Hongera Lowassa, Hongera CCM kwa kukata ngebe

Haihitaji kusoma gazeti kujua kuwa lowasa ni mwizi wa kutupwa.
Cha maana hapa ccm imsimamishe uyo lowasa ili mpate akili kuwa watanzania sio wapumbavu kama mlivyokariri.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Prove kwamba EL ni Mwizi na usipoprove utakuwa mjinga.
 
Haihitaji kusoma gazeti kujua kuwa lowasa ni mwizi wa kutupwa.
Cha maana hapa ccm imsimamishe uyo lowasa ili mpate akili kuwa watanzania sio wapumbavu kama mlivyokariri.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

thanks Daud, hivi EL sialikuwa miongoni mwa wajivua gamba? waliamua kumtoa Rostam mbuzi wa kafara au...sisim waajabu sana
 
hivi kwa ccm hakuna mtu mwingine kijana msafi mwenye nguvu, mbunifu anayekubalika ambaye mnaweza kumuandaa kugombea urais 2015 zaidi ya mzee Lowassa? Lakini huenda yanatimia maana mkisukumwa na ulevi tu ulevi wa madaraka na rushwa mkamuweka Lowassa kuwa mgombea utabiri wa Anguko la ccm utatimia maana wananchi wanamjua lowassa fika kwa kashfa ya Richmond hatauzika hivo chadema njia itakuwa rahisi mno!!!

Hivi CDM hakuna mtu mwingine kijana msafi mwenye nguvu, mbunifu anayekubaliki ambaye mnaweza kumuandaa kugombea urais 2015 zaidi ya Slaa? Lakini huenda yakatimia maa maana mkisukumwa na ulevi tu ulevi wa madaraka mkamuweka Slaa kuwa mgombea utabiri wa CDM chama cha msimu utatimia maana wananchi wanamjua fika kwa kashfa ya kuishi kinyumba na mke wa mtu hivo CCM njia itakuwa rahisi mno.
 
Tutake radhi, huyo ni just mgombea wenu wa urais kupitia ccm.
Waambie na wengine watutake radhi EL si mgombea Urais wa CCM bali ni mgombea U-NEC wa Wilaya ya Monduli kelele na sifa zingeenda kwa wapiga kura wa M/mkuu wa CCM Wilaya ya Monduli
Kumleta hapa leo ni kuonyesha ulimbukeni wa kupendekeza jina la Mgombea Urais kupitia Vyama au ametumwa kupiga debe baada ya kuvuta mkwanja
 
alisha waeleza mwenye ushahidi wa jambo lolote lile atoke mbele,wapi hakuna mtu aliyejitokeza,mwacheni mzee wa monduli atumie nafasi yake kikatiba

acha ushabiki na inaonekana na wewe ni vijana anaowatumia kufanya rafu u ndani ya nchi hii jipange upya uje na maada wala si ushabiki
 
Naona umemchafulia hali ya hewa muumin wa TB joshua
muache amiin kile anachokiona yeye ni sahihi kwake kuamin...!!1
:biggrin:
:biggrin:
 
Nakuunga mkono mkuu. uko sahihi. Na hata zile kengele mbaya zilizokuwa zinalia juu yake zimetulia kimyaaa.

Hivi Lowasa kasafishwa lini na kashfa ya richmond na dowans? Mbona watanzania mnakuwa na akili za Panzi? ila namshukuru Mungu wa kudanganywa mmebaki wachache! Huu unafiki wa wnaCCM hauvumiliki tena.
 
Kama alivyosema W/Mkuu Mh Pinda kuwa "liwalo na liwe" kwa yanayozungumzwa kuhusu Lowasa ni mengi, mabaya na mema. Lakini mie nimpongeze Mh Lowasa kwa kuziba masikio na kusimamia kitu anachoamini bila kujali watu wengine wanasemaje, ameshakuwa waziri mkuu Tanzania na utendaji wake tuliuona. Kuwa na moyo mgumu wa uvumilivu ni kitu chema, ingawa inanipa hofu SANA pindi Lowasa huyu huyu akiendelea kuwa na moyo huu "mgumu" siku Tanzania ikimlilia kwa jambo baya linaloisibu nchi. Itoshe kusema kuwa kiongozi kuwa na moyo wa ujasiri kukabiliana na magumu yanayokusibu binafsi pamoja na watu unaowaongoza ni jambo jema sana, lakini siku ukiwageuka watu wako na kuwaonesha "ugumu" wa moyo wako bila shaka "patachimbika" kama alivyopata kujinasibu Mh Nimrodi Mkono (MB)
 
Tatizo ni kuwa wengi wetu tunamhukumu Lowassa bila ushahidi wowote. Ningekuwa tayari kutom-support Lowassa kama angekuja mtu na ushahidi wa ku-implicate katika kashfa yoyote. Kujiuzulu kwake U-PM ilikuwa ni kuwajibika kisiasa yaani- political responsibility'. Ali Hassani Mwinyi alifanya hivyo kati ya 1977 na 1978 kutokana na mauaji ya vikongwe waliohisiwa kuwa ni wachawi kule Shinyanga but in 1985 he was elected President. Let's speak with facts please. Can someone tell me how much did Lowassa receive from the Richmond deal?
 
Nimekuwa nikifuatilia sana siasa za ndani ya nchi yetu. Katika kipindi hiki hadi tarehe 12-11-2012 siku ambayo itakuwa ni mwisho wa uchaguzi wa ndani wa CCM(kama ratiba inavyoonesha), mengi yamesemwa juu ya hatma ya CCM na baadhi ya wagombea.

