Hivi kweli mama zetu ndio wawe watunzaji wa mali zetu? Mnawajua mama zetu walivyo?

Wamama wa bongo utakuta amegawia wadogo zako, wajomba zako, majirani, wajukuu. Labda uwe mtoto pekee! Na hapo uhakikishe ameandika kabisa wosia na kukupa umiliki wa hizo mali ikitokea akafariki kabla yako. msije kuiga, mtakuja kulia humu. Wamama wengi hata ukimkopesha usitegemee sana kulipwa. (Sio wote lakini)
 
Hujanielewa...!! Nimesema hivi, mkeo naye ni mama kwa watoto wako. Anzia hapo
Mimi nimekuelewa sana, na ndio nimekupa jibu hapo.
Mke wangu kwa sababu ananifaa sana mimi kama life partiner katika michongo ya maisha yangu binafsi niliyojipangia haina maana atawafaa watoto wangu katika michongo ya maisha yao na wakikuwa wakubwa.

Kuna kitu kinaitwai Zama (Nyakati), Interest, Personality, Mazingira na Malengo (Vision&Mision) hizo ndio ziliamua mtu aoe mtu wa namna gani, na hizo vitu ndio zinatofautisha kati ya ndoa ya babu yako, baba yako, wewe na watoto wako. Mke wangu ananifaa mimi tu kimaisha, watu wengine sio lazima awafae.
 
Wamama wa pwani wengi ni mashangingi tuu ,malaya na mambo mengi ya hovyo hovyo
Kwa hiyo wale wamama wa kule kaskazini wanaovuka boda kwenda kupigwa miti kule Kenya ni watakatifu?

Ama wale mama wa kule Arusha wanatafuna mrungi na kutupia konyaji kama maji ndio wapambanaji?
 
Wa mama wa pwani.

Wa mama wa kiislam

Wana tofauti kubwa na wamama wa bara na wamama wa kikristo.

Wamama wa pwani elimu dunia ama elimu ya kusimamia fedha na mali huwa hawafundishwi na jamii zao. ( dini ya kiislam na utamaduni wa pwani haumfundishi mwanamke mambo ya mali na pesa )

Wamama wa bara hata kama hawajaenda darasani..ila wanafundishwa elimu ya kusimamia fedha na mali kutoka kwa wakubwa zao.
Tusahau kuhusu wanawake wa kule Kaskazini (ambao kiasi ni wajanja katika kumiliki mali).

Ndugu unaposema bara unamaanisha pia Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Mara?
Nadhani ulimaanisha pia wamama wa vijijini?

Sasa pita hayo maeneo halafu nenda katazame ni mama zetu wangapi.
1. Walifanikiwa kusoma na kufika hata kidato cha nne.
2. Hawaamini kwenye ushirikina
3. Hawatumikishwi na waume au jamii zao kama manamba.
4. Waliwahi kumiliki mali binafsi za thamani katika maisha yao kama nyumba, kiwanja, shamba, gari au pesa angalau milioni moja.
5. Wana nguvu ya kimaamuzi katika maisha yao.
6. Wana akili na upeo wa kutafuta, kuzalisha na kutunza mali zao binafsi.

Bora hata wanawake wa pwani, japokuwa hawajatulia lakini wana exposure kubwa kuhusu mali. Sio wajinga au washamba wa kumiliki.
 
Kule kanda ya ziwa wamama wa umri huo ndio wanauwawa kwa Imani za kishirikina au jamii kuwafirisi mali walizorithi kutoka kwa waume zao waliofariki.

Hapo kuna usalama wa kuwamilikisha mali zako?
Jamii gani iwafirisi hacha uongo kila kabila lina tamaduni zake kwenye mirathi mfano kuna kabila Baba akifa Mama ana rithi mali na mfano Baba naama wakifa wanaotakiwa kurithi ni watoto wakiume tu, mtoto wakike harithi mali.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Screenshot_20230415-232739_WhatsApp.jpg
 
Jamii gani iwafirisi hacha uongo kila kabila lina tamaduni zake kwenye mirathi mfano kuna kabila Baba akifa Mama ana rithi mali na mfano Baba naama wakifa wanaotakiwa kurithi ni watoto wakiume tu, mtoto wakike harithi mali.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Sheria ya ndoa ya Tz iko wazi, mume akifa, mali zinabakia chini ya uangalizi wa mke, warithi ni mke na watoto tu.
Sasa nenda kanda ya ziwa ukaone wamama wanavyogeuka kuwa maskini na manamba mara tu waume zao wanapokufa hali walikuwa na mali.

Hivi unadhani ni kwanini, wazee wa kanda ya ziwa hawapendelei na hawataki vijana wao wakaoe Kaskazini (ususani Kilimanjaro)?
Kule Kilimanjaro, mume akifa, mara moja anachukua control ya mali zote walizochuma na muwewe, ndugu hagusi wala kuambulia hata kijiko.
 
Usisahau, mkeo naye ni mama kwa watoto wako..!! Kama wewe umemuamini ukamuandika kama mkeo, una hofu ipi mtu huyo huyo aliandikwa kama mama na watoto wako..!??
Awasomeshe na wao watamwandikisha Mama yao halafu yeye mamai yake atakuwa mzee au hayupo kabisa ndiyo atakumbuka
 
Wamama wa bongo utakuta amegawia wadogo zako, wajomba zako, majirani, wajukuu. Labda uwe mtoto pekee! Na hapo uhakikishe ameandika kabisa wosia na kukupa umiliki wa hizo mali ikitokea akafariki kabla yako. msije kuiga, mtakuja kulia humu. Wamama wengi hata ukimkopesha usitegemee sana kulipwa. (Sio wote lakini)
Wewe subili utasikia watu wanajitundika kila mahala baada ya kukuta Mama naye analea katoto ka watu kaserengeti kwa raha zake.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mama yako na mkeo.
Kwa haraka sana, mama yako ni mtu aliyekuzaa na kukulea, hakuna kitu kingine alichonacho cha zaidi. Unapaswa kumpenda, kumtunza na kumheshimu. Lakini mtu huyo (mama yako) anaweza kuwa mjinga, kichaa, mwizi, malaya, mchawi nk na isiweze kufanya chochote kumkwepa kama mzazi wako. Kiujumla jumla hatoshei kuwa mmiliki wa mali zako.

Mkeo ni mwenzi wako kimaisha (Life Partner), mbia kamili wa maisha yako, mrithi kamili wa mali zako ikiwa leo haupo duniani. Unaamua kumchagua katikati ya wanawake wote waliopo duniani. Kiujumla jumla ni mtu sahihi kuwa mmiliki wa mali zako.
Walishakataa hizo sifa unazowapa wanawake sasa unataka wanaume tujilazimishe. Mwanamke amefika hatua ya kusema hamuitaji mwanaume maishani mwake, nikuulize kwanini unatusumbua sisi kujipendekeza kwawatu wasiotuhitaji. Muache mtoto wa kiume naye afanye yake maana mlimuachia mtoto wa kike mpaka sasa hashikiki. Yawanaume waachie wanaume hayakuhusu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari yenyewe ya kutunga tu Wala Haina ukweli. Nyie mna komaa na Hakimi Huku mwenzenu kalipa kichwa na mkewe huko
 
Mfano hakimi angezitunza mwenyewe kwa jina lake sasa hivi tungekuwa tunamcheka, sajili hata kikampuni cha mchongo na uandike nyumba magari na viwanja ni vya kampuni leo na kesho mwenzio akibadilika unamwambia mm sina kitu nyumba magari yote nimepewa na kampuni
Kiujumla mleta uzi ana wivu ambao hauna maana
 
Wamama wa bongo utakuta amegawia wadogo zako, wajomba zako, majirani, wajukuu. Labda uwe mtoto pekee! Na hapo uhakikishe ameandika kabisa wosia na kukupa umiliki wa hizo mali ikitokea akafariki kabla yako. msije kuiga, mtakuja kulia humu. Wamama wengi hata ukimkopesha usitegemee sana kulipwa. (Sio wote lakini)
Sasa kwa akili zako unategemea kulipwa na mama embu fikiria mtu amekubali kukubeba miezi 9+ alafu mtu anakuja kuropoka kwamba mama sio mtu wa kumwachia mali zako
 
Mimi nimekuelewa sana, na ndio nimekupa jibu hapo.
Mke wangu kwa sababu ananifaa sana mimi kama life partiner katika michongo ya maisha yangu binafsi niliyojipangia haina maana atawafaa watoto wangu katika michongo ya maisha yao na wakikuwa wakubwa.

Kuna kitu kinaitwai Zama (Nyakati), Interest, Personality, Mazingira na Malengo (Vision&Mision) hizo ndio ziliamua mtu aoe mtu wa namna gani, na hizo vitu ndio zinatofautisha kati ya ndoa ya babu yako, baba yako, wewe na watoto wako. Mke wangu ananifaa mimi tu kimaisha, watu wengine sio lazima awafae.
Upupu
 
Kisa cha mchezaji wa PSG Achraf Hakimi kuandikisha mali zake kwa jina la mama yake halafu mkewe kuambulia patupu mara baada ya kuachana kimewafanya wanaume wengi kupata muamko wa kutaka kuiga hiyo style. Lakini kuna mambo watu huenda wanasahau kuhusu hawa mama Zetu hususani huku Afrika. Kwa uchache sana nitaweka hapa.

Mama zetu wengi (huenda 90%) wako hivi;
1. Upeo duni wa kutunza na kuendeleza mali. (Kumuachia mali zako ni zaidi ya kucheza kamari)

2. Wako chini ya himaya ya waume zao (waume hao wanaweza kuwa ni baba zetu wa kutuzaa au baba wa kambo)

3. Wanategemewa na familia na koo zao. (Yaani kuna msururu wa ndugu wamekaa wanasubiri kuvuna kwa migongo ya mama zetu).

4. Waumini holela wa imani tofauti tofauti. (Leo unaweza kumkukuta kwa mganga wa kienyeji, kesho kwa Mwaposa, keshokutwa kwa Sharif Majini nk. Kote huko anamwaga pesa).

5. Hawajatulia kabisa (wengi ni single mothers walioshindikana, wadangaji, mijishangazi, walevi, washirikina, wafitini nk)

6. Maisha yao yamezungukwa na kuathiriwa na watu wa ovyo ovyo balaa (hapo kuna majirani, ndugu, jamaa, marafiki, mashosti nk na hao ndio wenye kuamua mtindo wa maisha ya mama zetu hususani mama zetu wakiwa na mali).

Hitimisho langu.
Mtu sahihi wa kumuandikisha umiliki wa mali zako:
-Wa kwanza ni wewe mwenyewe
-Wa pili ni mkeo
-Wa tatu ni mtoto wako wa kumzaa.
Mi namuamini mama yangu kuliko hata ninavyojiamni mwenyewe,

Alafu we sikia kama umeandika huu ujumbe ili kumridhisha mke wako shauri yako..

Lakini pia Kila mtu anajua namna anavoishi na mke wake kwahyo hili ni jukum la mwanaume mwenyewe eidha ajifunze kitu kwa hakimi au laa!

Kiukweli binadam saiv hatuaminiani sio mwanaume Wala mwanamke ukibahatika kuisoma akili ya mwenzio mapema we fanya tu maandalizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom