Utafiti: Asilimia 70% ya wanawake wanavutiwa kimapenzi na wanaume wenye ndevu

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Wanangu fugeni Ndevu.

Utafiti umeonesha Wanawake wanawapenda Wanaume wenye Ndevu kuliko wasio na Ndevu.

Asilimia 70% ni kubwa so no way out Wanangu tufuge Ndevu.

=======

ndevu-pic.jpg


Kumekuwa na mijadala kwa baadhi ya wanawake kuhusu mwanamume mwenye ndevu na asiyekuwa nazo yupi ana mvuto zaidi.

Wengine wanadai mwanamume mwenye ndevu ana mvuto zaidi na huwa mtanashati.

Utafiti uliochapishwa na Tovuti ya VWO Testing inayojihusisha na masuala ya mitindo kwa wanaume kupitia mfumo walioupa jina la A/B Testing umebaini kuwa wanawake wengi huvutiwa na wanaume wenye videvu vyenye ndevu kuliko wale wasiokuwa nazo.

Utafiti huo ulifanywa kwa njia ya mtandao kwa siku 15 kupitia tovuti hiyo kwa kuweka picha mbili, moja ikiwa ni ya mwanamume mwenye ndevu na asiye na ndevu.

Asilimia 70 ya walioshiriki katika utafiti huo wanaokisiwa kuwa ni wanawake wameeleza kuvutiwa zaidi na wanaume wenye ndevu, huku wakibainisha sababu mbalimbali.

Utafiti mwingine uliofanywa na Mwanasaikolojia na Mtafiti Tessa Clarkson na kunukuliwa katika tovuti ya Phychology Today, unaungana na ule uliochapishwa na VWO, kwamba wanaume wenye ndevu huwavutia zaidi wanawake.

Utafiti huo wa Phychology Today uliofanywa katika Chuo cha Queensland uliohusisha wanawake 919 raia wa Marekani wenye umri kati ya miaka 18 hadi 70 kwa kuweka picha za wanaume wakiwa na viwango tofauti tofauti vya ndevu huku wanawake hao wakitakiwa kuchagua kati ya picha hizo, ulibaini walioonekana na ndevu walichaguliwa.

Moja kati ya maoni yaliyotolewa na wanawake, ni kwamba wanaume wenye ndevu pia wana nguvu na afya.
Hata hivyo, utafiti huo unaeleza kuwa si wanawake wote walionekana kuvutiwa na picha za wanaume wenye ndevu, wapo baadhi waliochagua za wale walioonekana kutokuwa na ndevu huku wakibainisha sababu za kuwachagua.

Baadhi ya sababu hizo zilizobainishwa na wanawake hao ndevu kuharibu muonekano wa mwanamume na kuwafanya wasionekane nadhifu.

Wanawake wanasemaje?
Stumai Shamge, anasema anapokuwa na mwanamume mwenye ndevu katika uhusiano huwa anajenga kujiamini zaidi.

Mkazi wa Mbagala, Anna Anord anasema suala la ndevu katika muonekano wa mwanamume hajalipa kipaumbele, hivyo awe na ndevu au hana kwake ni sawa, cha msingi ni upendo.

“Mimi upendo ndio unanifanya nivutiwe na mwanamume, haijalishi awe na ndevu au asiwe nazo, kama nimempenda kwangu ni sawa,” anasema Anna.

Kauli hiyo inatofautiana na Elizabeth Ngonyani, ambaye anasema mwanamume mwenye ndevu anavutia zaidi kuliko asiyekuwa nazo, huku akitoa angalizo kuwa zinatakiwa kuwa za wastani, safi na zinazotunzwa vizuri.

Wanaume je?
Khamis Khamis, mkazi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam anasema mwanamume anapokuwa hana ndevu huwa anadharauliwa na baadhi ya watu na kuonekana kuwa hawajakua.

“Mwanamume usipokuwa na ndevu unadharaulika kwa kuonekana una upungufu fulani, kwa kuwa imeshazoeleka kwa baadhi ya jamii kuwa moja ya sifa ya mwanamume aliyekamilika ni kuwa na ndevu,” anasema.

John Mwakangale anasema anafikiri wanawake kupendelea wanaume wenye ndevu kuliko wale wasiokuwa nazo kunatokana na dhana mbalimbali zilizopo miongoni mwa wanajamii kuwa mwanamume kuwa na ndevu ni ishara ya uimara, nguvu na ukomavu.

“Katika baadhi ya jamii au maeneo mbalimbali mwanamume ambaye hana ndevu hudharauliwa na wale wenye nazo huonekana wababe,” anasema.

Kwa upande wake Shushu Othman, anasema mwanamume kuwa na ndevu haimaanishi yeye ni mtu mzima kuliko yule asiye na ndevu kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya jamii, huku akitolea mfano wa mstari mmoja wa wimbo “ndevu amenyimwa ng’ombe lakini mbuzi kapewa.”

Mtaalamu wa Saikolojia, Charles Mhando anasema tangu enzi za kale kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wanajamii kuwa ndevu hudhihirisha uwezo kinguvu, uimara, heshima, ukomavu kijamii na mvuto, pia alama ya kuonesha ukomavu kibaolojia.

Anasema pengine kutokana na dhana hizo inaweza ikawa moja kati ya sababu ambazo huenda zinasababisha wanawake wengi kupendelea mwanamume mwenye ndevu kuliko yule asiyekuwa nazo.

“Hiyo husababisha baadhi ya wanaume wasioota ndevu kwa wingi kutumia njia mbalimbali ili waweze kukuza ndevu zao, ikiwamo kutumia mafuta wanayoamini yatawasaidia kukuza ndevu zao,” anasema.

Anasema uwepo wa dhana hizi huweza kusababisha wanaume wasio na ndevu kupata matatizo mbalimbali ya kisaikolojia, hasa sonona kutokana na kujiona na upungufu fulani.

“Unaweza kukuta wanaume wamekaa mahala wanabishana juu ya hoja fulani, pengine yule asiye na ndevu akatoa hoja zenye nguvu zaidi na kuonekana kama anataka kushinda, unaweza msikia aliyeshindwa akisema tulia mtoto mdogo wewe hata ndevu huna,” anasema na kuongeza kauli kama hizo na nyinginezo huweza kuwaathiri kisaikolojia.

Mhando anasema mwanamume kuwa na ndevu chache au kukosa kabisa ni masuala ya changamoto katika homoni na haina uhusiano na dhana hizo zilizojengeka miongoni mwa wanajamii.

Daktari wa binadamu, Samweli Shita anasema suala la mwanamume kuwa na ndevu nyingi, chache au kukosa kabisa husababishwa na homoni au urithi.

Dk Shita anasema mwanamke na mwanamume wote wana homoni za kike na kiume ndani yao, ila mwanamume ana homoni kidogo za kike na mwanamke ana homoni kidogo za kiume na hiyo ndiyo sababu inapotokea hitilafu na zikazalishwa kwa wingi husababisha mwanamke kuwa na ndevu nyingi.

Anasema wakati wa kubalehe, homoni za kiume, androgens husababisha mabadiliko mbalimbali, ikiwamo mwanamume kuwa na ndevu, hivyo inapotokea changamoto husababisha kuota ndevu chache.

Mwananchi
 
Tafiti hupingwa na tafiti nyingine, ila mkuu ndevu ata mambuzi (mabeberu) wanazo, tafuta hela mkuu.
 
Mimi sifugi ndevu wala sharubu lakini nawakula kadiri nitakavyo.

Nikiwa mdogo nilimuuliza babu yangu mbona kila mara anapara tu kidevu chako hataki ndevu? akanijibu kufuga fuga midevu ni sawa na kutojiamini na jinsia yako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nifunge ndevu sina hela, mwisho zione sina hela imladi zijae tu puani nikose pumzi nife🤣😂😂
 
Back
Top Bottom