huyu jamaa alikuwa anaongiza humu sasa hivi kimyaa anamshangilia john!Kuna Radio ziliwahi fungiwa kwa mijadala ya aina hii, haya tuendelee.
Hivi sisi wasabato tunapo amrishwa kufanya usafi siku ya jumamosi ni sahihi? Au kwa kuwa hatuna wa kutusemea? Au mnataka kutupima imani? Najua enzi zile tungeandamana lakini duhh, mtupe pole hapa wanataka kutupima imani zetu?
Ibada huwa na heshma yake na siku yake, sie kwetu Jumamosi ndio siku yetu kwa mujibu wa imani yetu kama zilivyo itikadi nyinginezo.Haya ni matatizo yenu - kwani mkisali Jumapili Mungu hasikilizi maombi yenu. Ua mnadhani kuwa Mungu analala Jumapili? Mbona wengine wanasali Ijumaa - tena siku ya kazi! lakini wapo Kimya!
Mchakato wa katiba mpya lilikuwa ni dili la wapigaji tu!!!
Si kwa unafiki huu aisee! Hatari sana, hata vyama vya upinzani huwa vinapata nguvu kama raisi ni wa dini.... , akishaondoka wapinzani na CCM wote wanakuwa kitu kimoja kuna watu kibao sasa hivi wamerudi CCM kimyakimya na kumsapoti raisi Joni, akishamaliza muda wake akaja ile imani nyingine wanakuwa wapinzani tena, so upinzani unakuwa na maandamano yanaanza tena
Mimi mwenyewe muislamu ila muislamu aliepita alikua ameifikisha pabaya kijiji chetuPengine hatokuja atokee JK mwingine kwa ubora, pamoja na figisu zote zile Mzee aliendelea kutabasamu... Sipatii picha Dr. Slaa angekuwa amefikisha 40% kama aliyopata Mamvi TZ isingetawalika. Ila kwa kuwa 2015 walikuwa WAO peke yao hata matokeo yangekuwa 51-49 kusingekuwa na shida:::::::: wanafiki sana watu hawa
Dah! eti kila mfanyakazi was serikari bosi wake atakuwa MACCM, ni kaulu ya magufuli"Sisi kama CCM, kwa wingi wetu tunashindwa kuishauri Serikali kwa mambo ya ukweli, hatuna sababu ya kubaki kuwa madarakani".
Mhe. Hussein Bashe (MB).
Huyu jamaa nimemvulia kofia natamani CCM ingekuwa na Wabunge wengi na hata Viongozi wa juu wa CCM wenye mtazamo kama wa huyu lakini kwa MACCM wengi chama kwanza na nchi baadaye na hii inaigharimu sana nchi yetu na hivyo kukosa maendeleo ya kweli kwa miaka chungu nzima sasa pamoja na utajiri mkubwa tuliokuwa nao.
Ndugu yangu Pohamba jaribu kufafauna, maana nimejaribu kusoma kwa makini na kurudia lakini bado sijakupata kabisa.SOTE tunapaswa kuamini tatizo la sukari limetokana na 'wafanyabiashara wasio waaminifu kuficha sukari.' Ingekuwa wakati wa Jakaya lingekuwa limetokana na udhaifu wa Serikali kukurupuka na kuzuia sukari kutoka nje bila ya kufanya tathmini ya Mahitaji na upatikanaji wa sukari.Kuongoza Nchi ukiwa Rais 'Dhaifu' ni kazi ngumu sana
Siasa zetu ni nzuri sana kwa kuwa huhitaji Degree ya Political science kuwajua Wanafiki
Ukimsoma padri John C Sivalon kwenye kitabu chake KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA utaelewa sana kwanini kiongozi yeyote muislamu lazima apigwe vita. Wakati wa nyerere hakuwahi kuandikiwa barua za kichungaji kumlaumu. Kaja Mwinyi kaandikiwa barua za kumlaumu za kichungaji zaidi ya 13. Huku yeye na familia yake wakitukanwa kuwa wezi wa mali ya umma. Jengo lolote zuri tuliimbiwa kuwa ni la mama Sity Mwinyi.Napenda nyinyi wasema ukweli!