Hotuba ya Rais ya Kikwete kwenye baraza la Idd-Mawazo yangu

Haya ndio matatizo yetu watanzania pamoja na viongozi wetu kila kitu mpaka upande mwingine ufanyareact.
Rais akiongea jambo litakalowapendeza Wakristu Mashekh wanatoa tamko na kipiga vijembe, Rais akiongea jambo litalowapendeza Waislam Maaskofu nao wanatoa tamko la kupiga vijembe.
Hii tabia naona inazidi kushika kasi na sijui nani kaileta
Rais amewai kutoa jambo gani lililo wafurahisha waislam na kupigwa vijembe na maaskofu??? Itapendeza great thinkers tukijadili jambo kwa facts na credible source. Taja tarehe,siku na mahali ilipotolewa hotuba hiyo iliyowafurahisha waislam na maskoofu wakaipiga vijembe bwana mdogo.
 
Naungana na mleta mada kuwa kuna media zinapotosha ukweli. Mimi nimeisikiliza hotuba ya Kikwete na nikaisoma yote humui JF. Sijaona ni wapi JMK alipokosea. Kaongea vizuri sana, na kwa mtazamo wangu JMK kawalaumu Waislaam kwa kuwa wamechelewa kupeleka maombi yao.
Safi sana, leo yamekukuta mbwa mwitu jike, unajibu hoja kwa upole ila moyoni mwako unayajua maumivu mwenyewe.Hongera kwa kuonyesha political tolerance juu ya hotuba hii ya uyu mkuu wako.
 
Waislamu, Wakristo kila mara.Mjadala gani huu.Mantiki yake nini? Ni udini unaowasukuma kujadili hoja za kidini hapa.Nyote ni aibu ya Taifa hili.Ndugu zetu Waislamu na ndugu zetu Wakristo, pamoja na ndugu zetu wa dini nyingine,na wapagani pia ni watu wa Taifa hili. Wamoja.Tuna interest zetu tofauti, haziwezi kuwa reconciled hata kidogo.Ila kila mmoja wetu aachiwe afanye mambo yake mwenyewe bila kuhusisha seikali.Kuihusisha serikali ni kujaribu kuipasuwa, na hata kuwagawa Watanzania.Jambo la muhimu ni kufuata sheria za nchi ktk kuendesha mambo yetu.Basi.Ubinafsi ndio unaosabaisha migogoro ya kidini.Why you Christians,and why you moslems? How about other religions?
Mlimtaka Rais aseme nini mbali na hayo aliyoyasema? Je mlitaka awe upande gani? Acheni upuuzi huu.Tanzania hii yetu haihitaji mijadala ya udini, bali wadini ndio wanaoihitaji ili kujihalalisha udhaifu wao. Unataka shule za udini jenga zako sio serikali ikujengee shule hizo za udini.Ukitaka mahakama za za udini jenga mwenyewe uone kama serikali itakuzuia.Ukitaka shule za wanawake wasioolewa watawa ama wanaume wasioowa jenga zako mwenyewe.Siyo serikali ikujengee.Kama pia unataka shule za maimamu pia jenga zako mwenyewe. Acheni kutugawa Watanzania.

OTE=Mkandara;2436600]Mkuu wangu, hizi ni kamba tu hakuna kitu ambacho Pinda wala JK wanaweza kufanya kwa sababu makanisa hawataki kabisa kusikia hili.. Na italeta matatizo makubwa nchini mbali kabisa na kwamba Mahakama ya kadhi haiwezi kuwa suluhisho la matatizo ya Waislaam nchini. Binafsi nishasema sana kwamba hii mahakama ya kadhi ni mtaji kwa Bakwata wanatafuta mahala pa kuvuta posho kama wabunge wetu na vikao vyao kupitisha hizo bajeti za wizara na kadhalika..

Katika mfumo wa mahakama ya kadhi, huwezi kuhukumu watu wanaofunga ndoa bila kujali dini zao, bila kujali haramu zilizowekwa na dini ili mradi wanataka kumkejeli Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo JK alitakiwa toka mwanzo kuwaambia waislaam hili swala haliwezekani kwa sababu 1,2,3. na kama mtakuja na majawabu kuhusiana na maswala haya na haya basi serikali itayatazama. Na ili mahakama ya kadhi ifanye kazi vizuri itabidi hata serikali ipigi marufuku kutambua ndoa ya Muislaam kuoa nje ya dini yake na pia Waislaam kuzaa nje ya ndoa zao ili kuiwezesha sheria toka ktk shina la matatizo yenyewe..This case is a no no! - Tanzania bado tunafuata jadi zetu ktk ndoa zaidi ya mafundisho ya dini na lazima tukubali ukweli huu maana mtu anatozwa mahari na mkaja juu ni lazima, kuna Kitchen Party, Reception..

Wakristu pia wanazitoa talaka kama hawana akili ili hali Biblia inakataza kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinifu, halafu wapo wengine hawatoi hizo talaka lakini hawaishi na wake zao kama kwamba dini imekataza kutoa kipande cha karatasi lakini unaruhusiwa kutoishi na mkeo - Hizo ni vows gani ktk dini?..Hivyo basi sii wakristu wala waislaam tunafuata ibada zetu ktk maswala ya ndoa na mirathi. lakini something has to be done kwa sababu wanawake wajane na watoto wetu wanaonewa sana na hawa Wajomba, mashangazi na hata wanafamilia wakubwa.

JK hakutakiwa kabisa kujihusisha na maswala ya mahakama ya kadhi kwa sababu sheria zake haziwezi kuwa applied Tanzania kwani hao waislaam wenyewe katika maswala ya unyago hawana Mungu, wameitupa Kuran pembeni...Na please tafadhali Makamba, Mwinyi na Lipumba kusoma shule za Wakristu enzi za mkoloni hujui adha walizopitia.. Na hata siku moja usifikirie ilikuwa fun kwa sababu nimesoma shule hizo na nililazimika kubalisha jina hadi Nyerere alipozitaifisha.. Mzee Moses Mnauye unafikiri hilo jina alipenda kujiita Moses?..Acheni kutoa hukumu ktk vitu ambavyo hamvitambui kwa sababu hizi shule sasa hivi ni shule za kidini na upo ubaguzi mkubwa sana tofauti na wakati wa mwalimu.

Hizi chuki za waislaam zimetoka wapi jamani?.. mbona wakati wa Nyerere tulikuwa tukila na kusherehekea Idd pamoja tukila kusherehekea Christimas pamoja nakumbuka vizuri zile misa za St. Peters wakati wa Pasaka na Christmas vijana wote tunakutana huko kisha tunaanguka mangomani, waya mkali wa Ujamaa na Kujitegemea![/QUOTE]
 
Mimi nashangaa sana waislamu wanapodai sheria wasizozipenda. kama kweli muslims wanataka kutumia sheria zao za kidini hasa kwenye masuala ya mirathi me nafikiri itakuwa ni rahisi hata sasa wakiamua kuitumia pasipokuwa na mahakama ya kadhi coz wana viongozi wa dini wanaozifahamu sheria hizo na kama kweli wanazipenda sheria hizo ni vyema wakazitekeleza pasipo na haja ya kulazimishana kwa kutumia mahakama.

Kuwapo na sheria hakuna maana kulazimishana. Kumbuka kuwa si wote wanaozijuwa hizo sheria na pande mbili zinapo hitilafiana lazima kuwe na msuluhishi ambae anakubalika kisheria na lazima awe na support ya dola husika.

Hata mkicheza mpira uwanjani kuna refa, kwani wanaocheza wote hawajui sheria za mpira? ya nini wawe na refa anaekubalika kisheria?

Mahakama zinakuwepo pale ambapo hakuna maelewano na kila mmoja anajiona yeye ndiye mwenye haki zaidi, hapo inatakiwa chombo "neutral" kinachokubalika na pande zote kuwasuluhisha. Kwa Waislaam chombo chao cha kusuluhishwa ni kadhi. Kadhi inabidi nchi ambazo hazifati sheria za kiislaam zikubali uwepo wake na kipi anachoweza kuamuwa. Kwa Tanzania, kama ulivyomsikia Kikwete, Kadhi ataruhusiwa kuamuwa kesi za mirathi, ndoa, wakfu na zinazohusiana na hizo. Zaidi ya hapo hakuna.

Mimi naona "something is better than nothing". Nyerere aliondoa kabisaa. Sijui kwanini? lakini my guess ni ukurusedi wake na hayo ndio kati ya mambo yanayotaka kumpatia utakatifu. Au kuna zaidi ya haya ya kuuwa Uislaam kwa makusudi kabisa yanayofikia kumpatia utakatifu? kwani kama ni nchi basi ilimshinda kuongoza na akang'atuka huku kaiacha nchi taabani hata senti za kigeni haina.

Mpaka sasa ni nchi nyingi sana zinakubali makadhi kisheria kabisa. Namsifu sana Kikwete kuwafunguwa macho Waislaam na sijui kwa nini hawaoni kuwa, Serikali kuridhia wao wenyewe waendeshe mahakama yao ya kadhi ni faraja kubwa kuliko ingekuwa chini ya Serikali. Mradi Serikali imetowa Ruksa inatosha kabisa.

Sidhani kama ni jambo baya kuwa "independent". Kwa mtazamo wangu ni jambo jema sana kuliko kung'ang'ania kuwa chini ya Serikali. Kuwa chini ya Serikali kwa mahakama ya kadhi kutapelekea iwe kama Bakwata, chombo cha serikali na si cha Waislaam wenyewe.
 
Kuwapo na sheria hakuna maana kulazimishina. Kumbuka kuwa si wote wanaozijuwa hizo sheria na pande mbili zinapohitilafiana lazima kuwe na msuluhishi ambae anakubalika kisheria na lazima awe na support ya dola husika.

Mahakama zinakuwepo pale ambapo hakuna maelewano na kila mmoja anajiona yeye ndiye mwenye haki zaidi, hapo inatakiwa chombo "neutral" kinachokubalika na pande zote kuwasuluhisha. Kwa Waislaam chombo chao cha kusuluhishwa ni kadhi. Kadhi inabidi nchi ambazo hazifati sheria za kiislaam zikubali uwepo wake na kipi anachoweza kuamuwa. Kwa Tanzania, kama ulivyomsikia Kikwete, Kadhi ataruhusiwa kuamuwa kesi za mirathi, ndoa, wakfu na zinazohusiana na hizo. Zaidi ya hpo hakuna.

Hapo kwenye red; kati ya matatizo ya kifikra tuliyo nayo watanzania ni kutokuwa na fikra huru. Leo hii unaanza kuona umuhimu wa kuwa "independent" simply kwa kuwa Mkuu kaongelea kwanye hotuba yake. I am sure, hoja hii ingekuwa imeletwa kabla ya hotuba ya Rais, ungebisha hadi kufa. Jamani, jambo haliwi halali kwa kuwa tu fulani (mf. Rais) kasema, bali kwa mantiki na kisheria. Tuache kuwa bendera fuata upepo.

Hapo kwenye
green; nashangaa suala la Mahakama ya Kadhi ambalo ni suala la IBADA (ukitaka liite la KIIMANI) kuhitaji "support" ya dola. Hivi kati ya dola na ALLAH, mkuu nani? Tuitafute "support" ya ALLAH, tuachane na dola.
 
Mkuu wangu, hizi ni kamba tu hakuna kitu ambacho Pinda wala JK wanaweza kufanya kwa sababu makanisa hawataki kabisa kusikia hili.. Na italeta matatizo makubwa nchini mbali kabisa na kwamba Mahakama ya kadhi haiwezi kuwa suluhisho la matatizo ya Waislaam nchini. Binafsi nishasema sana kwamba hii mahakama ya kadhi ni mtaji kwa Bakwata wanatafuta mahala pa kuvuta posho kama wabunge wetu na vikao vyao kupitisha hizo bajeti za wizara na kadhalika..

Katika mfumo wa mahakama ya kadhi, huwezi kuhukumu watu wanaofunga ndoa bila kujali dini zao, bila kujali haramu zilizowekwa na dini ili mradi wanataka kumkejeli Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo JK alitakiwa toka mwanzo kuwaambia waislaam hili swala haliwezekani kwa sababu 1,2,3. na kama mtakuja na majawabu kuhusiana na maswala haya na haya basi serikali itayatazama. Na ili mahakama ya kadhi ifanye kazi vizuri itabidi hata serikali ipigi marufuku kutambua ndoa ya Muislaam kuoa nje ya dini yake na pia Waislaam kuzaa nje ya ndoa zao ili kuiwezesha sheria toka ktk shina la matatizo yenyewe..This case is a no no! - Tanzania bado tunafuata jadi zetu ktk ndoa zaidi ya mafundisho ya dini na lazima tukubali ukweli huu maana mtu anatozwa mahari na mkaja juu ni lazima, kuna Kitchen Party, Reception..

Wakristu pia wanazitoa talaka kama hawana akili ili hali Biblia inakataza kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinifu, halafu wapo wengine hawatoi hizo talaka lakini hawaishi na wake zao kama kwamba dini imekataza kutoa kipande cha karatasi lakini unaruhusiwa kutoishi na mkeo - Hizo ni vows gani ktk dini?..Hivyo basi sii wakristu wala waislaam tunafuata ibada zetu ktk maswala ya ndoa na mirathi. lakini something has to be done kwa sababu wanawake wajane na watoto wetu wanaonewa sana na hawa Wajomba, mashangazi na hata wanafamilia wakubwa.

