Kwa nini iliitwa majina hayo?
Azikiwe, Samora, Pamba, Garden, Mkwepu, Makunganya, Shauri Moyo, Jamhuri,
Uhuru, Kongo, Chole,............ongezea mingine,
Asante Ritz kwa swali lako.
Awali ya yote napenda kukuelewesha kuwa sijasema mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko yote Kariakoo.
Nimesema mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko yote hapo Dar na unaanzia Mnazi mmoja mpaka Ilala...
je asili ya jina la Yombo au Buza limetokana na nini mkuu?Nitakujibu mawili matatu
1 Ubungo Maziwa kuliwa na Kiwanda cha Maziwa, sijui bado kipo !sina uhakika.
2 Msasani inasemekana kulikuwa na Mzee mmoja maarufu aliyekua akiishi maeneo hayo aliyekuwa akiitwa Musa Hassan, sasa watu walikuwa wanasema tunakwenda kwa Musa Hassan,au kuna shughuli fulani kwa Musa Hassan. Baadaye ikaja kufupishwa Msasani.
3. Kariakoo inatokana na neno Carrier corps, yaani ushirika wa wapagazi(wabeba mizigo, makuli).
Kibirizi asili ni eneo/kitongoji/Kijiji (sina uhakika) huko Kigoma.
Sasa kama Dar kuna eneo au mahali panaitwa Kibirizi ,labda kuna jamaa mwenye asili ya Kibirizi Kigoma alikaa maeneohayo alikuwa na biashara mfano Duka,Karakana,Bar, Lodging(Guest House) au chochote akakiita jina Kibirizi.
Magomeni Mapipa kuna mtaa unaitwa Michuzi Mikali.Kwa nini iliitwa majina hayo?
Azikiwe, Samora, Pamba, Garden, Mkwepu, Makunganya, Shauri Moyo, Jamhuri,
Uhuru, Kongo, Chole,............ongezea mingine,
Sahihisho dogo tu: Samora alikuwa anapigana na utawala wa Wareno (siyo Afrika ya Kusini). Halafu maneno "Mjane wake (yaani mjane wa Samora) ndiyo mke wa Mandela sasa" yangewekwa kwenye past tense kwani tunafahamu kwamba Mandela amekwisha fariki.Samora Machel naye, kama Azikiwe, alikuwa ni kiongozi wa Msumbiji aliyepinga utawala wa amakaburu wa Afrika Kusini. Alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1986. Mjane wake ndio mke wa Mandela wa sasa.
ILALA NI MUADHINI WA KIISLAM ALITEKUA AKIADHINI" LAILAA HAILALAA"Sahihisho dogo tu: Samora alikuwa anapigana na utawala wa Wareno (siyo Afrika ya Kusini). Halafu maneno "Mjane wake (yaani mjane wa Samora) ndiyo mke wa Mandela sasa" yangewekwa kwenye past tense kwani tunafahamu kwamba Mandela amekwisha fariki.
Hii post ni ya mwaka 2012 enzi hizo Mandela akiwa hai. Wewe unaijibu leo?Sahihisho dogo tu: Samora alikuwa anapigana na utawala wa Wareno (siyo Afrika ya Kusini). Halafu maneno "Mjane wake (yaani mjane wa Samora) ndiyo mke wa Mandela sasa" yangewekwa kwenye past tense kwani tunafahamu kwamba Mandela amekwisha fariki.
je asili ya jina la Yombo au Buza limetokana na nini mkuu?
Kawe- Car wayMikocheni = michael chain
Dar es Salaam ilikuwa ikiitwa
“Mzizima"
(Ikimaanisha mji wenye neema), ni mji wa zamani ulioanza mwanzoni mwa miaka ya 1857 .
Ingawa historia ya Mzizima ilianza tangu miaka 1000 iliyopita ambapo watu wa Bara (ambao walijichanganya na Wazaramo na kuwa kati yao)
ambao walitulia na kulima katika maeneo ya mbwa maji magogoni (kwa sasa kivukoni), Mjimwema na Gezaulole.
Jiji la Dar es Salaam
Mji ulianza kuonesha mabadiliko kutokana na ujio wa wa Masultani, Wajerumani na Waingereza.
Mwaka 1866 Sultan Seyyed Majid of Zanzibar aliupa jina la ambalo ndilo linalotumika sasa neno la kiarabu lililomaanisha “Mbingu ya Amani”.
Baaba ya kifo cha Sultan Majid mwaka 1870, Dar es Salaam ilianguka lakini iliinuka tena mara baada ya ulio wa kampuni ya Kijerumani ( German East Africa Company ) iliyoanzisha kituo cha biashara mwaka 1887 na kuuondoa utawala wa Kiarabu hata kutawala pwani ya Africa Mashariki.
Walijenga mamlaka kwa ajili ya kusimamia mambo malimbali ndani ya Africa Mashariki na kuanzisha biashara kwa ajili ya maendeleo ya njia ya reli ya kati.
Iliweza kukua kwa haraka kutokana na utawala pamoja na biashara ya Wajerumani Afrika ya Masahriki.
Mwaka 1891 ulikuwa mji mkuu wa “Gerrnan East Africa“.
Dar es Salaam zamani Mzizima, ni mji mkubwa katika Tanzania na unapatikana pembezoni mwa bahari ya Hindi.
Ni mji mashuhuri na ni muhimu kwani ni mji wa Kibiashara.
Jiji la Dar es Salaam
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia Wajerumani Afrika Mashariki waliangushwa na Waingereza na tangu hapo ilijulikana kama Tanganyika.
Baada ya vita vya pili vya dunia, Dar es Salaam ilikuwa kwa haraka ikiwepo kuanzishawa kwa chama cha TANU(Tanganyika African National Union) ambacho kilisababisha Tanganyika kujipatia uhuru tarehe 9 Desemba 1961.
Dar es Salaam iliendelea kuwa mji mkuu mpaka ulipohamishiwa Dodoma mwaka 1973 , ambao ni mji ulio katikati ya nchi ya Tanzania.
Licha ya kutokuwa na tawala za mji mkuu lakini Dar es Salaam iliendelea kuwa makao makuu ya serikali.
Historia ya Ujerumani bado imekuwa ikionekana katika mji. Dar es Salaam ni mji muhimu kwa biashara na serikali.
Dar es salaam Ina Maeneo mengi Sana na Yana Asili yake
Ningependa kujua Maeneo Hayo Na Asili Ya hayo Majina Yanayopatikana Katika Mji wa Dar es salaam
Kwa Mfano
Kunduchi
Tegeta
Posta
Sinza
Manzese
Kariakoo
Kigambon
Ubungo
Mbagala
Kimara
Mbezi beach
Mbezi kimara
Gongo la mboto
Kawe
Morocco
Kinondon
Keko
Temeke
Ilala
Magomeni
Na maeneo mengine Kadha wa Kadha..........
Nawasilisha
Kvp mkurugenzUpo uzi unaozungumzia hayo majina.