thnkx ndugu kwa historia yangu nzuri yenye kuvutia, imenifanya nijitambue vema na vizaz vya wazee wetu kulewalikotoka...maswali
1-kabla ya yote hayo kutokea na kupelekea wachaga kutengana kwa tofauti zao. Je! Ni lugha ipi ya pamoja uliyokuwa inatumika, ukiacha kwa sasa kuna kimachame, kimarangu, kirombo, nk?
2-Napenda kufahamu koo cha machame, kunakoo ngapi!? Ukizi orodhesha chache kubwa kabisa itakuwa vema.
Uronu,
Kuhusu tofauti tofauti zilizopo kati ya wachaga nadhani unaweza kusoma utangulizi kwenye hii website itakupa mwanga ingawa kidogo: Machame - Wikipedia, the free encyclopedia.
Juu ya koo za Machame ni vigumu sana kujua leo hii kutokana na kuongezeka kwa watu na wengine kutumia majina mbalimbali hasa ukichukulia kwamba hizi mila na desturi na koo ni za siku nyingi sana. Ningekushauri uulize wazee wa maeneo hayo (Machame) kama utafanikiwa kuwaona watakusaidia. Kichaga, kwa kawaida wamekuwa wakitumia majina ama ya familia au ya ukoo (kwa upana wake zaidi). Kwa mfano, Marealle ni jina la familia na siyo la ukoo. Kama wakitumia jina la ukoo ni Lyimo. Vilevile Shangali ni jina la familia. Wakiamua kutumia jina la ukoo ni Kombe. Pia wachaga, hasa wamachame, wanaonekana kwa asili walitumia jina la mtoto na la baba yake zaidi. Inaonekana siyo asili ya wamachame kutumia jina la ukoo. Ukoo ulifahamika tu katika jamii kutokana na watu kujuana sana miaka hiyo na hasa ukichukulia kwamba wabantu kwa asili waliishi kiukoo kwenye maeneo mamoja. Kwa hiyo waliweza kujua huyu anayeishi sehemu fulani ni wa ukoo fulani. Hii pia nayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza historia za koo siku hizi labda mpaka watu waulizeulize sana.
Hata hivyo kuna koo kubwa zinazofahamika Machame. Nyingine zipo ingawa si rahisi kujua kama ni majina ya mababu au ni ya ukoo. Ukiulizia kwa uhakika utaweza kufahamishwa zaidi na wenyeji wa huko. Nitataja koo chache hapa:
Sawe (au Massawe), Lema, Nkya (wengine wanatumia Munisi), Kombe (ingawa kutokana na sababu za kisiasa kule uchagani na inaaminika pia na ushauri wa wakoloni, wengi wa ukoo huu wametumia Mushi pia, ili kufananisha koo za kiutawala kule uchagani kwa kutumia jina moja kuondoa migongano na uhasama iliyokuwepo; Mashariki ya uchagani wanatumia Moshi kama jina la ukoo), Shoo, Mboro (wengine wametumia Ndossi, Makere, n.k. kwa sababu ya machafuko ya kisiasa yaliyotokea kule Masama wakati wa utawala wa mangi Ndesserua), Kimaro, Swai, Mwaanga, na Mfuru (hawa walikuwa maarufu kwa ufuaji chuma). Kuna koo zingine ambazo siyo kubwa sana kama vile Urassa, Shuma, Kweka, Uronu, Mwasha, na Tarimo (huu ni ukoo mdogo sana Machame na asili yake ni tata kidogo. Pamoja na kutokuwa na uhakika sana lakini inaonekana kwamba walihamia kwanza Masama wakiwa ni jamii ya wamasai. Ni vigumu kujua kwa nini walitumia jina la Tarimo ambalo ni maarufu kule mashariki ya uchagani na siyo Machame. Pamoja na kwamba ulikuwa ni ukoo mdogo lakini ulikuwa na utajiri wa mifugo na uliheshimika sana Masama. Kumbukumbu kubwa ni kwamba binti wa kiongozi wa familia hiyo ndiyo alikuwa mama yake na Ndesserua. Hata hivyo wakati wa machafuko kule Masama wakati wa utawala wa Ndesserua mwenyewe, ulisababisha ukoo huo ugawanyike, wengine wakimbilie Rombo na wengine wachache sana wabaki Masama. Kule Rombo wametumia majina ya Tarimo, Marandu, na Maruma).
Hiyo ni kwa ufupi sana. Kama nilivyokuelekeza, nadhani itakuwa vizuri zaidi ukipata ufahamu zaidi kwa kuwauliza wazee wa koo mbalimbali kule Machame, wanaweza kukusaidia sana.