Je, kuna uhusiano wotote kati ya nyumba unayoishi na kufunguka mambo yako?

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,131
8,655
Habari,

Dah leo nimekumbuka jambo ambalo lilishawahi nitokea miaka 7 nyuma sasa katika kuunganisha kwangu dot naona kuna kitu ambacho naweza kuwa sahihi ama la hasa kwenye swala la nyumba zetu hizi za kupanga na upatikanaji wetu wa ridhiki. Na hizi ndo historia ya nyumba nlizokaa kwa upande wa ridhiki

1: Hii nilikuwa nakaa magomeni mapipa dah bwana hii nyumba ilikuwa ukipata hela nyingi kwa week basi ni elfu 50 na kuumwa kila siku kama ni chuo basi ilifikia kipindi nkawa na sapu mpaka 3 dah sema nlihama kwa mbinde mno full uswahili nyumbani mpka mtaa mzima

2: Kinondoni
Hapa nlihamia nkiwa chuo mwaka wa kwanza semester ya 2 hapa nili clear sapu zangu zote na mwishoni wa semester nilifanikiwa kununua gari nikiwa mwanafunzi na siku na ajira rasmi bali mission town tu.

Mpaka kufikia mwaka wa pili semester ya pili nlikuwa na gari zangu mbili huku mitikasi yangu ikienda vizuri mno mpaka nikaamua kuchange kutoka full time kwenda night chuoni.

Mungu si athumani ile nyumba ikauzwa so ikabidi nitafute nyumba nyingine ilala.

3 ILALA
Hapo ndo kimbembe kilipoanzia kwani niliingia nikiwa na gari tatu mambo yalikuwa yanakwenda hovyo mno, ilikuwa inafikia kipindi mpaka hela ya kula huna gari zote zikauzwa kwa hasara ikawa ni mtu wa daladala hela haipatikani kabisa ukipata tu hela ujue kesho ni siku ya kodi au ya kula tu ila maendeleo zero.

Kila ukitaka kuhama misuko suko au unakosa kabisa hela hela yani ukitoka tu kwenye kazi zako unamkuta mwenye nyumba kibarazani hali hyo ilidumu kwa miaka 3 kila nikisema niondoke inashindikana lakini mungu si athumani nikahama .

Ajabu baada tu ya kuhama mambo yakaanza kurudi tena vizuri walau ya kupata maendeleo inapatikana.

Je hii ni kwangu tu au kuna wenzangu ilishawahi watokea?
 
Watanzania na Ushirikina.

DWBj9M_XkAEbADd.jpg


KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom