Mchawi mpe mwana alee: Uteuzi wa mh. Zambi ni kumpa kaa la moto mtoto mtukutu

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Uteuzi alioufanya Mhe. Rais kwa kumpa wadhifa wa Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mbunge wa Mbozi Mashariki, Mhe. Geoffrey Zambi ni kwa nia ya kumweka kikaangoni Mbunge huyo na kumfanya Mbunge huyo aende akatekeleze kwa vitendo yale ambayo wenzake aliona hawayawezi. Japo wengine wanadai kuwa Zambi ameteuliwa ili kutoa uwakilishi kwenye Baraza kwa mkoa wa Mbeya baada ya kuondolea wa Mwalimu Agustino Mulugo, "Mzee wa Zimbabwe", kuna dalili zote za kuwa uteuzi huu umefanyika kwa nia ya "kumpa mchawi mwana alee".

Mhe. Zambi ni miongoni mwa wabunge ambao kwenye rekodi amekuwa akiiponda sana mafanikio ya Serikali ya JK hasa Wizara ya Kilimo na utendaji wa Mawaziri wa Wizara hiyo utadhani yeye sio mwana CCM. Sasa wamemwaona anafaa.

Hapa chini ni sehemu tu wa yale ambayo Mhe. Zambi ameilalamikia SERIKALI kupitia kile alichodai ni udhaifu wa watendaji na Mawaziri wa Wizara ya Kilimo :

1. Zambi amewahi kuichanganya Serikali na Waziri Mkuu kuhusu uteuzi na uendeshaji wa Bodi ya Kahawa Tanzania mpaka Bodi yake ya wakurugenzi ya Bodi hiyo chini ya mwenyekiti Dr. Hawa Sinare kuvunjwa;

2. Zambi amewahi kupigia kelele za Kanuni za Kahawa mbivu (ripe cherry) na kupelekea Serikali kuahidiu kurekebisha Kanuni za Kahawa na kuonekana kuna ubovu kwenye Kanuni hizo zilizoandaliwa na Waziri wa Kilimo ambazo ziliruhusu ununuzi wa kahawa mbivu;

3. Zambia ndie aliesababisha Mhe. Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza kuitwa Mzigo kule Mbeya;


MBUNGE wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi amepinga uteuzi wa mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete.
Amepinga pia uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na kile alichoita "utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu."
Februari mwaka huu, rais alimteua Dk. Eve Hawa Sinare kuwa mwenyekiti wa TCB; hatua iliyofuatiwa na waziri wa kilimo (wakati huo Prof. Jumanne Maghembe) kuteua wajumbe wa bodi.
Hivi sasa Prof. Jumanne Maghembe ni waziri wa maji.
Katika barua ambayo Zambi amemwandikia Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza, ambayo ----------- imeona, mbunge huyo anachambua mjumbe mmoja baada ya mwingine na kusema hawakupatikana kwa uwiano wa kikanda.
Zambi anasema katika barua yake kwamba Dk. Sinare "hafai kuwa mwenyekiti wa bodi" kutokana na kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi.
"Naomba ieleweke kwamba, Dk. Eve Hawa Sinare, mwanasheria wa kampuni ya uwakili ya Rex Attorneys, ndiye alipewa kazi na Benki ya NMB kwa ajili ya kulipiga mnada jengo la Kahawa Moshi (ofisi kuu ya TCB). Hadi sasa jengo hilo lina mgogoro," anaeleza Zambi.
Anasema, "…inashangaza kumteua mtu ambaye amepewa kazi ya kulipiga mnada jengo hilo…kuwa mwenyekiti. Atakwepaje mgongano wa kimaslahi?"
Zambi anasema ana uhakika Rais Kikwete "amedanganywa" kuhusu mteuliwa wake. Anasema Dk. Sinare hawezi kutetea maendeleo ya Bodi kama mwenyekiti; na wakati huohuo kusimamia uuzwaji wa jengo ambamo ndipo zilipo ofisi kuu za TCB.
Anamshauri waziri Chiza amshauri rais kutengua uteuzi wa Dk. Sinare ili kuitendea haki bodi ya wakurugenzi; na menejimenti ya Bodi ya Kahawa iweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.
Barua ya Zambi ya 4 Juni 2012, imenakiliwa kwa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
Wajumbe wa bodi ambao kuteuliwa kwao kumepingwa na Zambi, ni pamoja na mhandisi mstaafu wa maji, Miraji Omari Msuya.
Zambi anasema uteuzi wa Msuya haukuzingatia sheria kwa sababu hajulikani anawakilisha kundi gani.
Mjumbe mwingine ni mwanasheria na mwenyekiti wa kampuni ya Lima anayosema inahusika na ununuzi wa kahawa, Eric Ng'maryo.
Anadai vyama ambavyo vinatambuliwa na vinaweza kuwakilishwa kwenye bodi ni Tanzania Coffee Association na Association of Coffee Growers, lakini siyo Lima anakotoka Ng'maryo.
Zambi ameituhumu pia Lima "kushawishi wakulima kuuza kahawa mbichi (mbivu) au red cherry kwa bei ndogo sana."
Kuhusu Prof. James Teri, ambaye ni mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kahawa (TaCRI), Zambi anasema "Taasisi yake siyo ya serikali na hivyo kumteua mtendaji wake mkuu kwenye bodi kama mwakilishi wa serikali, si sahihi hata kidogo…"
"Mheshimiwa waziri, sababu nyingine kubwa ya kupinga uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Kahawa ni kutozingatia uteuzi wa wajumbe kwa kuzingatia maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa nchini," anaandika Zambi katika barua ya kurasa nane.
Anataja kanda ya Kaskazini, yenye mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga; Mbinga (mkoani Ruvuma), Mbeya, Kagera, Kigoma na Tarime (mkoani Mara), kuwa ndiyo maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa.
Analalamika kuwa Mbeya ambako inalimwa kahawa nyingi, hawakupata mwakilishi kwenye bodi.
Anasema, "…inashangaza sana kuona kwamba kati ya wateuliwa wote kumi (10) kwenye Bodi, watano (5) wanatoka mkoa mmoja wa Kilimanjaro…"
Tuhuma za upendeleo kwa misingi ya ukanda, ziliwahi kutolewa mwaka jana wakati wa mkutano wa bajeti.
Zilikuwa zikilenga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo. Alikuwa akidaiwa kuwa chanzo cha watu kutoka sehemu moja kujazana idara ya wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Ezekiel Maige.
Kabla ya kwenda ikulu kuwa katibu mkuu kiongozi, Luhanjo alikuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Alihamia huko akitokea Wizara ya Maliasili na Utalii anakodaiwa alishawishi uteuzi wa watendaji kwa misingi ya ukabila katika Idara ya Wanyamapori.
Aidha, kanuni mpya za zao la kahawa ambazo Zambi anadai kupinga ni zile zilizojadiliwa kwenye mkutano wa wadau wa kahawa tarehe 24 na 25 Mei mwaka huu, mjini Morogoro.
Zambi anadai mkutano wa Morogoro uliambiwa kuwa kanuni mpya tayari zimesainiwa na waziri husika tangu 18 Aprili mwaka huu.
"Mheshimiwa waziri, napenda ufahamu kuwa kanuni hizo zimwetungwa kinyemela kwa sababu wadau wa kahawa hawakushirikishwa kabisa," anaeleza Zambi.
Anadai kuwa kikao cha TCB mjini Moshi mwaka 2011, ambacho inadaiwa ndiko zilitungiwa kanuni, hakikuwa na ajenda hiyo na kwamba yeye mwenyewe alikuwepo.
Anasema, hata hivyo, kikao hicho hakikuwa cha wadau kwani kilikuwa cha wajumbe 30 tu. Amemweleza waziri kuwa kikao cha wadau kina wajumbe zaidi ya 200.
Zambi anasema hajaona kanuni hizo lakini anadai "…zitakuwa kanuni mbaya. Kanuni ambazo hazina faida kwa mfanyabiashara."
Akiandika kwa niaba ya "Wanambeya (wakulina wa kahawa)," anasema wana imani na waziri.
"Tunatumaini masuala haya mawili mazito sana, moja uteuzi wa wajumbe wa bodi bila kufauta sheria na utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu, utayafanyia kazi kama ambavyo nimeshauri," anahitimisha barua yake.

Wakulima wakiendelea kusikiliza mjadala baada ya baadhi yao nao kuchagnia.

Injinia Christopher Chiza (kushito) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi jana katika ziara hiyo.

Zao la kahawa likiwa limebeba matunda wilayani Mbozi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye.


SERIKALI imelaumiwa kuhusika moja kwa moja kuwahujumu wakulima wa zao la Kahawa wilayani Mbozi kwa kutoa vibali vya ununuzi wa kahawa mbichi kinyume na sheria inayowataka wafanyabiashara kununua kahawa kavu.


Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki,Godfrey Zambi aliitupia lawama serikali kuwa ndiyo inayopaswa kulaumiwa kwa kuwa kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiwachanganya vichwa wananchi ambao hawastahili kuyumbishwa katika kuuza kahawa yao ili waweze kupata faida ya kutosha.


Zambi alizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Naibu Waziri wa Kilimo chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza, wafanyabiashara wa Viwanda na Wakulima wa kahawa wilayani humo,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.





Alisema kuwa wakulima wa kahawa hawaelewani wilayani humo kutokana na Serikali kutoweza kuainisha vema sheria na kanuni za ununuzi wa zao la Kahawa huku ikitoa maagizo ya kubahatisha yakiwemo maagizo ya kununua kahawa mbichi (Ripe Cherry) na kukataza huku ikiendelea kutoa vibali hivyo kwa siri.


''Naibu Waziri nalisema hili mbele yako hata Waziri Maghembe angefika hapa ningemweleza na ninataka Bodi ya Kahawa nchini TCB ifutwe ama Meneja wake afukuzwe mara moja maana inachangia kuwagombanisha wakulima wetu na hata bungeni nitalisema hili kwa maandishi'' alisema Zambi.


Mbunge huyo alisema vigogo wa bodi hiyo wanatoa maamuzi yanayoonesha wazi kuwa wanamaslahi yao binafsi na wala si kwa lengo la kuwakomboa wakulima.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Mbozi Erick Ambakisye aliitupia lawama moja kwa moja kampuni ya Kahawa ya Lima ambayo alisema inaongoza kununua kahawa mbichi katika wilaya hiyo.


''Kampuni ya Lima haiwasaidii wananchi kwa kuongoza kununua kahawa mbichi wakati tayari Halmashauri tumetoa agizo la kusitisha ununuzi na Meneja wa Bodi ya kahawa TCB hajaja kwa kuogopa kwasababu tungemwambia ukweli juu ya hujuma zake na Mkuu wa mkoa wa Mbeya anasingiziwa wakati chanzo cha matatizo ni wao'' alisema Ambakisye.


Diwani wa kata ya Ipunga Burton Sinyenga na diwani wa kata ya Myovizi Sunday Shulla walipendekeza ununuzi wa kahawa hiyo mbichi upigwe marufuku wilayani humo.


Mwenyekiti wa Umoja wa vikundi vya wakulima wa kahawa Mbozi (MVIKAMBO) Fredy Mgalla alisema baadhi ya madhara ya ununuzi wa kahawa hiyo mbichi ni pamoja na kudhoofisha mashamba ya kahawa, wizi wa matunda mashambani, bei isiyozingatia ubora wa kahawa na kudhoofisha uelewa wa kanuni za uzalishaji wa zao hilo.


Naye Meneja wa kiwanda cha Lima kinchojishughulisha na usindikaji wa kahawa wilayani humo Kingson Nzunda alisema madhara yatokanayo na hatua ya kupiga marufuku ununuzi wa kahawa hiyo mbichi ni wananchi kuanza kuuza mazao ya chakula kama Mahindi kwa ajili ya kujikimu huku wanaojiita vikundi vya wakulima wakiendelea kuwalangua wakulima.


''Naibu Waziri upotoshaji wa makusudi unaofanywa na Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gilbert Komolo hauvumiliki na unakusudia kulinda maslahi binafsi kwasababu hata hivyo vinavyojiita vikundi vinanunua kahawa mbichi na kwa bei ya ulanguzi'' alisema Nzunda.


Alisema mbali na hili bodi ya kahawa nchini ni kikwazo kikubwa kwa wakulima wa kahawa wilayani humo na kwamba licha ya Halmashauri ambayo wengi wao pia ni wafanyabiashara wa zao hilo, alitoa angalizo kuwa njaa itakapotokea wilayani humo viongozi wa Halmashauri wawe wa kwanza kulaumiwa.


Sanjari na hayo alishauri kuwa Serikali iruhusu ushindani, kati ya makampuni na vikundi vinavyohusika kufanya biashara hiyo na vikundi hivyo visajiliwe na kulipa kodi Serikalini kwasababu yote hayo yanatokea kutokana na mgongano wa kimaslahi.


Mkulima wa zao hilo la kahawa wilayani humo Dickson Mashambwa alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa asikubali upotoshwaji unaolenga kunufaisha upande wa kundi moja kwasababu wakulima wanaendelea kunufaika na biashara hiyo licha ya kuwepo madhara.


''Mimi ni mcha Mungu niseme ukweli, kampuni ya Lima imekuwa ikitusaidia kwasababu inanunua kahawa hiyo mbichi kwa Shilingi 1,000 wakati hawa wa vikundi wananunua Shilingi 8,00 na ninaishukuru Serikali kwa kuleta soko huria'' alisema Mkulima huyo.


Mkulima mwingine mkazi wa kata ya Igamba Moses Shela na Yangson Shitindi waliitetea kampuni hiyo na kwamba hata utaratibu wa kujiunga na vikundi hivyo vya wakulima kuna urasimu ambapo wenye vipato vikubwa ndiyo wanaruhusiwa kujiunga na vikundi hivyo.


Akijibu hoja za wajumbe hao kwa ujumla, Naibu Waziri alisema Serikali isingeweza kutoa majibu ya moja kwa moja bali itayafanyia kazi maoni ya wadau wote na baadaye itatoa majawabu.


''Ndugu zangu mawazo yenu yamenisaidia sana kujua hali iliyopo na siwezi kutoa majibu sasa bali yote nimeyachukua Serikali itatoa majibu hapo baadae na ushauri wa kuunda kikosi kazi kuchunguza nao nimeuchukua'' alisema Naibu Waziri Chiza.


Mwisho.
KALULUNGA MEDIA, SAUTI YA WASIOSIKIKA.: Serikali lawama kuhujumu kilimo cha kahawa Mbozi.

Wanunuzi wa kahawa wawajia juu wabunge

IJUMAA, JUNI 29, 2012 05:56 NA UPENDO MOSHA, MOSHI

CHAMA cha Wanunuzi wa Kahawa Tanzania (TCBA), kimewajia juu wabunge wanaomshinikiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, atangaze kupiga marufuku ununuzi wa kahawa mbivu.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Eric Ng'maryo, aliwaambia waandishi wa habari mjini Moshi jana kuwa, Waziri Mkuu anapaswa kushauriwa vizuri na wasaidizi wake, kwa vile kutoa tamko kama hilo ni kinyume cha sheria.

"Nimefuatilia kwa karibu hoja zilizoibuliwa bungeni na waheshimiwa wabunge wawili kutoka mkoa wa Mbeya, lakini namsihi Waziri Mkuu kuwa suala hilo liangaliwe kisheria na si kisiasa," alisema Ng'maryo.

Kwa mujibu wa Ng'maro, biashara ya kahawa nchini inatawaliwa na Sheria ya Tasnia ya Kahawa ya Mwaka 2001 na kanuni zake, hivyo kama zinatakiwa kutenguliwa, lazima utaratibu ufuatwe.

"Kanuni za biashara ya kahawa mbivu, iliridhiwa na wadau wa kahawa katika mkutano uliofanyika Morogoro, Aprili mwaka huu na hii ndio jukwaa sahihi la maamuzi," alisema.

Alisema uamuzi wa wadau ambao ni pamoja na wanunuzi binafsi, wakulima wadogo na wakubwa na wasafirishaji nje ya nchi, ndio unaompa nguvu ya kisheria Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, kutunga kanuni.

Alisema uamuzi wa wadau wa kutaka kuendelea kwa biashara ya kahawa mbivu, ulitungiwa kanuni na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na kanuni hizo, zilipata nguvu ya kisheria Mei 25, mwaka huu.

Alisema kanuni hizo, zilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwa G.N namba 187 la Mei, 25 na kuhoji "Waziri anahusikaje na kanuni hizi…haya ni makubaliano ya wadau, tusipotoshe umma".

Kuhusu suala la ununuzi wa kahawa mbivu kuwa linamnyonya mkulima, Ng'maryo alisema hiyo ni dhana potofu na propaganda chafu ili kuua ushindani wa kibiashara mkoani Mbeya.

"Ili kupata kilo moja ya kahawa ya maganda, utahitaji kilo tano za kahawa mbivu na kama kilo moja ya kahawa mbivu ni Sh 1,000, kilo tano itakuwa Sh 5,000, mkulima ananyonywaje?" alihoji.

Aliwataka wanaopotosha suala hilo kutokana na maslahi binafsi, waache kuwayumbisha wakulima ambao ndiyo wenye uamuzi wa wapi wakauze kahawa yao.

Wakichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu unaoendelea bungeni, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na wa Rungwe Magharibi, David Mwakyusa (CCM), walipinga biashara hiyo.

Wanunuzi wa kahawa wawajia juu wabunge
GODFREY ZAMBI AINGIA MATATANI



MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI, GODFREY ZAMBI (CCM), AMEINGIA MATATANI BAADA YA KAMPUNI MOJA YA UNUNUZI WA KAHAWA KUMSHTAKI MAHAKAMANI IKIMDAI FIDIA YA SH2.4 BILIONI.
KWA MUJIBU WA HATI YA MADAI ILIYOWASILISHWA KORTINI NA MKURUGENZI NA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA LIMA LTD, ERIC NG'MARYO, ZAMBI AMEWASABABISHIA HASARA YA SH1.8 BILIONI KUTOKANA NA MATAMSHI YA KUIKASHIFU.
"MDAIWA AMEANZISHA KAMPENI ZA KUCHAFUA KAMPUNI YETU ILI KUUA USHINDANI ILI VIKUNDI VYA WAKULIMA ANAVYODAI KUVIWAKILISHA VISIWEZE KUPATA USHINDANI," AMEDAI NG'MARYO.
MSINGI WA KESI HIYO NI MAKALA YALIYOCHAPWA KATIKA GAZETI MOJA CHINI YA KICHWA CHA HABARI "MBUNGE CCM APINGA UTEUZI WA JK".
KATIKA MAKALA HAYO, ZAMBI AMEKARIRIWA AKIPINGA UTEUZI WA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA KAHAWA TANZANIA (TCB), DK EVE HAWA SINARE NA BAADHI YA WAJUMBE WA BODI HIYO. NG'MARYO PIA NI MMOJA WA WAJUMBE WA BODI HIYO YA WAKURUGENZI.
KUPITIA TAARIFA HIYO, MBUNGE HUYO ANADAIWA KUITUHUMU KAMPUNI YA LIMA LTD YENYE MAKAO YAKE MJINI MOSHI KUSHAWISHI WAKULIMA KUUZA KAHAWA MBIVU KWA BEI NDOGO.
"UHALISIA NA TAFSIRI YA KAWAIDA YA KAULI HIYO YA ZAMBI NI KWAMBA LIMA LTD NI WALANGUZI WANAOPATA FAIDA KUBWA KWA KUWANYONYA WAKULIMA WA KAHAWA," AMELALAMIKA NG'MARYO.
KATIKA KUTHIBITISHA UHALALI WA FIDIA HIYO, KAMPUNI YA LIMA LTD ITAEGEMEA USHAHIDI KUWA ZAMBI NI MBUNGE ANAYETUMIA NAFASI YAKE KUANZISHA VITA BINAFSI NA KAMPUNI HIYO.
"ZAMBI NI MBUNGE WA BUNGE LA JAMHURI, LAKINI ANAFANYA MAMBO KINYUME NA SHERIA ZA NCHI ANAZOPASWA KUZILINDA ZIKIWAMO KANUNI ZINAZOSIMAMIA SEKTA YA KAHAWA," AMEDAI.
KAMPUNI HIYO INAIOMBA MAHAKAMA KUMWAMURU MBUNGE HUYO AWALIPE SH2.4 BILIONI, KAMA FIDIA NA IWE FUNDISHO KWA WENGINE.
PIA KAMPUNI HIYO INAIOMBA MAHAKAMA KUU KUTOA ZUIO DHIDI YA MBUNGE HUYO KUENDELEA KUCHAPISHA TAARIFA ZA KUIKASHIFU KAMPUNI HIYO.
ZAMBI ALIPOULIZWA ALISEMA HAJAPATA TAARIFA YA KUSHTAKIWA, LAKINI KAMA ATAARIFIWA RASMI NA MAHAKAMA, ATAKAA NA WANASHERIA WAKE KUJUA NINI CHA KUFANYA.
KESI HIYO ILIYOFUNGULIWA JUMATAN

ZAMBI amewahi kuandikwa sana hapa JF:
Baada ya kuona jina la Zambi katika list ya majina yanayopigiwa chapuo juu ya uwaziri, ilinibidi nifanye ufuatiliaji kidogo kwa wenyeji wa hapa Mbozi kwa kuwa nipo huku. Na majibu niliyopata ni kama haya:

Godfrey Zambi hatakiwi Mbozi kwa taarifa yako. Huyu jamaa ni corrupt sana
tofauti na anavyojitambulisha bungeni. Zambi hupata ubunge kwa rushwa ya kusaidiwa na wafanyabiashara Wakinga wa Vwawa na Mloo. Wafanyabiashara hao humsaidia kwa imani kuwa atalinda interest za wakaazi wa Mbozi ambao si Wanyiha.

Na politics zinekuwa hivyo tangu wakati wa mbunge Halinga, ambaye hapo nyuma alionekana kuwanyanyasa wakaazi wa Mbozi ambao si Wanyiha. Zambi ndiye amekuwa kimbilio la hawa wakaazi kwa matumaini ya ulinzi.

Nakuhakikishia akipewa uwaziri yataanza kuibuka madudu ya rushwa yakitokea Mbozi mashariki. We subiri tu. Sana sana tukio hilo litamuongezea kijana Mwampamba wa chadema nguvu zaidi ya kushinda 2015. Nipo hapa.

My take: Sehemu kubwa ya wabunge wa CCM wanaojifanya kupiga kelele bungeni ni wanafiki. Kama Zambi anashinda kwa rushwa anawezaje kusimama kuipinga rushwa kwa dhati? Huyu akipewa kitu kidogo si anafunga mdomo au hata kugeuza mwelekeo kabisa? Na akipewa uwaziri je, anawezaje kujitenga na wizi na dhuluma ilhali na yeye ni uzao wa dhuluma?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/258033-godfrey-zambi-katika-sura-mbili-ya-bungeni-na-ya-jimboni.html

Huyu ndioZambi na Serikali ya CCM:
[h=1]Bungeni Dodoma . Mh.Godfrey Zambi akizungumzia swala la kuuzwa kwa UDA[/h]

http://www.youtube.com/watch?v=w2UuyKbd7M4
 
Aliakim Simpasa- alinyanyasa sana waandishi wa habari na wabunge wenzie kama Mrema sasa hivi hukaa IFM kijiwe cha kupiga rangi viatuakijidai anapiga kiwi kumbe anaangalia watu wanaoingia steers restraurant awakimbilie akawadowelee, ameoigika ile mbayaaaa
 
Hivi karibuni nakumbuka alikuwa na hoja ya mbolea ya MINJINGU na usambazaji wa pembejeo Kwa mfumo fulani nadhani wa VOUCHER kama sikosei. Akisema wakulima hawaitaki mbolea ya MINJINGU. Je, atasimamia usitishwaji wa usambazaji wa mbolea hiyo? Nachelea kusema, mtoto kalilia wembe na huenda mkuu kaamua kumnunulia GILETTE imkate kabisa. Tusubiri.
 
Ndie huyo aliejifanya kinara wa kuwashawishi wana Mbozi wamchukie Waziri wa Kilimo Christopher Chiza baada ya Maghembe. Ndie aliekuwa mwiba wa Mhe. Waziri Mkuu kwenye utekelezaji wa Ilani ya CCM hususan Sera ya Kilimo, leo kakabidhiwa funguo ya kabati ajichagulie nguo za kuvaa.
Kama haikuwa kumkomoa basi wamempatia alichotaka. Tunatarajia aimarishe kelele kama sio kuisaidia Serikalu ya Chama chake kuleta yale ambayo wenzake alidhani wameshindwa.


Hivi karibuni nakumbuka alikuwa na hoja ya mbolea ya MINJINGU na usambazaji wa pembejeo Kwa mfumo fulani nadhani wa VOUCHER kama sikosei. Akisema wakulima hawaitaki mbolea ya MINJINGU. Je, atasimamia usitishwaji wa usambazaji wa mbolea hiyo? Nachelea kusema, mtoto kalilia wembe na huenda mkuu kaamua kumnunulia GILETTE imkate kabisa. Tusubiri.
 
Back
Top Bottom