Uchaguzi 2020 Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Juni 08, 2020

Ebu fikiria mkuu. Lissu anatangaza kugombea akiwa nj ya nchi. Anawaponda askari Polisi, Jeshi, TISS na Rais aliyepo, halafu anasema haji nchini mpaka Serikali anayoiponda imhakikishie usalama! Hapo anatumia akili au matope!?
Inastajabisha sana, kwanza chama kumchagua kuwa makamu mwenyekiti akiwa nje ya nchi na kwa msimamo wa kutorudi mpaka ahakikishiwe usalama na serikali anayoitukana. Waendeleze kufanya harakati tu, wale wapiga virobo wa mwaka 2015 serikali ya JPM imeshawazibiti kwa sasa hata vijana wanafikiri kwa akili zao timamu hawashawishiki kwa viroba tena.
 
Ubarikiwe sana mkuu kwa post iliyo shiba busara
TL ametoa hotuba nzuri sana inaleta matumaini mapya katika nyanja zote kiuchumi na kijamii inaponya majeraha,inaonyesha matumaini ya uhuru wa wananchi ambao unazidi kupotezwa.
Inaleta matumaini ya mahusiano mazuri ya kimataifa na kuondokana na dhana ya "ubeberu"

Inaleta matumaini ya sekta binafsi kuongoza uchumi wa nchi badala ya serikali kufanya biashara jambo ambalo linaleta mgongano wa kimaslahi.
Imeleta matumaini mapya ya kuleta katiba mpya ya wananchi, ambayo itaondoa ukiritimba wa kiimla kutoka kwa watawala.
Inaleta matumaini ya maridhiano kataifa kuondoa uhasama unao zidi kukua kati ya wanavyama wa vyama tofauti Tz

Ni hotuba inayo ponya inayotibu inayotia matumaini.

Hongera TL kwa kuonyesha nia
 
Hapana chama chake kinaweza m-shape. Kwa mfano timu ya kampeni sharti imsaidie kuandaa hotuba zake. Inawezekana wakampa semina hiyo na akabadirika kwa maslahi ya emage ya chama. Unajua timu ya kampeni ikiwa organized inaweza kuleta impact mpaka kwa mgombea.
Huwa kuna kuandaa hotuba na mgombea anaweza pewa vimemo kuhusu maswala flani flani akiwa anahutubia.
Public speaking is an art sema Lissu yupo too emotional na ndio anapoharibu.
Lissu ni mr. I know everything! Sidhani kama wataelewana.
 
Utetezi wa JPM ni tathmini ya utekelezaji wa ahadi zake kwenye hotuba ya kufungua Bunge la kwanza alipoingia madarakani. Atahukumiwa kwa kile alichoahidi mithili ya mpandaji kuchuma alichopanda.

Hakutuahidi kuua uchumi, kuwazurumu wakulima korosho zao kuingiza nchi katika dimbwi la umaskini uliokithili.
 
Hill la kutangaza nia nje ya nchi lazima liwaume sana maana awamu ya tano kimataifa imekuwa sawa na uyawala was Nduli Amini na Mabuto.
Wakati ninyi mnaona ni ujiko, mimi naona AIBU sana! Ebu nikuulize, fomu za kugombea atachukulia huko? Wadhamini ataenda mikoa ya Ubeleji? Kampeni atafanyia huko? Ukiwa na akili timamu, lazima uone aibu kama mimi!!
 
Ndugu zangu,

Huenda maisha ya lockdown yamemwathiri Tundu Lissu,ukimsikiliza utagundua walemgwa wa "urais" wake sio Watanzania bali ni mabalozi na raia nchi za ulaya na Amerika waishio Tanzania.

Nilifikiri kukaa Ubelgiji angekutana na akina Mouse Katumbi au marafiki wa Tshisekedi ambao wangemfunza jinsi ya "kufanya siasa ughaibuni'.Leo wananchi wa Ikungi wameshasahau kama walishawahi kuwa na Mbunge anaueitwa Tundu Lissu sababu hazungumzi kero yao hata moja japo kwa unafiki.

Nimalize tu kwa kumtakia maisha mema huko ughaibuni ahakikishe wanae wanasoma nayeye alinde kibarua chake.
Mimi ni mtanzania
 
Wakati ninyi mnaona ni ujiko, mimi naona AIBU sana! Ebu nikuulize, fomu za kugombea atachukulia huko? Wadhamini ataenda mikoa ya Ubeleji? Kampeni atafanyia huko? Ukiwa na akili timamu, lazima uone aibu kama mimi!!
Tatizo lako lipo kwenye uelewa. Tulia tafakari upya majibu utayapata
 
Inastajabisha sana, kwanza chama kumchagua kuwa makamu mwenyekiti akiwa nje ya nchi na kwa msimamo wa kutorudi mpaka ahakikishiwe usalama na serikali anayoitukana. Waendeleze kufanya harakati tu, wale wapiga virobo wa mwaka 2015 serikali ya JPM imeshawazibiti kwa sasa hata vijana wanafikiri kwa akili zao timamu hawashawishiki kwa viroba tena.
Mbowe na Lissu sana dili la "kuwapiga" hao wanywa viroba. Kesho tu utamsikia Mbowe akiwataka wamchangie Lissu hela ya fomu. Kisha nauli. Baadae anatangaza Lissu ameahirisha kugombea kwasababu akija nchini atakamatwa. Washapiga hela zao hapo watabaki wanawacheki tu wanywa viroba!
 
Daah mhe.Lissu ni zawad kwa watanzania kutoka m/mungu... jamaa anajua kuongea na kupangilia namna ya kuwasilisha hoja...ndg watanzania wenzangu, October tumchagueni huyu mtu ..huyu Lissu ni mtu mwenye utu na anastahili kuwa rais wa nchi hii...2015 tufanye tulipotea lkn muda wa kurekebisha Mambo ni huu ...tusirudie makosa tena na tumuombe mungu atusamehe kwa yale maamuzi ya mwaka 2015 kwn tulidhani alivyo mahiri kujenga barabara tukadhani ndo hvyo hvyo ataijenga nchi kumbe la hasha...uchumi umedorola..uhuru wa vyombo vya hbr umedolora..uhuru wa kujieleza umekufa...ushirikiano wa kimataifa umekufa na hd watanzania tunaonekana kituko kimataifa...jamani jamani jamani, October mwaga pombe , mwaga udikteta, mwaga kila baya la utawala kisha tumchagueni mhe.Lissu kwa maendeleo ya vizazi vijavyo...nadhani madhara ya kumchagua mkemia tumeyaona sasa ni zamu ya kuchagu sheria na utawala bora...karibu sana mhe.lissu nyumbani nadhani hata wana ccm wana imani na ww tena kuliko hata wana chadema... people's
Zile Njemba zilizoondolewa ubongo kutoka Lumumba FC ukijumlisha MATAGA FC wakiuona huu mchango wako wanajihisi kila aina ya ghasia
 
Back
Top Bottom