Hivi hili la walimu ni kubwa kuliko matukio mengine nchini?

Ukitaka kujua kunya anye kuku akinya bata kahalisha basi chukua tukio hili linalovuma sasa nchini kuhusu walimu mafunzoni waliomuadhibu mwanafunzi huko mbeya

Kila mtu anasema lake kila raia anasema lake kisa kuna jina mwalimu, nauona ukandamizaji na udhalilishaji, hili si kubwa kuliko mengine yaliyopo na yaliowai kuwapo nchini..

Leo media ndio mjadala, nimeamka asubuhi mada ni hii redioni, kwenye tv, magazeti na huko whasapp na kwingineko ndio usiseme.

Hivi waandishi wa habari mna weledi kweli? Hivi kipigo cha mtoto ambae hata hajajeruiwa ni kikubwa kuliko watafiti waliouwa Dodoma?

Ni kikubwa kuliko Kifo cha Mwangosi mikononi mwa Polisi?

Mbona mijadala haikufika hapa, wala hatukumuona mawaziri watatu mpaka wanne wakisimama ndani ya masaa machache baada ya uvumi/tukio kutoa matamko na hukumu kwa watuhumiwa?

Hivi hili limewauma sana serikali kuliko mengine?
Kwanini haikuwa busara liende kwa taratibu za kisheria mpaka mahakamani walimu hawa waliokuwa mafunzoni wapewe haki yao na chombo cha kutoa haki?

Siwezi sema walichotenda walimu hawa ni sawa lakin je hatua za hukumu pia zipo sawa? Tunasikia hadi vyuo wameshafukuzwa, je hii ni hukumu ya haki?

Mbona scorpion aliemtoa mtu macho sijasikia hata waziri mmoja akisema auwawe? Au alichofanya scorpion, wale wanakijiji wa dodoma kuwauwa watafiti ni zuri kuliko hili?

Watanzania tuache mihemuko, na ndio maana nchi hii ina wanafiki wengi, wasioweza kuhoji wala kuchanganua wapo kumfurahisha fulani wapate vyeo, fulani nae yupo kutoa tuzo kwa kila mnafiki.

Lazima ifike wakati tuishi ndani ya haki na kweli.

Wengine wanasema yani katoto kadogo vile walimu watano? Mbona hamuulizi yani vi walimu viwili tu vilivyopo mafunzoni mawaziri watatu na waandishi wa habari wote wamesimama? Na wakiungwa mkono na Watanzania kibao

Hali halisi zilizopo Mashuleni:

Wengi hamjui hali halisi zilizopo mashuleni, walimu wenzangu wanajua sana tena vema hali halisi mashuleni, na hali mbaya ya utovu wa nidhani mashuleni, ambayo imeletwa na serikali ya kuchanganya siasa na taaluma.

Wanafunzi wanajua wana haki kubwa sana mashuleni kuliko walimu, kama hamjui mlijue hilo, siku hizi watoto hawafukuzwi mashuleni maana siasa za wanasiasa na sera za serikali zinasema watoto wabembelezwe wamalize shule.

Ndio maana michujo na mitihani kama ya kidato cha pili haipo, lengo ni amalize shule hayo mengine si ya muhimu kabisa kabisa

Viboko na adhabu za kawaida ni haramu shuleni, serikali haina msimamo thabiti, waraka wa adhabu uliopo hauna mwanya wa kutoa adhabu za maonyo kwa wanafunzi, leo linatokea hili nchi inasimama, kweli?

Nitoe mifano halisi mwaka jana kuna walimu walikuja mafunzoni shule nnayofundisha, wanafunzi wawili wakamshika matiti mwalimu wa kike alipokuwa darasani, mwalimu alifadhaika sana. Tukatoa adhabu kwa hawa watoto ya suspension (kurudishwa nyumbani) na viboko vinne kila mmoja.

Usiku ule ule wakamvizia mwalimu mwingine wa kiume alie mafunzoni alieonesha kuguswa na tukio wakampiga mawe na akapasuliwa juu ya jicho

Hivi katika mazingira haya unafanya nini? Nani ana wajibu wa kumlinda mwalimu dhidi ya watoto na jamii iliooza? Sisemi wanastahili kipigo kiasi kile ila nataka kila anaesoma hapa achukue nafasi ya Mwalimu. Na ajiulize kama yeye ni mwalimu angejiteteaje na wapi?

Sisi tunakutana na mengi msioyajua, watoto hawa ni wala bange, anakuja shuleni asubuhi kala bangi, kanywa viroba na anakuona mnalingana, huwezi kumwambia kitu, unaweza kuwa unafundisha yupo bize na kipenzi chake wanafanya yanayowapendeza, ukichukua hatua hata ya kupeleka ofisi ya nidhamu basi wewe ni mnoko bifu zinahamia mtaani/kijijini mnakoishi.

Na kadri mtoto mmoja anapoharibikiwa na shule inashindwa kumfukuza (kwasababu ya Siasa) wanaiga waliopo nyuma yake. Tunaishi katika vijiji na miji ambapo walimu ni adui namba moja wa jamii kama tu mwalimu huyo ataonekana ana deal na nidhamu vema. Hata kesi utazushiwa za uongo

Nitoe mfano mwingine, wiki tatu zilizopita nilikuwa na adhibu watoto waliochelewa namba nikiwa zamu, nilipofika kidato cha nne niliadhibu wote isipokuwa mtoto mmoja nilipomfikia akasema sitaki, mie huwa sichapwi, nikatoka nje lakini nimefedheheshwa sana.

Chukua nafasi yangu alafu uamue, ukimwangalia ni mtoto wa kumzaa kabisa ama mdogo wako wa mwisho, vipi ukiwa na hasira katika mazingira kama hayo?

Ndio maana nasema watanzania tunakurupuka na kuongea bila kutazama pande zote hili hukumu ya haki ipite.

Walimu wanastahili haki yao lakini pia ni wakati walimu walindwe dhidi ya watoto wakorofi ama serikali iweke mazingira ya adhabu na watoto walioshindikana.

Wapo walimu waliokwisha zira kabisa wao wame declare kufundisha tu hata mtoto apande juu ya bati hawatamgusa kwakuwa mtoto analindwa kuliko mwalimu, hivi mtoto aliekushika matiti utaendelea kufundisha akiwa hapo shuleni?

Yapo mengi siwezi kuandika yote ila walimu wanajua vema sana mambo haya, wanajua kadhia zinazowakabiri usiku na mchana, kupigwa mawe mitaani, kurushiwa mayai viza, kuzushiwa kesi vijijini kwakuwa tu anachukua hatua za nidhani haya watu hawayaoni, mnaona tu kilichomkuta mtoto ambae hata hajalazwa hospitali.

Kesi za mimba hasifiki mbali kwakuwa walimu uamua kuachana nazo, maana jamii inakubaliana wanayamakiza na mwalimu unaefatilia utakiona cha moto. Walimu wasioyajua haya ni wale wa dar es salaam and the likes. Lkn mwalimu anaeishi nje ya miji mikubwa haya kwake si ya ajabu.

Kwenu mnaoyaona ya ajabu haya.
Ndio maana nikauliza hivi hili ni tukio kubwa nchini kuliko lililo wakuta watafiti Dodoma?

Na ninyi waandishi wa habari na watangazaji wa TV hili ni kubwa kuliko kuuawa kwa au polisi aliemuua Mwangosi?

Ninyi watanzania huko mitaani, bar, na makazini kwenu hamshikani mashati kwa hasira za ubinadamu? Mbona walimu?

Hivi la walimu ni dhambi kuliko la Scorpion alietoa macho watu na hakupewa hukumu ya hapohapo kafikishwa kwenye vyombo vya sheria?

