Hivi hawa Bongo Movie wanatuonaje?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,017
2,384
Leo nikasema ngoja niangalie vya nyumbani nimefungua YouTube. Nikawa naangalia tamthilia moja ya bongo muvi, asa kuna sehem mama mjamzito amepigwa risasi basi watu waliomzunguuka wakaita ambulance. "hallo ambulance kuna ajali hapa" na yule ambulance akajibu "sawa nakuja" 😂

Nikajisemea mwenyewe asa anakuja, anakuja wapi wakati aliepiga simu ata hakutoa maelezo juu ya tukio na sehem ajali ilipotokea 🤦‍♀️

Haikuishia hapo mara ambulance ikafika wakachukua majeruhi wakampeleka hospital. Kufika hospital badala ya kumpeleka emergency wakampeleka chumba cha mapunziko wakati kwa maelezo yao na muonekano wa majeruhi alikua ameumia damu kila sehem alaf ni mjamzito. Nilivoona ivo tu nikaacha kuangalia, sijui wanatuchukuliaje hawa wanatuona mazoba flani ivi

Muvi na tamthilia zao hazina uhalisia. Kabla ya kuigiza nendeni sehem husika mkapate maelezo kwanza kabla ya kuigiza vitu ambavo havina uhalisia.

Kwa Kawaida mtu ukiita ambulance anaepiga simu lazime aeleze mahali tukio limetokea na atoe adresi ili iwe rahisi ambulance kufika. Na anatakiwa aeleze hali ya mgonjwa ilivo kwa kifupi. Kama ni mjamzito inabidi useme. Na ni ajali ya nini. Inabidi aeleze yote haya kwa ufupi kwa mda usiozidi hata dakika 3.

Alafu sio lazima muigize kila kitu. We tangu lini Tanzania kukawa na ambulance za kufata watu nyumbani kama sio uongo nini. Jirekebisheni au kama sio mtazidi kulamika hatupendi vya kwetu wakati nyie mnatufanya sisi wajinga. Sijui huwa mnatuchukuliaje 👀
 
Ukitaka kuinjoi bongo movies usiangalie details wewe furahia story inavyoenda.
Kama hapo ungeangalia tu mama mjamzito aliipigwa risasi mwisho wa siku akapelekwa hospitali inatosha, tena ukiandikiwa Watch out part two

Unakaa na hamu ya kujua kama alifariki au la
 
Kuna movie moja gari ilipata ajali waligonga mti , ili kuonyesha gari limeharibika mara watu wanatoka kwenye screpa ya gari lingine ,kumbe wameleta screpa wakaweka pale ili ionekane gari ilivyoharibika kwa ajali,bongo movie bado sana
 
kwahiyo umeacha kuangalia hiyo movie ya kibongo baada ya ambulance kumfikisha majeruhi hospitali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom