Taarifa ya diwani wa Igoma dhidi ya sakata la umeya jijini Mwanza na mbunge Wenje

Peres

Member
Aug 15, 2011
7
7
Taarifa kwa umma wa Tanzania na vyombo vya usimamizi wa sheria za nchi.


Naomba nitumie fursa hii kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizojiri kwenye kikao cha baraza la madiwani tarehe 15/05/2012 la halmashauri ya jiji la mwanza na hujuma na uonevu ninazofanyiwa mimi chagulani adams iblahim diwani wa kata ya igoma kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) na mbunge wa nyamagana ezekia dibogo wenje, kutokana na mchango wangu wa kutoa mawazo nilioufanya tarehe tajwa hapo juu ya kusema mstahiki meya josephat manyere kuwa sina imani naye, hoja yangu ilisimama na kujikita katika vipengele vya kikanuni, sheria na katiba ya nchi yetu.

Ni haki yangu ya kikatiba ibara (18) - ya jamhuri muungano wa tanzania kuwa na uhuru wa kutoa mawazo na maoni pia kanuni za kudumu za halmashauri za jiji la mwanza kanuni ya (24) - kuhusu uhuru wa kutoa mawazo wakati wa majadiliano inasema hivi, kutakuwepo na uhuru wa kutoa mawazo wakati wa majadiliano katika mikutano ya halmashauri na uhuru huo hautaweza kuhojiwa katika mahakama yoyote au mahali popote nje ya mkutano wa halmashauri. (22) - hivyo kanuni katiba na sheria zinanipa mamlaka ya kuwa huru kuchangia kwenye baraza la madiwani.

Hoja za kamati ya madiwani wa chadema ilikuwa ni kugomea bajeti kwa kigezo kuwa mkurugezni hajaitisha mkutano wa kikanuni.
1. Wa kanuni ya halmashauri utakaoitishwa miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha kuisha ili kujadili tu.
a) utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka uliopita
b) mpango wa bajeti wa mwaka ujao.
2. Katika kabrasha na taarifa ya mipango ya robotatu ya mwaka pia mkutano wa kawaida wa halmashauri wa robotatu haujafanyika.
3. Mapendekezo ya bajeti na vigezo vilivyotumika kuandaa bajeti hawajavipata na hawavijui.
• mpango mkakati wa halmashauri wa jiji la mwanza city strategic development plan 2008/13 hawajaupata.
• mpango shirikishi wa fursa na vikwazo vya maendeleo o & od.
• ilani ya uchaguzi wa ccm hatujafundishwa inasemaje.
• dira ya taifa ya maendeleo (national vision 2015)
• malengo ya milenia
• mpendekezo ya viongozi wa halmashauri ya jiji, mkoa na taifa.

4. Kanuni za halmashauri zimekiukwa kwa kutangaza tenda za halmashauri zikiwa hazijaruhusiwa na baraza la madiwani kwa kupitisha bajeti.

Hizo ndizo zilizokuwa hoja za madiwani wenzangu zikiongozwa na mbuge wa nyamagana, katika mapitio ya kanuni zetu na mapendekezo ya bajeti, nilibaini mapungufu mengi na makosa katika makubaliano ya madiwani wenzangu, nilibaini kasoro zifuatazo katika msimamo wa kugomea bajeti ya 2012/2013 kwa kutumia kigezo cha kutoitishwa mkutano unaotamkwa kwenye kanuni ya tano (5) ni makosa ya mstahiki meya josephat manyerere kutokana na sababu zifuatazo:-

Kanuni ya nne (4) - inampa mwenyekiti mamlaka ya kuitisha “ mkutano maalumu wa halmashauri unaweza kuitishwa na mwenyekiti ndani ya siku ishirini na moja baada ya kupokea maombi ya maandishi yaliosainiwa na wajumbe wasio pungua theluthi moja ya wajumbe wote. Kutaka – mkutano huo ufanyike na maombi hayo yaeleze wazi madhumuni ya kuitishwa kwa mkutano huo maalumu”.

Hivyo sababu ya kuahirisha mkutano kwa kigezo cha mkurugenzi nilibaini meya haelewi majukumu yake, hivyo aliyepaswa kuitisha mkutano ni yeye, kazi ya mkurugezni ni kutoa taarifa ya mikutano hii ni kwa mujibu wa kanuni ya (7) “ mkurugenzi atatoa taaarifa ya mkutano kwa maandishi kuwa kila mjumbe katika muda usiopungua siku saba akieleza mahali, siku na saa ya mkutano unaokusudiwana mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo” hivyo ni jambo la ajabu meya aliahirisha mkutano aliouunda yeye bila kuzingatia kuwa kanuni ya tano ilitaka aitishe kwanza mkutano huo, hii ni dhahiri meya tuliyenaye hajui majukumu yake.

Madiwani wenzangu wakiongozwa na mbunge wa Nyamagana waling’angania tugomee kabrasha ambalo wenje kwa nafasi yake ya ubunge ni mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi (utawala) na mwenyekiti wa kamati hii ni meya jukumu la kwanza la kamati hii ni “kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango wa maendeleo ili kupata idhini ya halmashauri (kanuni ukurasa 60) hivyo bajeti ambayo mbunge alitoa hoja ya kuikata kuwa haikuzingatia vigezo na sababu aliyotoa yeye ni sehemu ya bajeti.

Haya ni matunda yake hivyo kitendo cha kushiriki kuandaa bajeti kisha unaigomea ni uvivu wa kufikiri, na kutaka umaarufu wa usio tija. Chadema ndiyo tunaongoza halmashauri hivyo kama bajeti ni mbovu basi wajumbe wote wa kamati ya fedha wajiuzuru maana hawafai, kazi yao ni kuchukua posho tu bila kutoa miongozo ya kuandaa bajeti bora.

Kigezo cha kugomea bajeti kwa kigezo cha kanuni ya kutangaza tenda zimevunjwa kwa kutangaza tenda kabla ya baraza la madiwani kupitisha bajeti hii hiki nacho ni kigezo dhaifu na inaonyesha uwezo wa wabunge wetu na madiwani ni wakutilia mashaka. Kanuni ya (77) - inahusu utiaji mhuri kwenye nyakara
(1). Lakiri ya halmashauri haitabandikwa katika hati yoyote mpaka ubandikaji huo umeidhinishwa na azimio la halmashuri likiidhinisha kukubaliwa kwa zabuni, ununuzi, uuzaji au upangishaji au kuchukua mali yoyote, utoaji wa hati yoyote ya ukopeshaji fedha, uwakilishaji wa madai yoyote, uwekaji wa viwango vya kodi, uingizaji kwenye mkataba, kutunga sheria ndogo, na hati yoyote iliyorasmi ambayo kwa mujibu wa sheria au kanuni yoyote inahitaji kuwekwa lakiri ya halmashauri.
(2) itashuhudiwa au kuthibitishwa na mwenyekiti au makamu mwenyekiti na mkurugenzi na hati zilizowekwa lakiri zitasainiwa na mwenyekiti au makamu wa mwenyekiti kama hali itakavyokuwa.

Hoja ya zabuni kutangazwa kabla ya baraza la madiwani hili nalo wa kulaumiwa ni meya maana ili tangazo la tenda liwekwe lazima atie saini kwa mujibu wa kanuni (77) - kama ilifanyika bila kujulishwa basi hiki nacho ni kigezo cha kudhihilisha meya amepwaya na hajui majukumu yake. Pia amevunja kanuni ya (77) (1) inayotaka idhini ya baraza la madiwani liidhinishe lakiri yeye ametia saini bila kufuata taratibu kanuni inasema baraza la madiwani liidhinishe kwanza ndipo atie saini kitendo cha yeye kutia saini kimetufehedhesha na kulifehedhesha baraza la madiwani na chadema kwa ujumla.

Nilipinga kuahirisha kikao cha baraza kwa kutumia mwongozo wa kikanuni, kanuni ya (37) (1) kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (2) ya kanuni 17 na kanuni ndogo ya 2 ya kanuni hii. “halmashauri haitaahirisha – mkutano wake hadi agenda zote za mkutano huo zitakapojadiliwa na kutolewa uamuzi”.

hivyo niliwaomba wajumbe wenzangu tuendelee na mjadala ili tubaini mapungufu yoliyomo katika kabrasha na tutoe mapendekezo ya nini? Kifanyike na mwisho tungeamua kwa kutumia kanuni ya 26 (1) kuhusu maamuzi ya mikutano ya halmashauri inasema” masuala yote yaliyojadiliwa na kupendekezwa katika mkutano wowote wa halmashauri yataamuliwa kulingana na wingi wa kura za wajumbe waliohudhuria mkutano huo na ikitokea kura za wajumbe zikalingana basi mwenyekiti au mjumbe mwingine anayeongoza mkutano atapiga kura ya turufu mbili ya kura ya kawaida. Tungejadili na kutoa mapendekezo ya kipi kifanyiwe marekebisho na kutoa uamuzi kwa njia ya kura. Kuliko kutumia kodi za watanzania vibaya maana vikao vina gharama kubwa.

Hivyo sikuona umuhimu wa kugomea kikao kutokana na sababu zifuatazo:-

(1) bajeti hii imetokana na chama changu chadema hii ni kwa mujibu wa majukumu ya kamati ya fedha na utawala. Baadhi ya majukumu hayo ni:-
(i) kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mipango ya maendeleo ili kupata idhini ya halmashauri.
(ii) kuratibu mapendekezo katoka kwenye kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyapeleka kwa halmashauri (rejea uk 6 na kanuni za halmashauri ya jiji.
hivyo kugomea bajeti ilikuwa ni kukosa umakini na weledi maana kila kamati –huandaa bajeti ya fedha na utawala ambayo huijadili bajeti kwa ujumla kisha meya hutia saini na bajeti hii huwasilishwa hazina, hatua zote zilifuatwa katika kuandaa bajeti. Wafuatao ndiyo wajumbe wa kamati ya fedha na utawala na ndiyo wenye jukumu kubwa la kuandaa bajeti.
(1) mstahiki meya
(2) wajumbe wawili wateule wa meya
(3) wenyeviti wa kamati
(4) wabunge
(5) katibu /mkurugenzi (hapigi kura) wataalam

hivyo kugomea bajeti tuliyoiandaa wenyewe ni udhalimu ni vema wenje aseme kuwa hajui kazi zake kama mjumbe wa kamati ya fedha kuwa ni kuandaa mapendekezo hivyo bajeti anayodai ni mbovu ni zao lake yeye na wajumbe wote wa kamati ya fedha ambayo hukutana kila mwezi.

Hivyo walikuwa na fursa ya kutuandalia bajeti madhubuti yenye vigezo kuliko kupotosha umma wakati walishiriki vikao vyote na posho walichukua haya ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

(2) kigezo kuwa kikao cha kanuni ya tano haikuwa hoja ya kufanya mkutano uhairishwe, aliyepaswa kuitisha mkutano ni meya na kazi ya mkurugenzi ni kutoa taarifa ya mkutano kwa mujibu wa kanuni ya saba (7) pia kama meya aliona kikao hicho hakijaitishwa kwa nini? Aliitisha kikao cha pili wakati cha kwanza hakijafanyika, hapa wa kumlaumu ni meya kutojua majukumu yake. Maana kanuni ya nne kazi yake ni kuitisha mikutano kanuni inampa mamlaka ya kuitisha.
(3) kigezo cha kuahirisha kikao eti tenda zimetangazwa bila kuhusishwa na baraza hapa wa kulaumiwa ni meya. Kwa kubaka mamlaka ya baraza. Kanuni ya 77 (2) inasema ili tenda zitolewe meya au makamu wake lazima wasaini. Swali kwanini meya amesaini lakiri ya tangazo bila idhini ya baraza la madiwani huu ni udhalilishaji wa baraza la madiwani na mamlaka yake na ndiyo chanzo cha meya kusaini shule ya msingi mbugani ichukuliwe na taasisi ya kiislamu bila idhini ya baraza pia ujenzi wa kliniki ya utemini na ofisi za afya huku baraza la madiwani likiwa halina taarifa yeyote. Ikumbukwe kuwa majengo haya ni kama vile makongoro kliniki wameuziwa benki kuu, hiyo hoja ya tenda kutangazwa bila idhini ya baraza hapa meya ametumia mamlaka vibaya ni udhaifu wa hali ya juu, hivyo meya ameshindwa na hajui mamlaka yake.
(4) kigezo cha kwamba vigezo havijulikani havina mashiko maana meya wenyeviti na wabunge wote ni chanzo cha bajeti hii maana majukumu yao ni kuandaa mapendekezo na kuwasilisha kwenye baraza la madiwani hoja ya vigezo vya uandaaji bajeti kwa kufuata ilani ya ccm dira ya taifa ya maendeleo 2015 haya yote wajumbe wa kamati fedha walipaswa kuyajua kabla ya kuandaa ni kuiwasilisha bajeti maana ni kazi yao ya kikanuni ni kuandaa bajeti na kuiwasilisha hivyo madai ya wenje kudai hajui vigezo vilivyotumika kuandaa bajeti hii, inaonyesha hajui majukumu yake kama mjumbe wa kamati ya fedha na utawala na ikizingatiwa wajumbe wote wa kamati ya fedha na utawala ni kutoka chadema kasoro watatu. Wajumbe hao ni:-

1. Josephat k. Manyerere (chadema) m/kiti
2. Charles chinchera chadema.
3. Rosemary brown chadema.
4. Henry matata chadema.
5. Ezekia wenje chadema.
6. Highness kiwia chadema.
7. John minja (ccm).
8. Maria hewa (ccm).
9. Mkiwa adam (cuf).
hivyo bajeti ambayo wenje anadai hajui vigezo vilivyotumika ameonyesha upogo wa kutojua majukumu yake kama mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi.

Hivyo hawa wajumbe na chadema kwenye kamati ya fedha ya uongozi wajiudhuru maana wameenda kinyume na katiba ya chadema kuhusu kanuni za kusimamia shughuli , mwenendo na maadili ya halmashauri zilizo chini ya chadema kanuni ya 2:0 kanuni za halmashauri za chadema.

Bila kuathiri kanuni na taratibu zilizowekwa kisheria kusimamia halmashauri, halmashauri zote zilizo chini ya chadema zitaendeshwa kwa kufuata kanuni na taratibu zifuatazo kwa kutaja baadhi:-
(a) halmashauri zote zinazoongezwa na chadema zitatakiwa kuongozwa kwa mujibu wa sera na ilani ya uchaguzi ya chadema
hivyo kupinga bajeti ambayo chadema wameiandaa mi kutojua kanuni za kudumu za halmashauri na majukumu ya kamati nyeti ya fedha na uongozi. Wenje alitakiwa awaongoze wajumbe kuandaa bajeti ya kichadema na siyo kupiga propaganda tujiulize je tunaongoza halmashauri kwa kufuata ilani na sera za chadema kama kusomesha watoto bure bila kuleta visingizio kuwa hatukuongoza nchi nzima. Je wenzetu wa tarime waliweza vipi? Kulipia ada wanafunzi, hii ni kutokana na ubinafsi wa wenje na wajumbe wenye mawazo mgando waliojaa kwenye kamati ya fedha na uongozi, wanaosubiri posho hawaibui hoja na ajenda toka kwenye kamati wamewaacha wataalamu badala ya wao kuwa chanzo cha agenda za kuongoza halmashauri kichadema chadema na siyo kungoja posho.
nilienda kinyume na wenzangu kwa sababu bajeti waliokuwa wanaigomea wao ndio chimbuko la bajeti hivyo nikatumia kanuni ya 68 (2) inayohusu utekelezaji na wajibu wa diwani kuwa atazingatia:-
(a) maslahi ya taifa na maslahi ya wananchi katika eneo la halmashauri.
(b) katiba , sheria kanuni sera na miongozo mbalimbali ya kitaifa.
(c) kanuni za maadili ya madiwani na miiko mingine ya kitaalamu.

Hivyo kutaka kikao kiendelee nilizingatia maslahi ya wananchi wa mwanza kwa kuwa vikao vyetu vinatumia pesa nyingi sana tulikaa takribani kwa siku mbili tunatumia shilingi milioni kumi na mbili hivyo ni vema kuendelea na kikao na tuichambue bajeti na kisha tuwape mapendekezo na tuainishe mapungufu yaliyomo kuliko kuahirisha kikao kama walivyokuwa waking’ang’aniza wenzangu, hivyo kuahirisha kikao bila kujadili ni kutumia pesa za walipakodi vibaya bila kujadili lolote kwa siku mbili huu ni ukosefu wa huruma kwa wanamwanza.

Nilipinga kuahirisha kikao maana kufanya hivyo ni kuidhalilisha chadema uhalisia ni kwamba bajeti hii imetokana na chadema, hivyo na ikumbukwe chadema ndiyo tunaongoza halmashauri pia kanuni ya (37) ya kanuni za kudumu za halmashauri ya jiji inapinga kuahirisha kikao bila kumaliza ajenda na kuzitolea maamuzi hivyo kanuni pia kanuni ya 68 imezungumzia wajibu wa diwani pamoja na kufuata kanuni, taratibu na sheria.

Kwa nini nilisema sina imani meya wa jiji la mwanza.
hoja yangu ya kutokuwa na imani na meya imezua minong’ono miongoni mwa najamii wa mwanza na tanzania kwa ujumla. Wapo wanaoniona mimi kama shujaa na jasiri kwa kusema ukweli wengine hawakuipenda sana hoja hiyo na kuiona kama dhambi kubwa sana ambayo haikutakiwa kufanywa na wengine waliniona kama msaliti nimehongwa na chama cha mapinduzi na wengine walizungumza huku mishipa na mate yakiwatoka kuwa huu ni usaliti mkubwa sana na kutengeneza hata ushahidi wa uongo, uzushi na propaganda. Pia maadui wangu ndani na nje ya chadema wameitumia fursa hii ipasavyo kuhakikisha chagulani adams ibrahim wanamuangamiza aonekane hafai si lolote si chochote ninaweza kusema wapo waliopata na mshituko mkubwa sana na wengine wakadiriki kutangaza kata ya igoma iko wazi, wakaanza kupiga jalamba la propaganda kwenye vijiwe mbalimbali na viunga vya jiji la mwanza na tanzania kwa ujumla.

Nikayakumbuka maneno ya baba wa taifa letu j.k.nyerere (tusijisahihishe)
ukweli unatabia moja nzuri sana haujali ukubwa wala mdogo, haujali adui wala rafiki kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni mpira natumai utaniponya lakini nikilipuuza onyo lako eti kwa sababu wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwa.

Hivyo nilisema ukweli ili historia inihukumu na wakati uje utuambie nani alikuwa sahihi na nani hakuwa sahihi niaminivyo palipo na mvutano wa kimawazo baina ya pande mbili historia ituhukumu na wakati utasema nani alikuwa na kosa na nani alikuwa sahihi.

Wengine wakatumia historia yangu ya mimi kuwa mgombea kipinidi cha 2010 kuwa ninautaka umeya hivyo kuiona hoja yangu kama chuki binafsi.

Sababu za kutokuwa na imani na Mstahiki Meya Josephat Manyerere
1. Hajui majukumu yake na mamlaka yake kama mwenyekiti na msimamizi mkuu wa shughuli za halmashauri ameshindwa kujua kuwa jukumu la kuitisha vikao na mkurugenzi kazi yake ni kutoa taarifa kwa mujibu wa kanuni ya saba hivyo kutoa visingizio vya kushindwa kufanya vikao kuwa mkurugenzi hajaitisha mikutano (vikao)ni kutojua jukumu lake.

2. Amevunja kanuni 77(1) – (2) kwa kutia saini lakiri ya utangazaji tenda bila idhini ya baraza hivyo kuingilia mamlaka na madaraka ya baraza la madiwani kwa kutangaza tenda kabla baraza halijaidhinisha. Alisaini sheria ya usafi (sharifu) ikaanza kutumika bila idhini ya baraza, pia utaifishaji wa shule ya msingi mbungani ulifanyika yeye kusaini bila idhini ya baraza la madiwani.

3. Ana upendeleo katika kusimamia ugawaji wa miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali amekuwa akitumia nafasi yake kujilimbikizia miradi katani kwakwe yeye na naibu wake mfano kata yangu mwaka wa fedha 2011/2012 ilipangiwa miradi takribani kumi na saba mpaka leo hii hakuna hata mradi mmoja uliofanyika kwenye kata yangu. Pia bajeti ya 2012/13 kata yake amejitengea mradi wa kujenga barabara yenye urefu wa 0.5 kwa milioni sabini, huku kata yangu km 6 kwa 50 millioni hapa uwiano uko wapi km 6 kwa 50 milioni huku nusu kilometa kwa 70 milioni.

pia katani kwake na naibu meya walijengewa madaraja kadhaa mwaka huu wa fedha 2011 /12, nilipeleka mapendekezo ya kujengewa daraja la fumagila ambalo limekuwa kero kwa miaka 50 sasa ingawa kila mwaka nimekuwa nikipeleka mapendekezo lakini halimo kwenye miradi mipya 2012 / 2013 ikumbukwe wana igoma hawakunituma mimi kuwa vuvuzela la kusifia manyerere hata kama amepwaya lazima tuambiane ukweli wa mambo ili tuweze kusonga mbele bila kinyume na hapo tutakuwa tunaongelea kwenye mtaro wa chama cha mapinduzi.

4. Meya anatumia mamlaka yake na ofisi yake vibaya ikumbukwe iliwahi kuripotiwa na gazeti la sema uskike toleo la ……………………..yeye kama muumini wa kanisa la sabato alishiriki kuanzisha ujenzi wa ghorofa la kanisa bila kutabali ya ujenzi (building permit) leo hii baada ya kuripotiwa magazetini wamepata kibali kinyemela ikumbukwe kiongozi ni kuonyesha njia kama meya anashiriki katika ujenzi usiofaa kisheria ataweza kusimamia haki au kukemea ujenzi usio na taratibu.

5. Ameshindwa kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za halmashauri kwa kuwaacha watendaji watende watakavyo mfano kutojua kuwa mamlaka ya kuitisha mikutano (vikao vya halmashauri) ni jukumu lake lakini yeye amemwachia mkurugenzi.

6. Ameshindwa kuonyesha mabadiliko ya kiutendaji kati ya chadema na ccm kilichopo ni kujaza nafasi wanamwanza walituchagua kwa kuamini tungeshughulikia kero za wanamwanza kama inavyoagizwa kwenye katiba ya chadema kuhusiana na kanuni za halmashauri za chadema kifungu (g) kinasema halmashauri za chadema lazima ziwe mfano wa kuigwa katika :-
(i) ushugulikiwaji kero za wapiga kura
(ii) matumizi mazuri ya fedha za walipa kodi
(iii) kuwashirikisha wananchi katika kupanga kuamua na kutekeleza mipango mbalimbali katika maendeleo yao.
(iv) kupambana na rushwa na kutetea haki za binadamu.
(v) kubuni mbinu mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo
tulijiulize kero zimeshughulikiwa kwa kiwango gani nenda idara ya ardhi utadhani sekou toure manyerere ameshindwa kubuni namna ya kuondoa na kutatua kero za ardhi jijini. Rushwa imetamalaki ili kupata huduma mbalibali kwenye ofisi za idara mbalimbali wananchi hawapati tenda na wanaopata tenda malipo ni ya tabu mpaka ahonge fedha ndipo alipwe jasho lake. Je nini tofauti ya chadema na ccm. Kumekuwepo na malalamiko toka kwa wakandarasi kucheleweshewa malipo yao mpaka watoe chochote lakini meya ameshindwa kujisimamia malalamiko na kero za wapiga kura.

7. Mbinafsi asiyependa kuomba msaada kwa jambo asilolifahamu hivyo kuingiza halmashauri katika mavutano yasiyo na tija hataki kukiri jambo fulani hajui ili asaidiwe. Hajui kama kusaini mikataba yote ni lazima kuwe na azimio la baraza la madiwani kwa mujibu wa kanuni ya 77(1).

8. Mpaka dakika hii chadema tunaongoza halmashauri, meya kama kiongozi wetu mkuu hana mpango kazi unao muongoza na kutuongoza sisi kama chadema kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chadema ndiyo maana kuna mvutano na mikorogano ya kutojua kuwa tunatenda kazi kwa kufuata ilani ya chadema. Na moja kati ya mapendekezo ya madiwani wenzangu wa chadema kugomea bajeti wanasema hawajafundishwa ilani ya ccm, je kigezo hiki ni sahihi?

9. Manyerere hana msaada kwa madiwani wenzake kama msemaji wetu mkuu wa madiwani. Kwa mfano tangu mwaka 2010 aliyekuwa mtendaji wangu wa kata ya igoma gaudence bunwenge nimekuwa nikilalamikia utendaji wake kwake yeye pamoja na mkurugenzi alishindwa hata kulisimamia hilo ili nifanye kazi kwenye mazingira ya utulivu na amani kwa miaka miwili bila mafanikio mpaka wananchi walipoamua kufunga ofisi ya kata wenyewe na kumkataa kwa kuchoshwa na utendaji wake. Hii ndiyo hulka na kalba ya manyerere hana uwezo wa kuwakabili watendaji wabovu. Pia diwani wa ilemela alishalalamika kutolewa matusi na watendaji kitengo cha ardhi lakini hakumsaidia hivyo naona hana maana ya kuendelea kuwa meya.

10. Manyerere ameshindwa na amepwaya kutumia nafasi yake kama meya ili kuimarisha chama kwa fursa yake kama meya hii ni kutokuwa na uwezona maono ya siku za usoni. Nilitegemea tungetumia fursa hii ya kuongoza halmashauri watu waseme mambo kama mwanza. Ninachokiona sasa tumeshindwa kujenga ngome imara ya chadema kivitendo ili tuhamasishe majimbo ambayo bado ccm inaongoza kushawishika au kupokea mabadiliko. Hii ingewezwa kufanywa na meya makini na mwenye maono siyo anayesukumwa na matukio.

Kwanini tumefika hapa nini chanzo cha haya yote?
Kumekuwepo malalamiko na minong’ono miongoni mwa wapenzi wadau na wanachama wa chadema jijini mwanza wengine wakituhumu bila kusikiliza upande wa pili wa shilingi (sarafu) chanzo cha haya yote ni hofu za mbunge wa nyamagana ezekia wenje kufanya hila zake.