JK hakutakiwa kabisa kujihusisha na maswala ya mahakama ya kadhi kwa sababu sheria zake haziwezi kuwa applied Tanzania kwani hao waislaam wenyewe katika maswala ya unyago hawana Mungu, wameitupa Kuran pembeni...Na please tafadhali Makamba, Mwinyi na Lipumba kusoma shule za Wakristu enzi za mkoloni hujui adha walizopitia.. Na hata siku moja usifikirie ilikuwa fun kwa sababu nimesoma shule hizo na nililazimika kubalisha jina hadi Nyerere alipozitaifisha.. Mzee Moses Mnauye unafikiri hilo jina alipenda kujiita Moses?..Acheni kutoa hukumu ktk vitu ambavyo hamvitambui kwa sababu hizi shule sasa hivi ni shule za kidini na upo ubaguzi mkubwa sana tofauti na wakati wa mwalimu.

Hizi chuki za waislaam zimetoka wapi jamani?.. mbona wakati wa Nyerere tulikuwa tukila na kusherehekea Idd pamoja tukila kusherehekea Christimas pamoja nakumbuka vizuri zile misa za St. Peters wakati wa Pasaka na Christmas vijana wote tunakutana huko kisha tunaanguka mangomani, waya mkali wa Ujamaa na Kujitegemea!

Hapo kwenye red kwa JK na CCM
 
Mkandara,

Umeongea mambo mengi mazuri na kiasi fulani nimejifunza mengi. Tatizo langu ni moja tuu kuhusu mahakama hii ya Kadhi, je itajiendesha yenyewe au itategemea fungu toka serikalini? Na kama itategemea fungu toka serikalini, jee unadhani ni sawa kwa hela za walipa kodi wenye dini mbali mbali na wasio na dini kutumika kuendesha mahakama isiowahusu? Na jee kama tukiruhusu kufanya hivyo, dini nyingine nayo ikitaka fund kutoka serikali kuendesha shughuli zake tutawapinga?

Pili, mimi nadhani watu wengi hapa lengo lao sio kupinga uislamu kama ulivyosema bali wanatoa maoni yao. Kwa hiyo, tupingane bila ya kuitana majina.
 
Kuwapo na sheria hakuna maana kulazimishina. Kumbuka kuwa si wote wanaozijuwa hizo sheria na pande mbili zinapohitilafiana lazima kuwe na msuluhishi ambae anakubalika kisheria na lazima awe na support ya dola husika.

Hata mkicheza mpira uwanjani kuna refa, kwani wanaocheza wote hawajui sheria za mpira? ya nini wawe na refa anaekubalika kisheria?

Mahakama zinakuwepo pale ambapo hakuna maelewano na kila mmoja anajiona yeye ndiye mwenye haki zaidi, hapo inatakiwa chombo "neutral" kinachokubalika na pande zote kuwasuluhisha. Kwa Waislaam chombo chao cha kusuluhishwa ni kadhi. Kadhi inabidi nchi ambazo hazifati sheria za kiislaam zikubali uwepo wake na kipi anachoweza kuamuwa. Kwa Tanzania, kama ulivyomsikia Kikwete, Kadhi ataruhusiwa kuamuwa kesi za mirathi, ndoa, wakfu na zinazohusiana na hizo. Zaidi ya hpo hakuna.

Mimi naona "something is better than nothing". Nyerere aliondoa kabisaa. Sijui kwanini? lakini my guess ni ukurusedi wake na hayo ndio kati ya mambo yanayotaka kumpatia utakatifu. Au kuna zaidi ya haya ya kuuwa Uislaam kwa makusudi kabisa yanayofikia kumpatia utakatifu? kwani kama ni nchi basi ilimshinda kuongoza na akang'atuka huku kaiacha nchi taabani hata senti za kigeni haina.

Mpaka sasa ni nchi nyingi sana zinakubali makadhi kisheria kabisa. Namsifu sana Kikwete kuwafunguwa macho Waislaam na sijui kwa nini hawaoni kuwa, Serikali kuridhia wao wenyewe waendeshe mahakama yao ya kadhi ni faraja kubwa kuliko ingekuwa chini ya Serikali. Mradi Serikali imetowa Ruksa inatosha kabisa.

Sidhani kama ni jambo baya kuwa "independent". Kwa mtazamo wangu ni jambo jema sana kuliko kung'ang'ania kuwa chini ya Serikali. Kuwa chini ya Serikali kwa mahakama ya kadhi kutapelekea iwe kama Bakwata, chombo cha serikali na si cha Waislaam wenyewe.

Leo umeongea pointi ya maana sana hasa ile ya mwisho ya kuwa independent kwa chombo hicho kutokuwa na uegemezi wa serikali, point hii nilishaizungumza siku za nyuma kuwa unapotegemea serikali kwa jambo lolote lile basi ujue uhuru na hutu wako umeshautoa na kuukabidhi kwa serikali. ukishakubali kupokea pesa zao basi usishangae kesho wakija na kukuambia nini cha kufanya which is dangerous. ila ktk hili nina swali kama swala la kadhi ni la waisalamu wenyewe na linawahusu wao wenyewe sasa hivi sasa serikali chini ya Pinda inafanya nini kusimamia utaratibu wa kuratibu ofisi hii ambayo ni sehemu ya ibada ya kidini ?? kusema serikali inafanya hivyo ili kuakikisha kuwa inakidhi sheria za nchi hiyo si kweli tena ni kuwadharirisha waislamu kwani binafsi ninawafahamu wasomi na wanasheria wazuri wa kiislamu ambao wangeweza kuakikisha hayo hayatokei. binafsi mimi naona ni kosa kubwa sana kwa waislamu kuendelea kuiachia serikali kuendelea kutia mkono wao kwenye swala hili nina amini waislamu hawaitaji serikali kuwasimamia mambo yao wanao uwezo mkubwa sana wa kuweza kufanya mambo yao bila usimamizi wa Pinda.
 
Nadhani ndugu zetu waislamu wamepata walichokitafuta! Wakati wa kampeni walishiriki kwa nguvu zote kuipigia kampeni ccm kwa kuamini kwamba muislamu mwenzao akishinda agenda yao ya kulazimisha uislamu kujipenyeza kwenye system ya serikali itafanikiwa. Siwaonei huruma kwani juzi tu waliwatukana wanaharakati juu ya kuipinga ccm kwenye uchaguzi, hivyo wanapaswa kumeza hiyo shubiri ya Kikwete! Kudai serikali ya wote , yaani dini zote kuhudumia maslahi ya dini moja ni dhana isiyostahili hata kujadiliwa sio tu kusikilizwa. Ni sawasawa unaenda kuoa mke halafu unalazimisha gharama za kumtunza atoe jirani yako! Haiingii akilini kuona watu wazima wanalalamika serikali kuikataa hoja hiyo wakati wanajua si kazi ya serikali kuhudumia shughuli za uendeshaji dini. Kama suala ni imani kila mtu anayo yake na hakuna ajuaye ipi ni bora ila mwenyezi Mungu, hivyo hatupaswi kushurutisha watu wafuate imani zetu kwa hoja za nguvu bali kwa nguvu za hoja!
Kama kila mtu akifikiri kama mkristo, au muislamu au dini nyingine yoyote then hatutakuwa na Tanzania! Nadhani imefika wakati wa kufikiri kama watanzania na si kama wakristo au waislamu. Kuna matatizo mengi ya msingi tunayopaswa kuyashughulikia tukiwa kama watanzania zaidi ya kufikiri katika mipaka ya dinin zetu.
 
Naomba maelezo:
1. Shule zipi za kiislam zilizotaifishwa na je zikirejeshwa wataziendesha kwa ufanisi?

2. Tatizo ni uanzishaji wa
mahakama ya kadhi au nani wa kugharamia uendeshaji wake?

3. Hivi ni taasisi gani itakayokuwa na mamlaka ya uendeshaji kwani Bakwata imaonekana ni taasisi ya kiserikali zaidi?

4. Kwa kuwa Bakwata haitambuliki na baadhi ya madhebu ya kiislam na kwa kuwa waislam kama waislam wanataka wawe na taasisi inayounganisha maslahi ya waislam, nini kinawashinda kuanzisha umoja huo?

5. Kwa kuwa sasa ni miaka 50 tangu tupate uhuru ni matatizo gani ambayo yamekuwepo na kuleteleza waislam wengi wasisome ili tuweze kupata utatuzi?
6. Hivi matatizo yanayoleteleza performance mbovu ni yapi?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo yakijibiwa naweza nikachangia vizuri mada hii.
 
Hapo kwenye red; kati ya matatizo ya kifikra tuliyo nayo watanzania ni kutokuwa na fikra huru. Leo hii unaanza kuona umuhimu wa kuwa "independent" simply kwa kuwa Mkuu kaongelea kwanye hotuba yake. I am sure, hoja hii ingekuwa imeletwa kabla ya hotuba ya Rais, ungebisha hadi kufa. Jamani, jambo haliwi halali kwa kuwa tu fulani (mf. Rais) kasema, bali kwa mantiki na kisheria. Tuache kuwa bendera fuata upepo.

Hapo kwenye
green; nashangaa suala la Mahakama ya Kadhi ambalo ni suala la IBADA (ukitaka liite la KIIMANI) kuhitaji "support" ya dola. Hivi kati ya dola na ALLAH, mkuu nani? Tuitafute "support" ya ALLAH, tuachane na dola.

Kwenye green hukuelewa maana yangu. Na maanisha kuwa Mahakama ya Kadhi kama ipo au itakuwepo iwe imeruhusiwa rasmi kuwepo na dola husika na si maana yangu iwe "supported" ki mali.

Kwenye red pia naona una walakin wa kufaham. Kikwete ni kiongozi wa nchi na ni Muislaam ingawa Serikali anayoiongoza haina dini. Na ndio maana ukamuona ana swali na Waislaam na haendi kusali na mabaniani au Kanisani. Kama katoa wazo zuri sioni sababu ya kumpinga eti kwa sababu tu yeye ni Rais. Unanshangaza.

Hata wewe ukileta hoja nzuri na yenye manufaa, sioni sababu ya kukupinga, kwa sababu kila mmoja wetu yupo katika kujenga na si kubomoa. Na iwapo ntaiona hoja au wazo lako halifai pia sito sita kuachana nayo. Kama vile hoja ya miungu mitatu kwa mmoja ambavyo hainiingii akilini na ndio maana naipinga na siifati. Nakubaliana na yoyote ambae ana hoja ya Mungu mmoja, hajazaa wala hajazaliwa, hali bali hulisha.
 
Naomba maelezo:
1. Shule zipi za kiislam zilizotaifishwa na je zikirejeshwa wataziendesha kwa ufanisi?

2. Tatizo ni uanzishaji wa
mahakama ya kadhi au nani wa kugharamia uendeshaji wake?

3. Hivi ni taasisi gani itakayokuwa na mamlaka ya uendeshaji kwani Bakwata imaonekana ni taasisi ya kiserikali zaidi?

4. Kwa kuwa Bakwata haitambuliki na baadhi ya madhebu ya kiislam na kwa kuwa waislam kama waislam wanataka wawe na taasisi inayounganisha maslahi ya waislam, nini kinawashinda kuanzisha umoja huo?

5. Kwa kuwa sasa ni miaka 50 tangu tupate uhuru ni matatizo gani ambayo yamekuwepo na kuleteleza waislam wengi wasisome ili tuweze kupata utatuzi?
6. Hivi matatizo yanayoleteleza performance mbovu ni yapi?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo yakijibiwa naweza nikachangia vizuri mada hii.

Hiyo haikuanzia katika miaka 50 ya Uhuru, baada ya Uhuru ulikuwa ni muendelezo uleule wa kikoloni wa kuwanyima Waislaam haki ya kusoma. Hilo halina shaka kabisa kwani wakoloni walijenga shule za kikanisa kwa kuwa wakoloni wenyewe walikuwa wakristo. Na hili la elimu ndio lilipelekea wazee wa Kiislaam Tanganyika kuanza kudai uhuru ili wawe na fursa sawa za elimu. Wengi hawakupeleka shule watoto zao enzi za ukoloni kwa kuhofia kuwa shule zakikanisa ni lazima zitawatoa watoto wa Kiislaam kwenye dini yao ya Kiislaam, na naam hilo kweli limetokea, halina ubishi.

Historia ya elimu Tanganyika na Tanzania ni ndefu kiasi kwamba hapa itaharibu mjadala unaoendelea, hapa naona si mahala pake unaweza kufunguwa nyuzi nyingine tukaujadili huko.
 
Kuwapo na sheria hakuna maana kulazimishina. Kumbuka kuwa si wote wanaozijuwa hizo sheria na pande mbili zinapohitilafiana lazima kuwe na msuluhishi ambae anakubalika kisheria na lazima awe na support ya dola husika.

Hata mkicheza mpira uwanjani kuna refa, kwani wanaocheza wote hawajui sheria za mpira? ya nini wawe na refa anaekubalika kisheria?

Mahakama zinakuwepo pale ambapo hakuna maelewano na kila mmoja anajiona yeye ndiye mwenye haki zaidi, hapo inatakiwa chombo "neutral" kinachokubalika na pande zote kuwasuluhisha. Kwa Waislaam chombo chao cha kusuluhishwa ni kadhi. Kadhi inabidi nchi ambazo hazifati sheria za kiislaam zikubali uwepo wake na kipi anachoweza kuamuwa. Kwa Tanzania, kama ulivyomsikia Kikwete, Kadhi ataruhusiwa kuamuwa kesi za mirathi, ndoa, wakfu na zinazohusiana na hizo. Zaidi ya hpo hakuna.

Mimi naona "something is better than nothing". Nyerere aliondoa kabisaa. Sijui kwanini? lakini my guess ni ukurusedi wake na hayo ndio kati ya mambo yanayotaka kumpatia utakatifu. Au kuna zaidi ya haya ya kuuwa Uislaam kwa makusudi kabisa yanayofikia kumpatia utakatifu? kwani kama ni nchi basi ilimshinda kuongoza na akang'atuka huku kaiacha nchi taabani hata senti za kigeni haina.

Mpaka sasa ni nchi nyingi sana zinakubali makadhi kisheria kabisa. Namsifu sana Kikwete kuwafunguwa macho Waislaam na sijui kwa nini hawaoni kuwa, Serikali kuridhia wao wenyewe waendeshe mahakama yao ya kadhi ni faraja kubwa kuliko ingekuwa chini ya Serikali. Mradi Serikali imetowa Ruksa inatosha kabisa.

Sidhani kama ni jambo baya kuwa "independent". Kwa mtazamo wangu ni jambo jema sana kuliko kung'ang'ania kuwa chini ya Serikali. Kuwa chini ya Serikali kwa mahakama ya kadhi kutapelekea iwe kama Bakwata, chombo cha serikali na si cha Waislaam wenyewe.
Foxy, mkuu wangu mnakosea sana mnapotazama vitu kwa ujumla wake. JK ni rais wa nchi yetu kama marais waliotangulia na kuna makosa makubwa yamefanyika ambayo hayakutakiwa kutolewa majibu rahisi kama ya JK ktk hotuba yake. Pengine wewe umeyatazama haya kama vile JK ni mfadhili fulani ambaye anaweza kutoa majibu kihuni kama alivyopfanya JK..

Kwanza ni lazima utambue ya kuwa CCM wamekuwa wakicheza karata mbaya sana ya Udini toka Nyerere ameondoa madarakani. Na hili swala la mahakama ya kadhi limeondolewa wakati wa Nyerere lakini kwa shinikizo la waislaam wenyewe wakati huo mwanasheria mkuu nadhani akiwa Sheikh Amri Abeid Karuta..Na wala tusitake kujidanganya kuwa haya maswala ya ndoa, mirathi, wakfu na kesi nyingine za madai zinaweza kutolewa hukumu kirahisi na chombo ambacho hakitambuliwi na serikali ati kwa kufananisha na mpira wa kwenye vumbi..

Pengine wewe na utawala wa JK hamfahamu haswa sababu ya Waislaam kuomba mahaka aya kadhi kiasi kwamba ndio maana mnatoa majibu ya kipuuzi kama mpira wa vumbi usiohitaji refa. Foxy nikukumbushe tu kwamba madai yote ya ndoa, mirathi wakfu yanaweza kutolewa ufumbuzi hata msikitini tu na yakaisha bila hata ya kuwa na mahakama ya Kadhi, isipokuwa kilichotokea ni pale anapotokea mtu mkorofi ambaye hakubaliani na sheria za kidini isipokuwa zile za serikali at his/her advantage.

Huyu mtu huweka madai yake ktk mahakama za serikali ambazo pengine zinapingana ktk maamuzi na sheria za dini, mathlan masharti ya utoaji talaka, kugawana mali, mirathi na kadhalika sasa inapofikia hapo hukumu ya serikali ambayo yaweza kuwa pizani na ile ya Kidni ndio sababu haswa Waislaam wametaka mahakama ya kadhi kwa kuwa kesi nyingi za kiislaam zimehukumiwa kinyume cha mafundisho ya dini...Sasa inapotokea Waislaam wengi wanaitaka mahakama hii ujue pengine kuna sheria kweli ktkmahakama zetu ambazo zinawakinza Waislaam wake kwa waume na tunaweza vipi kuzitatua..

Sasa unaposema huu ni mpira wa vumbini mkuu wangu nashindwa kuwaelewa wewe na JK kama mnaelewa vizuri uzito wa swala hili kwa sababu huwezi kusema mahakama ya kadhi ni suala la waislaam ili hali mahakama za kawaida zinaweza kuingilia maamuzi ya mahakama ya kadhi na ndio kitu kilichosababisha waislaam kuomba mahakama ya kadhi inayotambulika ili kuondoa migogoro ya kimaamuzi baina ya sheria za dini na sheria za binadamu.

Sote tunaweza ku argue kwamba inatakiwa sheria moja kwa watu wote lakini come to think of that ni sheria gani itumike?. maanake sheria nyingi za madai ktk mahakama zetu zimejengwa ktk misingi ya Kikristo na tamaduni za nchi za magharibi ambao hakuna makosa wala dhambi kutembea nje ya ndoa wala hata kuzaa nje ya ndoa isipokuwa ni swala la wana ndoa wenyewe. Sasa ni vigumu sana kuweza kupata maamuzi yenye haki ikiwa wananchi wenyewe wametawaliwa na sheria nyingi tofauti na zinaweza kuchezewa at ones advantage.. Maskini wengi wamekosa haki zao kutokana na kukosa nguvu ama kuwa na imani ya dini lakini mahakama za serikali zikawanyima haki hizo kutoana na makosa ya tamaa zetu wenyewe.

Huko ndiko tulipotokea mkuu wangu hadi mahakama ya kadhi zikaombwa na Waislaam, sasa ni jukumu la JK na utawala wake kutafuta mbinu ambayo itaweza kutumika kuondoa dosari hizi dhidi ya wanandoa Waislaam waliofunga ndoa wakaweka vows zao ndani ya misingi ya kiislaam lakini siku ya siku ya talaka au mirathi mmoja wao anaenda korti za serikali ambazo zina mtazamo tofauti kabisa na mafundisho ya dini.

Kwa hiyo huwezi sema ni bora kuwa independent wakati hujui tumeshindwa kuwa independent kutokana na sheria za serikali kuwa pinzani na zile za kiislaam hivyo kutoa hukumu kinyume cha mafundisho ya Kiislaam laa sivyo haya maswala yangekuwa yakimalizwa nyumbani au hata miskitini tu...Hili ni tatizo dogo sana ukilitazama at face value lakini ni kero kubwa sanakwa waislaam na hasa Bakwata ambao hupokea malalamishi kila siku kutoka kwa Waumini wake, pia kwa upande wao wameshindwa kuelewa kwamba sisi Waislaam wenyewe ni wanafiki wa imani ya dini yetu wenyewe. Kwa matatizo mengi yanayotokana na kutopata suluhisho hutokana na uzinifu, talaka ambazo bwana kapata kitu kimpya, urithi wa mtoto wa nje ya ndoa na kadhalika ili mradi huwezi kutoa kuhumu ya haki pale Waislaam wenyewe wamepindisha mafundisho ya dini..

JK hakutakiwa kuwaahidi waislaam lolote mwaka 2005 or 2010, hili ndio kosa lake kubwa sana na hayomajibu yake ya kebehi hayawezi kuondoa makosa yaliyotangulia kwa rais kuwadanganya waislaam... HE LIED which makes him a LIAR! Alipowaahidi Waislaam mahakama ya kadhi hali akijua fika kwamba hatawapa wala haiwezekani kuwapa ndilo kosa lake kubwa acha kabisa habari ya kusema ukweli ambao aliuficha miaka yote iliyopita. na hakika anapowaambia waislaam kwamba swala la mahakama ya kadhi ni suala la Waislaam yaonyesha kwamba JK hajui kilichotokea huko nyuma kwa sababu hata siku moja haikuwa mahakama ya kadhi sii swala la waislaam.

Pili, mkuu wangu JK kama rais wa nchi huwezi kuwaambia Waislaam ati wamechelewa wapi kuja nao kuomba mkataba kama wa MoU.. Ule mkataba ni makosa makubwa yalifanywa na Mh. Mwinyi kwa sababu huwezi kuongoza nchi kwa kugawa makundi. Huwezi kufanya mkataba na dini moja ukitegemea wengine wakija utafanya nao pia mkataba hali kazi ya serikali ni kujenga policy ambayo vyombo, taasisi na jumuiya zote wanatakiwa kuwa obliged to na sii kimakundi. Sasa kama kesho waislaam wataenda kuweka mkataba, kesho kutwa watafuata Baniani, Ismailia, Budha - why not have One policy for all?..

Hapa JK na utawala wake wanacheza karata mbaya sana za kujenga udini na kesho wakristu watataka kuona Waislaam wamepewa nini ktk mkataba wao, wahindi vile vile na kuendeleza kujenga matabaka baina ya wananchi wake. Halafu kama ameshindwa kuwapa Mahakama ya kadhi alowaahidi na kuapa una uhakika gani atawapa mkataba wa MoU pengine atasema tena mkataba mnaoutaka ni suala la Waislaam!..The guy is a liar!

Believe me, JK ktk hotuba zake hakunifurahisha hata kwa moja.. The only hotuba nilomvulia kofia JK ni ile ya kwanza bungeni na kichekesho ni kwamba kashindwa kukamilisha hata MOJA la hotuba ile..
 
Hiyo haikuanzia katika miaka 50 ya Uhuru, baada ya Uhuru ulikuwa ni muendelezo uleule wa kikoloni wa kuwanyima Waislaam haki ya kusoma. Hilo halina shaka kabisa kwani wakoloni walijenga shule za kikanisa kwa kuwa wakoloni wenyewe walikuwa wakristo. Na hili la elimu ndio lilipelekea wazee wa Kiislaam Tanganyika kuanza kudai uhuru ili wawe na fursa sawa za elimu. Wengi hawakupeleka shule watoto zao enzi za ukoloni kwa kuhofia kuwa shule zakikanisa ni lazima zitawatoa watoto wa Kiislaam kwenye dini yao ya Kiislaam, na naam hilo kweli limetokea, halina ubishi.

Historia ya elimu Tanganyika na Tanzania ni ndefu kiasi kwamba hapa itaharibu mjadala unaoendelea, hapa naona si mahala pake unaweza kufunguwa nyuzi nyingine tukaujadili huko.

@FaizaFoxy, on the red: Nadhani unaposema wakoloni unaamanisha watawala toka Ujerumani na Uingereza maana hawa ndio walijenga shule na kati ya kundi hili la wakoloni walikuwepo WAMISIONARI (Missionaries). Hata hivyo kabla ya kutawaliwa na Wajerumani na Waingereza Tanganyika tuliwahi kuwa chini ya waarab and unlike those two groups waarab walijikita zaidi kwenye biashara ya utumwa! Sasa unapolalamika waislam kukosa fursa ya kupata elimu kwa nini hujati waarabu? Unaweza kueleza waarab waliwandelezaje waislam?

Fast foward - post independence; Wakristo wameendelea kujenga shule kwa wingi kushinda waislam (I wonder why?) hata hivyo watoto wa dini zote wanaruhusiwa kusoma kwenye shule zilizo chini ya umiliki wa wakristo. Sijui huku kunyimwa fursa ya elimu kuna maanisha nini hasa na pengine muda umefika kuweka mambo wazi kama alivyofanya Rais Kikwete. Hivi wanafunzi wa kiislam walikataliwa kusoma kwenye shule zilizokuwa chini ya wakristo? Au kulikuwa na sheria inayokataza wazazi wa kiislam kupeleka watoto shule? Mwl Nyerere alifanya nini specifically kilichowakwaza waislam kusoma lakini wakristo wakasoma? Na waislam waliosoma chini ya utawala wa Nyerere walifanyaje? walibadili dini? (kama sikosei Kikwete aliwahi kusoma shule ya mission). Na kama walihofia watoto kubadili (hofu sio evidence) kwa nini hawakuanzisha shule zao?

Na leo hii 2011 kwa nini waislam wana shule chache? Hawana hela za kujenga shule? (nauliza tena hawana hela za kujenga shule?) Wakristo wanapata wapi hela? Kama wanaomba, waislam waliomba wakakataliwa? lini na wapi? Na kama mtu huna uwezo kwa nini unaoa wake wanne? Unazaa ukitagemea nani awalishe wanao? (dont tell me wake wanne ni mambo ya dini I've heard about that convinient clause!).Tungefanya sensa leo hii unafikiri ni jamii ipi itakuwa na watoto wengi wako ndani hawaendi shule? Kwa nini?

Bila kukukwaza Faiza, kuna kasumba mbaya sana viongozi wa kiislam wamerathisha watoto/vijana. Kasumba ya kulalamika na kuendesha maisha kwa misaada. Kwa mfano Mahakama ya Kadhi sasa naelewa shida (walau kwa mtizamo wa baadhi ya watu toka BAKWATA) sio kuwa na mahakama tu, bali gharama za kuendesha mahakama zitoke kwa mtu mwingine i.e serikali! Hivyo hivyo tumeona ugomvi juu ya kujiunga na OIC kisa? misaada. Sasa ukijumlisha hapa unapata picha inayosema kuwa watu wazima wanafikiria sehemu za kuomba omba badala ya kubuni namna ya kuendesha maisha wenyewe!
 
Kuwapo na sheria hakuna maana kulazimishana. Kumbuka kuwa si wote wanaozijuwa hizo sheria na pande mbili zinapo hitilafiana lazima kuwe na msuluhishi ambae anakubalika kisheria na lazima awe na support ya dola husika.

Hata mkicheza mpira uwanjani kuna refa, kwani wanaocheza wote hawajui sheria za mpira? ya nini wawe na refa anaekubalika kisheria?

Mahakama zinakuwepo pale ambapo hakuna maelewano na kila mmoja anajiona yeye ndiye mwenye haki zaidi, hapo inatakiwa chombo "neutral" kinachokubalika na pande zote kuwasuluhisha. Kwa Waislaam chombo chao cha kusuluhishwa ni kadhi. Kadhi inabidi nchi ambazo hazifati sheria za kiislaam zikubali uwepo wake na kipi anachoweza kuamuwa. Kwa Tanzania, kama ulivyomsikia Kikwete, Kadhi ataruhusiwa kuamuwa kesi za mirathi, ndoa, wakfu na zinazohusiana na hizo. Zaidi ya hapo hakuna.

Mimi naona "something is better than nothing". Nyerere aliondoa kabisaa. Sijui kwanini? lakini my guess ni ukurusedi wake na hayo ndio kati ya mambo yanayotaka kumpatia utakatifu. Au kuna zaidi ya haya ya kuuwa Uislaam kwa makusudi kabisa yanayofikia kumpatia utakatifu? kwani kama ni nchi basi ilimshinda kuongoza na akang'atuka huku kaiacha nchi taabani hata senti za kigeni haina.

Mpaka sasa ni nchi nyingi sana zinakubali makadhi kisheria kabisa. Namsifu sana Kikwete kuwafunguwa macho Waislaam na sijui kwa nini hawaoni kuwa, Serikali kuridhia wao wenyewe waendeshe mahakama yao ya kadhi ni faraja kubwa kuliko ingekuwa chini ya Serikali. Mradi Serikali imetowa Ruksa inatosha kabisa.

Sidhani kama ni jambo baya kuwa "independent". Kwa mtazamo wangu ni jambo jema sana kuliko kung'ang'ania kuwa chini ya Serikali. Kuwa chini ya Serikali kwa mahakama ya kadhi kutapelekea iwe kama Bakwata, chombo cha serikali na si cha Waislaam wenyewe.
umezungumza vizuri ila hapo kwenye bold umeharibu ..!
 
Leo umeongea pointi ya maana sana hasa ile ya mwisho ya kuwa independent kwa chombo hicho kutokuwa na uegemezi wa serikali, point hii nilishaizungumza siku za nyuma kuwa unapotegemea serikali kwa jambo lolote lile basi ujue uhuru na hutu wako umeshautoa na kuukabidhi kwa serikali. ukishakubali kupokea pesa zao basi usishangae kesho wakija na kukuambia nini cha kufanya which is dangerous. ila ktk hili nina swali kama swala la kadhi ni la waisalamu wenyewe na linawahusu wao wenyewe sasa hivi sasa serikali chini ya Pinda inafanya nini kusimamia utaratibu wa kuratibu ofisi hii ambayo ni sehemu ya ibada ya kidini ?? kusema serikali inafanya hivyo ili kuakikisha kuwa inakidhi sheria za nchi hiyo si kweli tena ni kuwadharirisha waislamu kwani binafsi ninawafahamu wasomi na wanasheria wazuri wa kiislamu ambao wangeweza kuakikisha hayo hayatokei. binafsi mimi naona ni kosa kubwa sana kwa waislamu kuendelea kuiachia serikali kuendelea kutia mkono wao kwenye swala hili nina amini waislamu hawaitaji serikali kuwasimamia mambo yao wanao uwezo mkubwa sana wa kuweza kufanya mambo yao bila usimamizi wa Pinda.

Haya ni mambo yanayohusu sheria, na inabidi serikali iitambuwe hiyo mahakama na maamuzi yatayotolewa na hiyo mahakama na si serikali kutoa mchango wa fedha. Kama Serikali inaweza kutoa fedha za kusomesha wasio waislaam na kutoa fedha za kusikiliza kesi za wasio waislaam kutokana na kodi za waislaam pia na kama wanaona hilo kwa waislaam si haki yao. Sioni sababu ya kuendelea kuwalazimisha, ni kuanza wenyewe na mradi waitambuwe kisheria kuwa hii mahakama ipo. Hayo mengine yatafatia baadae, hakuna sheria za kibinaadam ndio zikawa za mwisho na zisitenguke. Ni rahisi zaidi kudai hatua ya pili ukishaianza ya kwanza. kuliko kudai hatua ya pili hata ya kwanza hujaipata.

Msimamo wangu ni kuwa Serikali imekubali na sasa Waislaam wakae chini kupanga utaratibu baina yao na Serikali na mengine yatafatia.

Maaskofu hawataki kabisa Serikali ijiingize katika hili lakini mantiki yao imeeleweka, na sisi Waislaam inatakiwa tutumie "Hap Ki Do". Tusiendelee kubishana nao, tuanze, mambo mengine yatajipa taratibu tukiwa tayari tumeanza tena.
 
@FaizaFoxy, on the red: Nadhani unaposema wakoloni unaamanisha watawala toka Ujerumani na Uingereza maana hawa ndio walijenga shule na kati ya kundi hili la wakoloni walikuwepo WAMISIONARI (Missionaries). Hata hivyo kabla ya kutawaliwa na Wajerumani na Waingereza Tanganyika tuliwahi kuwa chini ya waarab and unlike those two groups waarab walijikita zaidi kwenye biashara ya utumwa! Sasa unapolalamika waislam kukosa fursa ya kupata elimu kwa nini hujati waarabu? Unaweza kueleza waarab waliwandelezaje waislam?

Fast foward - post independence; Wakristo wameendelea kujenga shule kwa wingi kushinda waislam (I wonder why?) hata hivyo watoto wa dini zote wanaruhusiwa kusoma kwenye shule zilizo chini ya umiliki wa wakristo. Sijui huku kunyimwa fursa ya elimu kuna maanisha nini hasa na pengine muda umefika kuweka mambo wazi kama alivyofanya Rais Kikwete. Hivi wanafunzi wa kiislam walikataliwa kusoma kwenye shule zilizokuwa chini ya wakristo? Au kulikuwa na sheria inayokataza wazazi wa kiislam kupeleka watoto shule? Mwl Nyerere alifanya nini specifically kilichowakwaza waislam kusoma lakini wakristo wakasoma? Na waislam waliosoma chini ya utawala wa Nyerere walifanyaje? walibadili dini? (kama sikosei Kikwete aliwahi kusoma shule ya mission). Na kama walihofia watoto kubadili (hofu sio evidence) kwa nini hawakuanzisha shule zao?

