Hivi sasa Kikwete anajiandalia tena "bomu" lingine kwa sababu serikali yake imeshaanza kutuma madaktari vijana wakajifunze Afrika Kusini na Ulaya jinsi ya kufanya operesheni kwa kutumia kamera (laparoscopic operations), vijana hawa wakirudi watafunguliwa vituo vya kufanya operesheni hizo ambapo mtu anaweza kufanyiwa operesheni ya tumbo na kurudi nyumbani siku hiyohiyo bila kovu! Ninapata hisia kuwa vijana hawa nao wataanzisha mgomo wa kutaka huduma iwe ya kiwango cha juu kama kule walikotoka kujifunza na kumtupia lawama muasisi wa utamaduni wa kuheshimu taaluma ya udaktari kwa kuwapa madaktari wa Tanzania exposure.

Nyongeza: Utamaduni huu wa Rais Kikwete kuleta maendeleo ya kweli umemgharimu pia katika sekta ya elimu ambapo alihamasisha kuwepo kwa shule za kata na kuwapa fursa watoto ambao wangekosa kabisa elimu kupata angalau fursa fulani ya kuelimika kwa kiwango fulani. Hivi sasa shule za kata ndio zimekuwa kigezo cha kulaani jitihada za serikali kwa kuwa wanafunzi "wanafeli". Kikwete angewaacha waishie darasa la saba kama ilivyokuwa kipindi cha Mkapa na marais wengine, wasingekuwa shule, hata kufeli wasingefeli na Kikwete asingelaumiwa kwa matokeo mabaya.

Hofu: Kwa mafunzo haya yanayotolewa na wananchi kwa Kikwete, Rais ajaye atatakiwa kuchagua mtindo wa Mkapa au Kikwete! Mpaka hapa tulipo inaonekana kuwa mtindo aliotumia Mkapa una manufaa zaidi kwake na chama chake kisiasa, lakini je vipi kuhusu maisha halisi ya watu wetu?

Nini kifanyike: wataalam, wanaharakati na wananchi ni wajibu wao kudai huduma bora na kuishinikiza serikali ifanye kila liwezekanalo kutoa kilicho bora zaidi kwa watu wake. Hata hivyo makundi haya yanawajibika kutambua, kuheshimu na kutamka hadharani jitihada za viongozi wanaojitoa kimasomaso kuzisaka huduma bora kwa watanzania ili kuwatia moyo waendelee kufanya hivyo. Tukilalamika zaidi kuliko kuonyesha moyo wa shukurani tutaishia kuambiana "LIWALO NA LIWE".
Huwezi kujustfy wema wako kwa kuhakikisha unawapatia kila hitaji familia yako wakati huo huo mkeo anakudanganya juu ya madai ya wanao wanaohitaji matumizi zaidi mfano ya kishule, wanao wataendelea kulalamika hata kama ukijafanya mwema kiasi gani, cha maana ni kuwasikiliza hoja zao, na kuwa nao karibu ili uelewe shida zao
 
Guys we all fight for this country, tatizo liko pale pale ni
mfumo ndio unaotuangusha na sio mtu, tatizo la nchi hatuna plan kama taifa na
ikajulikana hvyo ndio maana unaona kila mtu anasema yake,
ama anaamua kusema yake kutokana utashi kwa mtu huyo.

Haiwezekani Kikwete kukosa mazuri aliyoyafanya na pia kwa
Mkapa haiwezekani kukosa mazuri aliyofanya lakini ni kwa kiwango gani
na matakwa ya uwajibikaji wake kipindi hicho!

Yes Mkapa alisema tukaze mkanda lakini watu wachache walidhulum
mali za watu through ujambazi na waliachwa bila kuchukuliwa hatua
haya Kikwete kadhibiti ujambazi what about ufisadi?

Hata tukimuweka nani, kwa mfumo huu tutabaki kuchagua ya kusifia.

Kwa akili ya kawaida, dhumuni la thread ni kuonyesha kuwa hali ya
kiafya ni nzuri ukilinganisha na mtangulizi wake, yawezekana ikawa kweli kutokana
na data ulizotoa na sababu ulizotoa lakini nyuma ya hili pia ni
kma unahoji uhalali wa mgomo wa madaktari...

Inawezekana Watz wengi tusiweze kuhalalisha huu mgomo kwa
vigezo thabiti, la kwa kuhisi tu ama kwa kusikiliza watu fulani pia
hata kwa madaktari wenyewe, swali ni je kwa nn watu wengi
wapo nyuma ya madaktari japo wanajua kuna watu wanakufa?

Kama nilivyosema, tatizo ni hatuna mustakabali wa nchi mambo
yanaenda ili mradi, kwa kiongozi makini kama alikuwa ana mpango
na mambo yote hayo uliyosema, kwa nn hakuandaa mazingira
ya kuboresha huo mpango, Urais ni kazi kubwa na una mapana yake
sio kma gengeni unapeleka nyanya tu watu watanunua,
lazima kuwe na upembuzi yakinifu kwa kila jambo hasa kwa
maslahi ya Taifa.....

Leo ukimsifia Rais kuhusu bilioni alizotoa kila mkoa utakuwa umekosa
upeo, ndio maana nasema nchi inakosa mwelekeo hela zote zile
ni kama zimeliwa na wajanja bila kuwafikia walengwa na hii kutokana
na kukosa mipango endelevu.....

Watu wanasikia kwamba, EPA, Richmond, Change ya Rada,Nyongeza
ya posho kwa Wabunge halafu wanasikia eti wanashindwa kukidhi
mahitaji ya madaktari hapa ndipo kunapoleta tatizo.....

Hakuna mtu anayetumwa haya mambo yataendelea sana tu,
bado hali ni mbaya kote huku ni kwa sababu taifa limekosa
mipango makini kwa wananchi wake katika sekta zote.....
 
Back
Top Bottom