Kimbweka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2009
- 8,597
- 1,683
Habarini wakuu!
Kama mnakumbuka kuna thread moja niliweka " KILA NIKIAMKA" wengi walinipa ushauri wa kuoa haraka kutokana na sababu mbalimbali walizonipa! Nilichukua ushauri wao nami nikaa na GF wangu kipenzi nikamuelezea juu ya mawazo na maamuzi niliyofikia naye akakubaliana nami! GF wangu ni wa kiislam na mimi ni wa christian! Alipeleka mawazo yake kwa wazee ila upande wao hawakuwa tayari kutokana na tofauti za itikadi zetu za kuabudu! ila walipenda mie niingie uislam na tufunge ndoa msikitini na nifuate mafundisho yao! Sasa bado sijafanya maamuzi yeyote juu ya hili ila nina swali " Kumekuwa na hii kitu, Mdada wa kikristo akitaka kuolewa na muislam huwa hamna vipingamizi saaaana na wala hakuna milolongo ya mambo yanayopelekea kutofunga ndoa , ila mdada wa kiislam akitaka kuolewa na mkristo basi panatokea mapingamizi makubwa kiasi kwamba wengine hutofautina na wazazi na pengine hupelekea kufunga ndoa za kiserikali na kukaa pamoja" Hii ni kwa nini inakuwa hivi???? Wadau naomba tujadili kwa kina hasa?!!!