Hivi kuna ukweli kwamba, mtu anakuwa na hela nyingi halafu hana furaha?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,363
6,903
Wengi wetu ambao hatuna hela za kukidhi mahitaji yetu vuzuri kv. mavazi, mlo kamili, usafiri, kutembea sehemu za starehe, kutalii, kutembea nchi za nje huwa tuna misemo fulani hivi ya kukatisha tamaa.
Misemo hiyo ni kama ifuatavyo;

Unaweza kuwa na hela nyingi lakini ukawa huna furaha.

Tunajihangaisha kwenye haya maisha lakini wote tutakufa.

Yote kwa yote ni ubatili

Unaweza kuwa na hela lakini huna mtoto

Hela hainunui furaha

Lakini wenye hela maisha yao ni mazuri na wanafanya wanachokipenda kushinda wasiokuwa na hela. Na wasiokuwa na hela ndio wanahangaika sana katika haya maisha.

Japokuwa kila mtu ana hela tofauti ni kiwango, mwenye mia ya kununua sigara tu hawezi kumfikia mtu mwenye uwezo wa kupata elfu kumi, ambapo hapo atanunua sigara na kula vizuri. Mwenye elfu kumi hawezi kumfikia mwenye uwezo kuingiza milioni kwa siku kwani yeye anaweza kusafiri nje ya nchi na kufanya biashara zake.

Ukweli hapo ni upi mbona tusiokuwa na hela ndio tunakuwa na kelele nyingi?

Mimi naamini asiyekuwa na hela hana furaha hata kidogo hata kama anayo hamfikii mwenye hela.
 
1.Una billions of money bank ila moyo umefungwa "pacemaker" ile feeling ya kuwa utakata moto mda wowote inakuandama utapataje furaha.?

2.Una billions of money ila kila ukigongana na wanawake hautungishi mimba. Umenyimwa uwezo wa kuzaa ila wadogo zako wote wana watoto. Furaha inatoka wapi?

3. Una billions of money ila wewe ni mgonjwa wa sickle cell au cancer ya ini inakutafuna. Anytime parapanda inaweza ikalia hio furaha inatoka wapi.

Somo:
Utajiri wa kwanza ni afya njema tu kisha ndio pesa inafuata. Tofauti na hapo ni kujilisha upepo.
 
Sawa mkuu uko sahihi! Na vipi unaumwa U.T.I na hauna hata mia tano ya panadol? Furaha utaipata?
Au haujapata hata andazi la shilingi mia tangia asubuhi, furaha utaipata?
 
Unaweza kuta hela kazipata kimagendo labda

Halafu furaha(happiness) ni tofauti na kuridhika(fulfilment).
Ukiwa na hela hata kiduchu unaweza kununua kitu kitakachokupa furaha, hata kwa muda mfupi tu.

Kuridhika sasa ndo changamoto, labda umefiwa ghafla na mtu wa karibu machungu yanakulemea, unajilinganisha na watu nk nk

Halafu kuna watu wao kuwa na mihela mingi ndo kuridhika kwao, wao wanatafuta hela tu mpaka wanakufa hawatosheki....
 
Hapa kuna jambo lililojificha kiroho maana kuna hela sio kila kitu duniani
1.kadiri unavyopata hela na majukumu pia yanazidi

2. Unaweza kuwa na hela huna furaha kwenye ndoa

3.unaweza kuwa na hela magonjwa ndo yakainuka kwenye familia zote na hapo hapo kila mwanafamilia anakuangalia ww tuu

4.unaweza kuwa na hela halafu magonjwa pia yakakuandama na ukalazimika hata soda na kuku unawangalia wenzako wakutumia tuu ww ni mchemsho hata chumvi hakuna mwanzo mwisho

5. Unaweza kuwa na hela pamoja na u star kila wakagi kujifungia hakuna hata kusalimia ndg jamaa na marafiki ukitoka kwako ni mwendo wa magari ya Tinted tuu
Hapo ndipo uone hela ilivyokuwa na siri nzito

Lakini waza chizi hajui kutafuta yy ni mtu wakula majalalani na kuomba omba ila Mungu alivyo wa ajabu hata tumbo halijawahi kumuuma

Nb sichangii ili watu wasitafute hela bali wakizipata wamshukuru Mola wao na kutoa zaka
 
Unaweza kuta hela kazipata kimagendo labda

Halafu furaha(happiness) ni tofauti na kuridhika(fulfilment).
Ukiwa na hela hata kiduchu unaweza kununua kitu kitakachokupa furaha, hata kwa muda mfupi tu.

Kuridhika sasa ndo changamoto, labda umefiwa ghafla na mtu wa karibu machungu yanakulemea, unajilinganisha na watu nk nk

Halafu kuna watu wao kuwa na mihela mingi ndo kuridhika kwao, wao wanatafuta hela tu mpaka wanakufa hawatosheki....
Una kitu
 
1703761438017.jpg
 
Back
Top Bottom