Sio kweli kuwa Wananchi hawajui katiba bali ni mbinu za CCM kuchelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Inashangaza na kuchukiza kusikia Eti Wananchi wa Nchi hii Hawaijui KATIBA ya NCHI yao.

Wenye AKILI KUBWA TULISEMA Mapema kuwa CCM haitaki WATANZANIA wapate KATIBA MPYA .Dalili za KUKATAA zilianza Wakati wa BUNGE la KATIBA Yaliyompata Mwenyekiti wa TUME ya KATIBA Mh JAJI WARIOBA na Wajumbe wake wote tunajua.

Kama mnakumbuka CCM iliweka Ajenda ya Katiba Mpya katika ILANI yake ya UCHAGUZI wa 2025 Lakini HAYATI MAGUFULI alipopata URAIS alisema hana BAJETI na pia Sio KIPAU mbele cha CCM.

Rais Samia nae alipoingia Madarakani badala ya kuendeleza ULE MCHAKATO uliotumia MABILIONI ya Fedha ambazo ni KODI za Wanyonge yeye akaamua kuturudisha Nyuma kabisa kwa KUUNDA KIKOSI KAZI ETI cha kukusanya Maoni ya baadhi ya Watu mashuhuru badala ya Wananchi wote ambao ndio wenye KATIBA YAO huo nao ni UCHELEWESHAJI.

Leo RAIS SAMIA anadai ETI Wananchi hawaijui KATIBA wanatakiwa Wapatiwe ELIMU ya KATIBA kwa Miaka 3 jambo ambalo wenye AKILI KUBWA tunajua ni KUTOKUWA Tayari kwa CCM kuwapatia WANANCHI KATIBA
YAO.

TUME ya Jaji WARIOBA ilizunguka NCHI ZIMA kutoa Elimu ya KATIBA na kugawa Nakala za KATIBA na Vipeperusha kwa Wananchi wote iweje leo tunaambiwa eti Wananchi hawana ELIMU ya KATIBA?

Ukweli usemwe CCM HAITAKI KATIBA MPYA
 
Mwananchi siyo lazima aijuwe katiba kufahamu kwamba ni mbovu.

Matokeo yake yakiwa mabovu, wananchi tayari wanafahamu.

Wananchi wanachotaka ni muongozo. Wanafahamu katiba iliyoko ni mbovu.

Hata Masai wa loliondo anaweza asijuwe hata kusoma na kuandika lakini akafahamu kuwa katiba hii tuliyonayo ni mbovu.

Pia tume ya jaji Warioba ilishafanya kazi yake kwa kuchukua maoni ya wananchi.

Inaudhi sana.
 
Mwache Rais mpaka Amalize awamu yake ya pili, akiruhusu katiba simtamnyongelea mbali wakati kiti kitamu😁😁
 
Wajinga wanafanya wananchi hawana akili.

Hivi waliotunga katiba ya mwanzo walifundishwa kwanza kuijua katiba ipi ndipo wakatengeneza katiba yao ya mwanzo?

Hii ni sawa na mtu uone kitamda chako cha awali ni hovyo kwa kuwa kinakuumiza mbavu, kisha useme kuwa unahitaji kununua kitanda kizuri kipya, halafu aje mwendawazimu mmoja akuambie kuwa hutakiwi kununua kitanda kipya, kwanza nikufundishe kuhusu ubora wa kitanda chako hiki cha zamani.
 
Huyu mama alipokuwa anaambiwa unaupiga mwingi aliamini anaongoza vizuri nchi na anapendwa sana na wananchi ndiyo maana akajichomeka kwenye issue ya kuunda katiba mpya.

Amestuka Sasa kuwa katiba mpya ikiundwa na tume huru ikapatikana atakuwa hana chake. Sasa ameamua kutafuta mlango wa kutokea kwenye hii issue ya katiba
 
Miaka 3 kujua katiba sawa na degree!

Siku chache sana hata masaa 3 yanaweza kutosha kumwelewesha mwananchi kwa nini tunahitaji katiba bora na madhara ya kutokuwa nayo
 
Mimi ninaamini elimu imekuwa ikitolewa na vyombo mbalimbali kiaina kwenye mijadala,malumbano, majibizano, na mawanda ya majukwaa ya kisiasa kwa kuirejea katiba maramara. na hususani kwenye matukio ya nchi,tunasikia NGO zinahusisha suala la Ngorongoro, DP World,Ufisadi,Rushwa, majukumu ya wananchi na katiba iliyopo, na mapungufu haki za wananchi, na hata kwenye mawanda ya siku mahakamani na vyombo vya usalama,mashirika ya dini kwenye nyaraka mbalimbali,hotuba za Rais na Mawaziri.

Katiba ni suala la maisha ya kila siku katika kusaka haki za ardhi,afya,elimu, mahitaji uchumi, biashara,kuchagua viongozi, kilimo, ufugaji,kulipa kodi na wajibu wa kutii sheria na mipaka ya haki hizo,madaraka ya Rais,kuruhusu mikutano,maoni mbadala,uwepo wa magazeti vimechangia sana.

Hivi vyote vinawafanya wananchi waijue katiba kama Taifa na mtu mmoja mmoja (automatically)kivitendo ingawa inaweza ikawa siyo katika sura ya kitaaluma(academically)kama wengine wanavyotaka iwe, bali katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Na hilo ni mwanzo mzuri kuwaelemisha kuhusu katiba mpya
 
Ni nchi Moja afrika inayotazamwa bado ikijaribu kushika madaraka kwa nguvu kwa kisingizio Cha kubadilisha maraisi ambao ni ccm.
 
Back
Top Bottom