1. Wenje kupanga safu ya nani awe nani na nani asiwe wenje alinihujumu kwa kiasi kikubwa kipindi kile cha mchakato wa umeya ingawa alikuwa akitumia jina langu kuombea kura kwenye uchaguzi mkuu 2010 kwa kuwalaghai wananchi wa mwanza kuwa chagulani adamu ndiye atakayekuwa meya baada ya uchaguzi kuisha nilimfuata aliruka mithili ya mtu aliyechomwa mwiba mkali na kuanza kudai unajua nafasi hii inahitaji mtu mkubwa ikumbukwe kipindi hicho nilishafanya mazungumzo na manyerere katika hotel ya mashy na nikitaka kujua kwanini anataka awe meya jibu alilonipa aliniambia unajua nafasi hiyo inahitaji mtu mkubwa tu. Nami nikamwambia hiyo siyo hoja mzee wangu ninachoomba uniambie unataka kuwafanyia nini wanamwanza hivyo hoja kusema umeya unahitaji mtu mkubwa haikuwa na mashiko hapa ndipo zengwe la umri lilipoanzishwa nilipata maswali mengi sana je suala la umri wana igoma hawakuliona wakati wananichagua. Hii yote ilikuwa mizengwe ya Wenje na ndipo alipoamua kumlipia Chinchibera pesa ili achukue fomuya kugombea unaibu kama njia ya kunizuia mimi, hapo ikaanzishwa hoja ya kuwa naibu akitoka ilemela meya atoke nyamagana bila kujua wanajenga ubaguzi ili kufanikisha mradi wa kumsimika manyerere. Alimtumia rosemary brown diwani wa pasiansi kuwa atamsaidia kupata unaibu ili amuunge mkono Manyerere kufanikisha mradi wake. Hii yote ni jitihada za wenje kupanga safu ya uongozi kama wanavyofanya ccm bila kuzingatia uwezo. Manyerere haikuwa chaguo la madiwani bali Wenje.

2. Wenje amekuwa chanzo cha uyumbishaji wa maamuzi mbalimbali ya halmashauri ya jiji la mwanza ikumbukwe wenje alipinga mchakato wa kusomesha watoto bure kipindi cha bajeti ya mwaka 2011/2012 tulikubaliana kuongeza kodi ya pango soko kuu kutoka laki moja na ishirini kwenda shilingi laki tatu maana utafiti tuliofanya halmashauri inapoteza pesa nyingi kwa watendaji kupanga kodi kiwango kidogo ili kufanya udalali wa kodi ya vyumba soko kuu, hivyo pesa nyingi kupotelea mikononi mwa wachache.

Tulichogundua chumba cha nje si chini ya shilingi milioni tisa na ndani shilingi milioni sita hadi saba. Tulifanya hesabu kama tukakubaliana kuwa tuongeze kodi ya pango toka shilingi laki moj ana ishirini hadi shilingi laki tatu. Tulipiga hesabu tukapata ongezeko la shilingi bilioni moja poini mbili (1.2) tukakubaliana kwenye kikao cha madiwani wa chadema kuwa tusiipitishe bajeti hiyo hadi mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi. Na mabadiliko hayo kuingizwa kwenye kablasha au bajeti.

Cha kushangaza Wenje alikiuka makubaliano na kuwaambia madiwani wapitishe bajeti akakiuka maazimio yetu kama kamati ya madiwani wa chadema lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yake kwa kitendo cha kuyumbisha maamuzi. Lakini leo kwa kuwa kafanya chagulani wenje ameshikilia bango ili kutimiza azma ya kumuangamiza kisiasa.

Kama tungesimamia maamuzi tuliyopanga leo hii nyamagana na ilemela tungekuwa tunasomesha wanafunzi bure kama tusingetanguliza ubinafsi kwamba mimi mbunge ninasomesha watoto 819 kupitia nyamagana education foundation tusingekuwa hapa tulipo. Lakini leo yako wapi watoto wamemshinda wengine wanarudishwa nyumbani sababu ya ada kama jambo lingebebwa kama la chama tusingekuwa hapa tulipo sasa na sifa zingeenda kwa wanachama lakini hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake wenje. Meya aliwahi kutugomea kuahirisha kikao kama tulivyokubaliana kamati ya madiwani wa chadema iliyoketi 5/6/2011 na kufuatiwa na kikao maalumu cha baraza tarehe 6/11/2012 katika kujadili taarifa ya utekelezaji na uwajibikaji ya mwaka 2010 /2011 hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao lakini kwa vile chagulani adams kasema ukweli imekuwa nongwa hapa napata falsafa kunya anye kuku akinya bata kaharisha.

3. Wenje anatumia nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu kutengeneza na kuhalalisha uondoaji wa viongozi pasipo kufuata taratibu na katiba ya chama. Asilimia 98% ya viongozi waliopo nyamagana hawakuchaguliwa kikatiba wamewekwa na wenje ukiwa kinyume na mambo yake anakutengenezea zengwe ili utoke katika chama bila kufuata taratibu. Chacha okong’o ingawa alikuwa mkosaji aliondolewa bila kuzingatia katiba ya chadema ibara ya 6.3.6 inayohusu nidhamu na uwajibishaji wa viongozi. Chacha aliondolewa kinyemela bila kufuata taratibu bila kuitisha vikao akafuata deus lutalagula (katibu mwenezi wilaya) aliyekuwa kampeni meneja wake naye aliondolewa kinyemela bila kufuata taratibu, akafuata lucy ngotezi naye akaondolewa. Nafasi ya mwenyekiti ikachukuliwa na mzee makelemo shigamelo aliyekuwa mgombea udiwani mkuyuni ingawa hivi karibuni alimwondoa kwa kutaka kitendo cha wenje kutishia bastola wenje, gwanchele na lutalagula waitwe alimtengenezea zengwe akamuondoa akamkaimisha mzee sukari. Viongozi wote wa nyamagana ni wakuwekwa na wenje bila kufuata taratibu za katiba ya chama hatimaye leo ameangukia kwangu baada ya kuniwinda akatumia kikao batili kufanya maamuzi batili ili atimize azima yake ya kujenga mtandao wa watu kutoka mkoa wa mara na wasioweza kumweleza ukweli au yale asiyopenda kuyasikia bali anayopenda kusikia.

4. Kikao cha baraza la madiwani cha tarehe 15/5/2012 msimamo wangu ulikuwa tujaili mapendekezo ya bajeti kisha tutoe mapendekezo na kuainisha mapungufu ni yapi na kisha tukubali au tukatae kuipokea bajeti maana kukataa bila kujadili ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi wenje ni vema ukaaacha unafiki kama anayetaka bajeti yenye sura ya kichadema angetoa maelekezo na mchango wake maana yeye ni mjumbe wa kamati ya fedha na utawala na siyo kutafuta sifa binafsi na umaarufu wa kijinga anashangaza kusema hajui vigezo vilivyotumika kuandaa bajeti wakati yeye ni mjumbe na kazi yake ni kuandaa bajeti huu ni uhuni ameshiriki vikao na amechukua posho zote kwa nini hakupinga na kuuliza kwenye vikao vya kamati. Kama mkweli kwa nini alichukua posho zote na kushiriki kuandaa bajeti kisha anadai hajui vigezo vilivyotumika kuandaa bajeti. Huu ni ulaghai kwa wananchi na matumizi mabaya ya pesa za walipakodi. Agenda yangu ni kutaka kujadili kisha tutoe mapendekezo nini kirekebishwe, kuliko wenje alivyosimama na kumshinikiza meya ahirishe kikao hii inaonyesha meya asivyo na maamuzi binafsi anasukumwa na matukio.

Propaganda zilizoenezwa dhidi yangu:
1. Kiliitishwa kikao tarehe 17/5/2012 cha kamati ya madiwani ili kufanya tathmini ya kikao cha 15/05/2012 agenda ilikuwa tumefanikiwa au la wenje alianza kushinikiza chagulani adams na henry matata washitakiwe kwa kukiuka maadili ya chama kitendo cha chagulani kusema hana imani na meya yeye alitafsiri ni kuvunja maadili ya chama bila kuainisha msingi wa mashitaka yangu. Maana kutokuwa na imani na meya siyo kosa hata katika mkutano wa furahisha wananchi walimkataa na kumzomea mbele ya viongozi wa kitaifa. Ikumbukwe lengo la wenje ilikuwa kufanikisha azma yake kwa mara ya pili kutaka chagulani, lutalagula na vijana anaohisi ni tishio kwake siku za usoni waondolewe ndani ya chama.

Kikao hicho tulieleza jinsi tulivyosimamia kanuni na kanuni zinavyozuia kuahirisha kikao bila kumaliza ajenda na kutoa maamuzi ndipo katibu wa mkoa Wilson Mshumbusi akasimama na kusema hata kama tumekosea tungekufa sote kwa kusimamia maazimio yetu, nilisema niaminivyo mimi majadiliano lazima kuna mambo utapata na mengine utapoteza (lose and gain) hivyo ni vema tujadili kisha tukaamua kutopitisha kwa njia ya kura maana chadema tulikuwa wengi tungefikia muafaka maana agenda ilikuwa kupitisha bajeti, azma ya wenje ilikuwa ni kunihujumu alimtuma katibu wa wilaya na katibu mwenezi wa wilaya kupanga mamluki mazingira na mradi wake wa kunihujumu alikusanya kundi lake likiongozwa na mzee tuguro kinyeti na genge lake kuandaa tamko kuwa wanachama wa igoma hatuna imani na diwani huku akijua kuwa wale siyo viongozi halali wa kata yangu. Pia akiwa ametafuta mtu anayemuandaa kugombea udiwani kata ya igoma hii ilikuwa inafanyika tukiwa kwenye kikao hicho cha madiwani midland hotel nilimweleza hujuma anazofanya dhidi yangu kuwa ni batili na jinsi anavyotuma.

Mamluki wake waliokuwa wamekaa shule ya msingi shamaliwa, nilipata taarifa ya wajumbe wa kamati tendaji za ilemela na nyamagana siku ya tarehe 15/05/2012 baada ya kuvunjika kwa baraza la madiwani wamealikwa kwenye kikao tarehe 18/5/2012 wenje alianza kusuka mipango ya jinsi ya kuninyang’anya kadi kikao cha madiwani hakikufikia muafaka kutokana na mabishano makali mwenyekiti wa madiwani wa kata ya isamilo aliahirisha kikao na tukatawanyika ndani ya dakika 5 baada ya kutoka kikaoni katibu wa mkoa alinipigia simu na kuniambia kuna barua yako alinipa barua ikinitaka nifike kesho yake saa 4 asubuhi kuleta utetezi ndipo nilipomuuliza hii barua ndani ya dakika tano umeiandika saa ngapi? Maana kikao cha madiwani hakikutoa maamuzi nini kifanyike ila kwa kuwa walikuwa wanatekeleza matakwa ya wenje na kikao kiliandaliwa mapema ili wenje atimize azma yake ya hujuma dhidi yangu.

2. Wajumbe walikuwa wamepangwa na wenje ili kutekeleza azima ya wenje nilifika kwenye kikao saa tano agenda zilikuwa uchaguzi, malalamiko ya chagulani na matata na mengineyo. Niliuliza uhalali wa kikao kile maana katiba yetu haina kikao kinachounganisha wilaya mbili na ziwe na mamlaka ya kufanya maamuzi yenye nguvu ya kisheria ikumbukwe hata kama ingekuwa wilaya moja bado kamati tendaji haina nguvu hiyo wala siyo jukumu lake majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya chadema ibara ya 7.4.10 ni ishirini na moja (21) kamati haina majukumu la kunyang’anya kadi mwanachama.

3. Malalamiko dhidi yangu yalisomwa mbele ya wajumbe wa kamati mbili kuwa nimevunja katiba na kukiuka maagizo na maadili ya chama bila kusema maagizo yapi viliyovunja kisha ukaonyeshwa mkanda wa video wa kikao cha baraza tarehe 15/5/2012 jinsi nilivyokuwa nachangia ndani ya baraza. Aliyejiita mwenyekiti wa kikao kile katibu wa mkoa akiwa na diwani wa viti maalum (mpenzi wake) ndiye aliyekuwa katibu wa kikao hicho. Kikao hicho kilijaa wajumbe wasio halali bila kunisikiliza baada ya kunishushia tuhuma. Wajumbe wakaanza kuachangia, aliyekuwa wa kwanza kuchangia ni katibu wa mbunge kwamba tuchukue maamuzi magumu bila hata kunisikiliza upande wangu na kusema kuwa huyu anyang’anywe kadi niliomba muongozo kwa mwenyekiti wa mazungumzo wa wadau wa wenje alikataa. Kisha wajumbe wakaendelea kuachangia kwa kuwa walikuwa wameshapangwa na wenje siku mbili kabla nilibeba vifaa vyangu nikaondoka. Maana aliyekuwa anatafutwa ni chagulani, matata, rosemary brown hawakuguswa zengwe lilitengenezwa dhidi yangu kikao kile kilitengeneza azimio la kunivua uanachama ili kumfurahisha bosi wao wenje. Kitendo ambacho ni batili kwa kuingilia na kupoka mamlaka ya kamati kuu ya chama na tawi ndio ngazi zenye mamlaka ya kuachisha au kufukuza uanachama.

Katiba ya chadema
Kuhusu kukoma uanachama ibara ya 5 .4.3 kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake na ngazi nyingine ya chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa wanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na itikadi, falsafa , madhumuni kanuni, maadili na sera za chama.

Mwanachama atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo. Pia ibara ya 5.4..4 bila kuathiri kifungu 5.4.3. Cha katiba. Kamati kuu inaweza kumuachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za cahma.

Kikao kinachojinasibu na kutangaza kunivua uanachama ni batili hivyo maamuzi yake ni batili maana hakina nguvu ya kisheria kutenda hilo.

Popote palipo na mvutano baina ya pande mbili historia itahukumu na wakati utasema nani alikuwa sahihi na nani hakuwa sahihi maana tusipojenga mazingira ya kuambiana ukweli chadema tutakuwa hatuitakii mema nayo huenda ikaogelea kwenye mtalo wa ufisadi ambao ccm wanaogelea, ikumbukwe wanamwanza walikataa ccm 2010 si kama walaji wa zamani na kutukaribisha / kutuchagua chadema kama walaji wapya walitegemea mabadiliko katika sekta ya ardhi, elimu bure, afya, miundo mbinu na maisha ya wanamwanza ya kila siku ninachokiona ni kujaza nafasi ujanja ujanja ni lazima tukosoane tuelezane ili tuweze kusonga mbele kama chama tukijenga ushabiki upenzi. Wanasaikolojia wanasema ukipenda sana kitu uwezo wa kufikiri unapungua inawezekana tunaipenda sana chadema na kuichukia ccm ikumbukwe ili iweze kuwa madhubuti ni vema watu waelewe tofauti kati ya kashfa na ukosoaji wa kisiasa.

Msema kweli mpenzi wa mungu huchukiwa na binadamu wenye roho mbaya hutengwa na rafiki zake wenye roho nyepesi siwezi kuogopa kusema ukweli eti kwa kutishiwa kunyang’anywa kadi lakini nikaja kuonekana shujaa uongo utakaposhindwa inawezekana wengine mtaniona msaliti leo lakini historia na wakati vitanihukumu hata kama mtalipinga hili leo nitasema kweli tu ili kweli iniweke huru kwelikweli chagulani haongwi hafungwi mdomo mwenye ushahidi wa kuwa nimehongwa atoe ushahidi siyo majungu niko tayari kuwajibika na kuachia nafasi zote ikibainika nimetenda makosa ya kuhujumu chama na siyo majungu.

Chagulani Adams Ibrahimu
Diwani halali kata ya Igoma - Mwanza

mawasiliano
email: chagulaniadams@ymail.com
simu: 0767 137831/ 0717 137831/ 0783 137831
 
kaandaliwa na CCM hayo

Tatizo la watz asilimia kubwa tunakariri na wavivu wa kufikiri!badala ya kusikiliza pande zote mbili na kuchanganua hoja,we umeamua kukurupuka..no wonder ccm wanaendelea kupeta
 
Chagulani wewe huna kaliba ya kisiasa, yale uliyosema kwenye kikao ungeyasema kwenye kamati yenu kabla ya baraza lote kuketi. Katiba inaruhusu mawazo yako popote pale, ila hukujua athari zake unaziona baada ya kufanya madudu yako na sasa unamtafuta MCHAWI. Kama ni wewe ninayejua jina la hiyo familia hujachelewa unaweza kugombea kule kwetu NKENGE ukitokea pale KYAKA,kama siyo wewe basi ujana ndio umekusumbua ukajua upo pale Mlimani kumbe upo uraiani. Jifunze kukaa vyema na jamaa zako maana ndege wa kundi moja huruka pamoja, usiwe Diwani (SHIBUDA)
 
Ndugu diwani tumekusikia na kukuelewa,acha nasi tufanye utafiti juu ya uliyoyasema na suluhisho litapatikana.
Ila du!mwenzetu ni bingwa wa kujieleza nadhani siku ukikabidhiwa wizara bajeti yako itakuwa vitabu 10 vyenye kurasa elfu moja kila kimoja.
 
Peres/Chagulani,

Hapa jamvini ndio mahali stahili pa kutoa hayo? Ok, ni zama za uwazi ngoja tusome upande wa pili wa sarafu halafu tutarudi.

Any clue.......Shonzi, Shibida, Chagulani ....list ya Wassira inaendelea.
 
Hivi Chadema hamna utaratibu wa kumaliza matatizo yenu ya ndani kwa kutumia vikao vya chama? Huu mchezo wa kubuka na kutundikiana siredi hapa JF kwa mambo yanayohusu chama chenu utawatokea puani wakati fulani.
 
sasa huku JF unataka nani akusaidie kama siyo kukianika chama ulichopitia kuupata huo udiwani? kama CDM hawakutendei haki achana nacho kwani CDM ni mama yako? Unapotuletea maelezo haya marefu humu ndani ni kujidharirisha wewe na chama chako, jifunzeni CCM hata kama wana matatizo ni nadra sana kukuta upuuzi wao kwenye hadhara kama hii, lakini du Dr. Slaa na Mbowe mna kaazi kweli
 
Kampeni za kulegeza nguvu za upinzani zinashika kasi, someni kauli ya Wasira.

Wananunua watu sasa. Ila CCM wajiangalie Mapenzi hayanunuliwi, unaweza muua mpenzi wa unayetamani akupende na baadae akampenda mtu mwingine huku wewe ukibakia na dhambi za uuaji.
 
MIMI DOGO CHAGULANI NAMJUA,
1.NI MUONGO
2.MZUSHI
3.HANA MAPENZI NA CHADEMA
4.HATA KAKA YAKE NA MAMA YAKE HAWAPATANI WAMEKOROFISHANA ITAKUA CDM?
5.HASHAURIKI,,WAZEE IGOMA WAMEONGEA MPAKA WAKACHOKA.
SASA NAELEZA NNAVYOYAJUA,,CHAGULANI ALIWASALITI WENZAKE KWANI WALIKUBALIANA KUIPINGA BAJETI MPYA YA MKURUGENZI SI KWAKUA HAIKIDHI VIGEZO,,NO NO NO....KWAKUA WALITAKA KUIPITIA BAJETI ILIYOPITA AMBAYO WALIGUNDUA INAMADUDU MENGI IKIWEMO HIYO MIRADI ANAYOLALAMIKA KUA IGOMA ILITENGWA,,,HAPOOO NDO PALIKUA MAHALA PAKE MKURUGENZI ABANWE KWANZA,,,
NASIKIA DOGO AKAOGOPA KWAKUA KUNA ELA KAMA M.72 KWENYE BAJETI ILOPITA ALISHAATWANGA SO KAMA BAJETI ILOPITA INGECHUNGUZWA...MADUDU MA MAULAJI YAKE YANGEGUNDULIKA!!!!!!UNADHANI KWANINI AKATAE TENA KWA VIFUNGU BAJETI ILOPITA ISIGUSWE KAMA HAINA NEG. IMPACT KWAKE??NDO HAPOOO DOGO JINGA AKAJA NA HOJA YA KUTOKUA NA IMANI NA MEYA!!!!!!!WENZAKE WAKAMSHANGAA TAYARI ANASAINI 15 ZA MADIWANI WA MAGAMBA PLUS YEYE NA MATATA(cdm) ALOOMBA MSAMAHA TAYARI..
KOSA LA DOGO JANJA....ALIPOITWA KWENYE KIKAO AKAWADHARAU HAO WAJUMBE ANAOWAITA SIO HALALI,,,AKATOKA NJE YA KIKAO NA KUONDOKA AKIFOKA KAMA PDIDY VILE...
2.DOGO AKAITISHA MKUTANO WA HADHARA,,HAPO WANA FALSAFA TUKAJUA DOGO KALA BINGO..KWANI ANAENDA KUOMBA RADHI KWA WANANCHI NA KUWAOMBA WAKAMUOMBEE RADHI KISHA AENDELEE NA SERA ZA MAENDELEO KWENYE HUO MKUTANO...LOOOOOOO DOGO AKAINGIA NA MBWEMBWE,,,JEBEHI,,MATUSI AKIHUTUBIA KUANZIA SAA 9 MPAKA 12 JION PEKE YAKEEEE..HANA HATA KIONGOZI MMOJA NA KIKAO ALIKIITISHA KWA JINA LA HUYOHUYO WENJE,,KWAMBA WENJE ATAKUWEPO...
MIMI NILISHINDWA KUMUAMINI PALE ALIPOANZA KUPAKAZIA MATUSI NA MASUALA YA KUKIVUA CHAMA NGUO HADHARANI NA HAPO NIKAJUA DOGO KATUMWAAAAAAA....SI YEYEEEEEEE.....YUPO MTU NYUMA YAKEEEEE...
BAADA YA KIKAO VIJANA WALIKASIRISHWA SANA NA HATA KUFIKIA HATUA YA KUFANYA MAAMUZI KUANDAMANA ILI DOGO AVULIWE HUO WADHIFA
HALAFU DOGO UNASEMA ETI WEWE NI MWAJIRIWA HALMASHAURI YA MISUNGWI KAMA MWALIMU NA WALA HUTEGEMEI POSHO ZA JIJI,,,JE UNAWEZA KUAJIRIWA SERIKALINI ILIHALI UNAWADHIFA HUO WA KISIASA??SI KWAMBA MIMI NA WEWE TUMEAJIRIWA MWEAS AMBAPO PIA UNATUVURUGA KILA SIKU?(PRIVATE INSTITUTION,,,AS TEACHERS).DOGO SIKU ILE BAADA TU YA KIKAO WAZEE WALIKUTEMA MATE WAKIKUITA MDUDU....KAMA UKUSIKIA WALISEMA HIVIIII....IGOMA ATA LIKISIMAMA JIWE KUPITIA CDM LINASHINDA...WAKASEMA PIA HIVIIIIII INAKUAJE ARUSHA CDM WALIWATEMA WADUDU 4 IJE KUA MDUDU MMOJa??
USHAURI WANGU...BADO UJACHELEWA...FUTA HARAKA HUU UPUUZI ULOUWEKA HUMU JF,,THEN KIMBIA KWA WAZEE WA IGOMA KAWATAKE RADHI,,,RUKA HADI CDM MKOA KALIE MACHOZI NA UTASAMEHAWA....
KUMBUKA:TANZANIA TUNAAMINI JUU YA CDM KAMA CHAMA PEKEE CHA KUTUKOMBOA,,,,UKIWA TOFAUTI NA CDM TUNAAMINI WEWE UNASHIRIKI KUZINYONYA DAMU ZETU NA HAPO WEWE NI ADUI YETU SI KIVITA..LAAAA KIHITIKADI
CHADEMA HAITKUFA KABLA YA KULETA UKOMBOZI WA 2 TANZANIA ALAFU WEKA WAZI ELIMU YAKO HUNA DEGREE
 
Nimeisoma yote japo ndefu lakini nimegundua matatizo mawili: Kuna dalili za ufisadi kwenye miradi: huo mradi wa 0.5km sijui ni wa lami yaani kwa Shs.70 million wakati mradi wa km 6 chini ya million 70. Naona kuna kujipigia pasi za kifisadi. Pili limejitokeza suala la mapenzi kwenye siasa; kuna mtu ametajwa kama mpenzi wa mtu fulani.Tatu naona CDM huko Mwanza hawajui wanalolitenda.
 
Nimeisoma yote japo ndefu lakini nimegundua matatizo mawili: Kuna dalili za ufisadi kwenye miradi: huo mradi wa 0.5km sijui ni wa lami yaani kwa Shs.70 million wakati mradi wa km 6 chini ya million 70. Naona kuna kujipigia pasi za kifisadi. Pili limejitokeza suala la mapenzi kwenye siasa; kuna mtu ametajwa kama mpenzi wa mtu fulani.Tatu naona CDM huko Mwanza hawajui wanalolitenda.
kimbunga umekuaje??na wewe gamba??yoote ya msingi ujayaona ila hayo ya kipuuzi tu???usimruhusu mjinga kueneza ujinga kwani ujinga utawapumbaza wajinga
 
kimbunga umekuaje??na wewe gamba??yoote ya msingi ujayaona ila hayo ya kipuuzi tu???usimruhusu mjinga kueneza ujinga kwani ujinga utawapumbaza wajinga

Jaduong' mosimosi! Huo ni ujinga wa wanachama wa CDM. Yote hayo ya nini kwenye huu mtandao? Ya nini watu kuvuana nguo humu mtandaoni? Wewe unaona ni sawa yaliyosemwa? Yanaijengaje CDM? Mambo mengine yanatakiwa kumalizwa huko huko siyo kuyaleta mitandaoni. Mimi naona wote hao wana shida. Kuna tuhuma zinazohusisha uwezo wa viongozi wa CDM kuanzia Chagulani, Manyerere na Wenje. Mtandao una pande mbili: unaweza kujenga na pia unaweza kubomoa inabidi utumiwe vizuri.
 
Back
Top Bottom