Kwanini ndoa za sasa nyingi zinafungwa na ujauzito, nini shida?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,967
22,161
Nimejaribu kuwaza ndoa za enzi zetu

Hivi majuzi nilihudhuria ndoa 3

Kila ndoa mdada kabakisha kama mwezi kujifungua hii waliweka mpaka na ambulance na nurse ikitokea emergency

Mwingine jumamosi iliopita huyu afadhali kitambi kilikuwa si kikubwa sana

Mwingine huuu dah mpaka nilikuwa naogopa kumwangalia mwili mkubwa na mbele ana exp wiki kadhaa kjjifungua dah

Sijajua nini shida kwani kuolewa lazima mpeane maimba kwanza??

Unajua mtoto n wa Mungu..unaweza zini ukiona Mimbaa unaazimisha ndoa..baada ya ndoa akachukua chake

MUNGU Akusaidie ukaolewe ukiwa safi bila Mimba ukaheshimikee milleleee

Amen
 
Vijana tunaogopa kuuziwa mbuzi Kwenye guniaa maana unakutana na Binti ana miaka 27 Toka akiwa na miaka 18 kashajua aina za d*d* tofauti na hapo kati kashachomoa mimba kama 2 hv .hvyo hakuna budi kijana akikutana naye atest mitambo yake naye ipo au ndio zile mimba Binti alitoa ziliondoka na kizazii
 
Nimejaribu kuwaza ndoa za enzi zetu

Hivi majuzi nilihudhuria ndoa 3

Kila ndoa mdada kabakisha kama mwezi kujifungua hii waliweka mpaka na ambulance na nurse ikitokea emergency

Mwingine jumamosi iliopita huyu afadhali kitambi kilikuwa si kikubwa sana

Mwingine huuu dah mpaka nilikuwa naogopa kumwangalia mwili mkubwa na mbele ana exp wiki kadhaa kjjifungua dah

Sijajua nini shida kwani kuolewa lazima mpeane maimba kwanza??

Unajua mtoto n wa Mungu..unaweza zini ukiona Mimbaa unaazimisha ndoa..baada ya ndoa akachukua chake

MUNGU Akusaidie ukaolewe ukiwa safi bila Mimba ukaheshimikee milleleee

Amen
Wadada wengi mayai wamelia chips...mtu anameza P2 kma paracetamol
 
Sio jambo zuri, lakini siku hizi wanawake wengi hasa mabinti wa umri wa kuolewa wanapata changamoto sana ya kupata watoto.
Kwaio wengi wetu tunahakikisha tumetest mitambo kwanza b4 hatujaeka ndani. Maana raha ya ndoa ni watoto
 
Sema hii dhana ya 'kutest mitambo' naona kama ni mbaya, possibility zote mbili(anaweza apate mimba, au asipate) tayari unazijua,

Kwanini uje utest mitambo kama kigezo cha kuoa, ina maana tokea mmekutana mpaka mkakubaliana kuwa wapenzi mlipendeana nini?

Au wewe mwanaume chukulia mwanamke anakuacha kwasababu huwezi zalisha, kwa sababu hiyo tu. Ni vizuri?

Kupata mimba inapaswa iwe matokeo tu ya kushtukiza....
 
Ni mizagamuano kwa kwenda mbele
zamani nilikuwa naona ni vibaya kuzindua albamu kabla ya ndoa, ukiwa mvumilivu mpaka siku ya ndoa ndio uzindue, kuna wengine wanakula mchumba wako bila hofu. Ya nini kusubiri mpaka siku ya ndoa ndio ule asali? Uasherati umekuwa mwingi sana, wachumba wakikutana faraghani huzinduana na matokeo yake wanapeana mimba kabla ya ndoa na kuwahi kuifunga haraka kabla mimba haijawa kubwa ili kukwepa aibu na kutengwa kanisani kwa kufanya uasherati
 
Back
Top Bottom