Nimeamua kuachana na mwanamke wangu sababu ni mazoea na wanaume

martial jb

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
864
1,456
Habari wakuu,

Ni mwezi wa tatu sasa nipo kwenye uhusiano na binti mmoja niliekutana nae chuoni. Ni binti fulani hivi wa kawaida kimuonekana kutoka mkoa X niliekutana nae Dar es salaam kimasomo, kiukweli tulikuwa tukipendana licha ya kuwa na migogoro ya kila kukicha.

Migogoro hii ilisababishwa na wivu wa mapenzi nilionao juu ya mpenzi wangu huyo hali kadhalika tabia aliyonayo ya mazoea na wanaume pia. Ni msichana ambae hupenda kujichatisha kwa wanaume na kujichekesha kwao kitu ambacho kinapelekea mara nyingi kutengeneza mazingira kwa wanaume hao kumtongoza. Ni mwepesi wa kugawa namba kwa wanaume na mtu mwenye marafiki wengi wa kiume.

Binti huyu ni mkorofi pale ninaposhika simu yake na kutaka kukagua japokuwa mara kadhaa nimekuwa nikimruhusu kutumia na kukagua simu yangu na amekuwa akikataa kabisa kufanya hivyo.

Jambo lililonichanganya ni hivi karibuni amekuwa akinitambulisha dereva bajaji mmoja kuwa ni kaka yake wa nyumbani kwao( rafiki wa kaka yake), na kuwa na ukaribu nae sana. Amekuwa akitolewa out na kaka yake huyo, amekuwa akichati nae mara kwa mara na kaka yake huyo, amekuwa akimuongelea pia pindi tunapokuwa wawili, na mwisho kabisa aliniambia kuwa amempa kaka yake huyo nguo ili amtunzie ili akiondoka asindikizwe nae. Na mara nyingi hutumia dakika nyingi akiongea pale wanapokutana.

Binafsi me ni mtu mzima, na wanawake nawafahamu sana. Na pindi panapokuwa na udanganyifu nafahamu piaa. Nimeamua kuchukua maamuzi ya kutemana nae kwa ajili ya Elimu yangu, Afya yangu, Uchumi wangu boom langu na mengine.

Ni changamoto sana kudate na mwanamke mwenye mazoea na wanaume amini usiamini iwe wanakula mzigo au hawali jua tu ni Changamoto sana.

Sioni faida ya mahusiano pasipokuwa na uaminifu na mapenzi ya dhati. Naumia kichwa sana kuona wanawake hawaridhiki kwa any commitment ya mwanaume anapojitolea. Kiukweli inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom