Wakuu nimekuwa nikisikia neno hili changudoa na kujiuliza nini hasa chanzo cha hawa ndugu kujiingiza na tabia changu aifanyao?wakati mwingine nimekuwa nikijiuliza kuwa hii biashara ni wadada maskini au ambao hawajasoma au laah.Mpaka hivi ninavyoandika hii hoja sijapata jibu.
ukienda casino,Jolly Club,maisha club,club ambience kwa ufupi tu japo zipo kumbi nyingi ambazo unaweza kutana na hao wadada achilia mbali kwa mama cheni na kinondoni makaburini,temeke na mahosetli mengi (hostel ya Buguruni,mabibo Hostel kwa ufupi tu.
Wakuu nini hasa kinachopelekea dada yangu mkubwa kujiuza?ni kweli nikutafuta kipato au ni hulka?nikufuata mkumboa au ni sifa za kijinga?
kama nikutafuta kipato mbona wenye kazi zao utawakuta wapo kwenye biashara hiyo?
Na kama ni ukosefu wa elimu mbona walioko vyuoni ndo wanaongoza jahazi?
reference hall three,mabibo hostel,mzumbe,St gasper Mwanza tumaini university?
wakuu nisaidieni maake imekuwa kero na tabia hii ya ndugu zangu.
Binafsi, naona ni tatizo linalohusu jinsia zote mbili. Kenye social anthropology nilijifunza, mfano, kwamba kwa kawaida inaonekana mwanamme ndiye anayechagua amwoe nani lakini ukweli ni kwamba ni mwanamke ndiye anayechagua aoelewe na mwanamme gani.
Hii inaonekana hata kwa hao tunaowaita machangudoa. On the surface, inaokana ni wao wanaojiuliza lakini 'behind that' kuna wanaume wanaotaka 'behaviour' hiyo wanayoifanya na ndiyo maana wao wanafanya hivyo. Kwa maneno mengine, wanakidhi mahitaji ya soko. Kwa hiyo, ni soko (wanaume) ndilo linalowafanya wawe hivyo.
Hao wanaume wakitaka vinginevyo, mfano, watu wenye heshima, hakutakuwa na machangudoa tena. If I have to blame anybody, ni wanaume wenyewe!