Hivi idara ya usalama wa taifa wa Tanzania inahusika na kila kitu hadi uuzaji wa nyanya na vitunguu magengeni?

Kwasasa ma DSO hapanga Dili na wakuu wa idara wote including DED Kufisadi pesa za miradi mbalimbali ,unadhani kutakuwa na jipya hapo?🤣🤣🤣🤣🪑
Pesa zote za zinazotoka serikali kuu, kwenye malipo lazima wawepo kuanzia DC na watu wake (Kamati ya ulinzi na usalama, akiwemo huyo DSO), halafu DED then DT (Mweka hazina) baadaye Kuna watu wa mipango na Wakuu wa Idara, hasa Mkuu wa Idara ambaye mradi unamhusu.

Na siku hizi ni wajanja wameshajua CAG anakagua COMPLIANCE na siyo wizi, kwahiyo wanakula nyuma ya mgongo watu.
 
Nadhani ni kwa sababu Watanzania tumekuwa na mentality ya kuamini kuwa Usalama wa Taifa ni Malaika wanaojua kila kitu,kiasi kwamba cho chote ambacho hakipendezi kikitokea katika Taifa letu tunaamini ni uzembe wao.
 
Nadhani ni kwa sababu Watanzania tumekuwa na mentality ya kuamini kuwa Usalama wa Taifa ni Malaika wanaojua kila kitu,kiasi kwamba cho chote ambacho hakipendezi kikitokea katika Taifa letu tunaamini ni uzembe wao.
Wabongo wengi ni WAVIVU, Wana TAMAA halafu ni WABINAFSI.

Wabongo wanapenda KUFANYIWA kila kitu. Ndio maana hata Sasa utakuta watu wanamlaumu Nyerere kwanini maji ya mgawo.

Wabongo wakisikia ,wamasai wanataabishwa na Utawala hawajali Kwasababu wanaona wao haiwahusu. Wakiona wastaafu wanaatishwa wanaona hawahusiki.

Ndio maana Watawala wanaburuza kila kundi nchi hii kwa ZAMU Kwasababu hatuwezi kuungana.

Kwetu tunachojua ni kujipendekeza na sisi tuwekwe kwenye hiyo mifumo katili na sisi TUPIGE Basi.
 
Hata nikishindwa kumpatia mimba bebe wangu lawama ziende kwao tu..

Hao ndio wapokea lawama wa taifa
 
Usalama wa Taifa wanahusika na Kila Jambo linaloendelea kwenye nchi, lakini kazi yao kubwa ni kukusanya taarifa, kuchakata na kupeleka taarifa. Wa kulaumiwa ni wale wanaopelekewa taarifa kutochukua taarifa.
Usalama wanakusanya taarifa gani?

Sana sana labda hizo wanazopelekewa na wananchi au watendaji wa kata na vijiji.


Hakuna taarifa zozote za maana
 
Usalama wa Taifa wanahusika na Kila Jambo linaloendelea kwenye nchi, lakini kazi yao kubwa ni kukusanya taarifa, kuchakata na kupeleka taarifa. Wa kulaumiwa ni wale wanaopelekewa taarifa kutochukua taarifa.
Source ya madai yako ni nini? Hisia zako tu au?
 
Siyo mjuzi sana wa habari za idara ya usalama wa taifa, Tanzania.

Lakini katika pitapita zangu humu JF, nimekutana na mada kadhaa zilizonishangaza kidogo.

Mtu akienda dukani akikuta bidhaa ambayo haipendi, lawama anabebeshwa usalama wa taifa.

Msanii Diamond umaarufu wake ukianza kupungua, lawama zinaenda kwa usalama wa taifa!

Timu za mpira za Tanzania zisipofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, lawama kwa usalama wa taifa!

Ni mimi tu ambaye sielewi dhima nzima ya usalama wa taifa au inakuwaje?

Kwa mfano, usalama wa taifa wanahusikaje na uwepo wa bidhaa za Kenya kwenye maduka ya Tanzania?

Kwa akili zangu hizi za panzi, waamuzi wa mafanikio ya bidhaa ni wateja/ wanunuzi.

Kama wateja/ wanunuzi wanaona bidhaa fulani ni bora kuliko bidhaa ingine, basi wataendelea kuiunga mkono kwa kuinunua.

Na ubora wa bidhaa sidhani kama unahusiana chochote na idara ya usalama wa taifa.

Ubora wa bidhaa unatokana na ubunifu wa mzalishaji. Mzalishaji anapotengeneza bidhaa iliyo bora halafu akaitangaza kwa umma, umma huo ndo utaamua mafanikio ya hiyo bidhaa.

Sasa kama makampuni ya Tanzania hayatengenezi bidhaa zilizo bora kutokana na kushindwa kuwa wabunifu, lawama kwa usalama wa taifa zinahusikaje?

Hmm…..yawezekana ni mimi tu na hizi akili zangu za panzi ndo maana labda sielewi.

Wajuvi na wajuzi wa mambo nijuzeni, tafadhali.
Nikupe mfano mdogo tu Ila usiniulize nimeutoa wapi.
Mwaka 2019/20 TISS iliasisi mpango wa Siasisha TISS, yaani TISS imiliki siasa za nchi. Waasisi na watoa wazo walikuwa TISS waliojifungamanisha na CCM. Lakini Kwa nguvu ya mamlaka wakataka ionekane Jambo hili ni Kwa faida ya Nchi likakubalika bila kujua litaleta madhara mnayoyaona Leo bungeni. Wakajipanga kutoa Wabunge wanaotokana na TISS (Kila mkoa yupo angalao mmoja). Wakijua ni kazi kufanikiwa, wakajipa kazi ya kuchapa karatasi za Kura kuanzia za udiwani Hadi Urais. Waziri Sera, uratibu na Bunge akatangaza 2020 nchi itajitegemea katika Uchaguzi.
Sina haja ya kueleza Kila kitu maana wengine mnaita Uchaguzi wa 2019+20 kuwa ulikuwa Uchafuzi. Mimi sina jina halisi la kuuita lakini nilisema TISS walifanya uteuzi wa watu waliowataka kuwa Wabunge/madiwani. Kule upinzani ulikoshinda yalikuwa makosa ya maDSO na ndo maana DSO wa Mtwara na Nkasi (CUF na CDM) tunavyoongea ni wahudumu ofisi za RSO mikoa husika.
Kwa kadhia ya Uchaguzi ule na uendeshaji wa nchi unaotokana na Uchafuzi ule, wanakosea nini wanaoilaumu TISS Kwa Kila Jambo?
 
Usalama wa taifa katika uchumi.

Watu wako inapaswa wawe salama kiuchumi. Ukiona kuna bidhaa inatoka nje ni bora kuliko ya kwenu mnatakiwa mfanye namna mjifunze mbinu na technology yao ili wananchi went wawazidi wale wa nje

Usalama ktk mpira.

Kama viongozi wa mpira wanapanga kikosi cha taifa kibwegebwege na kuna watanzania wazuri ndani na nje ya nchi
Sabuni zetu za komoa zikowapi ,mafuta ya korie
 
Sawa Bwana Junya mwenzangu,mimi nafanya Biashara ya Cosmetics,wambie TIC wafanye updatio masuala ya Cosmetics and foods yapo TBS na masuala ya Drugs and medical devices yapo TFDA.
Sasa tulejee mada yetu;umo TBS na TFDA,TISS wamo kama wote kuanzia Maabara mpaka kwenye masuala management.
Mashirika yote ambayo yanadili na masuala nyeti kama Afya ya Mtanzania TISS wapo Mkuu.
Ulizungumzia nyanya,kama zinatoka nje ya nchi pia jicho la TISS lipo na kama zinazalishwa nchini basi Madawa yote yanayotumika kwenye Kilimo husika ni lazima yathibitishwe.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Sio razima TISS wawepo ndani ya ofice yako, hata wakiwa huko nje, hao TBS, na TFDA wanaanzia huko unakosambaza kuuza.
Bidhaa imetoka kiwanda gani?
Ina ubora gani?
Je , kiwanda hiko ni halali?
Vipimo vya ujazo sawa?
Wakija kwako ujue wanakuja kuhakikisha mazingila ya kiwanda kama kimekizi vigezo.
Na hapo sasa ndio idara ya usalama nayo inaanza kukufanyia kazi kwa kile unachofanya au unachozalisha.wakiona tapeli ndio hapo utaona, unavyopigwa danadana usipoangalia utahama nchi na hutojua tatizo limeanzia wapi. Hata ungekua mkubwa kiasi gani, unapesa kiasi gani. Utashushwa. Kila kukicha TRA, kukicha TFDA, kukicha watu wa AFYA, mwisho wanamalizia police , washakupoteza tayari.

Wakenya ni wajanja sana, nao kama wachina tu, wanaweza kujifungia hata ndani kwao wanatengeneza vitu, wanapackaging, lakini bidhaa hiyo ukiifuatilia imetoka kiwanda gani hakun jibu. Kwanini isipigwe malufuku.!
 
Sasa naanza kuelewa kwa nini Tanzania ni banana Republic!

Ni kwa sababu ya ujinga kama huu.

Kudhani kuwa usalama wa taifa ndo watengeneza sera za kiuchumi.

Kudhani kuwa usalama wa taifa ni wataalamu wa uchumi na maendeleo!

Hapa tulipo kiuchumi si bahati mbaya wala si ajali.

Ni matokeo ya kutojua cha kufanya.
Unaakili sana mkuu..maana umejibu kwa kuelimisha kwa njia ya beza kwamba , wao ndio watunga sera.
Na hivyo ndivyo ilivyo.
 
Kuna mmoja humu kaulalamikia usalama wa taifa kwa uwepo wa sabuni ya jamaa. Duh! Kama ni hivyo basi usalama wa taifa labda utakuwa unahusika na bidhaa kama nyanya na vitunguu huko masokoni. Hata mimi pia sijui mukhtadha wa usalama wa taifa shughuli zao zinaanzia na kuishia wapi zaidi ya stori za vijiweni kuwa usalama wa taifa wapo kila idara
Upepo wa Pesa
 
Back
Top Bottom