Bongo movie wapi mnakwama?

Harunahoba

Member
Oct 15, 2019
33
45
Taasinia ya Sanaa ya michezo ya kuigiza hapa Tanzania inapitia changamoto nyingi sana zipo tunazoziona sisi mashabiki na pia zipo wanazokumbna nazo wasanii husika. Binafsi hiz ni baadhi ya changamoto ninazoziona kama mdau.

1. UKOSEFU WA SIMULIZI ( STORIES)NZURI. story nyingi za hapa kwetu hazina uhalisia ndani yake na pia ni za kujirudiarudia. ni rahis sana kujua nini kinafata utazamapo movie zetu (sisemi kwa ubaya). kuna mambo mengi ambayo Tanzania inapitia au iliwahi kupitia na raia wake tunayapitia lakin ni ngumu kuyaona. mda mwingine yanaonekana lakin katika namna ambayo sio ya kiuhalisia mfano kuna mda mtu anakamatwa na polis lakin hicho kituo cha polis unaona kabisa ni duka la mtaani hapa sijui shida nini serikari haiwaruhus kutumia sehem kama vituo vya polis vinavyojulikan kabisa?

pia unakuta mtu anaenda kazini yupo ofisin kampun inadeal na nin haijulikani ni mapenzi tu ofisin secretary kamtega boss. kuna jamaa wanaitwa BONGO HOODS hawa wanachangamoto nyingi lakin atleast unaona ideas tofauti mara madawa ya kulevya na adhari zake changudoa mara mtu anahustle na mziki lakin huku bongo movie ni mapenzi mwanzo mwisho.

hiv hatuwezi kuigiza hata visa vya kina chief mirambo na kinjekitile ngwale tuujue uhalisia wa mambo haya yanawezekana kwa maana watu wanaojua history vizuri ya Tanzania wapo taasisi pia za kufanya nao kazi ili kuongeza bajeti zipo ila tumetulia tulii

2. UKOSEFU WA WASANII WALIOSOMEA KAZI HIYO. wengi wa wasanii wetu sio watu wanaopatikana kutokana na mafunzo ya sanaa hata wanapopata nafasi kujiendeleza kielim hua hawataki kujiendeleza hivyo kukuta story zinajirudiarudia tu mfano ukiangalia yellow banana ya ray 2008 mpka akiigiza leo story kama hiyo hiyo na makosa ni yaleyale.

3. KUKOSEKANA KWA BARAZA LENYE NIA YA DHATI NA UEREDI MKUBWA KUHUSU TASINIA HII. BASATA wanatakiwa kujiangalia upya kama kweli hii ndio njia sahihi ya kuipeleka mbali sanaa yetu. Sanaa ya maigizo ni sehem ya utalii mtu anapoigiza lazima baraza limsaidie kwa kila hali hata kama ni ushauri, mafunzo, kua na vitendea kazi vya kisasa, kua na majukwaa makubwa ya sanaa hii, kuwasaidia wasanii kupata vibali vya kutumia vitu vya umma ilikupata uhalisia, kuandaa semina mbalimbali na kujifunza kuendana na technology, na mengine mengi?mbona nchi za wenzetu watu wanaigiza mpka marais kwann sisi n mapenzi tu?
 
tatizo kubwa la Bongo Movie ni Low Budget na watangenezaji wa filamu kwa maana pamoja na crews wote kwa ujumla wenye weledi mzuri, Kuwashutumu waigizaji ni kutokuelewa kutokuielewa undani wa hio Sanaa.
waigizaji lazma.watahusika kwa namna moja au nyingine maana n ngum kukuta hata muigizaj mmoja anajiendeleza kimasomo baada ya kutoboa zaid na yy ataanza kuandaa movie
 
Hamna waandish hoolwood script ni siri na unakuwa hujui next season nini kinakuja kama ndo mkatab unaisha wakat wa kipind cha kusoma kabla kwenda kushoot ndo unajua kuwa we mwish wak ndo hap unauliwa mamb yanasonga.
Mfano JUAKALI WANABADILI WAHUSIKA
WAKAT KWENY SERIES INAITWA SUIT KUNA DADA NAITWA MEGHAN ALIPOOLEWA WAKIMTOA TU WALA HAWAJUSITA.
XO DIRECTIORS NA WAANDISH
WAWE WANAFANYA RESEARCH KATIKA KILA KIT WANAIGIZA MFANO SEREIS INAITWA WESTWORLD NDO UTAGUNDUA JAMAA WANAFANYA KAZ HAKUNA ROOM KWA MAKOSA YA WAZI

THANX KWA KUWAFANYA WAKE ZETU WAFURAHI ILA FANYENI KAZ NA KAZ ZITAWALIPA

NETFLIX IS FOR ALL
 
naangalia PAZIA dude ni msanii mkubwa ktk tasnia ameigiza kama mkuu wa kituo.

ajabu begani kavaa cheo cha nyota 3 na anajiita inspector🤣🤣🤣,hivi unajiuliza hawa watu hata huwa hawakamatwi waone jamaa huwa wanabehave vipi???

yaani mko serios ila watizamaji tunaona mnatufanyia mzaha.hakuna umakini katika kazi.detail ndogo ndogo hizo ni muhimu sana,ila mnachukulia poa.
 
Kitu cha kwanza bongo movie wanacho chemka ni Casting. Siku hizi wanachagua mabinti warembo, wenye makalio makubwa na upande wa wanaume shombe shombe,maybe na mabody builder,wanao trend social networks.Talent hawa tizami kabisa, kuna wasanii wenye talent tena za wapo vizuri hawapewi nafasi,sababu hawana makalio makubwa,so mahb nk.

Tasnia ya bongo movie imeanza kutrend walivyo anza kuingia hawa mamiss na malaya wanao tafuta soko waka ingia humo humo matokeo yake industry yao imekuwa ni industry iliyo jaa malaya walio jificha kwenye kichaka cha uigizaji na sikia kuna mabinti wengine wapo tayari kuigiza hata bure anajua kwenye biashara yake ya udangaji au umalaya rahisi kuonekana.
 
waigizaji lazma.watahusika kwa namna moja au nyingine maana n ngum kukuta hata muigizaj mmoja anajiendeleza kimasomo baada ya kutoboa zaid na yy ataanza kuandaa movie

Matatizo kutoka kwa waigizaji ni madogo sana mkuu, kama unaelewe vizuri role za Directors, Screenplay writeers, art directors, na wengineo ndio utaelewa matatizo yetu yalipo. tatizo letu sisi tunasukuma shutuma kwa Actors kwa matatizo yanayotokana na Film Makers. Hata actor akiwa mbovu akipata Director mzuri akawa ndani ya control ya huyo director basi anaweza perfom vizuri.
 
tatizo kubwa la Bongo Movie ni Low Budget na watangenezaji wa filamu kwa maana pamoja na crews wote kwa ujumla wenye weledi mzuri, Kuwashutumu waigizaji ni kutokuelewa kutokuielewa undani wa hio Sanaa.
Waigizaji siku zote wapo. Hakuna nchi inayokosa waigizaji. Tatizo linakuja namna wanavyopatikana. Wengi ni watu waliojiongoza na kuingia kwenye uigizaji kwa sababu tu ya uthubutu au wana sura nzuri. Kwa kifupi tatizo liko kwenye utalaam na wataalam.
 
Kwenye content hata nusu ya Nollywood hawafiki, ukiangalia movie za kina Ousofia nadhani ndo wasanii Nigeria wanaogengeneza movie za budget ndogo,quality na sound ni low lakini wanavyoigiza ni uhalisia ukianza movie unatamani isiishe maana hujui kitakachotokea
 
Kwenye content hata nusu ya Nollywood hawafiki, ukiangalia movie za kina Ousofia nadhani ndo wasanii Nigeria wanaogengeneza movie za budget ndogo,quality na sound ni low lakini wanavyoigiza ni uhalisia ukianza movie unatamani isiishe maana hujui kitaka

Hamna waandish hoolwood script ni siri na unakuwa hujui next season nini kinakuja kama ndo mkatab unaisha wakat wa kipind cha kusoma kabla kwenda kushoot ndo unajua kuwa we mwish wak ndo hap unauliwa mamb yanasonga.
Mfano JUAKALI WANABADILI WAHUSIKA
WAKAT KWENY SERIES INAITWA SUIT KUNA DADA NAITWA MEGHAN ALIPOOLEWA WAKIMTOA TU WALA HAWAJUSITA.
XO DIRECTIORS NA WAANDISH
WAWE WANAFANYA RESEARCH KATIKA KILA KIT WANAIGIZA MFANO SEREIS INAITWA WESTWORLD NDO UTAGUNDUA JAMAA WANAFANYA KAZ HAKUNA ROOM KWA MAKOSA YA WAZI

THANX KWA KUWAFANYA WAKE ZETU WAFURAHI ILA FANYENI KAZ NA KAZ ZITAWALIPA

NETFLIX IS FOR ALL
huku kwetu mambo yatachelewa sana mkuu kila nikifikiria naona safari n ndefu sana
 
Hujui kitu kuhusu uigizaji....shida ipo Kwa directors..
Ukipata director mzuri Hata wewe waweza kupafomu better
uigizaji sio simple kama unavyodhan mpanda? huyo anaeigiza lazim ajue mising na mwenye talent kwel discipline ya kutosha muonekano hiv vyote hafanyi director
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom