Hivi haya maandiko yana maanisha hivi?

Kwenye Biblia,Mw 2:18 imeandikwa;"BWANA Mungu akasema,Si vema huyo mtu awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae".Ndipo akamletea wanyama kibao lakini hakuonekana wa kufanana nae,Mw 2:19-20,ndipo Mungu alipomuumba mwanamke kutoka ubavuni mwa Adam. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Hapa nimegundua kuwa,Mwanaume alianza kuhitaji msaidizi wa kawaida lakini ngono sio sababu ya kuumbwa mwanamke.Pili,mwanaume alihitaji kusaidiwa,hii maana yake ni kwamba,Mwanaume kamwe hawezi kutimiza majukumu yake bila mwanamke.Tatu,mwamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume,lakini mwanaume hakuumbwa kwaajili ya mwanamke.Nne,kazi iliyomleta au kusababisha mwanamke kuumbwa ni kumsaidia mwanaume tu.Tano,malengo ya uumbaji wa Mungu hayakumhusisha mwanamke,yaani mwanamke yupo duniani si kwaajili ya kutimiza malengo ya uumbaji wa Mungu bali kumsaidia mwanaume kuyatimiza malengo ya Mungu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Jamani msinirushie mawe,kama Mungu hakumaanisha hivyo leta tafsiri yako,unless uwe huiamini Biblia.Hebu tujadiliane inawezekana nimepotoka!

Eiyer hapo kwa red pakisomeka hivi nitakosea? "yaani mwanamke yupo duniani si kwa ajili ya mwanaume bali kutimiza malengo ya uumbaji wa Mungu kupitia kwa mwanaume"
 
Eiyer hapo kwa red pakisomeka hivi nitakosea? "yaani mwanamke yupo duniani si kwa ajili ya mwanaume bali kutimiza malengo ya uumbaji wa Mungu kupitia kwa mwanaume"

Kwani mwanamke aliumbwa kwaajili ya nani?
 
Suala la nyoka umelitoa wapi?
Heeheee! Nimelitoa kwenye Biblia! Na suala la kusudi la kuumbwa kwa mwanamke, na tukio zima la mwanamke huyohuyo kudanganywa na yule nyoka vina maelezo ya aina nyingi na mengine ya ajabu sana! Vipi unawaogopa sana nyoka?!
 
Siogopi nyoka bana,ila sijamtaja kwenye mada pia sijazungumzia kudangaywa pia!
 
Eiyer , kama kila mtu kaumbiwa wake, mbona mpaka leo ni single.......na kwanin Bikira Maria awe single woman kama alishawekewa mwenzi wake?

Na kwanini Mungu apoteze hesabu ya kuwa wanawake wazidi population ya wanaume, hakujua kama kutasababisha excess supply?

Bikira Maria alikua virgin pindi anamzaa Yesu ila baada ya hapo alipata watoto wengine yani wadogo zake Yesu hivyo hakuendelea kuwa virgin. Nadhani Mungu kaona mwanaume anataka msaada zaidi ndo maana kaongeza idadi ya wanawake so mkiona wanaume tuna warembo saba saba msishangae huo ni mpango.
 
Sisi wapagani tunaamini kwamba Mungu wetu aliumba mwanamke na mwanaume ili waijaze dunia kwa kuzaana bila masharti, na ndio maana wazee wetu walioa wanawake wengi bila masharti, lakini hawa wakoloni wametuletea dini ambazo zinatuwekea msharti, mara kuoa mke mmoja, mara kuoa mwisho wanawake wanne..... na masharti kibao.
Sisi wapagani hatujui kuoa tunajua kuzaa tu basi, hakuna mahali Mungu alisema muoane, bali alisema muende mkazaane muijaze dunia........

Mnaniudhi nyie na dini zenu hizo..................LOL
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mtambuzi bana,nijuavyo mimi ni kuwa mpagani haamini katika Mungu wala uumbaji,unaposema "sisi wapagani tunaamini Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume" unanichanganya.Pia unaposema kuoa wanawake wasiokua na idadi,nafikiri hiyo sio tabia ya kibinadamu,wanyama wasiofikiri ndo wanafanya mapenzi bila kupima wala kufikiri.Kuwa na mwanamke mmoja ni nature ya ubinadamu!
 
Sina nguvu na mood ya kubishana leo!

Lkn umejiuliza kwanini wanyama na mimea ameumba ke na me? Kama sio kuendeleza reproduction?

Hongera kwa mashoga wao ndio wamekamilika kwa mahitaji ya ngono lkn si kireproduction.

Na kumbuka 95% ya vitabu vya biblia vimeandikwa na wanaume!
 
Adam aliona wanyama wengine wanakula bata na wenzi wao, Mungu akaona si vyema aendelee kula chabo nitamfanyizia wa kwake
 
Hivi nilishakuambiaga kuwa nakupendaga sana my lil bro? Kama bado, its official! I love you!
Mtambuzi bana,nijuavyo mimi ni kuwa mpagani haamini katika Mungu wala uumbaji,unaposema "sisi wapagani tunaamini Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume" unanichanganya.Pia unaposema kuoa wanawake wasiokua na idadi,nafikiri hiyo sio tabia ya kibinadamu,wanyama wasiofikiri ndo wanafanya mapenzi bila kupima wala kufikiri.Kuwa na mwanamke mmoja ni nature ya ubinadamu!
 
Mtambuzi bana,nijuavyo mimi ni kuwa mpagani haamini katika Mungu wala uumbaji,unaposema "sisi wapagani tunaamini Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume" unanichanganya.Pia unaposema kuoa wanawake wasiokua na idadi,nafikiri hiyo sio tabia ya kibinadamu,wanyama wasiofikiri ndo wanafanya mapenzi bila kupima wala kufikiri.Kuwa na mwanamke mmoja ni nature ya ubinadamu!
Mkuu kila dini ina Mungu wao, kwa mfano kule India kuna Miungu zaidi ya 1000, na hata wapagani wana Mungu wao............ Yaani yule wanayeamani kwamba ndio aliyewaumba na kuwaleta hapa duniani.
 
Kiufupi upagani ni kuamini kwenye Mungu asie hai. Kuamini jua, mlima, mnyama etc huo ndio unaitwa upagani. Well, definition ya mzungu akiuza sera za kubadilishana na chumvi, kahawa na pamba.
 
Mi sio mbishi kiviiileeee...wala sikubishiii wewe, wala siyabishii hayo maandishi. Swali moja najiuliza MWANAUME ni NANI? Na MWANAMKE ni nani? Ahii mi hata sijui nawaza nini wacha niende zangu......MWANAUME wakufanya mambo ya kiume hata yakaonekana kweli huyu ni MWANAUME anayestahili kusaidiwa na kuheshimiwa na kumtii yupo?

Hebu ngoja...MWANAMKE wakukaa na kumtii na kumheshimu MWANAUME na kukubali kutawaliwa kuanzia unywele wa kichwani hadi ukucha wa mguuni.

Kwa tabia hizi hizi, na dunia hii hii ya UBINAFSI UBINAFSI? aaah mi sijui bwana lakini hayo maandiko yakiitmia maishani mwako ukawa MWANAUME ukampata MWANAMKE...dunia itakuwa paradiso.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom