Hoja zipi zinakufanya kuchagua au kutochagua CCM, pia ni hoja ipi inakufanya uone kuwa upinzani ni mbadala wa CCM?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,549
2,989
Demokrasia imetutupatia machaguzi mengi ila tunahitaji kufanya au kuchukua uamuzi ambao ni busara zetu pekee zinaweza kuamua mustakabali wa jamii yetu kwa sasa na hata kwa baadae Siasa ni maamuzi ya kisera ambayo yanayojumuisha uchumi,jamii na utamaduni hivyo kwenye siasa ndio uwanja pekee unaotufanya wakazi au wananchi kubaki salama katika nchi yetu ili kuendelea na maisha mengine.

Ni miongo kadhaa kupita tangu uhuru wa nchi za kiafrika kutoka kwenye makucha ya wabepari ,ni miaka 47 imepita toka chama cha mapinduzi kimeitawala Taifa la TANZANIA,ndani ya miaka hiyo tumeshuhudia tawala 6 za uongozi chini ya chama kimoja yapo mengi yameanzishwa na kuendelezwa kwenye nchi hii ila kwa uchache MAGEUZI YA KILIMO,VIWANDA NA SEKTA YA USAFIRISHAJI ni sehemu kubwa ambayo chama cha CCM kimejaribu kutumia nguvu kubwa ya kiutendaji ili kuifungua nchi,upande wa HUDUMA ZA KIJAMII ikiwemo elimu na afya tumepiga hatua kubwa kwa kiasi fulani ingawaje bado changamoto bado ni kubwa mno.

MWISHO

Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu ila ili kuleta tija ya maendeleo ni muhimu kutoa fursa kwa kila mmoja kushiriki kwa namna ya tofauti.
 
Tatizo mbadala wa CCM hatajwi, unatajwa upinzani. Upinzani ni nani? Cheyo? Zitto, Mbowe, ?, Selasini, Shibuda? Dp? Mzee wa ubwabwa?
Tajeni tuone kama kweli ni mbadala vinginenyo CCM hana mbadala.
Kwann ccm ni mtu? Mbona unataka mbadala wa ccm awe mtu wakati ccm siyo mtu?

Sera za ccm zimepitwa na wakati ndiyo maana chama mbadala kinahitajika. The best replacement of ccm is chadema.
 
Niliwahi kusoma sehemu kuhusu siasa ya vyama vingi TANZANIA. Kuwa nchini watu hawakukubali mfumo wa vyama vingi. Inasemekana wananchi wa kipindi hicho wqlipiga kura kupinga mfumo wa vyama vingi lakini baadae walishauriwa wacha viwepo lakini viwe kama vipo tuu nyuma ya pazia kusudi tusije sumbuliwa na kuwekewa vikwazo na mabeberu. Ina maanisha kuwa mfumo wa utawala nchini kwetu ni wa chama kimoja.
 
Demokrasia imetutupatia machaguzi mengi ila tunahitaji kufanya au kuchukua uamuzi ambao ni busara zetu pekee zinaweza kuamua mustakabali wa jamii yetu kwa sasa na hata kwa baadae Siasa ni maamuzi ya kisera ambayo yanayojumuisha uchumi,jamii na utamaduni hivyo kwenye siasa ndio uwanja pekee unaotufanya wakazi au wananchi kubaki salama katika nchi yetu ili kuendelea na maisha mengine.

Ni miongo kadhaa kupita tangu uhuru wa nchi za kiafrika kutoka kwenye makucha ya wabepari ,ni miaka 47 imepita toka chama cha mapinduzi kimeitawala Taifa la TANZANIA,ndani ya miaka hiyo tumeshuhudia tawala 6 za uongozi chini ya chama kimoja yapo mengi yameanzishwa na kuendelezwa kwenye nchi hii ila kwa uchache MAGEUZI YA KILIMO,VIWANDA NA SEKTA YA USAFIRISHAJI ni sehemu kubwa ambayo chama cha CCM kimejaribu kutumia nguvu kubwa ya kiutendaji ili kuifungua nchi,upande wa HUDUMA ZA KIJAMII ikiwemo elimu na afya tumepiga hatua kubwa kwa kiasi fulani ingawaje bado changamoto bado ni kubwa mno.

MWISHO

Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu ila ili kuleta tija ya maendeleo ni muhimu kutoa fursa kwa kila mmoja kushiriki kwa namna ya tofauti.
Hakuna mbadala wa ccm Kwa Sasa wanatupigia kelele tuu
 
Tatizo mbadala wa CCM hatajwi, unatajwa upinzani. Upinzani ni nani? Cheyo? Zitto, Mbowe, ?, Selasini, Shibuda? Dp? Mzee wa ubwabwa?
Tajeni tuone kama kweli ni mbadala vinginenyo CCM hana mbadala.
Sio sahihi kulinganisha chama kizima na baadhi ya watu, unatakiwa ulinganishe CCM kama chama na CHADEMA, ACT, CUF n.k kama ni mtu linganisha mfano John Mnyika kama katibu mkuu wa CDM na Kinana kama katibu mkuu wa CCM n.k
 
CCM imechoka but pia vyama vya upizani havina mvuto wa sera mpya

Kiujumla siasa ya Tz imekosa mwelekeo,,

Haina mvuto kama miaka ya nyuma kipindi Cha kina mrema. Angalau watu walikuwa wanatabiri lolote lingetokea mbeleni.

Kwa hali ilivyo CCM inaweza kukaa zaid ya Karne madarakan hata mambo yawe hovyo kiasi gan coz hakuna upizani thabiti .
 
Niliwahi kusoma sehemu kuhusu siasa ya vyama vingi TANZANIA. Kuwa nchini watu hawakukubali mfumo wa vyama vingi. Inasemekana wananchi wa kipindi hicho wqlipiga kura kupinga mfumo wa vyama vingi lakini baadae walishauriwa wacha viwepo lakini viwe kama vipo tuu nyuma ya pazia kusudi tusije sumbuliwa na kuwekewa vikwazo na mabeberu. Ina maanisha kuwa mfumo wa utawala nchini kwetu ni wa chama kimoja.
ila katiba haijasema hivyo
 
Back
Top Bottom