Hongereni uongozi wa SUA kwa kufuta kozi za fizikia

Hot bird

Member
Jan 18, 2021
56
100
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano.

Leo napenda kuupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) kwa kufuta udahili wa kozi za shahada ya elimu zenye somo la fizikia.

Wamefanya hivi baada ya kukosa wanataaluma wenye uwezo na weledi wa kufundisha kozi husika ijapokua walijitahidi kudanganya umma kuwa kozi hizo ziko sawa na kuwa uwezo wa kuziendesha wanao wakati wakijua hawawezi kuendesha degree programme hizo.

Nimewahi kuleta uzi kuhusu hilo unaweza kusoma hapa👇:


Pamoja na pongezi hizi,naomba kutaarifu umma huu wa watanzania kuwa bado kuna wanafunzi wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili hapa SUA wanaotakiwa kuendelea kusoma kozi za fizikia huku chuo kikiwa hakina hata lecturer mmoja wa kozi husika,sio hivyo tu bali hata assistant lecturer wa fizikia hakina.

Hali hii inashusha ubora wa elimu na hata hawa waliohitimu mwezi huu wa saba hawako competent kwenye fizikia,atayebisha hii aje apewe faili.

Binafsi naona chuo kinaendelea kuwaibia wanafunzi hawa,inafaa kitoe taarifa TCU kuwa hakiwezi kuendelea kutoa elimu ya kozi husika kwa wanafunzi hao ili waamishiwe vyuo vingine vyenye kujali ubora wa elimu.

How can a university conduct the degree programme without even a single PhD staff in the degree?

Isn't that a deliberate sabotage of the quality of education?

Wewe mkuu wa idara ya Kemia na Fizikia SUA wajibika,hicho kiti ni cha muda tu,hii degree yenu haina maana,wanafunzi hawapati elimu yoyote ya maana.

Wewe mkuu wa hiyo idara,unakumbuka siku ile umewakimbia kwenye kikao wanafunzi wa mwaka wa tatu waliokuwa wamekukomalia kwenye kikao kuwa wanataka mwalimu wa radiology,ukajifanya unapokea simu ukatoka hukurudi?,sasa utaendelea kuaibika hivi hadi lini?

Wewe principal wa mazimbu wajibika japo najua unajifanya uko busy sana kila siku vikao tu,huku ukijua kabisa hao wanafunzi hawapati elimu yoyote kuwajengea uwezo wa kitaaluma kama wewe.

Wewe DVC academic wajibika,japo wewe unajulikana wazi hujui academic ya chuo ilivyoharibika,hata hii kozi hujui ukanjanja unaofanyika hapa mazimbu.

VC fatilia, japo wewe unaangushwa na hao wa chini.

Sisi tuko hapa lindoni kwa sababu ya elimu mbovu kama hizi.
 
Ila SUA, hicho chuo kwa sasa kinahitaji wakaguzi wa nje, pana siasa nyingi, chuo kina matatizo mengi ila wanafunzi wenyewe waoga
Sio siasa tu,SUA wanadanganyana kuwa ni chuo chenye elimu bora,wakati mambo ni kinyume chake huku mtaani.

Kauli yao huwa ni moja tu, "SUA ni ngumu", ugumu ukiwauliza wanakusimulia mambo yasiyoeleweka ikiwemo kozi nyingi kwa semester na mabadiliko ya ghafla ya ratiba za chuo au almanac yanavyowaumiza.

Wanafunzi wa hapo hata ukiwa umemaliza wana jina lao la kijinga wanitana mitandaoni,hao wako tayari kusema uongo ili kui-overate SUA yao.
 
Kweli wamefuta?
Hakuna udahili mwaka huu?
Ndio wamefuta.

Ila tatizo bado wana wanafunzi wa kozi husika wanaingia mwaka wa tatu na wengine wa pili,hata hao waliohitimu mwaka huu hawana uwezo kama ilivyoainishwa kwenye degree zao.

Ingekua ni private inafanya hivi ingefungiwa,ila Sua waliweza kuudanganya umma kuwa wana uwezo wa kozi hizo,ila kwenye uhalisia hawana.

Kwenye staff waliopo kwa sasa hakuna hata mmoja anayeweza kufundisha fizikia hapa,hata kipindi waanzisha kozi hii waliidanganya TCU kuwa wana staff kumbe hawana.

Mkuu wa idara husika kwa sasa ni mtu wa kuchenga wanafunzi tu,kwa kuwa yeye alipewa kijiti wakati tayari idara imekufa kitaaluma na hasa kwenye upande wa physics,mwenzake aliyeharibu na kuleta haya yupo anapeta tu hapa mazimbu.

KUHUSU ELIMU SUA KWA SASA,WANAANGUKIA PIA.

ninashukuru kuwa ni mara kadhaa nilileta tahadhali juu ya udahili wa kozu hii kwa wanafunzi,wengine walikejeli ila imetimia,wanafunzi waliobaki wanajuta kuchagua kusoma kozi haina lecturer hata mmoja.
 
Back
Top Bottom