Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,818
Kwema wadau?

Mwaka huu mwanzoni nikiwa nimetoka kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya na nikiwa nimefanya maombi ya mipango yangu mingi kwa mwaka huu na kumsihi sana Mungu wangu aliye hai anijalie afya, uhai, furaha na amani tu mengine nayaweza hayanisumbui kabisa, basi sikuwa najua siku chache zijazo nitakutana na jambo baya na la kutisha kiasi icho.

Siku ya Tukio;

Nikiwa nawahi zangu kwenye majukumu yangu ya kikazi asubuhi kabisa hapa ndani ya Dar es Salaam tena nikiwa sina hofu wala kuwaza lolote, ile wazungu wanaita "the fear of unknown" kwamba kama kuna jambo baya linaenda kutokea basi kuna ishara flani huwa zinakusumbua kama kukosa amani and so, but mie siku hiyo haikuwa hivyo wala na nilikuwa nawaza tu niwahi kufika ofisini.

Ni asubuhi hio nikiwa ktk mwendo wa kawaida kabisa katika chombo private tu, ghafla kitu kikaniambia "be very careful" na nikaitii hii sauti so nikapunguza kabisa mwendo wa chombo changu na nikawa kawaida kabisa, haikupita hata dk 10 mbele yangu nikaona daladala mbili zinafukuzana kuwahiana abiria, kama kawaida yao hawa mabwana na ujinga wao wa kuwawahi abiria wa mbele zao, so hizi daladala hazikuwa upande wangu zilikuwa kulia kwanguwmie nikiwa kushoto so nilikuwa naziona face to face na nikajua kila mtu ni lazima aheshimu sheria za barabara na kukaa upande wake, sasa haikuwa hivi, yule dereva aliyekuwa anapitwa akafanya kumu overtake mwenzake nadhani bila kuangalia na labda atakuwa ni mjinga wa kuzaliwa wa kweli kweli, na ikumbukwe njia ilikuwa imenyooka so nimeanza kuwaona toka ka distance flani hivi mbele yangu wakifanya huo ujinga na haikuchukua hata dakika tatu tangu nianze kuwaona na kuniletea changamoto mbaya sana, yule dereva mwingine wa daladala alie overtake bila kuangalia nadhani ile gari ilimshinda au sijui kama shetani aliingilia kati ila nilishangaa tu kishindo kanigonga face to face wakuu, aisee nilishangaa sana lakini kuja kustuka naona damu zimejaa chini ya gari langu, airbag na watu wanapiga kelele, sikuzimia wala sikuskia maumivu ila nilikuwa kwenye mshtuko mkubwa sana sana.

Ile gari ilivyonigonga na ilizima pale pale yenyewe tu na kwangu huku sikuona tena ya mbele, nikawa najipapasa nikihofu yasije yakawa mambo ya uti wa mgongo kushtuka na kushindwa kuamka forever, nikajaribu kutikisha miguu naona mguu mmoja haurespond na kama bega linaniuma hivi, sikujua tena nini kimetokea ila mguu ulivunjika, bega kustuka na huu mguu uliovunjika ni tuseme ulikuwa umepasuka na ndo chanzo cha zile damu, na hii baadae nilikuja kujua ni kwamba nilikanyaga break kwa nguvu na kunyoosha mguu kwa kukaza labda kwa kustuka au hofu so gari ilivyopigwa kwa nguvu na kubonyea so presha yake na effect ndo ikaniletea hayo madhara.

Kilichofuata kuanzia hapo ikawa sina sauti tena, naona naamriwa tu vitu na wananchi waliokuwa wamejazana pale, kila mmoja akisema hivi na mwingine akisema vile na wangine wakirekodi kwa simu tukio lile na mie mwenyewe nikiwa bado nna mstuko mkubwa sana nawaza hivi ni mimi au naota? Nikiaskia sauti mkagueni vizuri labda ameumia kichwa?

Nikaskia shauri likiendeshwa juu yangu, wananchi wakasema tumpeleke polisi tukachukue PF3, wakaja kunitoa huku naona watu wameshika vichwa wakina mama wanalia na mie sasa nikaanza kuogopa uende nimeumia sana kuliko ambavyo najiwazia wakati huo, so najaribu kusimama mwenyewe siwezi, wananibeba na wanasema twende polisi, damu kila mahala na huo ni mguu tu, japo nna maumivu ya bega na mkono lakini najishangaa nasema kwa namna damu hizi zinavyotoka huko polisi ntafika nikiwa mzima kweli? Na kwa maeneo hayo kituo cha polisi kipo wapi sasa? Na je kutokea hapo mpaka kufika Hospitali itakuaje? Naona kabisa wananchi hawana elimu juu ya kuzuia damu kutoka na i feel like labda nijisaidie ila siwezi kufanya lolote, moyo unaenda speed sana na bado niko shocked tu.

Polisi hapakuwa mbali na hawakuwa na hiyana, ni kakituo ka dogo hakukuwa na jam ni walinihudumia ndani ya dakika 5 tu nikaipata pf3 tukaondoka na wananchi ambao walikuwa wamenibeba kwenye kirikuu.

So tukaelekea hospitali na hapa ntaomba nisitaje majina ya hospitali wananchi wasije wakaamua kwenda kuzichoma moto, so nikapelekwa hospital ya wilaya, mpaka nafika hospitali hapo nadhani labda nilikuwa nimebakiza damu lita mbili tu nadhani, so jamaa hakuna wanachokifanya, manesi wananitizama tu, nikawa mkali, wakasema wewe mgonjwa unamfokea nani? Daah bongo😂😂, akaja muuguzi mmoja akanichoma sindano ya tetenasi na nyingine sijui ni nini, nikamwambia wewe bwana embu fanya kitu kuzuia damu basi, wakaanza kunizuia damu na wakafanikiwa lakini nadhani mpaka muda huo labda nilikua nna lita moja tu mwilini, nikaanza kuskia kabisa moyo unasukuma kitu kisicho kuwepo.

Lakini pale pale najiuliza ina maana nchi hii mtu anaweza kufariki kisa mguu, mkono na bega? how could that be possible? Ila nikajisemea "mimi sitokufa mahala hapa na wakati wangu bado haujafika, ewe Mungu wa haki usinichukue nikiwa katika umri huu nna deni na wewe", sasa Mungu ni muaminifu sana, baada ya kusema maneno hayo nikawa najipa moyo mkuu na imani na japo naskia sina damu na ata kuongea tu tabu, moyo una push kitu kisicho kuwepo, kazi yangu ikawa ni kurudia tu hayo maneno hapo juu, natamani labda nilale niamke nikiwa fresh ila hakuna kitu siwezi ata kusinzia au kuzimia.

Ile hospital ya wilaya wakasema hatuwezi kumtibu, mpelekeni hospital ile ya taifa, na mpaka muda huo hapo kwenye hio hospitali wamenichoma sindano mbili tu, drip ya maji na wakanipa rufaa kwenda kwenye ile hospitali nyingine baba lao.

Mpaka muda huo, wadau wangu washafika so ikabidi tutafute private ambulance sababu hio hospital wanasema ambulance ipo moja na imempeleka mgonjwa mmoja hospital ya taifa so tuisubirie na hapo tumesubiria saa na nusu haiji ndo kufanya maamuzi ya private ambulance.

Kufika kwenye ile hospital baba lao la taifa aisee kumbe bora kule wilayani ambako hawana kitu, wale wako too slow, yaani unawaona kabisa hakuna kitu kinachoweza kuwastua, wamezoea matatizo na kila mtu anapita tu ana shangaa shangaa hivi anaondoka, vijana wadogo ndo wajinga zaidi pale yaani wako sector ya emergence ila wanachezea tu simu ambazo ata ukiziangalia simu zenyewe ni tecno na samsung A series, hakuna humanity, samahani kwa kuyasema haya ila ndo nimeyaona tena emergence kabisa sasa fikiria kule kwengine ndo kupoje?

So wadau wangu wakaanza kutilia mkazo na mikwala mingi ndo na wale kuanza kunihudumia, na kila dakika hapo emergence wanaletwa watu ambao wanalia kila mtu kama anachinjwa hivi.

Sina damu na moyo unapambana sana kwa zaidi ya masaa matano sasa toka tukio litokee, naskia njaa naskia kiu na kama siwezi kupumua vizuri iv yaan nna fosi, ajab sizimii wala sisinzii, so hawa nao wakaniwekea drip za maji, nawaambia wazee nahitaji damu nitoleeni haya ma maji yenu hakuna kitu yanacho nisaidia hapa, wananiambia ngoja tukuchukue vipimo kwanza na tuone, basi wadau wangu waka fosi ki mjini mjini mambo yakaanza kukimbizwa na nini, mpaka naingia chumba cha upasuaji ni masaa 11 yamepita toka nipate ajali na damu kuniisha mwilini.

Basi baadae nikaingia wodini tena na nini, kuanza kupona sasa na nini ila expirience ambayo sio ya kuombea.

Namshukuru Mungu wangu alie mkuu sana, sikufa siku ile na sitarajii kufaa miaka hii hii na amenipa uhai na ataendelea kunipa uhai na tukio hili limeniweka karibu sana na yeye.

Kule wodini na tiba zingine unashangaa wataalam wanakwambia "aah kitu ichi hakiwi covered na bima ya nhif, aah hapa inabidi ulipe kiasi flani, aah kamuone flani" yaan unashangaa jambo dogo lina mlolongo mrefu ambao ni very unnecessary.

Wodini mule wadau wakaanza kunipa habari za namna watu wanavyoteseka na wengine ambao hua wanafia emergence, so scarry wazee. Bongo hauna kitu unaondoka unajiona wakuu, so hata kutafta room private nalo mpaka mchongo eti daah 😂😂 aisee.

Naomba kuishia hapo, nilitoka hospital sikumaliza hata siku saba, nilifosi nikaondoka kibishi tu na kuendelea na tiba tokea nyumbani kwangu na Mungu mwingi wa rehema na neema basi nimepona ndio niko narudi rudi na mimi kwenye majukumu yangu mengine, wale walionosababishia hayo matatizo ndo nataka kuanza kuwashughulikia sasa na sitokuwa na msamaha ktk hili. Lakini sitosahau miezi miwili iliyopita wazee nilikuwa kama niko Ukraine mstari wa mbele pale kumpinga bwana Putin asiendelee na majeshi yake kuichukua Kyiv.

Sijajua wewe umewahi kuyapata yapi au umewahi kuyaona yapi ya kuhusu ajali hizi za barabarani na experience za ma hospital yetu ambayo unaweza uka dead unajiona! Basi itakua vyema ukishare nasi basi tukapata la kujifunza.

Wasalaam.
 
Kwema wadau?

Mwaka huu mwanzoni nikiwa nimetoka kusheerekea sikukuu ya mwaka mpya na nikiwa nimefanya maombi ya mipango yangu mingi kwa mwaka huu na kumsihi sana Mungu wangu aliehai anijalie afya, uhai, furaha na amani tu mengine nayaweza hayanisumbui kabisa, basi sikua najua siku chache zijazo ntakutana na jambo baya na la kutisha kiasi icho.

Siku ya Tukio;

Nikiwa nawai zangu kwenye majukumu yangu ya kikazi asubuhi kabisa hapa ndani ya Dar es Salaam tena nikiwa sina hofu wala kuwaza lolote, ile wazungu wanaita "the fear of unknown" kwamba kama kuna jambo baya linaenda kutokea basi kuna ishara flani hua zinakusumbua kama kukosa amani and so, but mie siku hio haikua hivyo wala na nilikua nawaza tu niwai kufika ofisini.

Ni asubuhi hio nikiwa ktk mwendo wa kawaida kabisa katika chombo private tu, ghafla kitu kikaniambia "be very careful" na nikaitii hii sauti so nika punguza kabisa mwendo wa chombo changu na nikawa kawaida kabisa, haikupita ata dk 10 mbele yangu nikaona daladala mbili zinafukuzana kuwaiana abiria, kama kawaida yao hawa mabwana na ujinga wao wa kuwawai abiria wa mbele zao, so hizi daladala hazikua upande wangu zilikua kulia kwanga mie nikiwa kushoto so nilikua naziona face to face na nikajua kila mtu ni lazima aheshimu sheria za barabara na kukaa upande wake, sasa haikua hivi, yule dereva aliekua anapitwa akafanya kumu overtake mwenzake nadhani bila kuangalia na labda atakua ni mjinga wa kuzaliwa wa kweli kweli, na ikumbukwe njia ilikua imenyooka so nimeanza kuwaona toka ka distance flani iv mbele yangu wakifanya huo ujinga na haikuchukua hata dakika tatu tangu nianze kuwaona na kuniletea changamoto mbaya sana, yule dereva mwingine wa daladala alie overtake bila kuangalia nadhani ile gari ilimshinda au sijui kama shetani aliingilia kati ila nilishangaa tu kishindo kanigonga face to face wakuu, aisee nilishangaa sana lakin kuja kustuka naona damu zimejaa chini ya gari langu, airbag na watu wanapiga kelele, sikuzimia wala sikuskia maumivu ila nilikua kwenye mshtuko mkubwa sana sana.

Ile gari ilivyonigonga na ilizima pale pale yenyewe tu na kwangu huku sikuona tena ya mbele, nikawa najipapasa niki hofu yasije yakawa mambo ya uti wa mgongo kushtuka na kushindwa kuamka forever, nikajaribu kutikisha miguu naona mguu mmoja haurespond na kama bega linaniuma iv, sikujua tena nini kimetokea ila mguu ulivunjika, bega kustuka na huu mguu uliovunjika ni tuseme ulikua umepasuka na ndo chanzo cha zile damu, na hii baadae nilikuja kujua ni kwamba nilikanyaga break kwa nguvu na kunyoosha mguu kwa kukaza labda kwa kustuka au hofu so gari ilivyopigwa kwa nguvu na kubonyea so presha yake na effect ndo ikaniletea hayo madhara.

Kilichofuata kuanzia hapo ikawa sina sauti tena, naona naamriwa tu vitu na wananchi waliokua wamejazana pale, kila mmoja akisema iv na mwingine akisema vile na wangine wakirekodi kwa simu tukio lile na mie mwenyewe nikiwa bado nna mstuko mkubwa sana nawaza hivi ni mimi au naota? Nikiaskia sauti mkagueni vizuri labda ameumia kichwa?

