Je, waliochangia miswada ya Tume ya Uchaguzi asilimia 90 naona kama wanapinga mswada. Changia mawazo yako

Aug 9, 2023
20
21
Kwanini wengi wa wachangiaji wamepinga mswada kama wawakilishi wa Taasisi za Kidini, wakristo na waislamu wote wanapinga.

Kwa ushahidi uliowazi wawakilishi wa taasisi za kijamii na zenyewe zinapinga.

Je, Uchaguzi utakaofanyika 2025 wananchi watakuwa na Imani na tume ya Uchaguzi kwa kuwa wamepata elimu ya kutosha kuwa tume sio huru hasa suala la wakurugeni kuonekana ni wateule wa rahisi.

Je, bunge hili linaweza kutunususu kipindi hiki baada kuona walichofanya kwenye DP World jadili tuone tunatoka vipi kipindi kigumu?
 
Kilicho dhahiri, kutokana na mjadala wa sheria hii, ni kwamba Tanzania ina watu wengi wenye akili. Wenye akili wapo huko kwenye taasisi za dini, sekta binafsi, vyama vya upinzani, kwenye NGOs. LAKINI wajinga na watu wa hovyo wapo Serikalini na ndani ya CCM. Lakini hawa wajinga na watu wa hovyo ndio wanaoongoza nchi. Yumkini hatuendi kokote.
 
CCM wanashindwa kutambua kwamba ZAMA zimebadilika,Watz wa leo sio wa mwaka 1947..Wanatakiwa waheshimu mawazo na maoni ya Watanzania

Katiba Mpya iliyo bora toka kwenye Rasimu ya Jaji Wariaoba haikwepeki
 
wanapinga kwa sababu yaliyomo mengi 80% ni copy and paste ya mambo ya zamani yanayolalamikiwa.
 
Huwezi kutegemea jambo lolote lile jema, na lenye maslahi kwa mustakabali wa nchi yetu likatatibiwa na kufanikishwa na makada wachovu wa fikra pevu wa CCM. Tatizo kubwa kwao ni "the fear of unkown as well as the aftermath when changes will occur"

Wapo "skeptical" kwa kuwa historia ina washitaki kutokana na udhalimu na ufedhuli mwingi walioufanya kwa miaka mingi. Huwa wamejipanga kuvuruga michakato yote yenye faida kwa umma wa Watanzania, na mfano mzuri ni kilichofanyika katika Bunge la Katiba.

Ni wanafiki ambao hujifanya wana nia njema, kumbe kila hatua huweka mikwamo ili mchakato mzima ukwame ili usiendelee pasipo kujali gharama kubwa zinazotumika. Kiburi chote walicho nacho ni mbeleko wanalobebwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Kwanini wengi wa wachangiaji wamepinga mswada kama wawakilishi wa Taasisi za Kidini, wakristo na waislamu wote wanapinga.

Kwa ushahidi uliowazi wawakilishi wa taasisi za kijamii na zenyewe zinapinga.

Je, Uchaguzi utakaofanyika 2025 wananchi watakuwa na Imani na tume ya Uchaguzi kwa kuwa wamepata elimu ya kutosha kuwa tume sio huru hasa suala la wakurugeni kuonekana ni wateule wa rahisi.

Je, bunge hili linaweza kutunususu kipindi hiki baada kuona walichofanya kwenye DP World jadili tuone tunatoka vipi kipindi kigumu?
Hawajui wanachokitaka
 
Binafsi niseme "SITOPIGA KURA 2025"

Wakati wanataka kubadili sheria ya ulinzi wa rasimali mwaka pale bungeni binafsi niliwasiliaha maoni yangu kwa njia Email nikipinga marekebisho ya sheria ili kumpa hauei DP World, ijapokuwa hawakubadili sheria ila bado wameanza kumpa mikataba DP WORLD.

Kwenye marekebisho ya sheria ya uchaguzi nilikuwa na nia ya kuwasilisha maoni yangu ila maana kupakua miswada ile miwili na kuipitia na kuwasikiliza wadau, niliona dhahiri hatuwezi kupata Tume huru ya Uchaguzi bila kubadilisha Katiba au kufanya marekebisho ya Katiba! Kiukweli hicho kitu CCM hawataki kukisikia na marekebisho ya Katiba au Kupata Katiba Mpya.

Mpaka kufikia sasa sikuwasilisha maoni yangu cos niliona najisumbua tu, na nikajiapiza sitopiga kura 2025.
 
CCM hawana nia njema,ile miswada ni kwa ajili ya publicity stunts tu ili kuonyesha kwamba serikali ya Samia inaunga mkono demokrasia. Viongozi wa CCM kwao maslahi ya chama kwanza kisha maslahi ya taifa,hawawezi kuleta maboresho yatakayo tishio uhai wa chama chao.
 
Bila kufanyika marekebisho ya maana ya Tume ya uchaguzi, tutakuwa tunajidanganya na uchaguzi mkuu wa 2025.

Lakini bahati mbaya wapo watakaoshiriki na kuuhalalisha.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Na hilo ndilo lengo la ccm ili tujikite kuukusoa mwisho wa siku tunastuka siku zimeisha na uchaguzi huo.
 
Back
Top Bottom