Kwa heshima ya mama zetu

Paul dybala

JF-Expert Member
Jul 30, 2023
304
1,096
Poleni na majukumu,

Leo naomba niwakumbushe Wana JamiiForums wenzangu kupitia Uzi huu.

Naomba niwakumbushe juu ya kuzidisha upendo juu ya mama zetu najua mnafahamu Kuna,nyimbo wasanii mbalimbali wamewaimbia mama zetu, siku zipo za kina mama kusherehekea umuhimu wao...Yani mother's day...nawakumbusha kwa sababu binadamu tumeumbiwa kusahau..

Nimetoka kumpoteza mama yangu mwezi uliopita...hii kitu maumivu yake ni makubwa Sana ...licha ya kumpenda Sana Ila Bado naona sikuweza kufanikiwa kufanya kitu kikubwa katika maisha yake ....licha ya kumsapoti Sana Bado najiona Kuna sehemu niliacha kwa sababu nilikuwa naamini Kuna siku ningetoboa nikamchukua nakuishi nae kwenye nyumba ya kifahari lakini kwa mapenzi ya mungu sikufanikiwa kabisa..

Sasa licha ya bi mkubwa kutokuwa na uwezo wa kiuchumi Ila alinipenda Sana ..na gap lake nilianza kuliona siku ileile alipotangulia.

Point yangu Nini hapa ni kwamba vijana wengi tunajitafuta tunaamini msaada ni pale tunapotoa kitu kikubwa tu pesa nyingi au zawadi za magari kitu ambacho Sio sahihi kumbe hata kupiga simu tu inamaana kubwa Sana. Mimi sikuwa mpenzi wa kupiga simu Ila nilipopokea simu yake bhasi kwa mara moja nilisolve matatizo yake ...hapo nashukuru mpka anaondoka hakuwa na tatizo na Mimi.

Kupitia Uzi huu naomba ambao mama zetu tunao tuwapende Sana. Yaani unavompenda saivi zidisha na ambao hatunao tuzidi kuwaombea wapumzike salama.

Ombi langu la mwisho kwa WanajamiiForums wenzangu naomba baada ya kusoma Uzi huu mpigie simu mama yako umsalimie tu, kupitia hio nafasi na Mimi huku nitakuwa nimemuenzi na Imani na yeye anafurahi.
 
Pole sana kwa msiba wa mama brother!

Umeandika yaliyo ya kweli,august mwaka jana workmate wangu aged 51 mvi zimeshamtoka kichwani alifiwa na mama yake mzazi aisee jamaa na utu uzima wake alilia kama mtoto,hata nikajiuliza yeye vile mimi 30+ nitakuwa ktk hali gani?

Hakuna sababu ya kujiuliza kosa lolote mtoto analohisi mama yake alilitenda iwe kwa kujua au kutokujua,kama unaye mama mpende,mtunze muheshimu upo muda utafika utamani kufanya yote hayo umkose,kwa mara nyengine mleta mada pole sana kwa msiba wa mama Mungu Mwenyezi amrehemu.

NB;tusiwasahau na wazee nao bila wao tusingekuwa na mama tunaowathamini leo so wazazi wote wapewe heshima yao inavyostahiki bila kujiuliza uliza.
 
Asante Sana kaka...be blessed
 
Bora yenu nyie mliolelewa na mama zenu mkapata mapenz ya dhati kutoka kwa mama zenu kwenye matatizo bado anakupigania na kukuombea nawaonea wivu sana

Binafs yangu sijalelewa na mama angali nina miaka 4 walipoachana na mzee wang nmekuj kumjua bimkubwa 2012 nishakuwa kijana lkn sion thaman ya kuwa na mama kwasababu najiona km sina mama kwenye hii dunia nipo mm km mm tu yan mtu anakuwa km vile hana tym muda mwingine nachukulia km sina mama NATAMAN NA MM NINGEPATA MAPENZ YA MAMA WAOMBEENI MAISHA MAREFU SANA MAMA ZENU
 
Pole Sana mkuu...we mpende hivohivo
 
Back
Top Bottom