Nikaskia shauri likiendeshwa juu yangu, wananchi wakasema tumpeleke polisi tukachukue PF3, wakaja kunitoa huku naona watu wameshika vichwa wakina mama wanalia na mie sasa nikaanza kuogopa uende nimeumia sana kuliko ambavyo najiwazia wakati huo, so najaribu kusimama mwenyewe siwezi, wananibeba na wanasema twende polisi, damu kila mahala na huo ni mguu tu, japo nna maumivu ya bega na mkono lakini najishangaa nasema kwa namna damu hizi zinavyotoka huko polisi ntafika nikiwa mzima kweli? Na kwa maeneo hayo kituo cha polisi kipo wapi sasa? Na je kutokea hapo mpaka kufika Hospitali itakuaje? Naona kabisa wananchi hawana elimu juu ya kuzuia damu kutoka na i feel like labda nijisaidie ila siwezi kufanya lolote, moyo unaenda speed sana na bado niko shocked tu.

Polisi hapakua mbali na hawakua na hiyana, ni kakituo ka dogo hakukua na jam ni walinihudumia ndani ya dakika 5 tu nikaipata pf3 tukaondoka na wananchi ambao walikua wamenibeba kwenye kirikuu.

So tukaelekea hospitali na hapa ntaomba nisitaje majina ya hospitali wananchi wasije wakaamua kwenda kuzichoma moto, so nikapelekwa hospital ya wilaya, mpaka nafika hospital hapo nadhani labda nilikua nimebakiza damu lita mbili tu nadhani, so jamaa hakuna wanachokifanya, manesi wananitizama tu, nikawa mkali, wakasema wewe mgonjwa unamfokea nani? Daah bongo😂😂, akaja muuguzi mmoja akanichoma sindano ya tetenasi na nyingine sijui ni nini, nikamwambia wewe bwana embu fanya kitu kuzuia damu basi, wakaanza kunizuia damu na wakafanikiwa lakini nadhani mpaka muda huo labda nilikua nna lita moja tu mwilini, nikaanza kuskia kabisa moyo unasukuma kitu kisicho kuwepo.

Lakini pale pale najiuliza ina maana nchi hii mtu anaweza kufariki kisa mguu, mkono na bega? how could that be possible? Ila nikajisemea "mimi sitokufa mahala hapa na wakati wangu bado haujafika, ewe Mungu wa haki usinichukue nikiwa katika umri huu nna deni na wewe", sasa Mungu ni muaminifu sana, baada ya kusema maneno hayo nikawa najipa moyo mkuu na imani na japo naskia sina damu na ata kuongea tu tabu, moyo una push kitu kisicho kuwepo, kazi yangu ikawa ni kurudia tu hayo maneno hapo juu, natamani labda nilale niamke nikiwa fresh ila hakuna kitu siwezi ata kusinzia au kuzimia.

Ile hospital ya wilaya wakasema hatuwezi kumtibu, mpelekeni hospital ile ya taifa, na mpaka muda huo hapo kwenye hio hospital wamenichoma sindano mbili tu, drip ya maji na wakanipa rufaa kwenda kwenye ile hospital nyingine baba lao.

Mpaka muda huo, wadau wangu washafika so ikabidi tutafute private ambulance sababu hio hospital wanasema ambulance ipo moja na imempeleka mgonjwa mmoja hospital ya taifa so tuisubirie na hapo tumesubiria saa na nusu haiji ndo kufanya maamuzi ya private ambulance.

Kufika kwenye ile hospital baba lao la taifa aisee kumbe bora kule wilayani ambako hawana kitu, wale wako too slow, yaani unawaona kabisa hakuna kitu kinachoweza kuwastua, wamezoea matatizo na kila mtu anapita tu ana shangaa shangaa iv anaondoka, vijana wadogo ndo wajinga zaidi pale yaani wako sector ya emergence ila wanachezea tu simu ambazo ata ukiziangalia simu zenyewe ni tecno na samsung A series, hakuna humanity, samahani kwa kuyasema haya ila ndo nimeyaona tena emergence kabisa sasa fikiria kule kwengine ndo kupoje?

So wadau wangu wakaanza kutilia mkazo na mikwala mingi ndo na wale kuanza kunihudumia, na kila dakika hapo emergence wanaletwa watu ambao wanalia kila mtu kama anachinjwa hivi.

Sina damu na moyo unapambana sana kwa zaidi ya masaa matano sasa toka tukio litokee, naskia njaa naskia kiu na kama siwezi kupumua vizuri iv yaan nna fosi, ajab sizimii wala sisinzii, so hawa nao wakaniwekea drip za maji, nawaambia wazee nahitaji damu nitoleeni haya ma maji yenu hakuna kitu yanacho nisaidia hapa, wananiambia ngoja tukuchukue vipimo kwanza na tuone, basi wadau wangu waka fosi ki mjini mjini mambo yakaanza kukimbizwa na nini, mpaka naingia chumba cha upasuaji ni masaa 11 yamepita toka nipate ajali na damu kuniisha mwilini.

Basi baadae nikaingia wodini tena na nini, kuanza kupona sasa na nini ila expirience ambayo sio ya kuombea.

Namshukuru Mungu wangu alie mkuu sana, sikufa siku ile na sitarajii kufaa miaka hii hii na amenipa uhai na ataendelea kunipa uhai na tukio hili limeniweka karibu sana na yeye.

Kule wodini na tiba zingine unashangaa wataalam wanakwambia "aah kitu ichi hakiwi covered na bima ya nhif, aah hapa inabidi ulipe kiasi flani, aah kamuone flani" yaan unashangaa jambo dogo lina mlolongo mrefu ambao ni very unnecessary.

Wodini mule wadau wakaanza kunipa habari za namna watu wanavyoteseka na wengine ambao hua wanafia emergence, so scarry wazee. Bongo hauna kitu unaondoka unajiona wakuu, so hata kutafta room private nalo mpaka mchongo eti daah 😂😂 aisee.

Naomba kuishia hapo, nilitoka hospital siku maliza hata siku saba, nilifosi nikaondoka kibishi tu na kuendelea na tiba tokea nyumbani kwangu na Mungu mwingi wa rehema na neema basi nimepona ndio niko narudi rudi na mimi kwenye majukumu yangu mengine, wale walionosababishia hayo matatizo ndo nataka kuanza kuwashughulikia sasa na sitokua na msamaha ktk hili. lakini sitosahau miezi miwili iliyopita wazee nilikua kama niko Ukraine mstari wa mbele pale kumpinga bwana Putin asiendelee na majeshi yake kuichukua kyiv.

Sijajua wewe umewai kuyapata yapi au umewai kuyaona yapi ya kuhusu ajali hizi za barabarani na expirience za ma hospital yetu ambayo unaweza uka dead unajiona! basi itakua vyema ukishare nasi basi tukapata la kujifunza.

Wasalaam.
Hao wajinga wa dala dala walipishe kila kitu
 
So tukaelekea hospitali na hapa ntaomba nisitaje majina ya hospitali wananchi wasije wakaamua kwenda kuzichoma moto, so nikapelekwa hospital ya wilaya, mpaka nafika hospital hapo nadhani labda nilikua nimebakiza damu lita mbili tu nadhani, so jamaa hakuna wanachokifanya, manesi wananitizama tu, nikawa mkali, wakasema wewe mgonjwa unamfokea nani? Daah bongo, akaja muuguzi mmoja akanichoma sindano ya tetenasi na nyingine sijui ni nini, nikamwambia wewe bwana embu fanya kitu kuzuia damu basi, wakaanza kunizuia damu na wakafanikiwa lakini nadhani mpaka muda huo labda nilikua nna lita moja tu mwilini, nikaanza kuskia kabisa moyo unasukuma kitu kisicho kuwepo.

Lakini pale pale najiuliza ina maana nchi hii mtu anaweza kufariki kisa mguu, mkono na bega? how could that be possible? Ila nikajisemea "mimi sitokufa mahala hapa na wakati wangu bado haujafika, ewe Mungu wa haki usinichukue nikiwa katika umri huu nna deni na wewe", sasa Mungu ni muaminifu sana, baada ya kusema maneno hayo nikawa najipa moyo mkuu na imani na japo naskia sina damu na ata kuongea tu tabu, moyo una push kitu kisicho kuwepo, kazi yangu ikawa ni kurudia tu hayo maneno hapo juu, natamani labda nilale niamke nikiwa fresh ila hakuna kitu siwezi ata kusinzia au kuzimia.

Ile hospital ya wilaya wakasema hatuwezi kumtibu, mpelekeni hospital ile ya taifa, na mpaka muda huo hapo kwenye hio hospital wamenichoma sindano mbili tu, drip ya maji na wakanipa rufaa kwenda kwenye ile hospital nyingine baba lao.

Mpaka muda huo, wadau wangu washafika so ikabidi tutafute private ambulance sababu hio hospital wanasema ambulance ipo moja na imempeleka mgonjwa mmoja hospital ya taifa so tuisubirie na hapo tumesubiria saa na nusu haiji ndo kufanya maamuzi ya private ambulance.

Kufika kwenye ile hospital baba lao la taifa aisee kumbe bora kule wilayani ambako hawana kitu, wale wako too slow, yaani unawaona kabisa hakuna kitu kinachoweza kuwastua, wamezoea matatizo na kila mtu anapita tu ana shangaa shangaa iv anaondoka, vijana wadogo ndo wajinga zaidi pale yaani wako sector ya emergence ila wanachezea tu simu ambazo ata ukiziangalia simu zenyewe ni tecno na samsung A series, hakuna humanity, samahani kwa kuyasema haya ila ndo nimeyaona tena emergence kabisa sasa fikiria kule kwengine ndo kupoje?

So wadau wangu wakaanza kutilia mkazo na mikwala mingi ndo na wale kuanza kunihudumia, na kila dakika hapo emergence wanaletwa watu ambao wanalia kila mtu kama anachinjwa hivi.

Sina damu na moyo unapambana sana kwa zaidi ya masaa matano sasa toka tukio litokee, naskia njaa naskia kiu na kama siwezi kupumua vizuri iv yaan nna fosi, ajab sizimii wala sisinzii, so hawa nao wakaniwekea drip za maji, nawaambia wazee nahitaji damu nitoleeni haya ma maji yenu hakuna kitu yanacho nisaidia hapa, wananiambia ngoja tukuchukue vipimo kwanza na tuone, basi wadau wangu waka fosi ki mjini mjini mambo yakaanza kukimbizwa na nini, mpaka naingia chumba cha upasuaji ni masaa 11 yamepita toka nipate ajali na damu kuniisha mwilini.

Basi baadae nikaingia wodini tena na nini, kuanza kupona sasa na nini ila expirience ambayo sio ya kuombea.

Namshukuru Mungu wangu alie mkuu sana, sikufa siku ile na sitarajii kufaa miaka hii hii na amenipa uhai na ataendelea kunipa uhai na tukio hili limeniweka karibu sana na yeye.

Kule wodini na tiba zingine unashangaa wataalam wanakwambia "aah kitu ichi hakiwi covered na bima ya nhif, aah hapa inabidi ulipe kiasi flani, aah kamuone flani" yaan unashangaa jambo dogo lina mlolongo mrefu ambao ni very unnecessary.

Wodini mule wadau wakaanza kunipa habari za namna watu wanavyoteseka na wengine ambao hua wanafia emergence, so scarry wazee. Bongo hauna kitu unaondoka unajiona wakuu, so hata kutafta room private nalo mpaka mchongo eti daah aisee.

Naomba kuishia hapo, nilitoka hospital siku maliza hata siku saba, nilifosi nikaondoka kibishi tu na kuendelea na tiba tokea nyumbani kwangu na Mungu mwingi wa rehema na neema basi nimepona ndio niko narudi rudi na mimi kwenye majukumu yangu mengine, wale walionosababishia hayo matatizo ndo nataka kuanza kuwashughulikia sasa na sitokua na msamaha ktk hili. lakini sitosahau miezi miwili iliyopita wazee nilikua kama niko Ukraine mstari wa mbele pale kumpinga bwana Putin asiendelee na majeshi yake kuichukua kyiv.

Sijajua wewe umewai kuyapata yapi au umewai kuyaona yapi ya kuhusu ajali hizi za barabarani na expirience za ma hospital yetu ambayo unaweza uka dead unajiona! basi itakua vyema ukishare nasi basi tukapata la kujifunza.

Wasalaam.
Pole sana
 
Kwema wadau?

Mwaka huu mwanzoni nikiwa nimetoka kusheerekea sikukuu ya mwaka mpya na nikiwa nimefanya maombi ya mipango yangu mingi kwa mwaka huu na kumsihi sana Mungu wangu aliehai anijalie afya, uhai, furaha na amani tu mengine nayaweza hayanisumbui kabisa, basi sikua najua siku chache zijazo ntakutana na jambo baya na la kutisha kiasi icho.

Siku ya Tukio;

Nikiwa nawai zangu kwenye majukumu yangu ya kikazi asubuhi kabisa hapa ndani ya Dar es Salaam tena nikiwa sina hofu wala kuwaza lolote, ile wazungu wanaita "the fear of unknown" kwamba kama kuna jambo baya linaenda kutokea basi kuna ishara flani hua zinakusumbua kama kukosa amani and so, but mie siku hio haikua hivyo wala na nilikua nawaza tu niwai kufika ofisini.

Ni asubuhi hio nikiwa ktk mwendo wa kawaida kabisa katika chombo private tu, ghafla kitu kikaniambia "be very careful" na nikaitii hii sauti so nika punguza kabisa mwendo wa chombo changu na nikawa kawaida kabisa, haikupita ata dk 10 mbele yangu nikaona daladala mbili zinafukuzana kuwaiana abiria, kama kawaida yao hawa mabwana na ujinga wao wa kuwawai abiria wa mbele zao, so hizi daladala hazikua upande wangu zilikua kulia kwanga mie nikiwa kushoto so nilikua naziona face to face na nikajua kila mtu ni lazima aheshimu sheria za barabara na kukaa upande wake, sasa haikua hivi, yule dereva aliekua anapitwa akafanya kumu overtake mwenzake nadhani bila kuangalia na labda atakua ni mjinga wa kuzaliwa wa kweli kweli, na ikumbukwe njia ilikua imenyooka so nimeanza kuwaona toka ka distance flani iv mbele yangu wakifanya huo ujinga na haikuchukua hata dakika tatu tangu nianze kuwaona na kuniletea changamoto mbaya sana, yule dereva mwingine wa daladala alie overtake bila kuangalia nadhani ile gari ilimshinda au sijui kama shetani aliingilia kati ila nilishangaa tu kishindo kanigonga face to face wakuu, aisee nilishangaa sana lakin kuja kustuka naona damu zimejaa chini ya gari langu, airbag na watu wanapiga kelele, sikuzimia wala sikuskia maumivu ila nilikua kwenye mshtuko mkubwa sana sana.

Ile gari ilivyonigonga na ilizima pale pale yenyewe tu na kwangu huku sikuona tena ya mbele, nikawa najipapasa niki hofu yasije yakawa mambo ya uti wa mgongo kushtuka na kushindwa kuamka forever, nikajaribu kutikisha miguu naona mguu mmoja haurespond na kama bega linaniuma iv, sikujua tena nini kimetokea ila mguu ulivunjika, bega kustuka na huu mguu uliovunjika ni tuseme ulikua umepasuka na ndo chanzo cha zile damu, na hii baadae nilikuja kujua ni kwamba nilikanyaga break kwa nguvu na kunyoosha mguu kwa kukaza labda kwa kustuka au hofu so gari ilivyopigwa kwa nguvu na kubonyea so presha yake na effect ndo ikaniletea hayo madhara.

Kilichofuata kuanzia hapo ikawa sina sauti tena, naona naamriwa tu vitu na wananchi waliokua wamejazana pale, kila mmoja akisema iv na mwingine akisema vile na wangine wakirekodi kwa simu tukio lile na mie mwenyewe nikiwa bado nna mstuko mkubwa sana nawaza hivi ni mimi au naota? Nikiaskia sauti mkagueni vizuri labda ameumia kichwa?

Nikaskia shauri likiendeshwa juu yangu, wananchi wakasema tumpeleke polisi tukachukue PF3, wakaja kunitoa huku naona watu wameshika vichwa wakina mama wanalia na mie sasa nikaanza kuogopa uende nimeumia sana kuliko ambavyo najiwazia wakati huo, so najaribu kusimama mwenyewe siwezi, wananibeba na wanasema twende polisi, damu kila mahala na huo ni mguu tu, japo nna maumivu ya bega na mkono lakini najishangaa nasema kwa namna damu hizi zinavyotoka huko polisi ntafika nikiwa mzima kweli? Na kwa maeneo hayo kituo cha polisi kipo wapi sasa? Na je kutokea hapo mpaka kufika Hospitali itakuaje? Naona kabisa wananchi hawana elimu juu ya kuzuia damu kutoka na i feel like labda nijisaidie ila siwezi kufanya lolote, moyo unaenda speed sana na bado niko shocked tu.

Polisi hapakua mbali na hawakua na hiyana, ni kakituo ka dogo hakukua na jam ni walinihudumia ndani ya dakika 5 tu nikaipata pf3 tukaondoka na wananchi ambao walikua wamenibeba kwenye kirikuu.

So tukaelekea hospitali na hapa ntaomba nisitaje majina ya hospitali wananchi wasije wakaamua kwenda kuzichoma moto, so nikapelekwa hospital ya wilaya, mpaka nafika hospital hapo nadhani labda nilikua nimebakiza damu lita mbili tu nadhani, so jamaa hakuna wanachokifanya, manesi wananitizama tu, nikawa mkali, wakasema wewe mgonjwa unamfokea nani? Daah bongo😂😂, akaja muuguzi mmoja akanichoma sindano ya tetenasi na nyingine sijui ni nini, nikamwambia wewe bwana embu fanya kitu kuzuia damu basi, wakaanza kunizuia damu na wakafanikiwa lakini nadhani mpaka muda huo labda nilikua nna lita moja tu mwilini, nikaanza kuskia kabisa moyo unasukuma kitu kisicho kuwepo.

Lakini pale pale najiuliza ina maana nchi hii mtu anaweza kufariki kisa mguu, mkono na bega? how could that be possible? Ila nikajisemea "mimi sitokufa mahala hapa na wakati wangu bado haujafika, ewe Mungu wa haki usinichukue nikiwa katika umri huu nna deni na wewe", sasa Mungu ni muaminifu sana, baada ya kusema maneno hayo nikawa najipa moyo mkuu na imani na japo naskia sina damu na ata kuongea tu tabu, moyo una push kitu kisicho kuwepo, kazi yangu ikawa ni kurudia tu hayo maneno hapo juu, natamani labda nilale niamke nikiwa fresh ila hakuna kitu siwezi ata kusinzia au kuzimia.

Ile hospital ya wilaya wakasema hatuwezi kumtibu, mpelekeni hospital ile ya taifa, na mpaka muda huo hapo kwenye hio hospital wamenichoma sindano mbili tu, drip ya maji na wakanipa rufaa kwenda kwenye ile hospital nyingine baba lao.

Mpaka muda huo, wadau wangu washafika so ikabidi tutafute private ambulance sababu hio hospital wanasema ambulance ipo moja na imempeleka mgonjwa mmoja hospital ya taifa so tuisubirie na hapo tumesubiria saa na nusu haiji ndo kufanya maamuzi ya private ambulance.

Kufika kwenye ile hospital baba lao la taifa aisee kumbe bora kule wilayani ambako hawana kitu, wale wako too slow, yaani unawaona kabisa hakuna kitu kinachoweza kuwastua, wamezoea matatizo na kila mtu anapita tu ana shangaa shangaa iv anaondoka, vijana wadogo ndo wajinga zaidi pale yaani wako sector ya emergence ila wanachezea tu simu ambazo ata ukiziangalia simu zenyewe ni tecno na samsung A series, hakuna humanity, samahani kwa kuyasema haya ila ndo nimeyaona tena emergence kabisa sasa fikiria kule kwengine ndo kupoje?

So wadau wangu wakaanza kutilia mkazo na mikwala mingi ndo na wale kuanza kunihudumia, na kila dakika hapo emergence wanaletwa watu ambao wanalia kila mtu kama anachinjwa hivi.

Sina damu na moyo unapambana sana kwa zaidi ya masaa matano sasa toka tukio litokee, naskia njaa naskia kiu na kama siwezi kupumua vizuri iv yaan nna fosi, ajab sizimii wala sisinzii, so hawa nao wakaniwekea drip za maji, nawaambia wazee nahitaji damu nitoleeni haya ma maji yenu hakuna kitu yanacho nisaidia hapa, wananiambia ngoja tukuchukue vipimo kwanza na tuone, basi wadau wangu waka fosi ki mjini mjini mambo yakaanza kukimbizwa na nini, mpaka naingia chumba cha upasuaji ni masaa 11 yamepita toka nipate ajali na damu kuniisha mwilini.

Basi baadae nikaingia wodini tena na nini, kuanza kupona sasa na nini ila expirience ambayo sio ya kuombea.

Namshukuru Mungu wangu alie mkuu sana, sikufa siku ile na sitarajii kufaa miaka hii hii na amenipa uhai na ataendelea kunipa uhai na tukio hili limeniweka karibu sana na yeye.

Kule wodini na tiba zingine unashangaa wataalam wanakwambia "aah kitu ichi hakiwi covered na bima ya nhif, aah hapa inabidi ulipe kiasi flani, aah kamuone flani" yaan unashangaa jambo dogo lina mlolongo mrefu ambao ni very unnecessary.

Wodini mule wadau wakaanza kunipa habari za namna watu wanavyoteseka na wengine ambao hua wanafia emergence, so scarry wazee. Bongo hauna kitu unaondoka unajiona wakuu, so hata kutafta room private nalo mpaka mchongo eti daah 😂😂 aisee.

Naomba kuishia hapo, nilitoka hospital siku maliza hata siku saba, nilifosi nikaondoka kibishi tu na kuendelea na tiba tokea nyumbani kwangu na Mungu mwingi wa rehema na neema basi nimepona ndio niko narudi rudi na mimi kwenye majukumu yangu mengine, wale walionosababishia hayo matatizo ndo nataka kuanza kuwashughulikia sasa na sitokua na msamaha ktk hili. lakini sitosahau miezi miwili iliyopita wazee nilikua kama niko Ukraine mstari wa mbele pale kumpinga bwana Putin asiendelee na majeshi yake kuichukua kyiv.

Sijajua wewe umewai kuyapata yapi au umewai kuyaona yapi ya kuhusu ajali hizi za barabarani na expirience za ma hospital yetu ambayo unaweza uka dead unajiona! basi itakua vyema ukishare nasi basi tukapata la kujifunza.

Wasalaam.
umeongea kwa hisia
 
Pole sana mkuu kiukweli mpaka yakukute ndio utamuelewa mleta mada
 
pole sana, ni kweli nhif kuna huduma hazipo kulingana na kifurushi ulicho nacho.

next time kama unajitambua ni vzr kwenda private hospital utapata huduma haraka zaidi.

pale hospitali ya taifa pana mlolongo sana ni bora uende kama huduma unayotakiwa kupewa imeshindikana private.

ajali isike kwa jirani niliwahi kupata ajali mbaya sana ya basi wami.
 
Hii ya kusema kung'ang'ania brake ndio imekuvunja mguu ni kweli. Jamaa yangu mmoja nae hivyo hivyo ule mguu ulioshikilia brake baada ya kishindo ukasukumwa juu ukapachuka kwenye hip hapo sema mambo ya hela yakasaidia akaenda India wakamuweka sawa
 
Hospital ya maana kwa mwanza Ni bugando pekee..yaani Kama una pesa yakutosha au bima utapewa huduma ya kiwango Cha lami..
Watu wa emergency pale bugando Ni watu hodari Sana..mtoto wangu aligongwa na bodaboda..walimtibu kwa viwango vya kimataifa kuanzia emergency Hadi wodini..nilimuona nesi mmoja tu mpuuzi wengine wako vizuri..
 
Back
Top Bottom