Hivi Ulaya kuna utaratibu wa kuulizwa jina la balozi wa mtaa/mtendaji kata, diwani au mbunge ili kuthibitisha kama ni mkazi wa sehemu husika?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,059
10,510
Nikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi.

Wakaniweka mtu kati nakuanza kuniuliza maswali with confidence nikawaelezea kuwa naelekea nyumbani ila bahati mbaya nimekosea njia.

Wakaanza kuniuliza balozi wako anaitwa nani? Kimsingi sio kwa ubaya licha ya kuishi huu mtaa simjui balozi, mtendaji wala diwani. wakanituhumu kuwa mimi nitakuwa mtu mbaya na sio mkazi wa sehemu husika kisa simjui balozi.

Hivi kweli kwa ingia na kutoka ya jiji hili la Dar es salaam jumlisha wingi wa watu pamoja na harakati za kimaisha kuna umuhimu gani wa kuulizana majina ya viongozi wa ngazi za chini?
 
Nikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi...
Ni muhimu.

Ukipatwa na changamoto utaanzia wapi kutambulishwa? Jitahidi umjue balozi wako, Mwenyekiti serikali ya mtaa ama Mtendaji.
 
Pole sana; maswali ya kipumbavu sana kuulizwa dunia ya leo. Frankly speaking, sijawahi hata kujua majina ya hao watu mtaani ninakoishi!
Sure.. mimi ni Mtanzania mwenye kadi ya mpiga kura, Nida na cheti cha kuzaliwa popote pale kwenye nchi hii nina haki ya kuishi as long sivunji sheria... Kutojua jina la mtu sio sababu ya kuhisiwa ubaya.
 
Hapa mtaani kwetu Kimara B balozi lazima awe mtu aliyetuuzia viwanja. Kijumba chake Cha kizamani na mkewe lazima awe anauza samaki wa kukaanga na maandazi lkn pia huyu mama lazima awe mjuaji, mpenda Madera na sare.
Kama unakaa mtaa ambao balozi Ni mchaga, fanya mchakatouhame huo mtaa.
 
Kwa usalama ni lazima ujue hayo.
Bongo sio ulaya, kule mifumo yao ya ulizi ni thabiti kuna camera barabarani mpaka mitaani. Ungedakwa ulaya basi wangekucheki tu kwenye midatabase yao kukujua wewe ni nani.

Hapa kwetu balozi ndo ana database ya mtaa wake (kaikariri kichwani), hapo ponapona yako ni kumtaja mwenyenyumba wako( bahati mbaya vijana hawawajui majina wenye nyumba wao), au kama una kwako mtaje jirani yako ( hapa napo sababu ni zilezile za kipuuzi na kuiga umagharibi ati ngia toka ingia toka).

Nakukumbusha hii ni bongo, siku nyingine utapigwa kiberiti hivi hivi. Ama lah utaitiwa mwizi na balozi akaitwa akasema hakutambui, jirani nae humjui hakujui sijui utajitetea kwa ingia toka ingia toka za jiji.

Kibongobongo fahamiana na majirani wawili watatu just for backup sio mzoeane, fahamiana nao tu.
 
Mambo ya shortcut hayo hasa sehem mjini hayafai kabsa especially Kwa sehem ambazo siyo mwenyeji sana,,

Nakumbuka Kuna mshikaji alishawahi kuwekwa mtu kati hivohvo tena na police baada ya kukatiza sehem ambazo Huwa Kuna madada poa wanajiuza na yeye alikuwa ajui kuwa hizo Chocho Kuna hizo business,, so Ile anapita hizo Chocho akajikuta yupo chini ya ulizi wajomba wakajua ni mteja anatafuta huduma kumbe mshikaji hajui lolote.

So maeneo kama siyo mwenyeji shortcut au Chocho siyo nzur San unaweza katiza sehem kumbe kuna tukio lilitoke hivi soon may be la mauaji na we unakatiza hizo sehem na watu hawakuji unadhan what will happen.
 
Hapa mtaani kwetu Kimara B balozi lazima awe mtu aliyetuuzia viwanja. Kijumba chake Cha kizamani na mkewe lazima awe anauza samaki wa kukaanga na maandazi lkn pia huyu mama lazima awe mjuaji, mpenda Madera na sare.
Kama unakaa mtaa ambao balozi Ni mchaga, fanya mchakatouhame huo mtaa.
Balozi mchaga kwa nini nihame?
 
Kwa sasa BALOZI sio kivile ila kimjua MWENYEKITI WA MTAA WAKO ni jambo Muhimu sana
7bu yeye ndo mtu wa kwanza kukukutea katika kila jambo litakalohitaji mwanzo
Hasa mambo kama hayo na tena inakupaswa uwe na namba yake ya SIMU ishu kama hizo za kiduanzwi zikitokea inakuwa rahisi kuziweka sawa

Ulaya yapo ndio ila wenzetu wanaita SHERIFF ambapo anakuwa na majukumu mengi ambayo moja wapo ndo kam hayo ya Kibalozi nk
 
Hivyo vitu hakuna kabisa, wala hakuna hao mabalozi wala wenyeviti kila nyumba ina camera ya ulinzi imefungwa, jirani yako ambae umetenganishwa na ukuta huwezi jua yeye ni nani anafanya shuhuli gani au yeye ndio mmmiliki wa nyumba au laa.

Lakini hata huko kutembea tembea mitaa ya ushuani utajishtukia maana utajikita uko mwenyewe barabarani tena isiwe wakati na jioni maana utajiona ni mwizi
 
Daaah ni kwer wakuu
 
Kwa sasa BALOZI sio kivile ila kimjua MWENYEKITI WA MTAA WAKO ni jambo Muhimu sana
7bu yeye ndo mtu wa kwanza kukukutea katika kila jambo litakalohitaji mwanzo
Hasa mambo kama hayo na tena inakupaswa uwe na namba yake ya SIMU ishu kama hizo za kiduanzwi zikitokea inakuwa rahisi kuziweka sawa

Ulaya yapo ndio ila wenzetu wanaita SHERIFF ambapo anakuwa na majukumu mengi ambayo moja wapo ndo kam hayo ya Kibalozi nk
Balozi muhimu sana maana mwenyekiti wa mtaa hawezi kujua watu wake wote na hivi nyumba zimejazana hapa mjini
 
Kwa usalama ni lazima ujue hayo.
Bongo sio ulaya, kule mifumo yao ya ulizi ni thabiti kuna camera barabarani mpaka mitaani. Ungedakwa ulaya basi wangekucheki tu kwenye midatabase yao kukujua wewe ni nani.

Hapa kwetu balozi ndo ana database ya mtaa wake (kaikariri kichwani), hapo ponapona yako ni kumtaja mwenyenyumba wako( bahati mbaya vijana hawawajui majina wenye nyumba wao), au kama una kwako mtaje jirani yako ( hapa napo sababu ni zilezile za kipuuzi na kuiga umagharibi ati ngia toka ingia toka).

Nakukumbusha hii ni bongo, siku nyingine utapigwa kiberiti hivi hivi. Ama lah utaitiwa mwizi na balozi akaitwa akasema hakutambui, jirani nae humjui hakujui sijui utajitetea kwa ingia toka ingia toka za jiji.

Kibongobongo fahamiana na majirani wawili watatu just for backup sio mzoeane, fahamiana nao tu.
Naikubaligi sana hii avatar yako😂😂 imekaa kiutata kweli kweli
 
Back
Top Bottom