Kama kuna mgombea aliyesemwa sana katika mchakato huu, si mwingine bali ni mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Wapo waliokuwa wanasema, mabadiliko ya katiba ya CCM yalikuwa na lengo la kumwondoa/ kumzibia njia Lowassa. Waswahili wana msemo wao wa busara kabisa kuwa "wa mbili ni wa mbili, havai moja" na wengine husema "lililopangwa na Mungu, binadamu hawezi kulipangua" na pia "asiyekuwemo haingii, na aliyemo hatoki". Kusemwa kwa Lowasa ni muendelezo wa siasa za CCM kuelekea 2015. Binafsi hajaweka wazi kama atagombea urais 2015, na kila anapoulizwa husema "tutavuka daraja pindi tutakapoufikia mto"

Vikao vya uamuzi vya CCM vimemalizika. Jina la Lowassa limepitishwa kugombea nafasi ya U-NEC kupitia wilaya yake ya Monduli. Pamoja nae wapo Dr Salash Toure na kijana Nanai Konani. Mi si mtabiri wa kujua nani atafanikiwa kuwa M-NEC kutoka Monduli, ila ninachoweza kusema ni kuwa CCM wamekata ngebe za watu waliokuwa wanavumisha taarifa za uongo kuwa mwisho wa Lowasa katika siasa za CCM umefikia, kwa kuwa hataruhusiwa kugombea ujumbe wa NEC. Wapo wanaosema kuwa CCM imekata majina ya wagombea U-NEC wengi waliokuwa wanamtandao wa Lowasa. Inawezekana habari hii ikawa kweli, maana wanaojua ni CCM wenyewe. Ila tukumbuke kuwa: KAMA IPO, IPO TU

Nimalizie kusema kuwa "chochote tulicho nacho, hatujapata kwa ujanja wetu, bali ni makusudi ya Mungu". Kama Mungu amepanga Lowasa kuwa M-NEC atakuwa tu. Na kama amepanga Lowasa kuwa Rais, atakuwa tu. Hakuna wa kuzuia mipango ya Mungu.

Ngebe unazo ww unayetaka kutuaminisha kuwa EL ndo rais ajaye. Mwizi ni mwizi tu. Jamaa yako ni mchapa kazi sana tu lkn ana tamaa ya Mali. Angalia AICC, Wizara ya Ardhi jengo la kempisky na juzi vimemo vyake vya kuhusu Richmond, yote hayo huoni wala kusikia ina maana ww ni kipofu na kiziwi cjui tukusaidiaje. Tumia ubongo wako vizuri na soma kumbukumbu za mwl Nyerere kuhusu mtu huyu.
 
Ni yeye wa kuthibitisha kama utajiri wake huku akiwa mwajiriwa wa serikali ni wa halali. Aseme kuna biashara gani kwenye SIASA.
Wewe unayemshutumu unatakiwa kueleza. Je kaiba nini? wapi? jinsi gani? la sivyo utakuwa ni muongo na mchochezi.
Mfano: Unamtuhumu mtu kwa kuiba kitu yeye akasema sijaiba je anayetakiwa kuthitisha kuwa umeiba ni nani? kama sio anayekutuhum?
Tafakari
 
Ngebe unazo ww unayetaka kutuaminisha kuwa EL ndo rais ajaye. Mwizi ni mwizi tu. Jamaa yako ni mchapa kazi sana tu lkn ana tamaa ya Mali. Angalia AICC, Wizara ya Ardhi jengo la kempisky na juzi vimemo vyake vya kuhusu Richmond, yote hayo huoni wala kusikia ina maana ww ni kipofu na kiziwi cjui tukusaidiaje. Tumia ubongo wako vizuri na soma kumbukumbu za mwl Nyerere kuhusu mtu huyu.
Mimi nataka fact sitaki propagada. Toa maelezo yalinyooka. Kiongozi wenu Slaa mnasema makini basi alete utetezi kuwa EL anamiradi hii na hii ya kifisadi la sivyo mtakuwa watu waliopofushwa wasio na macho.
 
Wewe unayemshutumu unatakiwa kueleza. Je kaiba nini? wapi? jinsi gani? la sivyo utakuwa ni muongo na mchochezi.
Mfano: Unamtuhumu mtu kwa kuiba kitu yeye akasema sijaiba je anayetakiwa kuthitisha kuwa umeiba ni nani? kama sio anayekutuhum?
Tafakari
Ni nini kilimwondoa mapema sana kwenye kinyang'anyiro cha kugombea URAIS wa JMT mwaka 1995? Mwambieni Lowasa ajitokeze awaambie WATANZANIA mali alizonazo kazipata kihalali huku akiwa mtumishi tu wa UMMA miaka yote hii.
 
Ni nini kilimwondoa mapema sana kwenye kinyang'anyiro cha kugombea URAIS wa JMT mwaka 1995? Mwambieni Lowasa ajitokeze awaambie WATANZANIA mali alizonazo kazipata kihalali huku akiwa mtumishi tu wa UMMA miaka yote hii.
Tatizo lako ubongo wako mpaka tuufinye ndio uamke. Tatizo lako ninaweza nikafananisha na vitu viwili huenda umekariri au umefumbwa macho.
Tafakari.
Hivi mtumishi wa umma hawezi kuwa na shamba? hawezi kufuga? ukinijubu hapo basi utakuwa umemaliza yote.
 
Nakuunga mkono mkuu. uko sahihi. Na hata zile kengele mbaya zilizokuwa zinalia juu yake zimetulia kimyaaa.
Unaonaje mkuu huu ujumbe ukamfikishia Nape na Mkama, maana ndiyo waliozunguka nchi nzima wakifahamisha wananchi na wanachama kwamba magamba ni RA, EL na AC na kwamba hivi karibuni watang'olewa toka kwenye chama chao. Kama ni aibu, Nape na wenzake watakuwa wameivuna ya mwaka.
 
Back
Top Bottom