Rais Samia amteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
IMG_8332.jpeg

Rais wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Balozi Siwa ameapishwa leo tarehe 28 Agosti, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bw. Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

IMG_8333.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2023.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Balozi Siwa ameapishwa leo tarehe 28 Agosti, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bw. Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
D..jpg

D2.jpg
 
kumekucha, Enzi za mwenda zake hii mifuko ya NSSF ilihusishwa sana na ....... anyway tuseme most of hawa wakuu wa vitengo ni watu wa system..

hili bango chini ilikuwa December mwaka 2021
Screenshot_20230828-180253~2.jpg


Ndugu Ali Idd Siwa amekuwa katika utumishi wa umma tangu mwaka 1977 na kati ya mwaka 2001-2014 Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani.

Ndugu Ali Idd Siwa Agosti, 2014 Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kigali, nchini Rwanda akichukua nafasi ya Balozi Dkt Mwita Marwa Matiko. Majukumu aliyoendelea nayo pia mwaka 2018-2021 baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli kabla ya kurejea nchini na kuteuliwa kuiongoza bodi ya Mfuko wa NSSF na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Katika nafasi mbalimbali alizotumikia ametajwa kuwa mtu mahiri katika utendaji kazi wenye uadilifu, uzalendo, ubunifu na matokeo makubwa.

Tunamtakia utumishi mwema kwenye majukumu yake ya sasa
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Waadhamini ya NSSF, Balozi Ali Idi Siwa
1693236308140.png

13 July 2023

''NSSF INA UWEZO wa KULIPA MAFAO ZAIDI ya MIAKA 40 IJAYO, THAMANI YAKE ni KUBWA'' - BALOZI ALI IDI SIWA

View: https://m.youtube.com/watch?v=CcIR3esWuV8&pp=ygUMQWxpIElkaSBTaXdh
.
Mwenyekiti wa Bodi ya Waadhamini ya NSSF, Balozi Ali Idi Siwa amewahakikishiwa wanachama wa NSSF kuwa Mfuko upo imara na kwamba una uwezo wa kuendelea kuwalipa Mafao mbalimbali kwa zaidi ya miaka 40 ijayo.

Balozi Siwa ameyasema hayo Julai 11, 2023 wakati alipo tembelea Banda la NSSF katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayo endelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa Mfuko unaendelea kukua kwa kasi kubwa kwani hivi sasa ukwasi wa Mfuko umefikia thamani ya shilingi za kitanzania Trilioni 7.1 na kwamba NSSF inaendelea kuboresha mifumo ya ufanyaji kazi ili kuhakikisha kuwa huduma bora zinamfikia kila mwanachama


1693235531172.png

Picha toka maktaba : Balozi Ali Idi Siwa


Mambo juu ya mambo. Aliyemtangulia atapewa cheo kipi maana hajadumu sana


1693235330075.png

Ali Idi Siwa, Tanzanian Ambassador to Rwanda presents credentials to H.E President Paul Kagame - Kigali, 1 April 2015

“In respect to the relations between Rwanda and Tanzania, which had fallen into an unfortunate situation, we would like to say that let the bygones be bygones, we are starting a new chapter now,” said Siwa.

Describing past tensions as “unfortunate events”, the new envoy said that the two countries, which share a common border, have always enjoyed warm relations, which he said would continue in the interest of their citizens and the region.
 
Back
Top Bottom