Hivi kuna ukweli kwamba, mtu anakuwa na hela nyingi halafu hana furaha?

Wengi wetu ambao hatuna hela za kukidhi mahitaji yetu vuzuri kv. mavazi, mlo kamili, usafiri, kutembea sehemu za starehe, kutalii, kutembea nchi za nje huwa tuna misemo fulani hivi ya kukatisha tamaa.
Misemo hiyo ni kama ifuatavyo;

Unaweza kuwa na hela nyingi lakini ukawa huna furaha.

Tunajihangaisha kwenye haya maisha lakini wote tutakufa.

Yote kwa yote ni ubatili

Unaweza kuwa na hela lakini huna mtoto

Hela hainunui furaha

Lakini wenye hela maisha yao ni mazuri na wanafanya wanachokipenda kushinda wasiokuwa na hela. Na wasiokuwa na hela ndio wanahangaika sana katika haya maisha.

Japokuwa kila mtu ana hela tofauti ni kiwango, mwenye mia ya kununua sigara tu hawezi kumfikia mtu mwenye uwezo wa kupata elfu kumi, ambapo hapo atanunua sigara na kula vizuri. Mwenye elfu kumi hawezi kumfikia mwenye uwezo kuingiza milioni kwa siku kwani yeye anaweza kusafiri nje ya nchi na kufanya biashara zake.

Ukweli hapo ni upi mbona tusiokuwa na hela ndio tunakuwa na kelele nyingi?

Mimi naamini asiyekuwa na hela hana furaha hata kidogo hata kama anayo hamfikii mwenye hela.
Kwanza kabisa hutoijuwa furaha mpaka uwe Muislam mwenye kuishi na kutimiza mafundisho ya Kiislam.
 
E1F6CACC-93DC-441F-BBEF-99B23ED0222A.jpeg


Friends stars mpaka ilipoanza 1995 average salary ya cast member ilikuwa $22,000 per episode. Wakati inaisha 2004 walikuwa wanalipwa $1 million per episode.

Baada ya kuisha kila mwaka walikuwa wanapata rights za rerun zaidi ya mshahara wa episodes kila mwaka, yaani wanauwezo wa kuishi maisha yao yote bila ya kufanya kazi.

Sasa Warner Bros wanatengeneza $1 billion annually kwa reruns worldwide (more than today movie blockbusters), kila member wa friends anapata $20 million dollars.

Matthew Perry kafa kwa stress na drug abuse pamoja na kuwa stable financially.

Hela muhimu ila sio kila kitu.
 
pesa inanunua vitu sio furaha jomba. Unaweza ukawa na kila kitu ila still furaha huna. Ushajiuliza ukishanunua Ndinga kali, ukagonga mademu wakali, ukanywa mapombe ya gharama how long can you do that before boredom kicks in?😀

Kuna mambo nilitamani nikiwa mtoto but sikuwa na uwezo nayo ila leo kila kitu niko nacho. Nimeshavizoea sioni excitement tena.
Eti stress anazozipata mtu aliyekua ndani ya X5 ilingane sawa na stress anayeipata mtu aliyeshindia uji na muhogo! Sio kweli.
 
1.Una billions of money bank ila moyo umefungwa "pacemaker" ile feeling ya kuwa utakata moto mda wowote inakuandama utapataje furaha.?

2.Una billions of money ila kila ukigongana na wanawake hautungishi mimba. Umenyimwa uwezo wa kuzaa ila wadogo zako wote wana watoto. Furaha inatoka wapi?

3. Una billions of money ila wewe ni mgonjwa wa sickle cell au cancer ya ini inakutafuna. Anytime parapanda inaweza ikalia hio furaha inatoka wapi.


Somo:
Utajiri wa kwanza ni afya njema tu kisha ndio pesa inafuata. Tofauti na hapo ni kujilisha upepo.
bro unajifariji tu mtoto wa kwanza ni hela na mke wa kwenza ni hela....na uzima wa kwanza ni hela na pepo ya kwanza ni hela na mapenzi ya kwanza ni hela... (JIDANGANYE)
 
Masikini wengi ni wachoyo na wana roho mbaya sana na hata katika uzi huu unaona kabisa yaani wana wamejaa negativity nyingi mno.

Kuhusu magonjwa kila binadamu lazima apate haijalishi ni masikini au tajiri bt the worst part is Unaumwa haraf hauna pesa ya matibabu.

Furaha na huzuni ni temporary state na mara nyingi huwa vinapokezana and hauwezi kuwa na kimoja wapo permanently, But imagine una huzuni na matatizo kibao yame kuandama haraf hauna pesa

Yaani utaona dunia yote imekuangukia wewe utaishia kulalamika tu na kumuona kila mtu mbaya

Ukiwa na pesa furaha inakuja automatically coz utaweza kufanya vitu vya kukupa furaha muda wowote unaotaka wewe.

Njaa mbaya ndugu zanguni, Utamchukia kila mtu kwa umasikini wako wewe mwenyewe na utamuona kila mwenye pesa hana furaha kama wewe ili uiridhishe nafsi yako but ukweli ni kwamba you're wrong

Hivi ni nani asiependa kuwa na Nyumba kali, Ndinga kali na connection na watu wakubwa?
 
bro unajifariji tu mtoto wa kwanza ni hela na mke wa kwenza ni hela....na uzima wa kwanza ni hela na pepo ya kwanza ni hela na mapenzi ya kwanza ni hela... (JIDANGANYE)
Pambana sana uwe na hela za kutosha ili ubadili mentality
 
Pambana sana uwe na hela za kutosha ili ubadili mentality
vitu vyote vinavyomsumbua binadamu ni chanzo umaskini...na maskini...wivu umaskini wizi umaskini ufisadi umaskini uwongo umaskini husda umaskiniwatoto wa mitaani umaskini... fedha za kunitosha ninazo...
 
Wewe endelea kujifariji tu sasa kama utajiri wa kwanza ni afya njema basi itumie hiyo afya njema kununua bando la buku
Ubaya ni kwamba hio afya unayoibeza ndio inaku support kufungua macho, kutembeza miguu na mikono bila kusahau vidole unavyobofya bofya hio simu ili kuandika kebehi kama ulivyofanya humu. Unasahau kuna wenzako walioko Sewahaji na Mwaisela ambao pengine wana fedha hata kukuzidi ila wamelaza mbavu kwa miezi kibao hawana ubavu wa kubonyeza simu.
 
1.Una billions of money bank ila moyo umefungwa "pacemaker" ile feeling ya kuwa utakata moto mda wowote inakuandama utapataje furaha.?

2.Una billions of money ila kila ukigongana na wanawake hautungishi mimba. Umenyimwa uwezo wa kuzaa ila wadogo zako wote wana watoto. Furaha inatoka wapi?

3. Una billions of money ila wewe ni mgonjwa wa sickle cell au cancer ya ini inakutafuna. Anytime parapanda inaweza ikalia hio furaha inatoka wapi.


Somo:
Utajiri wa kwanza ni afya njema tu kisha ndio pesa inafuata. Tofauti na hapo ni kujilisha upepo.
Tugeuze sarafu. Vipi uwe hayo matatizo yote uliyotaja halafu HUNA HELA? Unafananishaje hayo mazingira?
 
Back
Top Bottom