Mwalimu ni mwanadamu kama walivyo wengine wote. Ukweli utasisimama daima

Mwalimu.
Umenena ndugu yangu.
Mwigulu Nchemba watu wanafia kwenye mahabusu kwa vipigo vya Polisi lakini hatukuoni kufukuza kazi askari ila hili la mwanafunzi uko mbele.
 
wasingechukua hatua angetekeleza mkubwa wao huo ndo utendaji kazi wa serikali hii hakuna mlolongo wa maagizo
 
Watu bana waajabu sana mbona mwalimu alivyong'olewa meno matano na wanafunzi hawakuyasema kama hili.
 
Sijui kama hata una shule kichwani mwako? Hivi unadhani kujifunza na kufundisha nikuja shuleni tu kisha wanafunzi wakaandika? Mbona hujauliza kwaini shuleni kuna kusafisha mazingira kabla ya kusoma? Na kama niliajiriwa kufundisha tu kwanini mnaleta kesi za wanafunzi mashuleni tuamue

Ninyi ndio divion zero serikali imewaharibu hata argument na reasoning hakuna

hawa ndio wale ma oya oya...hawafikiriii; wao ni oya oya tuu
 
Walimu wapuuzi sana! Mnashindwa kufundisha watoto kuiadabisha serikali mnakalia kushangilia shemeji unatuachaje?

Shame on youu...!
1475831192566.jpg
 
Mkuu sipingani na wewe. Ila waalim wanafundishwa saikolojia ili kujua mwanafunzi ana hali gani. Sasa kama mwl anaona mwanafunzi anakunywa viroba hahitaji kuanza kubishana nae anatakiwa aende akamripoti kwa mkuu wa shule ili waalim wenye ubavu waje wamwabie atoke nje ya darasa na wamsimamishe shule akakae na mzazi wake siku akirudi kama habadiliki wanamsimamisha tena. Sasa kama kila mara atakuwa anasimamishwa shule na mzazi wake akiona sawa basi ni hasara kwa familia na yeye mwenyewe. Sasa kuanza kubishana na jitu unaona limevuta bangi ni sawa? Au kwa kumwadhibu kama tulivyoona kwenye video ni sawa? Fukuza shule badala ya kujitakia matatizo na wavuta bangi.
Utafukuza wanafunzi wangapi kwa utovu wa nidhamu hasa shule hizi za Kayumba ikiwa sisi wazazi muda mwingine tunawambia walimu wetu wajitahidi kurekebisha tabia za watoto zetu ikiwemo kuwaadhibu mpaka wajirekebishe na tambua kuwa shule za serikali ni tofauti na binafsi hasa za seminari ambazo mtoto hata asipochomekea anarudishwa nyumbani..harafu siku hizi kijana anaenda shule ameshajibusti tayari na viroba,bange na kuberi mwalimu anafundisha anawaza kubeti au mwingine anawaza kutolewa out na mume wa mtu kiasi kwamba hata anapofundishwa anaona anapigiwa kelele na utakuta robo tatu ya darasa wanatumia vilevi kwahiyo hata akidanganya anaumwa ukimwangalia unakuta kalegea na usiyeelewa unaamini kuwa anaumwa kumbe viroba vinafanya kazi
 
Walimu acheni kuhangaika humu JF walimu wenzenu wametenda jinai na sheria inawakata kama msumeno.

Mfahamu mkiwapiga wanafunzi kwa kuwadhalilisha hatutofumbia macho mtakamatwa tu. Period.
 
Watu wanadharau sana watu waliofanya kuwa hapo walipo, walimu waje na kauli mbiu ya tenda wema uende zako. Nimesikitishwa sana na watanzania walio wengi kwa dharau walizoonesha kwa walimu, karibia kila aliyechukizwa na hicho kitendo anasema angekuwa ni mwanaye/mdogo wake angeenda kumpiga huyo/hao walimu, sijaona wanaosema wangeenda mahakamani ili kupata haki, kila mtu anasema angejichukulia sheria mkononi, na hiyo yote ni kwa sababu imefanywa na mwalimu, mnyonge wa kila mtu, sijawahi kuona coment za namna hiyo tukio la kufanana linapofanywa na mtu wa kada nyingine tofauti na mwalimu.

Tujifunze kuheshimiana kila mtu ana umuhimu katika nafasi yake, hata chizi anaumuhimu katika jamii.
Mkuu kwani wale vijana tayari walishafikia kuitwa walimu au ni walimu waliokuwa mafunzoni?
Anashindwa kuidhibiti hasira yake kwa mtoto mdogo kama yule. Akipata hiyo ajira kabisa ndio atawaadhibu na kuwatia ulemavu wa masikio watoto wetu.

Mwalimu anayejua weledi wa kazi yake hawezi kutoa adhabu ya kiwango kile ambacho anastahiki kupewa kibaka na wananchi wenye hasira.
 
Kwa hivyo ni sahihi mwalimu kupigana na mwanafunzi?
Je mwanafunzi angekua na nguvu zaidi akawarudishia na kuwaumiza ungesemaje hapo?
Sio sahihi hata kidogo ila kuna ubinadamu ambao huwa upo. Hapo tungepinga pia na adhabu kwa mwanafunzi ingetolewa ilabisingekuwa na uzito na athari kubwa kama waliyopewa waalimu.
 
Huyu naye ni mwalimu? Anashindwa kuandika maradhi na badala yake anaandika maladhi! Wanafunzi watajifunza nini toka kwake?

Halafu anaandika 'maladhi' mabovu, hivi ni wapi aliposikia kuna maradhi mazuri chini ya hili jua?

Busara ni pamaoja na kukubali kile usichokielewa na kuacha wanaoelewa kuchangia.Badala ya kumshambulia mtoa hoja pamoja na uandishi wake ulipaswa uchangie alichokileta jamvini.

Ukiishambulia hoja unaonekana wa maana kuliko kumshambulia mtoa hoja kwani unakuwa hujachangia lolote katika mjadala.

Kwanini umeuliza kama muandishi ni mwalimu?.Na kama ni kukosea uandishi mbona hata wewe umekosea sehemu nyingi?.Nb;Sitetei uandishi m'bovu ila kama kuna makosa sehemu unarekebisha ndipo uchangie mada.

Katika sentesi ya pili kwenye aya ya kwanza,Je unadhani ulipotumia alama (!) ni sahihi katika uandishi?.
Vipi kuhusu alama inayofuata baada ya ulizo (?),Unajua kuwa kila baada ya alama ya ulizo kuna alama nyingine ya nukta nyuma yake?.Yaani (?.).

Nirudi kwenye mada.Mtoa hoja uko vyema sana ila tatizo ni kwamba hili suala limeshaingiliwa na wanasiasa ndani yake.Walichokifanya walimu kwa adhabu ile siyo uungwana ila serikali ilipaswa kutafuta mbadala wa kutatua tatizo hilo na siyo kama walivyofanya.

Uchunguzi wa kina ufanyike na kama ni adhabu waalimu waadhibiwe kwa mujibu wa sheria na siyo kama hisia za wanasiasa wetu zinavyotaka.

Mwenye bikira ya Ubongo na sie tunaojua kuwa Lugha ni mawasiliano,Bendera kama kitambaa chenye rangirangi,Olimpiki kama michezo,Dini kama imani nk hatuwezi kuliona hili kulingana na kwamba hatuna utamaduni wa kudodosa,kusaili,kuuliza,kuwafuata wahusika wa tatizo fulani,Kutafuta mbadala wa utatuzi wa matizo yetu nk.

Tupo katika dimbwi kubwa lililojaa matope,kunahitajika nguvu ya ziada ili kuweza kutoa miguu yetu katika matope haya.
 
Watu wanadharau sana watu waliofanya kuwa hapo walipo, walimu waje na kauli mbiu ya tenda wema uende zako. Nimesikitishwa sana na watanzania walio wengi kwa dharau walizoonesha kwa walimu, karibia kila aliyechukizwa na hicho kitendo anasema angekuwa ni mwanaye/mdogo wake angeenda kumpiga huyo/hao walimu, sijaona wanaosema wangeenda mahakamani ili kupata haki, kila mtu anasema angejichukulia sheria mkononi, na hiyo yote ni kwa sababu imefanywa na mwalimu, mnyonge wa kila mtu, sijawahi kuona coment za namna hiyo tukio la kufanana linapofanywa na mtu wa kada nyingine tofauti na mwalimu.

Tujifunze kuheshimiana kila mtu ana umuhimu katika nafasi yake, hata chizi anaumuhimu katika jamii.

Great thinking!! Nimekuelewa sana Mkuu.

Tunaishi kishabiki sana kuliko ki-uhalisia.
 
Mi nadhan mizuka kama alivowahi kusema sugu ndio inayoendelea hapa. Tatizo la viongozi wetu wanafanya maamuzi bila kufuata principles za natural justice. Siwatetei walimu kwa walichokifanya ila cha msingi wanaotoa maamuzi wanapaswa kusikiliza pande zote. Huenda kuna mengi yaliyojificha nyuma ya pazia, waalim nao sio wajinga kushusha kipigo cha hatua ile kwa kesi ya dogo kutofanya homework tu. Huenda dogo nae alijifanya scorpion wa mbeya.
 
Nimekuja tena na kadhia nyingine, tuwaonee huruma Walimu. Naomba Viongozi watoe matamko makali makali kama yale ya jana. Unaweza kuongeza kama una tukio lingine la kuumiza kwa Walimu wetu ikiwemo lile la Walimu kuvamiwa na Popobawa

Mbona hili sikuwasikia wakiliakomalia??

Wanafunzi 15 waliocharaza viboko walimu
wasimamishwa
WANAFUNZI 15 wa Kidato cha Sita wa
Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele
Mkoa wa Katavi wameamriwa kurejea
nyumbani kwa wiki mbili kwa kosa la
kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko
walimu wao wawili akiwemo Makamu
Mkuu wa Shule, Makonda Ng’oka
‘Membele’ (34) ambaye ameng’olewa
meno matano kwa kipigo hicho.
Je! Hili vipi Mwalim kawa kilema???

Mke wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kelema Balai aliyeuawa kwa kupigwa mshale wa sumu na kijana ambaye mpaka sasa ametoweka hapo kijijini kutokana na ugomvi ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya mume wa marehemu na kijana huyo anayehisiwa kutenda unyama.

Imesemekana mtuhumiwa akiwa na wenzake wawili siku ya tukio majira ya saa mbili na nusu usiku walivamia nyumbani kwa marehemu na kuanza kumshambulia kwa fimbo mume wa marehemu na kukimbizwa hospital ya jirani kabla muhisiwa hajarejea na kutekeleza unyama huo.

Mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi ambao ni baba wa kijana huyo kwa kuwa alishiriki katika tukio la awali la kumjeruhi Mwalimu Manyama kwa kushirikiana na kijana wake kumjeruhi kwa fimbo.

(Mwl Manyama ndiye mume wa marehemu) Watu wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na Mtendaji wa Kijiji. Hawa wanashikiliwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya baada ya maelezo yao waliyoyatoa kuhusiana na namna walivyoshughulikia tukio hili kuanzia usiku mpaka asubuhi kuto mridhisha Mkuu wa Wilaya. Kwani toka usiku wa tarehe 3 mpaka saa tatu wahisiwa walikuwepo kijijini kabla ya kutoweka na Viongozi hao hwakuwa wamechukua hatua zozote.
 
chuo kikuu kipo chini ya wizara ya nani?
Umesema sheria ifuate mkondo, hao mawaziri na matamko yao wamefuata sheria gani? Hakuna sheria zinazofuatwa zaidi ya kupeleka mashitaka mahakamani ili yatafsiriwe kisheria, sasa Ndalichako na yule wa tamisemi wamekuwa wanasheria??
 
Umesema sheria ifuate mkondo, hao mawaziri na matamko yao wamefuata sheria gani? Hakuna sheria zinazofuatwa zaidi ya kupeleka mashitaka mahakamani ili yatafsiriwe kisheria, sasa Ndalichako na yule wa tamisemi wamekuwa wanasheria??
sheria ifuate mkondo wake.
 
Back
Top Bottom