Hivi jamani kuna vya wanawake na vya wanaume?

Kwangu mimi midume inayokulakula vyakula vya kike naona inapoteza hadhi ya kuitwa midume na kwa tamaduni zetu toto la kiume kuvaa shanga kiunoni ni uchuro mtupu.

Tamaduni zetu akina nani na zipi Mkuu?
Shanga hazihusiani na kula na kunywa tuakojadili sasa hivi.Hunda shanga tutajadili huo muda wake ukifika kwenye mapambo na mavazi.
Asante.
 
Sisi waafrika(naamini na wewe ni mmoja wetu), ni zipi? ni pamoja na kutofautisha kati ya wanaume na wanawake. Mila zetu zinatuelekeza ni jinsi gani mwanaume ale na ni jinsi gani mwanamke ale. Mbona unaonekana upo biased na hutaki kuthinki auti ofu ze boksi?Hilo la shanga ujumbe umefika mahala pake.
 
Tunaangalia preferences zinatokana na nini -
Inaonekana kuna imani zilizojengeka na ndio maana umesema huwezi kukuta mwanaume anakunywa kinywaji fulani hadharani ...kuna wengine kwenye vyakula pia wanazungumiza dhana hii ya kuonekana hadharani.... ina maana kama haonekani anakunywa pale roho yake inapomtaka.Kwanini basi wanaogopa kuonekana hadharani?

Ni imani potofu tu hizo! Jiulize wewe mwenyewe hapa ulimwenguni kuna imani ngapi zilizo potofu?

Katika jamii nyingi kuna imani potofu nyingi tu. Ndiyo malimwengu ya walimwengu hayo.
 
Sisi waafrika(naamini na wewe ni mmoja wetu), ni zipi? ni pamoja na kutofautisha kati ya wanaume na wanawake. Mila zetu zinatuelekeza ni jinsi gani mwanaume ale na ni jinsi gani mwanamke ale. Mbona unaonekana upo biased na hutaki kuthinki auti ofu ze boksi?Hilo la shanga ujumbe umefika mahala pake.

HAPANA mkuu... siko biased bali nachofanya ni moderation tu... nijuavyo mimi utamaduni siyo general wala universal.Utakachoamini au kuelekezwa na utamaduni wako siyo lazima kikawepo kwenye utamaduni wangu japo wote ni waafrika. Ndio maana nikauliza swali.
 
Ni imani potofu tu hizo! Jiulize wewe mwenyewe hapa ulimwenguni kuna imani ngapi zilizo potofu?

Katika jamii nyingi kuna imani potofu nyingi tu. Ndiyo malimwengu ya walimwengu hayo.

Kasema kuna imani zilizojengeka hajasema kama ni za kweli ama la, wewe unadiscuss kama ni potofu ama la!
 
Hakuna aliyebisha ama kukataa kuwa hizo imani hazijajengeka. Mimi ndiyo nimesema baadhi ya hizo imani zilizojengeka ni potofu. Tatizo liko wapi hapo?
 
MAVAZI:
Kuna midume mingine inapenda kuvaa heleni masikioni, sasa sijui tuieleweje. Bora walamba ice cream. Hebu angalia kama jamaa katika picha hii hapa chini:

gabu-albums-mapicha-picture756-5.jpg

Hahahahahahah!
 
Tamaduni zetu akina nani na zipi Mkuu?
Shanga hazihusiani na kula na kunywa tuakojadili sasa hivi.Hunda shanga tutajadili huo muda wake ukifika kwenye mapambo na mavazi.
Asante.

Wewe Vera mbona kama nimeanza kukupenda...Yaani nahisi kwamba ukitoka kwenye vinywaji mtiririko wako utakwenda kwenye;

3. Mapambo na Mavazi
4. Magari
5. Simu za mkononi
6. Mitaa ya kuishi
7. Kazi za kufanya/kuajiriwa
8. Biashara za kufanya
9.
10.
 
part 2. VINYWAJI

Kwenye unywaji, je kuna vinywaji vya kike na vya kiume? Mara nyingi utaona wanawake wakiagiziwa wine hata pale hawajaomba kinywaji hicho.Hata hivyo wine najua zinaywewa na wote, kadhalika beer. Wanawake wengi sasa hupenda kunywa gin and tonic, soda water n.k kama namna ya kuangalia uzito usiongozeke.Pombe kali kama whisky,brandy etc nani mnywaji ?
Nini maoni yako kuhusu unywaji? Na je kwa wale wenye uzoefu na vinywaji vya asili. kuna pombe za wanawake na za wanaume? TUJUZENI

Kwenye vinywaji bwana hapo ndipo patamu. My ex-girlfriend tulikuwa tukifika bar anaagiza Safari....Watu wanamshangaa wala hajali! Kweli watoto wa Arusha wamedata!
 
Wewe Vera mbona kama nimeanza kukupenda...Yaani nahisi kwamba ukitoka kwenye vinywaji mtiririko wako utakwenda kwenye;

3. Mapambo na Mavazi
4. Magari
5. Simu za mkononi
6. Mitaa ya kuishi
7. Kazi za kufanya/kuajiriwa
8. Biashara za kufanya
9.
10.
Yaani!
Ulijuaje?
 
Wakati na reply sikujua ni wewe nisingefanya huwa unaishiaga kutukana na nisingependa kuharibu mada kwa kwenda nje ya point. So let it be.

Safari ijayo ni vyema ukasoma jina la unayemjibu. Na nashauri ukiona bandiko langu lolote lile uliruke tu (au ukitaka kusoma soma lakini usijibu maana you rub me the wrong way) na tutaishi kwa amani.
 
Kwenye vinywaji bwana hapo ndipo patamu. My ex-girlfriend tulikuwa tukifika bar anaagiza Safari....Watu wanamshangaa wala hajali! Kweli watoto wa Arusha wamedata!

Watu wanamshangaa kuagiza beer ya safari? ..kwanini wakati ndicho kinywaji roho yake inataka?
 
Safari ijayo ni vyema ukasoma jina la unayemjibu. Na nashauri ukiona bandiko langu lolote lile uliruke tu (au ukitaka kusoma soma lakini usijibu maana you rub me the wrong way) na tutaishi kwa amani.

Hehehe! Vita tena? Kutoka mada ya misosi mpaka vita ya mabox Vs mavumbi! Natafuta taswira kamili.
 
Watu wanamshangaa kuagiza beer ya safari? ..kwanini wakati ndicho kinywaji roho yake inataka?

Unajua beer ya Safari kwanza imekaa kidume dume, pili inanywea na masela kwa mjini na kwa vijijini ndio bia yao ili walewe mapema.

Mijini kwenye baa za watu wenye kipato cha kati na cha juu ni nadra sana kumkuta mtu anakunywa safari. Sasa mimi nilikuwa nikienda naye ambao mademu wengine wanakunywa Savanna, wengine wine, kama ni bia basi ni Windhoek, Reds na zianzofanana na hizo! Wengine cocktails wanazozijua wao. Ila yeye anaagiza Safari...She is such a character!
 
Hahaha! Duh! Umeshawahi kumchunguza vizuri?
 
Back
Top Bottom