Hivi jamani kuna vya wanawake na vya wanaume?

Hebu jamani tuacheni mawazo potofu na kuwa gender sensitive kha! eti ohh mwanaume akila cone, kuna shida gani? tatizo munawaza madudu ya ajabu ndo maana kila jambo munarefer huko mie mume wangu anakula cone kama kawa na wala sijafikiria na katu sitafikiria upuuzi huo, TUBADILIKE
 
haha wanawake tunapenda vyakula vilaini jamani mie ugali napenda nile mala moja kwa miezi sita au mwaka

kwanza huwa napata mawazo sana kuula labda kwa mboga za majani
 
Haya kufuatana na mawazo yenu naomba ni summarize kama ifuatavyo:
1. Ulaji wa vyakula hutegemea mazoea toka tunavyokua
2. Upendelevu huo unatokana na mazingira au eneo nahata kabila la mhusika
3. Watu wakitoka kula nje hupendela kujaribu vyakula vigeni na siyo vile walivyozoea kuvila au kuvipika wenyewe majumbani
4. Kuna imani na tafsiri ambazo hupewa na jamii pale mwanamke au mwanaume anapokula vyakula fulani
5.Tafsiri hizi wakati mwingine huwa potofu na siyo kila mtu anakubaliana nazo.
6. Chakula ni chakula tu.Hakuna cha kike wala cha kiume.

part 2. VINYWAJI

Kwenye unywaji, je kuna vinywaji vya kike na vya kiume? Mara nyingi utaona wanawake wakiagiziwa wine hata pale hawajaomba kinywaji hicho.Hata hivyo wine najua zinaywewa na wote, kadhalika beer. Wanawake wengi sasa hupenda kunywa gin and tonic, soda water n.k kama namna ya kuangalia uzito usiongozeke.Pombe kali kama whisky,brandy etc nani mnywaji ?
Nini maoni yako kuhusu unywaji? Na je kwa wale wenye uzoefu na vinywaji vya asili. kuna pombe za wanawake na za wanaume? TUJUZENI
 
ukweli upo wa kupenda chakula fulani. lakini mtu anaweza kubadilika kutokana na mazingira aliyopo. nakumbuka enzi zileeeeeeeeee wakati najiiba kwenda kwa mchumba kumpikia, siku nikatokea na ndizi, mwenyewe nimezipika vizuriiii nikajua leo atafurahi sana. alikula (nadhani sababu alikuwa na njaa) na akasema chakula kitamu lakini yeye hapendi kula ndizi kwa hiyo sikupika tena.
Ila baada ya kuolewa, mimi napenda ndizi, na sina kwa kwenda kupika zaidi ya nyumbani kwangu. mwanzo nikawa nikipika ndizi napika na chakula kingine, akawa anaonja onja ndizi zangu mwisho siku akaniambia ukipika ndizi usipike chakula kingine. kwa sasa anapenda sana ndizi kiasi kwamba usipopika wiki nzima anaziulizia
 
part 2. VINYWAJI

Kwenye unywaji, je kuna vinywaji vya kike na vya kiume? Mara nyingi utaona wanawake wakiagiziwa wine hata pale hawajaomba kinywaji hicho.Hata hivyo wine najua zinaywewa na wote, kadhalika beer. Wanawake wengi sasa hupenda kunywa gin and tonic, soda water n.k kama namna ya kuangalia uzito usiongozeke.
Nini maoni yako kuhusu unywaji? Na je kwa wale wenye uzoefu na vinywaji vya asili. kuna pombe za wanawake na za wanaume? TUJUZENI

Yaani nilihisi tu kule mwanzo kwamba wewe mchokozi, sijui namba kumi itakuwaje

Tukija upande wa vinywaji, again its someones choice; lakini mara nyingi kuna influence kubwa sana ya partner katika chaguzi za vinywaji...

again, sidhani kama kuna specific drink ya akina mama au akina baba ila society imeviangalia vinywaji kwa mtazamo wa feminine drinks kama Redds, Wines, Amarula types, colourful cocktails with creams and fresh juices wakati beer, konyagi, whysky, brandy, cognac and the likes zinaonekana kama masculine drinks zifananzo zaidi na wanaume

binafsi hainisumbui sana ila napata presha nikiona mwanadada anagida konyagi au whisky dry!!
 
MTM nilijua tu lazima utie neno lol.
Namba kumi nitakuachia wewe useme cha kuzungumziwa.
Katika vinywaji na hiyo clustering uliyofanya - masculine and feminine drinks ina maana sweet drinks ni za wanawake na zile chungu chungu ni za wanaume?
Nimeshajaribu kuangalia sana kuona kama wanaume wanakunywa REDDS sijaona.Kuna mchangiaji mmoja amesema atashangaa kuona men akinywa ciders Ni kwanini?
 
This is just BS. Hakuna chakula cha kike wala cha kiume. Kama kipo basi hiyo ni perception ya mtu mwenyewe na insecurities zake. Other than that I think people are going too far in trying to find unnecessary differences.
 
MAVAZI:
Kuna midume mingine inapenda kuvaa heleni masikioni, sasa sijui tuieleweje. Bora walamba ice cream. Hebu angalia kama jamaa katika picha hii hapa chini:
gabu-albums-mapicha-picture756-5.jpg
 
Absolutely na ndiyo hitimisho.Sasa tunazungumzia vinywaji... any ideas?
 
MAVAZI:
Kuna midume mingine inapenda kuvaa heleni masikioni, sasa sijui tuieleweje. Bora walamba ice cream. Hebu angalia kama jamaa katika picha hii hapa chini:

gabu-albums-mapicha-picture756-5.jpg

Asante... tumemaliza kuangalia vyakula na sasa tunajadili vinywaji...mavazi na mapambo ni agenda itakayofuata.
 
Absolutely na ndiyo hitimisho.Sasa tunazungumzia vinywaji... any ideas?

Hata vinywaji sidhani kama kuna vya kike na vya kume ingawa mara nyingi, kwa mfano, huwezi ukakuta mwanamme anakunywa Daiquiries hadharani.

Kwa hiyo kwangu mimi mtu hapotezi jinsia yake kutokana na vile anavyokula na kunywa.
 
mavazi:
kuna midume mingine inapenda kuvaa heleni masikioni, sasa sijui tuieleweje. Bora walamba ice cream. Hebu angalia kama jamaa katika picha hii hapa chini:

gabu-albums-mapicha-picture756-5.jpg

life style ujana na mengineyo
 
Mkuu asante sana kwa kuleta dimension nyingine kwenye PART 1 ya mada -VYAKULA.

Kwanini unadhani wanawake wanapenda kula vyakula vile ambavyo huwa hawavipiki wenyewe? Nadhani assumption hapa ni kuwa mnapotoka kula out ndiyo choice waifanyayo wanawake. Je wewe kwa mfano, ukitoka kula restaurant, unapendelea zaidi kula vyakula gani/ ni vile ulivyovizoea au vile ambavyo mara nyingi haviko kwenye menu nyumbani?

Nikitoka nje au tikiagiza vyakula kutoka nje daima namwachia madam uchaguzi anacho chagua yeye ndio na mimi nachokula kama vile anacho nipikia nyumbani ndicho nachokula (hata nje namwachia yeye uchaguzi kwa sababu yeye ni mjuzi wa mambo ya jikoni kuliko mimi kwa hiyo namwachia uchaguzi yeye, kama piza basi wote piza, kama kuku basi wote kuku........).
 
Hata vinywaji sidhani kama kuna vya kike na vya kume ingawa mara nyingi, kwa mfano, huwezi ukakuta mwanamme anakunywa Daiquiries hadharani.

Kwa hiyo kwangu mimi mtu hapotezi jinsia yake kutokana na vile anavyokula na kunywa.

Tunaangalia preferences zinatokana na nini -
Inaonekana kuna imani zilizojengeka na ndio maana umesema huwezi kukuta mwanaume anakunywa kinywaji fulani hadharani ...kuna wengine kwenye vyakula pia wanazungumiza dhana hii ya kuonekana hadharani.... ina maana kama haonekani anakunywa pale roho yake inapomtaka.Kwanini basi wanaogopa kuonekana hadharani?
 
Kwa hiyo kwangu mimi mtu hapotezi jinsia yake kutokana na vile anavyokula na kunywa.

Kwangu mimi midume inayokulakula vyakula vya kike naona inapoteza hadhi ya kuitwa midume na kwa tamaduni zetu toto la kiume kuvaa shanga kiunoni ni uchuro mtupu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom