Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,231
- 113,591
Point yako kwamba historia huandikwa na mshindi ina reinforce ukweli kwamba notion hii ya kwamba mweusi ni inferior kwa mweupe si ya kweli, kwa sababu majority ya historia ina m potray mweuis kama inferior.Ni siku za karibuni tu ndipo watu wameanza kuandika historia objective inayoweza kuwa tested na branches nyingine za knowledge kama anthropology na archaeology.
I guess hapo kwa kiasi fulani tuko pamoja, au?
Mazingira ninayozungumzia ni shida.
Kama shida mbona tunazo lukuki tu na wala hazijaanza juzi, jana, wala leo. Zipo siku zote na zitaendelea kuwepo.
Shida inafundisha ubunifu.
Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na huu usemi kwani hata mimi ktk maisha yangu mafupi hapa duniani nimewahi kujikuta naibuka na mawazo ambayo yalinishangaza hata mimi mwenyewe pale nilipokumbwa na matatizo.
Afrika hatukuwa na shida sana (baridi, kipindi kifupi cha kulima etc) kwa hiyo hatukuwa na haja ya kwenda mbali kutafuta biashara, chakula na makoloni.
Unasema Afrika hatukuwa na shida kama vile sasa ndiyo tuna shida zaidi kuliko zamani. What the hell? Mbona sasa tunaona haja ya kwenda mbali kutafuta maisha na mengineyo? Watu tunalowea nchi za watu. Wengine wanalowea na kwenda huko kuishi kwa kubahatisha hadi wanashindwa hata kurudi kwao wanapofiwa na wapendwa wao. Sasa ni nini kinachowapeleka huko kama sio shida za huko watokako?
Wazungu walikuwa na shida, wakajua ukatili na uchumi mapema kuliko sisi, wakajua kwenda mbali kutafuta biashara na makoloni kabla yetu. Wakajua ukatili kuliko sisi, sisi tulikuwa good natured na overly trusting.
Unataka kuniambia joto la Afrika sio shida. Hebu nenda huko Bamako ukakung'utwe na jua na joto ndio utatambua kumbe hata joto nalo ni shida inayosababisha discomfort vilevile. Kwa nini Waafrika wa huko hawakuvumbua viyoyozi?
Na kama hayo mazingira ndio yalisababisha maendeleo ya wazungu na kwa vile mazingira yetu sisi (Waafrika) hayakuleta shida sana basi sisi tulie tu kwa sababu sidhani kama mazingira yetu yamebadilika sana na yalivyokuwa enzi hizo. Bado tuna hali nzuri ya hewa na kadhalika. Kwa hiyo hatuna shida za kutosha kuchochea ubunifu wetu. Hii hoja ni kichekesho kweli.
Winston Churchill alivyofika Entebbe Uganda, akaona jinsi nchi ilivyokuwa ya kijani kutokana na uzao uliostawi, nchi ilivyokuwa imeneemeka kwa sababu ya kupata lake effect rains za kutosha throughout the year, in his typical non politically correct maner alisema - paraphrasing- hawa watu bahati yao mbaya pekee ni kwamba wana bahati nzuri sana, kwamba wamebarikiwa mpaka hii baraka inakuwa inawafanya wabweteke sasa.
In other words I think Churchill was saying look at these negroes. They don't know any better coz they don't even realize what they have.
I have to agree.Huu ndio mzizi wa matatizo yetu, hakuna kitu genetic, ni mazingira tu. Kwa nini utake kwenda ku colonize nchi nyingine wakati kila kitu kipo nchini mwako?
Kila kitu kipo lakini hujui hata ukifanyie nini. Tatizo la nani hapo kama sio wewe mwenyewe (not you personally but I'm just speaking in general) na ujinga wako. Yaani mpaka aje mtu wa kutoka mbaaaaali ndo akuambie kuwa una hiki na kile cha thamani. Umeshindwa kutambua mwenyewe kwa akili yako? I'm sorry..something is wrong with that picture.
Huko Egypt wakati huo ndio kwanza watu wa Afrika walikuwa wanaanza kuchanganyika na watu wa the crescent region na southern Europe.Teknolojia ya Egypt ilitoka kusini, hata wa Egypt wenyewe katika ramani zao "kaskazini" yao ni kusini, upper Egypt ni southern Egypt na Sudan, lower Egypt ni northern Egypt, mindset yao ilikuwa oriented kuangalia Africa, si ulaya, kwa sababu walijua civilization yao ndipo ilipotokea.
Ustaarabu wao ulitokea Afrika? Una maana gani? Kwani Egypt sio Afrika?
Wagiriki walikuwa na vyombo vya usafiri, walikuja kwa sababu walitaka elimu na Egypt ndipo palipokuwa na makao makuu ya elimu dunia nzima.
Hivyo vyombo vya usafiri vilidondoshwa kutoka mbinguni au waliviunda wao wenyewe kwa kutumia ubunifu wao? Na unasema walikwenda Egypt kwa sababu walitaka elimu. Unajua inahitaji akili ya kiwango fulani kutambua ubora wa kitu fulani. Kwa hiyo walitambua kuwa ujuzi walio nao wao hautoshi na wakaona ni bora watembee wajionee na wajifunze. Nawaongeza kwa hilo. Kwa nini Wahehe au Waluguru hawakuunda mitumbwi au majahazi ya kwendea huyo Egypt ili na wao wakaelimike zaidi?
By the way wa Egypt nao walikuwa wanatengeneza vyombo vya kusafiri katika mto Nile na bahari ya Sham, waliweza kufanya biashara na nchi zilizokuwa kusini further into Africa kwani waliona huko ulaya ni kwa ma barbarian tu hakuna deal. there was a PBS Nova special on this a few weeks ago on Egyptian shipbuilding, kwa hiyo kama ulitaka ku imply kwamba wao hawakujua kutengeneza vyombo vya kusafiri hii si kweli.
Halafu mbona case in point ni Egypt tu? Hakuna kwingine?