Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,309
- 35,731
Kisa cha mchezaji wa PSG Achraf Hakimi kuandikisha mali zake kwa jina la mama yake halafu mkewe kuambulia patupu mara baada ya kuachana kimewafanya wanaume wengi kupata muamko wa kutaka kuiga hiyo style. Lakini kuna mambo watu huenda wanasahau kuhusu hawa mama Zetu hususani huku Afrika. Kwa uchache sana nitaweka hapa.
Mama zetu wengi (huenda 90%) wako hivi;
1. Upeo duni wa kutunza na kuendeleza mali. (Kumuachia mali zako ni zaidi ya kucheza kamari)
2. Wako chini ya himaya ya waume zao (waume hao wanaweza kuwa ni baba zetu wa kutuzaa au baba wa kambo)
3. Wanategemewa na familia na koo zao. (Yaani kuna msururu wa ndugu wamekaa wanasubiri kuvuna kwa migongo ya mama zetu).
4. Waumini holela wa imani tofauti tofauti. (Leo unaweza kumkukuta kwa mganga wa kienyeji, kesho kwa Mwaposa, keshokutwa kwa Sharif Majini nk. Kote huko anamwaga pesa).
5. Hawajatulia kabisa (wengi ni single mothers walioshindikana, wadangaji, mijishangazi, walevi, washirikina, wafitini nk)
6. Maisha yao yamezungukwa na kuathiriwa na watu wa ovyo ovyo balaa (hapo kuna majirani, ndugu, jamaa, marafiki, mashosti nk na hao ndio wenye kuamua mtindo wa maisha ya mama zetu hususani mama zetu wakiwa na mali).
Hitimisho langu.
Mtu sahihi wa kumuandikisha umiliki wa mali zako:
-Wa kwanza ni wewe mwenyewe
-Wa pili ni mkeo
-Wa tatu ni mtoto wako wa kumzaa.