Hivi Bongo movie hawawezi kuuza movie zao kwenye flash?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,261
12,786
Bongo movie inakufa, sababu si quality (japo kweli quality ni chini) kama wengi wanavyodhani bali ni hawana namna ya kuuza movie zao. Ilianza kwa kuuza VHS za kina Majuto. Ikaja CD na DVD. Kipindi hiki walau walikuwa wanapata chochote. Ghafla watu wakaanza kupirate DVD na kuziweka kwenye flash.

Hapa ndipo wizi mkubwa ulivyoanza, leo karibu kila nyumba yenye TV wana flash ya kuwekea movies, watu hawanunui tena DVD. Wabongo movie hawana namna tena ya kuuza kazi zao.

Hawawezi kupeleka kwenye majumba ya cinema kama Ulaya, au kuziweka kwenye streaming services sababu watanzania hatuna utamaduni wala uwezo wa mambo hayo. Kwa sasa households nyingi zinatumia flash kucheza movies.

Nafikiria kama inawezekana wakaziuza movies zao kwenye flash. Yaani movie inawekwa kwenye flash ambayo inakuwa encrypted, mtu anaweza kuicheza tu na si kuihamisha. naona wholesale ya flash za 1GB inaanzia kama 0.5$, kama Tsh 1,200 hivi. Inawezekana kuuza movies kwa mtindo huu, na pengine hata inaweza kutumika kuuza album za muziki pia. inawezekana?
 
Itachukuwa wiki moja tu watu kupata njia ya kuendeleza wizi. Kitu wanachotakiwa wafanye ni kutengeneza filamu nzuri zenye ushindani zitazouzika hata kwenye netflix nk.
 
Wewe wadhani wenyewe hawajawaza kuhusu hilo but all in all now days wanapeleka kwenye Channels za TV kama sinema zetu, TVE na nyingine kwa order or contract na wanapiga hela hatari zaidi ya CD, DVD na flash unayoisema wewe. Just Imagine Mama Kimbo ya Azam Tv watayarishaji wake wamechukua 100+ M pale Azam. Utamshaurije Mzee JB au Kitale wa maneno ya kuambiwa kuhusu Hizo flash zako
Over
 
Itachukuwa wiki moja tu watu kupata njia ya kuendeleza wizi. Kitu wanacho takiwa wafanye ni kutengeneza filamu nzuri zenye ushindani zitazo uzika hata kwenye netflix nk.
Netflix si rahisi sababu wabongo hawana utamaduni wa kustream na bei hizi. shida bei za vifurushi na fee.
 
Ww wadhani wenyewe hawajawaza kuhusu ilo but all in all now days wanapeleka kwenye Channels za TV kma sinema zetu,TVE na nyingine kwa order or contract na wanapiga hela hatari zaidi ya CD,DVD na flash unayoisema ww.Just Imagine Mama Kimbo ya Azam Tv watayarishaji wake wamechukua 100+ M pale Azam. Utamshaurije Mzee JB au Kitale wa maneno ya kuambiwa kuhusu Hizo flash zako
Over
Usiassume tu kuwa kuna watu wamewaza, huo ni uzembe. Na pia hizi TV channels zinalimit ya kiasi cha movies wanaweza kuchukua.
 
Usiassume tu kuwa kuna watu wamewaza, huo ni uzembe. Na pia hizi TV channels zinalimit ya kiasi cha movies wanaweza kuchukua.
Sija assume kijana sawa nakuambia true fact By my knowledge nafahamu Kwa mfano azamtv hawana limit ya kuchukua movies kupitia sinema zetu huwa wanatangaza live kuwa wamiliki wa filamu wapeleke zao na zitanunuliwa, je Dstv kupitia maisha magic na Startimes star swahili.

So ni wao directors na authors wa story za bongo movie kuleta innovation kwenye game sio mtu anaanza kuangalia movie direct anaeza kujua mwisho ni upi bila hata kuangalia movie na kingine ni quality ya movie.

Embu nikuulize swali umeangalia Tamthilia ya Kitasa wewe wadhani imegharimu how much kuwahusisha watangazaji wa azam, Boxer kama kina Ibra class na waamuzi Wa true from real life kama yule dada na unadhani hizo hela zimetoka wapi na watazipataje kama return of investment jibu nimekupa.

Kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Sija assume kijana sawa nakuambia true fact By my knowledge nafahamu Kwa mfano azamtv hawana limit ya kuchukua movies kupitia sinema zetu huwa wanatangaza live kuwa wamiliki wa filamu wapeleke zao na zitanunuliwa, je Dstv kupitia maisha magic na Startimes star swahili...
Kama wana options zote hizo na demand ni kubwa basi hali yao ni njema sana. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana.
 
Ww wadhani wenyewe hawajawaza kuhusu ilo but all in all now days wanapeleka kwenye Channels za TV kma sinema zetu,TVE na nyingine kwa order or contract na wanapiga hela hatari zaidi ya CD...
Uhai kapata kiasi gani?

Usichukulie poa CD wakati zinauzika pamoja na wizi muandaaji alikuwa anapata hadi kiwango kinachokaribiana na hicho kwa kuuza kabisa hakimiliki yake imagine hii ni zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Turudi kwa Uhai media pale ni ameinunua Mama kimbo na viewers wake ni wenye hivyo visimbuzi tu, mtu wa Startimes hata hajui lolote labda asome tu mitandaoni kama hivi inawapa hela ndio ila haiwapi fame kama ya enzi zile
 
Bongo movie inakufa, sababu si quality (japo kweli quality ni chini)kama wengi wanavyodhani bali ni hawana namna ya kuuza movie zao. Ilianza kwa kuuza VHS za kina Majuto. Ikaja CD na DVD. kipindi hichi walau walikuwa wanapata chochote. Ghafla watu wakaanza kupirate DVD na kuziweka kwenye flash.

Hapa ndipo wizi mkubwa ulivyoanza, leo karibu kila nyumba yenye TV wana flash ya kuwekea movies, watu hawanunui tena DVD. Wabongo movie hawana namna tena ya kuuza kazi zao.

Hawawezi kupeleka kwenye majumba ya cinema kama Ulaya, au kuziweka kwenye streaming services sababu watz hatuna utamaduni wala uwezo wa mambo hayo. Kwa sasa households nyingi zinatumia flash kucheza movies

Nafikiria kama inawezekana wakaziuza movies zao kwenye flash. Yaani movie inawekwa kwenye flash ambayo inakuwa encrypted, mtu anaweza kuicheza tu na si kuihamisha. naona wholesale ya flash za 1GB inaanzia kama 0.5$, kama Tsh 1,200 hivi. Inawezekana kuuza movies kwa mtindo huu, na pengine hata inaweza kutumika kuuza album za muziki pia. inawezekana?
Encryption ni 2 side. Huwezi weka encyption mwenyewe utegemee tu tv ama deki icheze ikifika kule haitacheza.

Hapa unawapa mzigo mwengine
1. Waingie patnership na makampuni ya kutengeneza TV ama deki kudecrypt hizo video
2. Watengeneza tv/Deki zao.

Option zote mbili ni almost impossible.
 
Nilikuwa namaanisha iwe inasoma kwenye deki zote, lakini isiwezwe kuhamishwa tu. Ni kufuata tu specifications za deki zilizopo, Hilo ndilo haliwezekani?
 
Nilikuwa namaanisha iwe inasoma kwenye deki zote, lakini isiwezwe kuhamishwa tu. Ni kufuata tu specifications za deki zilizopo, Hilo ndilo haliwezekani?
Kama inasoma kwenye deki ama tv hata kama haihamishiki inaweza kukopika. Zipo card maalum kwa ajili ya kazi hizo watu hutumia kurekodi Netflix, handheld games kama switch, Amazon prime, Azam tv na service nyengine ambazo haziruhusu mtu Kucopy.
 
Ndiyo maana series za Netflix inaweza toka leo, ndani ya masaa machache unaikuta torrent. Kumbe kuna vifaa kabisa vya kukopia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom