Inawezekana haya ni makosa makubwa ya Bongo Movie

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
Huwa napenda kujifunza mengi kuhusu filamu kwa sababu najiandaa kuingia kweynye ulimwengu huo hivi karibuni. Huwa najiuliza ni kitu gani hufanya Bongo Muvi kutokuwa na mvuto wa kuangalia? Nini kipo nyuma yake? Je, ni kweli hatuna watunzi? Hatuna maprofeshino wa kupiga kamera? Hatuna waigizaji ama tatizo huwa nini?

Kuanzia mwezi uliopita mpaka leo, niliamua kujifungia chumbani na kutazama muvi mbalimbali, nilihitaji niwe na majibu kamili kugundua tatizo kubwa huwa nini. Niliamua kutazama muvi na si kuangalia, elewa utofauti hapo, kuna vitu nikavigundua, hivi hapa chini, kama una vya ziada, unaweza kuongeza.

STORI

Hili ndilo jambo la kwanza kabisa. Dunia imebadilika, na inakwenda kasi sana lakini waandishi wa filamu hawataki kubadilika. Wapo palepale, hawataki kabisa kusogea mbele.

Muvi unayoitazama leo, ni sawa na ya kesho, ni sawa na keshokutwa.

Mpaka leo hii bado kuna waandishi wanaandika masuala ya baba kumpenda mtoto, dada na kaka kupendana bila kujuana kama ni ndugu, mama kumpenda mtoto, yaani mambo yaleyale ambayo zamani nilikuwa nayaona kupitia michezo ya kuigiza CTN ndiyo naiona leo hii.

Waandishi hawaruhusu mawazo yao yakue, wanaangalia sana filamu za wenzetu, ila ukimwambia niandikie script moja kali, unakuta mambo yale yale mpaka unajiuliza hivi huyu anaangalia muvi za wenzetu ama?

Mtu wa kwanza ambaye anatakiwa kuibadilisha muvi na kuipa mvuto ni mwandishi. Kuna muvi unaangalia, unajisemea tu kwamba hii muvi imeandikwa, yaani ukizisikiliza diology zao, mpaka unajisikia raha.

Hapa pia utaona ubovu wa script kwa kujaza maneno mengi yasiyokuwa na maana, hii naiona sana kwenye tamthilia zetu za Kibongo...mfano.....

“Mimi huniwezi, waulize wenzako wananijua mimi ni nani, yaani hapa mtaani hakuna mtu wa kunibabaisha, ukisikia Mwajuma Nchokonoe ndiye mimi, yaani hapa siondoki mpaka huyo unayemwamini aje, mimi ndiye Mwajuma, mwanamke anayelala na wanaume wote mtaa huu...”

Yaani utaona maneno ni mengi sana, halafu yote hayana maana. Script inaandikwa kwa urefu ili kula muda tu, wenzetu huwa hawafanyi kosa hili, hawapoteza muda kwenye mazungumzo, kuna mambo wanayatumia kula muda, tena ukiyaona, unasema kabisa yalitakiwa kuwepo.

Waandishi wanaliangusha soko la filamu mno mpaka mwenyewe nashangaa na kujisikia aibu, halafu mwandishi huyohuyo anasimama mbele za watu na kusema ile muvi nimeandika mimi, NI AIBU.

WAIGIZAJI

Siku zote mwandishi ndiye mtu pekee ambaye anaandika muvi huku akijua hii muvi inakwenda kuchezwa na nani. Mwandishi kuandika muvi bila kujua ni nani ataicheza, ni jambo baya sana.

Mfano unasema hii muvi nataka aigize Nyemo, utaiandika kwa muonekano wa Nyemo, utafanya kila kitu kwa jinsi Nyemo alivyo, sasa kibongobongo, unaandika muvi kwa kutaka Nyemo aigize, mwisho wa siku unaletewa Juma ndiyo aigize lazima utapotea.

Wakati James Cameron alipoandika filamu ya Titanic alitaka Leonardo DiCaprio aandike, na aliwaambia hata watu wa production kwamba ameiandika muvi hiyo kwa jinsi Leonardo alivyo, yaani filamu imembeba yeye moja kwa moja.

Production ikakataa, ikamwambia hiyo filamu ataicheza Tom Cruise kwa kuwa ndiye alikuwa na jina kubwa kipindi hicho. Ila naye akakataa, akawaambia hii filamu nimemuandikia Leonardo, na kweli akaigiza, muvi ikambeba na yeye kuibeba.

Mwaka 1976, muigizaji Sylivester Stallone, Rambo aliandika muvi ya Rocky, ile muvi aliiandika kwa kujiweka muigizaji mkuu yeye mwenyewe.

Aliandika tabia zake na kila kitu, yaani ni kwamba alijichora kwa maandishi jinsi alivyokuwa na kuweka kwenye script. Alipoipa kampuni ya kurekodi wakasema ile script acheze mwingine na si yeye, akakataa, akataka kuigiza mwenyewe, akafanya hivyo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Sasa hapa Bongo, mtu anaandika Script, halafu anakwenda kuiuza, anayeinunua, anamtafuta muigizaji, sasa mwisho wa siku kila kitu kinaharibika, yule jambazi mkali aliyeandikwa kwenye script ni tofauti na jambazi aliyeletwa kwenye muvi, mwisho wa siku muvi inaharibika.

MUOGOZAJI

Kila kitu kinakuwa kichwani mwa mwandishi, hata akiandika script, kitu kingine anachokifikiria ni muongozaji nani asimamie mzigo, hapo ndiyo maana wakati mwingine unakuta muandishi na muongozaji ni mtu mmoja. Hii ni kwa sababu mwandishi huwa hataki kuharibiwa kazi yake.

Script inapopata muongozaji mbaya, hawezi kufanya kazi ipasavyo. Waongozaji wengi wa Kitanzania hawajui kuzifanya kazi zao vizuri, ndiyo maana unaangalia muvi na kuona makosa kibao, yaani kuna vitu unaviona mpaka unashangaa, ndiyo yaleyale ya mzimu umefufuka huku umevaa sendozi na miwani, yaani muongozaji huyo naye akikaa sehemu anatamba kwamba muvi hiyo imeongozwa na yeye.
Ni aibu.

EDITOR

Editor na muongozaji ni baba mmoja na baba mmoja, wengi hawajui wanalolifanya, wamekuwa wababaishaji tu, wanataka kupiga pesa bila kuangalia umakini wa filamu.

Wakati mwingine unaangalia filamu unasikia sauti “Action”....”Cut off” Yaani mpaka unajiuliza, hivi hii kazi, editor alikuwa makini kuiangalia upya ama aliamua tu kupiga fastafasta apate hela akalewe?

SOUNDTRACKS

Hapa tunarudi kwa watu wa studio, hawa wanafanya kazi wewe muongozaji unavyotaka kifanyike, huwa wanavuruga sana lakini waongozaji wanaona sawa tu.

Soundtrack kwenye muvi ni kitu muhimu sana, tena sana. Ukitaka kuamini umuhimu wake, tafuta muvi ya kutisha, iweke, tena ile unaamini inatisha sana, halafu ondoa sauti, nikwambie tu haitotisha hata kidogo.

Wazungu wanatumia muda mwingi kuvuta hisia za mtu kupitia soundtrack, hapo wanapashikilia sana kwa kuwa ndipo kulipobeba hisia ya mtazamaji. Anapotaka kukutisha, anaweka sauti hizo ambazo ukizisikia, mwenyewe unaona kabisa kazi ipo.

Sisi Waafrika tunataka kumtisha mtazamaji kwa kutumia picha ila Wazungu wanakutisha kwa kutumia sauti, wao wanalifanyia kazi sana eneo hilo.

Majuzi nilikuwa naifanyia review muvi ya Conjuring bila sauti, oya wazee, ile muvi haitishi hata kidogo, ila ukiweka sauti, kazi unayo.

Mtu mwingine anakwambia muvi za Sharukh Khan za mapenzi ni hatari, yaani zinakuteka sana, hapo anayeanza kukuteka ni zile soundtrack halafu yeye Khan anakuja kumalizia kazi yake.

Wengi wanalia kwa sababu ya soundtrack tu, wanaogopa kwa sababu ya sauti hizo tu, ila kwa sisi wabongo, sauti zetu ni zilezile za kishamba, mbaya zaidi kuna mlio mmoja wa mtu kushtuka unasikika ukilia kwenye kila aina ya muvi ya kibongo.

Hili ni sehemu ya kulifanyia kazi sana.

SHOTS

Huu ni upigaji wa picha. Kuna muvi zinapigwa shots mpaka mwenyewe unashangaa, yaani zinakuwa si mchezo.

Kwa wapiga picha wetu wa Kibongo, nao sehemu hii bado kabisa, yaani utakuta mtu anajisifia mimi nashuti muvi hatari, ukiangalia muvi zenyewe, shots zake ni zilezile za muvi nyingine.

Mpiga picha hasifiki kwa kupiga picha za pembe nne, anasifika kwa kupiga shoti ambazo zitamshangaza kila mtu.

Majuzi kuna jamaa aliniambia “Unajua Nyemo ile shot kwenye muvi ya James Bond wakati dogo ameibuka uvunguni na kumpiga mwamba risasi pale mwanzo, ile shot hatari sana....” Nikacheka sana kwa kuwa nami nililiona hilo.

Ukiachana na shot hiyo, kuna ile ya kwenye muvi ya Fast And Furious, ya saba nahisi ambapo The Rock anapigana na Vin Diesel halafu wakati mmoja anamwangusha mwenzake, kamera nayo ikawa inaanguka naye, ile shot ilikuwa kali sana na baada ya hapo, muvi za watu wengine za mbeleni nao wakaanza kuitumia...niliona muvi zaidi ya nne, nazo walitumia shoti hiyo ya kamera kama kuanguka sambamba na mtu.

Mpiga video wangu mkali ni yule atakayepiga shots za uhakika na si ilimradi tu zipigwe tuwahi kwenda kula.

KWANGU MIMI NI HAYO TU, KAMA UMEONA MENGINE, UNAWEZA KUSEMA ILI KULIBORESHA SOKO LETU LA BONGO.

Imeandikwa na Nyemo Chilongani.
 
Umenifungua macho mimi mwenyewe najitahidi kufanya uchunguzi juu ya ubovu wa bongo movies wakati huo huo nikiandaa script za filamu.Bado naendelea kutafuta sababu za kukosa mvuyo lwa bongo movies
 
Kama alivyosema Da Gladiator , umejitahidi but you still have a lot to learn.

Mie nta-comment kuhusu uandishi tu maana umesema una mpango wa kuingia kwenye tasnia and I would feel bad if I didn't share my knowledge, alafu ukute unataka kuanza na uandishi ukiwa na mentality hiyo ya kuwa muandishi anaeandika bila kumfikiria msanii fulani sio muandishi anaejielewa.

Like seriously dude....ingekuwa hivyo kusingekuwa na auditions, wasanii chipukizi wala test shoots! Au unadhani the likes of Leornado, Brad, Angelina Jolie etc. have always been famous enough to have roles written specifically for them??

Trust me....unaposema mwandishi anapaswa kumuandikia msanii fulani unakosea sana....yani you completely miss the point because the point is...you can have an idea, you knoww...ya msanii gani who can really bring your character(s) to life na sio character wako anaweza kumfaa msanii gani. As a writer....your responsibility is to your characters & your story PERIOD!

Anyway.....kwenye storytelling kuna kitu kinaitwa CHARACTER DEVELOPMENT = character breakdown/profile.

Character Breakdown - Who is your character?
Backstory/Personality traits/Physical appearance/Interests and so so.....
1637052382906.jpg

Unapojua who your characters are in terms of their background, personality, appearance etc. (sio watachezwa na nani) inakuwa rahisi kuwaandikia because you already know the kind of trouble they could possibly get into, their attitude, actions & reactions etc. Etc.....
Na ukifika hapa ndo unaweza kuwa kama Cameroon na kusema "the only person I can see playing this character is fùlani" maana yeye ndo atakaeitendea haki!

Wish you all the best kwenye hiyo safari yako.

PS
Make time and read about CHARACTER BIBLE aswell. Itakusaidia kujua how to depict your character(s) visually.
 
View attachment 2012643

Shukrani sana mkuu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Well explained .. Ahsante sana!.
 
Kingine hakuna waigizaji wapya ,waigizaji ni wale wale tu,

Waigizaji wanao jua hawaweki watu wapya kwenye movies,kila siku ni wao tu, hawatengenezi waigizaji wengine
 
Back
Top Bottom