Zimmermann
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 2,790
- 1,232
Aiseee............! Kweli FaizaFoxy a.k.a mbwa mwitu jike ni zaidi ya umjuavyo!Hakuna amabe hajafanya biashara ya utumwa, na usitake kusema ni waarabu tu walijikita katika biashara ya utumwa. hao weuzi walioko kontinenti jipya, walipelekwa na Waarabu?
Biashara ya Utumwa ilifanywa na Waafrika na Waarabu na Wazungu hakuna ambae hajaifanya na usijidanganye kuwa biashara ya utumwa imekwisha, ina sura mpya tu. na ushahidi ni huu hapa:
What is modern slavery?
Millions of men, women and children around the world are forced to lead lives as slaves. Although this exploitation is often not called slavery, the conditions are the same. People are sold like objects, forced to work for little or no pay and are at the mercy of their 'employers'.
Source: Anti-Slavery - What is modern slavery
Kwa kukujuza tu, kanisa lilihusika direct na utumwa wa zamani na mpaka papa akaomba msamaha kwa kanisa kujihusisha na utumwa. Na ushahidi upo wa kanisa kuomba msamaha kwa hilo. Hayo mafundisho yako ya kuwa ni waarabu pekee waliojikita kwenye biashara ya utumwa hayana mshiko kwangu, na uwadanganye wengine.
Kuhusu mashule, ikiwa historia inafutwa makusudi unategemea utakuta nini kilichobakishwa cha waarabu baada ya kuingia wazungu kwa miaka kadhaa?
Historia ya wazungu na ukoloni hapaka kwetu haikuanzia kwa wajerumani na waingereza pekee, naona umewasahau wareno. Jee, hujui kwamba wareno kilichowaeta huku ni krusedi? na wajerumani huelewi ni kina nani wali resist (vita vya majimaji) kuingia mjerumani? hali kadhalika kwa waingereza?
Wazungu walipoingia hapa walikuta kuna nyumba za ghorofa Kilwa, walikuta kuna nyumba zinapakwa rangi wakati wao walikuwa hawajui rangi ni nini, walikuta watu wa kilwa wanasarafu zao za dhahabu wakati kwao ilikuwa hakuna, walikuta watu wa Kilwa wanafanya biashra na India na Uchina, wakati wao hata njia ya kufika huko walikuwa hawaijui. Kama kulikuwa hakuna elimu hayo yote yalipatikanaaje.
Unaonesha wewe historia yako umejifunza upande mmoja tu na zinatokana na haohao wazungu, ambao mpaka sasa wakichora picha ya Yessu wanamchora mzungu na wakichora picha ya sheta wanamchora mweusi. Huo ndio ujinga waliokujaza. Funguka na utazame ukweli.
Miaka nenda miaka rudi ya wazungu hapa kwetu ni nini walichokifanya zaidi ya kututia ujinga na kujitajirisha makwao? unafikiri utajiri wa Uingereza na Ujerumani umetokea wapi? Hao waarabu unaowasema wewe, hawana zaidi ya kuhamishia hata makao yao makuu kuwa hapahapa (Zanzibar), kama ni mali waliibakisha hapahapa.
Tanganyika inapata Uhuru baada ya Wareno, Wajerumani na Waingereza kukaa hapa zaidi ya miaka na vikaka walikuwacha na madaktari wangapi wa kiafrika? majaji wangapi? ma engineer wangapi? wasomi wangapi? mashuduuu. Kinyume na hayo, 90% ya madakatari, ma engineer, majaji, waalimu waliowaacha Waarabu Zanzibar walikuwa ni Wazanzibari, hiyo tu itakuonesha ni vipi tofauti ya hawa watawala wakiarabu na kizungu.