Na leo hii 2011 kwa nini waislam wana shule chache? Hawana hela za kujenga shule? (nauliza tena hawana hela za kujenga shule?) Wakristo wanapata wapi hela? Kama wanaomba, waislam waliomba wakakataliwa? lini na wapi? Na kama mtu huna uwezo kwa nini unaoa wake wanne? Unazaa ukitagemea nani awalishe wanao? (dont tell me wake wanne ni mambo ya dini I've heard about that convinient clause!).Tungefanya sensa leo hii unafikiri ni jamii ipi itakuwa na watoto wengi wako ndani hawaendi shule? Kwa nini?

Bila kukukwaza Faiza, kuna kasumba mbaya sana viongozi wa kiislam wamerathisha watoto/vijana. Kasumba ya kulalamika na kuendesha maisha kwa misaada. Kwa mfano Mahakama ya Kadhi sasa naelewa shida (walau kwa mtizamo wa baadhi ya watu toka BAKWATA) sio kuwa na mahakama tu, bali gharama za kuendesha mahakama zitoke kwa mtu mwingine i.e serikali! Hivyo hivyo tumeona ugomvi juu ya kujiunga na OIC kisa? misaada. Sasa ukijumlisha hapa unapata picha inayosema kuwa watu wazima wanafikiria sehemu za kuomba omba badala ya kubuni namna ya kuendesha maisha wenyewe!

Hakuna ambae hajafanya biashara ya utumwa, na usitake kusema ni waarabu tu walijikita katika biashara ya utumwa. hao weusi walioko kontinenti jipya, walipelekwa na Waarabu?

Biashara ya Utumwa ilifanywa na Waafrika na Waarabu na Wazungu hakuna ambae hajaifanya na usijidanganye kuwa biashara ya utumwa imekwisha, ina sura mpya tu na ushahidi ni huu hapa:

What is modern slavery?

Millions of men, women and children around the world are forced to lead lives as slaves. Although this exploitation is often not called slavery, the conditions are the same. People are sold like objects, forced to work for little or no pay and are at the mercy of their 'employers'.

Source: Anti-Slavery - What is modern slavery

Kwa kukujuza tu, kanisa lilihusika direct na utumwa wa zamani na mpaka papa akaomba msamaha kwa kanisa kujihusisha na utumwa. Na ushahidi upo wa kanisa kuomba msamaha kwa hilo. Hayo mafundisho yako ya kuwa ni waarabu pekee waliojikita kwenye biashara ya utumwa hayana mshiko kwangu, na uwadanganye wengine.

Kuhusu mashule, ikiwa historia inafutwa makusudi unategemea utakuta nini kilichobakishwa cha waarabu baada ya kuingia wazungu kwa miaka kadhaa?

Historia ya wazungu na ukoloni hapa kwetu haikuanzia kwa wajerumani na waingereza pekee, naona umewasahau wareno. Jee, hujui kwamba wareno kilichowaleta huku ni krusedi? na wajerumani huelewi ni kina nani wali resist (vita vya majimaji) kuingia mjerumani? hali kadhalika kwa waingereza?

Wazungu walipoingia hapa walikuta kuna nyumba za ghorofa Kilwa, walikuta kuna nyumba zinapakwa rangi wakati wao walikuwa hawajui rangi ni nini, walikuta watu wa kilwa wanasarafu zao za dhahabu wakati kwao ilikuwa hakuna, walikuta watu wa Kilwa wanafanya biashara na India na Uchina, wakati wao hata njia ya kufika huko walikuwa hawaijui. Kama kulikuwa hakuna elimu hayo yote yalipatikana aje?

Unaonesha wewe historia yako umejifunza upande mmoja tu na zinatokana na haohao wazungu, ambao mpaka sasa wakichora picha ya Yessu wanamchora mzungu na wakichora picha ya shetani wanamchora mweusi. Huo ndio ujinga waliokujaza. Funguka na utazame ukweli.

Miaka nenda miaka rudi ya wazungu hapa kwetu ni nini walichokifanya zaidi ya kututia ujinga na kujitajirisha makwao? unafikiri utajiri wa Uingereza na Ujerumani umetokea wapi? Hao waarabu unaowasema wewe, hawana zaidi ya kuhamishia hata makao yao makuu kuwa hapahapa (Zanzibar), kama ni mali waliibakisha hapahapa.

Tanganyika inapata Uhuru baada ya Wareno, Wajerumani na Waingereza kukaa hapa zaidi ya miaka na vikaka walikuwacha na madaktari wangapi wa kiafrika? majaji wangapi? ma engineer wangapi? wasomi wangapi? mashuduuu. Kinyume na hayo, 90% ya madakatari, ma engineer, majaji, waalimu waliowaacha Waarabu Zanzibar walikuwa ni Wazanzibari, hiyo tu itakuonesha ni vipi tofauti ya hawa watawala wakiarabu na kizungu.
 
Kwenye green hukuelewa maana yangu. Na maanisha kuwa Mahakama ya Kadi kama ipo au itakuwepo iwe imeruhusiwa rasmi kuwepo na dola husika na si maana yangu iwe "supported" ki mali.

Kwenye red pia naona una walakin wa kufaham. Kikwete ni kiongozi wa nchi na ni Muislaam ingawa Serikali anayoiongoza haina dini. Na ndio maana ukamuona ana swali na Waislaam na haendi kusali na mabaniani au Kanisani. Kama katoa wazo zuri sioni sababu ya kumpinga eti kwa sababu tu yeye ni Rais. Unanshangaza.

Hata wewe ukileta hoja nzuri na yenye manufaa, sioni sababu ya kukupinga, kwa sabau kila mmoja wetu yupo katika kujenga na si kubomoa. Na iwapo ntaiona hoja au wazo lako halifai pia sito sita kuachana nayo. Kama vile hoja ya miungu mitatu kwa mmoja ambavyo hainiingii akilini na ndio maana naipinga na siifati. Nakubaliana na yoyote ambae ana hoja ya Mungu mmoja, hajazaa wala hajazaliwa, hali bali hulisha.

Hapo kwenye red; ndio maana hata serikali imewashtukia kwa udini, ubinafsi, na agenda zenu zisizoeleweka. Sikutegemea kejeli kwa wengine; sawa wanaabudu miungu hata mia, ni imani yao waache. Msidhani imani yenu ni superior kushinda zingine. Hamjapata mnaleta matusi, mkipata si ndio mtakata watu vichwa hadharani?
 
una nuksi ya kuzaliwa.. kama washindwa tofatisha jema na baya.. pole sana
 
Back
Top Bottom